Uwezo wa kiakili wa mashine
Roboti zenye sura na tabia za binadamu zimewadia

Roboti zenye sura na tabia za binadamu zitaendelea kufanana zaidi na binadamu kadri muda unavyoendelea. Lakini bado kuna muda muda mrefu kuelekea huko.
Roboti zenye sura na tabia za binadamu zitaendelea kufanana zaidi na binadamu kadri muda unavyoendelea. Lakini bado kuna muda muda mrefu kuelekea huko. | Picha (maelezo): © picture alliance/Westend61

​Mitandao ya kimataifa ya utafiti inajaribu kuunda roboti mwenye uwezo kutembea, kuonesha tabia na hata kufikiri zaidi kama binadamu. Hata hivyo itachukua muda mrefu kwa uwezo wa akili ya mashine kukaribia uwezo wetu.

Mwaka 2013 Umoja wa Ulaya ilizindua mpango uitwao Human Brain Project (HBP) ambao tamanio la lengo lake ni kuongeza uwezo wa kiakili wa mashine hadi kufikia kiwango cha exaFLOPS moja katika kipindi cha miaka kumi ijayo. ExaFLOPS moja ni bilioni moja mara bilioni moja ya idadi yote ya nyota katika mifumo miwili ya nyota ijulikanayo kitaalamu kama Milky Way na Andromeda, ikiwekwa pamoja. Kila mwanadamu huzaliwa na uwezo wa kompyuta kama hiyo, katika bongo zetu. Mradi wa HBP unatarajia kutumia miaka kumi tu kuongeza uwezo wa kiakili wa mashine hadi kufikia kiwango hicho ambacho kimechukua mabilioni ya miaka kufikiwa na ubongo wa binadamu.

USHIRIKIANO HUKUZA UFANISI

Jumla ya taasisi za utafiti na makampuni zaidi ya mia wanahusika katika mradi huu mkubwa. Hatua ya kwanza ilikuwa kuanzisha mtandao wa kimataifa wa utafiti ili wataalamu wa sayansi ya akili, wanasayansi wa kompyuta na wataalamu wengine kutoka taaluma tofauti waweze kubadilishana taarifa na maoni. Kwa pamoja, wanachunguza ubongo wa binadamu kwa undani zaidi kuliko ilivyowahi kutokea wakati wowote – wakianzia katika ngazi ya molekuli na kuendelea hadi kwenye mishipa inayowezesha michakato migumu ya utambuzi. Wanafalsafa wamejumuishwa pia, kwa kuwa utafiti huu unagusa masuala ya maadili.
Ushirikiano wa kiwango cha shauku huu unaweza kwenda vizuri endapo kushirikishana miongoni mwa jamii ya jamii ya kisayansi kunaboreshwa. Hadi sasa hakuna viwango vya kimataifa vya utafiti katika elimu ya mishipa ya fahamu ambapo kila taasisi inatengeneza matokeo ya tafiti zake kwa namna ya peke yake, hivyo kupelekea ugumu wa kupata hali halisi ya utafiti katika mfumo unaofanana. Mradi wa HBP unatarajia kubadilisha hali hii, na utatoa nafasi kwa watafiti duniani kote ruhusa ya kutumia matokeo ya tafiti zake kwenye miradi yao. Mpango huu unalenga kuanzisha jukwaa la kimataifa linalochakata data za sayansi ya akili kwa namna inayofanana, ili maarifa yatakayopatikana yaweze kutumika kwenye tafiti za kitabibu halikadhalika.

KUSHIRIKIANA NA UWEZO WA KIAKILI WA MASHINE

Wakati wanasayansi kutoka mradi wa HBP huko Geneva wakichunguza muundo wa ubongo, watafiti huko Munich wanafanyia kazi roboti ambaye ataiga tabia zote za kimwili za mwanadamu. Roboti huyu aliyepewa jina Roboy siyo tu sura ya HBP. Tunaweza kusema roboti huyu pia mikono na miguu, viwiko, nyonga zinazonesa na macho yanayokonyeza ya mradi.

Hadithi ya Roboy ilianza katika Chuo Kikuu cha Zurich mnamo 2013, ambapo wanasayansi wa kompyuta, wahandisi na wahandisi wa vifaa vya elektroniki waliunganisha nguvu kutengeneza roboti anayeweza kutenda kazi mwenyewe sambamba na mwanadamu, walau kwenye nyanja ya ufundi. Watafiti kutoka kote Ulaya na hata mabara ya mbali wamejuika katika mradi huu, mfano ni watafiti kutoka Chuo Kikuu cha Melbourne ambao walitumia ujuzi wao wa udhibiti wa misuli kutoa mchango uliopelekea kutengenezwa programu ya kompyuta inayoratibu uwezo wa Roboy kujifunza mambo kwa mazoea. Matokeo yake, timu inayoshughulika na Roboy kwa upande wao ikachangia katika uundaji wa vifaa vya hali ya juu katika miradi yao.
Roboti Roboy anaweza kuendesha baiskeli na kupiga muziki. Kufikia mwaka 2020 watengenezaji wake wanasema atakuwa na uwezo wa kuchunguza hali za afya Roboti Roboy anaweza kuendesha baiskeli na kupiga muziki. Kufikia mwaka 2020 watengenezaji wake wanasema atakuwa na uwezo wa kuchunguza hali za afya | Picha: © Roboy 2.0 - roboy.org Robot huyu sasa amehamia Chuo Kikuu cha Ufundi cha Munich, ambapo kila muhula wa masomo timu mpya ya wanafunzi kutoka fani mbalimbali hufanya kazi ya kumfundisha Roboy kitu kipya. Kiwango cha akili za Roboy sasa kinadhihirika kwa mambo kama vile uwezo wa kuongea na watu wawili kwa wakati mmoja au kupiga marimba. Matokeo ya tafiti zao zote yanapatikana bure kwenye jukwaa la watafiti wa roboti mtandaoni. Kuanzia muundo wa kiufundi wa miguu yake hadi mchoro wa duru inayopelekea macho ya Roboy kupata uwezo wa kuona, mfumo mzima wa mwili ya roboti umeelezwa waziwazi mtandaoni na mtu yeyote, iwe ni yule asiyejua chochote, mtafiti, au bingwa wa teknolijia anaweza kupakua maelezo hayo, na kuchangia chochote kwa ajili ya mradi kupiga hatua.

Na roboti huyu mdogo anajifunza kwa haraka: Roboy anaweza kuendesha baiskeli na kuwasha muziki kwenye redio. Anapoendelea kukua kiakili, anaweza kuja kufanya kazi kama mhudumu wa hoteki au seremala, kazi ambazo uhodari wake hutokana na mazoea. 

MASHINE YENYE KUFANANA NA BINADAMU KUPITA ZOTE

Hadi kufikia mwaka 2030, Mradi wa HBP unatarajia kutimiza lengo lake la kugundua kompyuta itakayokuwa na uwezo wa kufikiri sawa kabisa na ubongo wa mwanadamu. Hata hivyo bado kuna viunzi vichache mbele ya safari. Kwa mfano, bado inahitajika kupitia hatua kadhaa zaidi za kiufundi ili kufikia ule uwezo wa kompyuta wa exaFLOPS moja. Na kwa kuwa hata kujaribu kuiga kasi na uwezo wa kumbukumbu ya ubongo mwanadamu kunahitaji kiwango cha kutisha cha umeme, inahitaji kupiga hatua kubwa kugundua kompyuta inayotumia vizuri umeme. Ugunduzi huu hatimaye unaweza kuleta mapinduzi katika mfumo wa sasa wa kompyuta.

Endapo itawezekana kuruka viunzi hivi, siku zijazo za Roboy zitakuwa njema sana: akiwa na “ubongo” wenye uwezo wa exaFLOPS, roboti huyu wa HBP atakuwa na uwezo ulimkaribia mwanadamu kuliko mashine yoyote iliyowahi kutokea. Jambo hili linaibua maswali ya msingi na dhahiri juu maadili, ndiyo maana kamati ya maadili daima imekuwa sehemu muhimu ya mradi. Roboy daima hujiweka katika nafsi ya kirafiki, na mwonekano wake mchangamfu huwavutia watu kuongea na mashine rafiki.