Uwezo wa Kiakili wa Mashine
Bwana au Mtumishi?

Uwezo wa Kiakili wa Mashine
Uwezo wa Kiakili wa Mashine: Dhana ya kwamba vitu anavyounda mwanadamu vinaweza kumwangamiza ubinadamu ni ya kale kama ulivyo ubinadamu wenyewe | Picha (maelezo): © Adobe

Kuhusu utofautishaji usioondoleka baina ya wanadamu na mashine - insha..
 

Mwaka 1997, mwanasayansi wa Kiingereza wa mawasiliano baina ya mashine na viumbe hai aitwaye Kevin Warwick alianza kitabu chake “Maandamano ya Mashine” kwa dira isiyo na mwanga juu ya mustakabali wa dunia. Hadi kufikiakatikati ya  karne ya 21, alitabiri Warwick, mtandao wa uwezo wa kiakili wa mashine na maroboti ya hali ya juu vitamtiisha mwanadadu, na kuwafanya wanadamu ‘kutumikia’ mabwana zao ‘mashine’  peke yao kama machafuko kwenye mfumo.

Je, mwanzoni mashine zitapata hisia ya aibu kwamba zilikuwa ni uumbaji wa wanadamu, kama ilivyokuwa udadisi wa mwanzo wa mwanadamu kutaka kujifunza juu wahenga wao masokwe? Katika miaka ya 1980s, muasisi wa Kimarekani wa uwezo wa kiakili wa mashine aitwaye Edward Feigenbaum alipata maono ya vitabu vikiwasiana vyenyewe kwa vyenyewe ndani ya maktaba za siku zijazo, kwa kujitawala huru vikitangaza maarifa vilivyokuwa nayo. “Labda,” mwenzake waliyefanya kazi pamoja anayeitwa Marvin Minsky alisema, “zitatugeuza kuwa kama wanyama wa kufugwa majumbani.” Mwaka 1956, Minsky alitoa msaada katika kuandaa warsha iliyofanyika Chuo cha Dartmouth mjini New Hampshire inayoheshimika kwa kutambulisha mtajo wa Kiingereza, “artificial intelligence” ukiwa na maana ya “uwezo wa kiakili wa mashine.”

Leo hii mashine hutumika kama wanyama wetu wa kufuga majumbani. Tunaweza siku moja kuwa wanyama wao? Leo hii mashine hutumika kama wanyama wetu wa kufuga majumbani. Tunaweza siku moja kuwa wanyama wao? | Picha (maelezo): © picture alliance / dpa Themendienst / Andrea Warnecke Kubahatisha juu ya  kuenea kwa akili zinazotokana na kompyuta kulipokelewa kwa mvuto na msisimko. Haukupita muda, wataalamu waliahidi, matatizo yetu yote yangepatiwa utatuzi na ubongo wa kielektroniki. Uhalisia haukutokea kama ilivyokuwa katika shauku ya kupindukia. Baadhi ya tabiri zilikuja kuwa kweli, ingawa baada ya miongo kadhaa baadaye na zikiwa katika upeo wa chini kulinganisha na matarajio, kama mchezo wa sataranji pamoja na utambuzi wa mpangilio wake. Maendeleo ya kiteknolojia ya hivi karibuni yameleta pumzi ya maisha mapya kwenye mpangilio huu wa matukio. Teknolojia bunifu za uhifadhi wa data, kompyuta zenye nguvu kubwa iliyopindukia, dhana za kanzi-data zenye kuchakata  kiasi kikubwa mno cha data, mamilioni ya fedha katika uwekezaji unaofanywa na makampuni ya intaneti, na mbio za mataifa kutaka kuongoza duniani kupitia “faida ya seti ya kanuni za kimahesabu itokanayo na kompyuta” vimepelekea watu kuanza kusadiki upya  zile hofu za zamani kuhusiana na uwezo wa kiakili wa mashine.

Mwezi Mei mwaka 2014, wanasayansi wanne waandamizi, mshindi wa Tuzo ya Nobel ya Fizikia Frank Wilczek, mtaalamu wa sayansi ya ulimwengu Max Tegmark, mwanasayansi wa kompyuta Stuart Russell na mwanafizikia maarufu kuliko wote duniani, Stephan Hawking, walichapisha maoni kwenye gazeti la Uingereza la The Independent. Walitoa tahadhari dhidi ya kujiamini kupita kiasi na kulewa mafanikio yaliyofikiwa katika mashine zinazotumia akili kama simulizi-bunifu ya kisayansi: “Mafanikio katika kuumba uwezo wa kiakili wa mashine yatakuwa ndiyo tukio kubwa kuliko yote katika historia ya mwanadamu. Kwa bahati mbaya, linaweza pia kuwa la mwisho, isipokuwa tu kama tunajifunza kuepuka hatari zake.”

Ubinadamu katika ukingo wa hatari ya uharibifu?

Ni jambo la kushangaza kwamba utafiti katika uwezo wa kiakili wa mashine umetawaliwa na wanaume, ambao shauku yao isiyo na maana ya kuumba maisha inawezaka inatokana na aina iliyopinduka ya husuda juu ya uume tunayoweza kuiita husuda ya kuzaliwa nayo. Ni shauku isiyozuilika ya kuzalisha uumbaji unaofanywa na kompyuta ambao siyo tu unalingana, bali umewapita wanadamu kushindana na kiumbe ambaye amezunguka dunia na mambo dhahiri ya kisasa kuliko wakati mwingine wowote tokea maisha yalipoanza takribani miaka milioni 400 iliyopita. Ni shauku ya kupumbaza inayoshusha chini hadhi ya wanadadu hadi kwenye hatua ya usuluhishi katika ngazi ya kimabadiliko ambayo inaangukia mahali fulani kati ya masokwe na fahari ya uumbaji wa kiteknolojia wa siku za hivi karibuni.

Mtazamo huu unaitwa  uwezo “thabiti” au “wa kweli” wa kiakili wa mashine, na una msingi wakekwenye dhana ya kwamba kila kazi ya ufahamu wa mwanadamu  inaweza kufanywa na kompyuta, jambo ambalo nalo linahitimisha kwamba ubongo wa mwanadamu hufanya kazi kama kompyuta. Tahadhari zote zilizojaa hamaki juu ya mashine kucharuka huja pamoja katika namna ya ajabu isiyo ya kawaida. Huu ni wakati ambapo mashine zinaendeleza uwezo wake wa kimabadiliko kwa kujitawala huru, ikiashiria maendeleo ya kasi katika utendaji. Washika gadi wanaotabiri kuongezeka huku kwa kiwango cha juu kabisa cha akili za mashine wanatoa tahadhari kwamba hizi mashine zenye uwezo wa juu kabisa wa kufikiri zitaendeleza hisia za nafsi zao mara tu mchakato utakapokuwa umeanza, hatimaye kuwa na akili, viumbe wenye uwezo wa kuhisi.

Dhana ya kwamba vitu anavyounda mwanadamu vinaweza kumwangamiza ubinadamu ni ya kale kama ulivyo ubinadamu wenyewe. Inatokana na hofu, lakini pia tumaini kwamba vitu visivyo na uhai vinaweza kupata uhai, pengine baada ya kudukuliwa kidogo kimiujiza. Wamisri wa zama za kale waliweka wakati wa maziko visanamu vyenye maumbo ya wanadamu vilivyoitwa shabti – ‘watumishi wangojao kuitwa’ – kwenye makaburi yaliyojengwa kwa mawe chini ya majumba yao kufanya kazi zinazohitaji nguvukazi kwenye maisha baada ya kifo kwa niabaya marehemu. Kihistoria, vinawakilisha wazo la kwanzala kompyuta, mtumishi anayeagizwa kuitikia na kufuata maelekezo. Maelekezo yaliyotengenezwa kwa kufuata kanuni au mtindo uliobuniwa kiufundi na kuandikwa juu ya visanamu vidogo yana mfanano unaoshangaza na mtiririko ya seti za kanuni za kimahesabu ya   programu ya kisasa ya kompyuta:

Salamu, mwanasesere waa kimiujiza!
Walinzi wa maisha baada ya kifo
Wakiniita kutenda kazi…
Utachukua nafasi yangu,
Endapo itakuwa
Kulima makondeni,
kujaza vijito kwa maji,
Au kubeba mchanga…


Na majibu ya kisanamu yaliyoandikwa mwishoni:

Nipo hapa na nitakwenda kutii amri zako.

Kupata majibu kutoka dunia ya zama za kale: Watumishi wa Kimisri waitwao shabti, walioagizwa kufanya kazi kwa ajili ya wafu katika maisha baada ya kifo. Kupata majibu kutoka dunia ya zama za kale: Watumishi wa Kimisri waitwao shabti, walioagizwa kufanya kazi kwa ajili ya wafu katika maisha baada ya kifo. | Picha (maelezo): © picture alliance / akg / Bildarchiv Steffens Leo hii tungeweza kuliita jambo hili kuwa ni “msingi wa mazungumzo wa kumshawishi mtumiaji” – na kukejeli imani kwamba nuio la kimiujiza lingekuwa na uwezo wa kufanya kisanamu kidogo cha udongo wa mfinyazi kipate uhai kuwa ni ushirikina. Lakini ushirikina huu njiaumejipenyeza hadi katika maisha ya kisasa ya leo hii. Waumini wa uwezo thabiti wa kiakili wa mashine wameridhika kabisa kwamba siku fulani, namna fulani ya ufahamu wenye uwezo wa kuhisi itaibuka kwenye kompyuta. Wanatoa nadharia tete kwamba kufikiri kunawezekana kupitia kazi ndogo ya kuchakata taarifa bila kuingiliwa na kitu chochote.  Ubongo, wanasema, siyo lazima; roho ya binadamu inaweza kwa urahisi tu kuingizwa kwenye mfumo wa kompyuta. Marvin Minsky, ambaye alifariki mwezi January 2016, aliona uwezo wa kiakili wa mashine kama jaribio la kuhadaa kifo.

Njozi za nafsi ya Mashine

Akifanya kazi katika Taasisi ya Teknolojia ya Massachusetts mwaka 1965, mwanasayansi ya kompyuta Joseph Weizenbaum alitengeneza ELIZA, programu ya kuchakata lugha kiasili   ambayo iliweza kuigiza mazungumzo. Aliitengeneza programu ya ELIZA kufanya kazi kama tabibu wa kisaikolijia anayeongea na mgonjwa. Mtu angeweza kuchapa maneno, “Mama yangu ni wa wa ajabu,” na kompyuta ingejibu, “Kwa muda gani mama yako amekuwa wa ajabu?” Je, mashine zilipata uhai? Je, kinachoongea nasi, kinachotufanya kuhisi kwamba nafsi yenye uwezo wa kuhisi yenye kufanana vya a kutosha na mwanadamu kiasi cha kubadilishana kinaweza kukua kirahisindani ya kompyuta?  

Kabla ya ELIZA, mashine ziliweza tu kutoa tahadhari zisizokuwa na hisia za kibinadamu – “mgandamizo wa vilainishi uko chini”, “mfumo umekwama”. Weizenbaum alishikwa na fadhaa kuona jinsi watu ‘walioongea’ na ELIZA walivyojenga kwa haraka ukaribu wa kihisia baina yao na mashine zilitumia seti ya kanuni za kimahesabu iliyofanya kazi kwa hila kwenye mfumo wa kompyuta. Baada ya muda mfupi wa kutumia programu hiyo, katibu muhtasi wake alimwomba atoke ofisini ili aweze kuishirikisha kompyuta mambo yake binafsi ya ndani na siri zaidi. Lakini mashine ambayo programu yake imetengenezwa na binadamu hadi kuweza kusema “mimi” haiwezi kueleweka kuwa ina nafsi halisi.

Mtazamo wa ubongo kama kompyuta haufanani na kile tunachokijua hasa kuhusiana ubongo, akili ya mwanadamu, au nafsi binafsi. Hii ni sitiari ya kisasa. Katika hadithi ya mwanzo ya uumbaji, wanadamu walisarifiwa kutoka kwenye udongo wa mfinyanzi ambao ulipuliziwa pumzi ya uhai. Dhana ya mfano wa uumbaji kwa kutumia maji ilikuja baadaye kupata umaarufu, wazo kwamba mtiririko wa vimiminika ndani ya mwili ndio uliofanikisha utendaji wa kimwili na kiakili. Karne ya 16 ilishuhudia ongezeko la vifaa ambavyo viliweza kusogea na ambavyo viliundwa kwa kuiga umbo la mwanadamu kwa kutumia manyoya na meno ya gurudumu, jambo ambalo liliwavutia wanazuoni waandamizi wa nyakati hizo, kama mwanafalsafa wa Kifaransa aitwaye  René Descartes, kudai kwamba wanadamu walikuwa ni mashine isiyoweza kuelezeka kirahisi. Katikati ya karne ya 19, mwanafizikia Kijerumani aitwaye Hermann von Helmholtz alilinganisha ubongo wa mwanadamu na mashine ya telegramu. Mwanahisabati aitwaye John von Neumann alitangaza mfumo wa fahamu wa mwanadamu kuwa wa kidijitali na alikuja na mfanano mpya na sambamba baina ya sehemu za mashine za kompyuta za nyakati hizo na sehemu zubongo. Lakini hakuna yeyote kati yao ambaye amegundua kanzi-data kwenye ubongo yenye mfanano hata kidogo tu kwa upande wa kazi kama kumbukumbu ya kompyuta.

Ni watafiti wachache sana uwezo wa kiakili wa mashine wenye hofu juu ya kuibuka kwa mashine za kiwango cha juu kabisa cha akili zenye uchu wa kuwa na nguvu dhidi ya binadamu. “Jumuiya mashine zenye uwezo wa kiakili kwa ujumla wake bado ni safari ndefu kuanzia kwenye kuunda kitu chochote ambacho kinaweza kujihusisha na umma,” Dileep George, muasisi-mwenza wa Vicarious, kampuni inayojishughulisha na uwezo wa kiakili wa mashine , anasema kwa uhakika. “Kama watafiti, tuna jukumu kuelimisha umma kuhusu tofauti kati ya sinema za Hollywood na ukweli halisi.”


Mashine yenye haki za kiraia: roboti mwenye mwonekano na tabia mithili ya mwanadamu Sophia anaweza kufanya mazungumzo na kuonesha hisia - na pia ni roboti wa kwanza kupewa hadhi ya uraia. Saudi Arabia ilimtambua kama mtu mwenye wajibu wa kisheria mwishoni mwa 2017. Mashine yenye haki za kiraia: roboti mwenye mwonekano na tabia mithili ya mwanadamu Sophia anaweza kufanya mazungumzo na kuonesha hisia - na pia ni roboti wa kwanza kupewa hadhi ya uraia. Saudi Arabia ilimtambua kama mtu mwenye wajibu wa kisheria mwishoni mwa 2017. | Picha (maelezo): © picture alliance / Niu Bo / Imaginechina / dpa Ikiendeshwa kwa msaada wa dola za Kimarekani milioni 50 kutoka mradi unaotoa fedha kwa kampuni za utafiti mpya na zinazochipukia katika uvumbuzi, unaofadhiliwa na wawekezaji kama Mark Zuckerberg na Jeff Bezos, Vicarious inafanyia kazi seti ya kanuni za kimahesabu za kompyuta ambayo inaigiza mfumo tambuzi wa ubongo wa mwanadamu, lengo lenye tamaa ya makuu. Mitandao mikubwa kuliko yote ya neva bandia za akili inayofanya kazi katika kompyuta leo hii ni mara elfu moja zaidi kuliko zilizotangulia miaka michache tu iliyopita. Lakini Hii haifui dafu ikilinganishwa na ubongo wa mwanadamu

Hati ya tatanishi dunia ndicho kikwazo kikuu dhidi ya uwezo wa kiakili wa mashine. Mtoto anayezaliwa leo huibuka akiwa amejitwika kikamilifu mfumo uliorekebishwa na mabadiliko ya asili ya ulimwengu ili aweze kukabiliana na hiyo hali tatanishi -- hisia, kiasi kidogo cha matendo-hiyari (mfano chafya) muhimu kwa ajili ya kuendelea kuishi na, huenda muhimu zaidi kuliko yote, uwezo wa kipekee wa kujifunza kwa ufanisi taratibu za kufanya mambo. Mambo haya humwezesha mtoto mchanga wa mwanadamu kubadilika kwa haraka katika mwitikio wa mazingira ili aweze kufanya maingiliano bora baina yake na dunia iliyomzunguka, japo ingawa siyo ile mbayo waliikabili wahenga wake wa mbali.

Kompyuta haziwezi hata kuhesabu hadi mbili; zinajua tu mamoja na masifuri, na huchanganya vitu kwa kutumia muunganiko wa ‘uzuzu’ na kasi, na huenda miongozo au misingi michache itokanayo na majaribio na siyo nadharia, ambayo tunazoweza kuiita mbinu za kujitambua na kujiongoza mwenyewe, na mkururo mzima wa mahesabu ya hali ya juu (neno la msingi hapa ni mitandao bandia ya neva za akili). Ili kuweza kweli kuelewa hata kidogo tu jinsi ubongo wa mwanadamu unavyoendesha akili ya mwanadamu, yawezekana isitoshe tu kujua hali ya sasa ya seli zote trilioni 86 za neva na mishipa yake trilioni 100, na uwezo utofauti wa muunganiko wa vitu hivi, na hali ya zaidi ya  protini 1,000 ambazo zipo katika kila mshipa wa fahamu. Tunaweza pia kutakiwa kuelewa jinsi shughuli ndani ya ubongo kwa wakati wote inavyochangia kwenye uaminifu wa mfumo mzima.
Hata baada ya kujua yote hayo, bado tutakuwa tunakabiliana na upekee wa kila ubongo kutoka kwenye maisha na uzoefu wa kipekee wa kila mwanadamu duniani.
 
Uwezo wa kiakili wa mashine, ambao unaelekea kuonekana kama seti iliyo na nguvu kubwa sana ya kanuni za kimahesabu za kompyuta,  ambao ni matokeo ya kijamii ya ulimwengu unaoendeshwa kwa kutumia kompyuta – Goethe.de hutoa makala za nyongeza ambazo huelezea na kujadili mada hizi na masuala kama haya.

Je, haki zetu za msingi bado zinatosha kuwa kama ulinzi katika zama za data nyingi, mitandao ya ya kijamii na seti ya kanuni za kimahesabu za kompyuta zenye uwezo wa kutoa maamuzi? Ili kuwa na uhakika, wataalamu wa mambo ya kidijitali kutoka Ujerumani wanahamasisha kuanzishwa kwa Mkataba wa Haki za Msingi za Watumiaji wa Mtandao wa Umoja wa Ulaya.

Siyo tu athari za kisheria au hali ya kuonekana tofauti na kawaida iliyozoeleka, bali lawama za kuwa kinyume na maadili nazo pia huibuka pale mashine zenye akili zinapofanya maamuzi kwa kufuata mantiki zake zenyewe. Kwa hiyo tume ya maadili inafanya tathmini, kwa mfano, juu ya suala la uwajibikaji katika utoaji wa maamuzi kwa magari yanayojiendesha yenyewe.

Uwezo wa kutoa maoni wa watoa huduma wasiotambulikana kutoka katika mitandao ya kijamii nao pia unafanyiwa uchunguzi mkali na makini: ili kubaini ni kwa kiasi gani wana uwezo wa kushawishi michakato ya kisiasa? Kampeni za uchaguzi mkuu uliopita zilitoa msingi wa kutosha kuanzisha majadiliano haya.

Kwa ujumla wake, mdahalo juu ya athari za seti ya kanuni za kimahesabu za kompyuta umegubikwa na hitaji la uwazi kwa upande mmoja na upande wa pili, matumizi ambayo daima yamekuwa yakiongezeka ya Google, Facebook na watoa huduma wengine.

Kupanuka kwa teknolojia ya kidijitali kunaifanya ionekane karibu kwenye kila nyanja wa maisha ya kila: matumizi ya roboti yamekuwa yakiongezeka katika biashara za kila aina – siyo tu katika uzalishaji, bali katika sekta ya huduma pia, kwa mfano. Licha ya kuongeza tishio katika usalama wa baadhi ya ajira, jambo hili hutoa pia fursa za uhuru zaidi na ufanisi mkubwa.

Ndoto ya Jiji la Kiteknolojia linalotoa huduma na kutatua matatizo kidijitali– jiji ambalo kutokana na teknolojia za uwezo wa kufikiri wa mashine, ni rafiki wa mazingira na mwokozi wa rasilimali – siyo tena jambo la kufikirika. Hata hivyo jamii kama hiyo ya kidijitali ina gharama yake: eneo na watu wanaoshughulika ndani mwake wamekaribia wote kuwa wa kidijitali.

Na kitu gani kinaendelea kwenye sanaa? Nayo pia hutumia uwezo wa kiakili wa mashine kwa makusudio yake. Kuna ongezeko la wasanii wa kibunifu waliojikita katika kazi zao wakihusianisha kanuni fulani, sanaa, na maisha katika dunia za kidijitali.