Tamasha la Kila Baada ya Miaka Miwili la Berlin 2018
Hatuhitaji shujaa mwingine

Onesho la sanaa kupitia video la Mario Pfeiffer “kwa mara nyingine tena” limejikita kwenye tukio lililotokea Saxony, mahali ambapo wanakijiji wanashukiwa kumfunga kamba mkimbizi kwenye mti.
Onesho la sanaa kupitia video la Mario Pfeiffer “kwa mara nyingine tena” limejikita kwenye tukio lililotokea Saxony, mahali ambapo wanakijiji wanashukiwa kumfunga kamba mkimbizi kwenye mti. | Picha (maelezo): © picture alliance/Carsten Koall/dpa-Zentralbild/dpa

Ulimwengu wa sanaa ulitarajia mambo makubwa sana kutoka kwenye awamu ya kumi ya Tamasha la Kila Baada ya Miaka Miwili la Berlin la Sanaa za Kisasa – tamasha la kwanza kufanyika chini ya uongozi wa mwanamke wa Kiafrika. Hata hivyo onesho lilikataa kuandaa masimulizi yaliyorahisishwa na yaliyonyooka juu ya ukoloni. 
 

Kaulimbiu ya awamu ya la Kumi ya Tamasha la Kila Baada ya Miaka Miwili la Berlin inayosema: Hatuhitaji shujaa mwingine, iliyobuniwa kutokana na na wimbo wa Tina Turner kwa ajili ya filamu ya Mad Max 3, inaonekana kuamsha hisia kali mwaka 2018. Maonesho katika tamasha hili la kila baada ya miaka miwili la sanaa za kisasa daima yamekuwa yakijihusisha na masuala ya a kisiasa na kijamii. Wakosoaji wengiwalitarajia ujumbe dhahiri juu ya ukoloni kutoka kwa mwongozaji wa kwanza wa kike wa a Kiafrika wa Tamasha; tafsiri ya kisanii ya  historia mbalimbali za ukoloni. Hata hivyo mwongozaji Gabi Ngcobo na wenzake – wote wakiwa ni weusi: Nomaduma Rosa Masilela, Serubiri Moses, Thiago de Paula Souza na Yvette Mutumba – kuchukua msimamo dhahiri dhidi ya mwelekeo wa juujuu wa historia. 
 
Onesho liliwasilisha uchanganuzi uliopangiliwa wa  mada kuu mbili: kwa upande mmoja ilikuwa juu ya kunyimwa haki, vitendo vya unyanyasaji na kifo katika zama za ukoloni mamboleo na kwa upande wa pili, harakati za kupinga ukoloni katika nyakati za sasa. Nyingi miongoni mwa kazi za wasanii 46 wa kimataifa  zilioneshwa kupitia vipande vifupi vya kazi za sanaa, sauti kutoka katika drama, athari za mada zinazowaunganisha wasanii na wadau wa utamaduni duniani na kujiweka kando na masimulizi yaliyonyooka. Tamasha lilitilia mkazo juu ya kuishi duniani kulingana na wakati uliopo kama njia ya kupinga mantiki iliyonyooka ya dhana ya Kimagharibi ya wakati na historia. Lilifanya kazi katika mwelekeo wa kuchimba historia iliyozikwa, kutoa nafasi kwa ajili ya mitindo ya kuiandika upya na uponyaji wa pamoja.

Sanaa kama nafasi ya harakati za mapambano

Filamu ya msanii na mwanaharakati Natasha A. Kelly, Milli’s Awakening (2018) ni taswira ya wasanii wa kike na wanaharakati nane ambao ni Wajerumani wenye asili ya Afrika na ambao wanasimulia hadithi zao binafsi za mapambano dhidi ya ubaguzi wa rangi, kunyimwa fursa na mfumo usiotoa haki ndani na nje ya ulimwengu wa sanaa nchini Ujerumani. Mmojawapo miongoni mwa wanawake hao, anayeitwa Nadu, anavuta kumbukumbu ya adha alizokutana nazo alipokuja Ujerumani kama kijana mdogo wa kike mwenye rangi tofauti ya ngozi. Ilimfanya ajihisi kuwa mwanadamu ambaye hajakamilika. Mwanaharakati mwingine, Maseho, anasoma kutoka kwenye mwongozo wake aliouandika kwa njia ya kejeli kwa ajili ya watu weusi wanaosafiri nchini Ujerumani. Mwongozo huo unawashauri kuokoa muda kwa kuwambia Wajerumani kwamba wanatoka Marekani au Afrika, kwa sababu jibu tofauti litaingiza uelewa wa dunia wa Wajerumani katika ghasia. Mwanamke mwanaharakati kutoka Bremen anayeitwa Maciré anakumbushia “kuzinduka” kwake pale alipogundua kwamba filamu yake ilikuwa inatumiwa kuhalalisha onesho kwa kutoa mtazamo wa mtu asiyekuwa Mzungu – hali ambayo inaweza kuonekana kuwa inafahamika kwa Kelly mwenyewe, msanii wa asili ya Jamaka aliyezaliwa nchini Uingereza. Hata hivyo filamu pia inaonesha namna gani wanawake hawa wamegundua katika jumuiya zao na katika kufanya sanaa njia ya kuishinda hali yao ya kutoridhishwa na njia ya kupigania haki katika jamii. 
Msanii kutoka Cuba anayeitwa Belkis Ayon hutengeneza taswira za kazi za sanaa ambazo zinazotoa mfanano kati ya maisha yake mwenyewe na maisha ya Sikán, mhusika wa kike kitabu cha simulizi la kale kinachoitwa Abakuá kuhusu watu wa Cuba wenye asili ya Afrika. Msanii kutoka Cuba anayeitwa Belkis Ayon hutengeneza taswira za kazi za sanaa ambazo zinazotoa mfanano kati ya maisha yake mwenyewe na maisha ya Sikán, mhusika wa kike kitabu cha simulizi la kale kinachoitwa Abakuá kuhusu watu wa Cuba wenye asili ya Afrika. | Picha: © picture alliance/Carsten Koall/dpa-Zentralbild/dpa Kwenye kipande cha mchezo wa kuigiza Sitting on a Man’s Head (2018), iliyotolewa kwa ushirikiani na mpenzi wake, Peter Born, pamoja na baadhi ya waigizaji kutoka Berlin, mchezaji wa miondoko ya dansi jukwaani na mwandishi anayeitwa Okwui Okpokwasili anaangazia mbinu ya kiasili ya amani ya harakati za mapambano iliyotumiwa na wanawake kutoka Mashariki mwa Nigeria. Ikijulikana kama “kukaa juu ya kichwa cha mwanaume”, inajumuisha kusababisha kwa pamoja uingiliaji kati dhidi ya walioshika hatamu za madaraka, mfano, kwa kucheza au kuimba mbele ya nyumba au ofisi ya mtu fulani, na hivyo kuwatia aibu mbele ya jamii. Inawawezesha wanawake wasiopewa kipaumbele, kama ambavyo msanii anaelezea, “kujibu, kutoa kero zao, na kutoa msukumo wa mabadiliko”. Desturi hiyo ndiyo iliyotoa ushawishi wa kuja na igizo hili , linaloanzia nje ya chumba ambacho kwa kuta za plastiki zinazopitisha mwanga mdogo, ambapo watu miongoni mwa hadhira hushiriki kwa kina katika mazungumzo yanayochochewa na maswali kama vile “ni kitu gani ambacho umekuwa mwoga kukisema na kwa nini?”. Mchezaji na hadhira wanapoingia chumbani taratibu, sehemu za mazungumzo zinatoa mwangwi kutokea ndani katika miondoko, mikao, na kauli ambavyo kwa  pamoja hutengeneza wimbo mpya wa pamoja. Tafsiri kutoka kwenye nafasi ya mazungumzo kutoka moyoni hadi kwenye miondoko ya pamoja una nguvu na huonesha upinzani wowote mwepesi usiotenda kazi kati ya upeke na ujumla wa watu. 

Utatanishi badala ya shujaa mwingine

Wazo kwamba uingiliaji kati unaweza kuleta mabadiliko ni kitu ambacho daima kimekuwa na mvuto kwa Lubaina Himid. Kwa ajili ya Tamasha la Kila Baada ya Miaka Miwili la Berlin , Himid alitengeneza mfululizo wa michoro ya kitamathali wenye kichwa cha habari Ndani ya Usiku wa Mwezi Mpevu (2018). Kwa kuvutiwa na mtindo wa vazi la “kanga” linalovaliwa na wanawake  waAfrika Mashariki, the michoro hiyo inawakilisha viungo vya mwili, kama vile ubongo, matiti, mapafu au mkono, wakati ambapo maneno kutoka kwa washairi kama Audre Lorde, Essex Hemphill, na Maud Sulter yameingizwa kwenye picha. Kuingizwa kwa maneno kunafanyika kama vile kukatisha tukio la kipande kilichotangulia cha masimulizi na hivyo kutoa nafasi kwa ajili ya kusimulia hadithi nyingine. 
Katika onesho la sanaa la “Toli Toli” kutoka kwa Minia Biabiany, sauti za wazee zinasikika wakiimba wimbo wa jadi wa chekechea kutoka kisiwa cha Karibeani cha Guadeloupe. Watoto wa Guadeloupe leo hii hawaujui tena wimbo huo. Katika onesho la sanaa la “Toli Toli” kutoka kwa Minia Biabiany, sauti za wazee zinasikika wakiimba wimbo wa jadi wa chekechea kutoka kisiwa cha Karibeani cha Guadeloupe. Watoto wa Guadeloupe leo hii hawaujui tena wimbo huo. | Picha: © picture alliance/Carsten Koall/dpa-Zentralbild/dpa Awamu ya Kumi ya Tamasha  la Kila Baada ya Miaka Miwili la Berlin  la Sanaa za Kisasa liliwasilisha nyakati za uingiliaji kati, mada zinazowaunganisha wasanii na wadau wa utamaduni duniani, kujitenga kando na kupata hali halisi ya mawazo ambazo hutoa nafasi kwa ajili ya kusimulia hadithi tofauti. Iliibua swali linalohoji jinsi gani sanaa inaweza kuwa nafasi ya kutuwezesha kutumia ukaidi kama njia ya pamoja ya kusalimika. Badala ya kutoa “shujaa mwingine” wa kuwasilisha majibu yanalokubalika na wote, onesho lilijielekeza kwenye utatanishi na kuhitilafiana kwa mada zinazokingama masuala ya ubaguzi wa rangi, ukoloni na uhamaji.