Mdahalo wa kurejesha vitu vya sanaa makwao
Kasi Ndogo Ya Mchakato Wa Kurudishia Taratibu Vitu Vilivyotwaliwa Na Wakoloni

Shujaa wa kitaifa wa Namibia Hendrik Witbooi labda hakuwahi kuota kwamba mjeledi wake na biblia siku moja itakuwa mambo ya mabishano ya kimataifa.
Shujaa wa kitaifa wa Namibia Hendrik Witbooi labda hakuwahi kuota kwamba mjeledi wake na biblia siku moja itakuwa mambo ya mabishano ya kimataifa. | Picha (maelezo): akg-images © picture alliance

Vitu hivyo vilitoka wapi hasa? Madai ya umiliki wa mali za kitamaduni tangu kipindi cha ukoloni mara kwa mara hugubikwa na utata na majadiliano juu ya uwezekano wa kuwarudishia wenyewe ni mchakato uliojaa mashaka unaokwenda kwa kasi ya kinyonga. Ujerumani inachukua hatua fulani za awali  katika kuelekea kufikia azimio.
 

Ukitumiwa na watawala wa kikoloni wa Kireno kutangaza umiliki wao wa Rasi ya Msalaba kutoka kusini mwa Afrika, ni mnara wenye urefu wa mita 3.50 kwenda juu, na umri wa walau miaka 530, na juu yake ukiwa na taji la msalama wa jiwe la chokaa. Kulingana na ngao ya taifa la Ureno, kwa mara ya kwanza ulisimikwa mwaka 1485 na kubakia barani Afrika hadi mwaka 1893, wakati ambao wakoloni wa Kijerumani waliokuwa wametwaa utawala wa himaya hiyo walipoileta mali hiyo ya kihistoria na kitamaduni hadi Berlin. Sasa, safari ya kurejea kwake kumekaribia: Taifa la Ujerumani limekubali kuirejesha tena  Sanamu ya Msalaba iliyotoka Rasi ya Msalaba nchini Namibia. Kamishna wa Utamaduni wa Vyombo vya Habari wa Serikali ya Shirikisho - Monika Grütter - aliuita uamuzi huu kuwa wa “kupiga hatua na wenye maana”. 
 
Hadi kufikia sasa hata hivyo, mchakato wa kuwarudishia wenyewe umekuwa wa hiyari zaidi kuliko kisheria nchini Ujerumani. Uamuzi wa jimbo la Baden-Württemberg kurejesha biblia na mjeledi wa shujaa wa kitaifa wa Namibia aitwaye Hendrik Witboo kwa serikali ya Namibia mwanzoni mwa mwaka 2019 ni mfano mwingine wa kuiga. Tofauti na hapo, mchakato wa kuwarudishia wenyewe ulikuwa umeishia kwenye mabaki ya wanadamu, kama vile mafuvu ya watu wenye asili ya Australi, na mifupa kutoka nchi za Kiafrika. Muungano unaotawala wa wapenda mabadiliko ya kijamii  na wahafidhina umeonesha kukubaliana na ukweli wa mambo yaliyotokea wakati uliopita wa kikoloni, zikiashiria katika iprogramu ya serikali yao kwamba uchunguzi wa makosa ya jinai yaliyofanywa wakati wa kipindi hicho ni sharti uwe sehemu ya  kumbukizi yautamaduni wa wa kitaifa.

Shujaa wa kitaifa wa Namibia - Hendrik Witbooi - huenda hakuwahi kuota kwamba mjeledi na biblia yake vingekuwa siku moja  kuwa vitu vya utata wa kimataifa Shujaa wa kitaifa wa Namibia - Hendrik Witbooi - huenda hakuwahi kuota kwamba mjeledi na biblia yake vingekuwa siku moja kuwa vitu vya utata wa kimataifa | Picha (maelezo): © picture-alliance/dpa

Mdahalo wenye ukomo juu ya wakati uliopita wa kikoloni

Mpaka sasa, Ujerumani imeshindwa kufuatilia kwa kina taarifa za Himaya ya Ujerumani mwishoni mwa karne ya 19 na mwanzoni mwa karne ya 20. Ufahamu wa makosa ya jinai yaliyofanywa wakati wa kipindi hicho umeongezeka hivi karibuni, kwa sehemu fulani kufuatia mdahalo kuhusu mauaji ya halaiki ya watu wa makabila ya Nama na Herero yaliyofanywa na vikosi vya wakoloni wa Kijerumani nchini Namibia. Serikali ya Shirikisho inatafuta maridhiano na koloni la zamani, ikiwa ni pamoja na mchakato wa kuwarudishia wenyewe mali za kitamaduni zilizoibwa. 
 
Makumbusho za Ujerumani zina maelfu ya vitu vya kibunifu kutoka duniani kote. Idadi kamili haijulikani, kama ilivyo katika swali, endapo vilitwaliwakisheria. Vitu hivi vinajumuisha vitu vya ubunifu wa kustaajabisha kama vile sanamu ya kichwa na mabega, ya Nefertiti – farao wa Kimisri. Madai ya Misri ya kurejeshwa kwa sanaa hiyo yamefumbiwa macho hadi wakati huu. Halafu kuna kiunzi chenye urefu wa kwenda juu wa mita 13 cha mifupa ya dinosauri ndani ya Makumbusho ya Berlin ya Historia ya Asili Ujerumani, ambayo wanasayansi waliivumbua na kuichukua kutoka Tanzania.
 

Utafiti wa chimbuko la kitu kama sehemu ya kuanzia

Vita inayoendelea ya mchakato wa kuwarudishia wenyewe: nani ni mmiliki wa kweli wa sanamu ya kichwa na mabega, ya Nefertiti? Vita inayoendelea ya mchakato wa kuwarudishia wenyewe: nani ni mmiliki wa kweli wa sanamu ya kichwa na mabega, ya Nefertiti? | Picha (maelezo): © picture alliance / Eventpress Herrmann Ni wazi kwamba watunzaji wa hizi hazina hawana mwelekeo wa kuanzisha jambo  muhimu kama hilo. Mwaka 2019, hata hivyo, serikali ya shirikisho na  serikali za majimbo walikubaliana katika baadhi ya hoja muhimu za kushughulika na hizi hazina. Tamko lao linasomeka:”Tunataka kutengeneza mazingira kwa ajili ya kurejesha makwao kwa mabaki ya wanadamu na wa vitu vya kitamaduni vya muktadha wa kikoloni ambavyo kutwaliwa kwake hakuwezi kuhalalishwa tena kisheria au kimaadili leo hii.” Katika uhalisia, Grütters alianza kwa kuunga mkono utafiti zaidi wa chimbuko la kitu, ambao unatoa asili na mazingira ya kutwaliwa kwa mali za kitamaduni.
 
Uamuzi huu umekumbana na ukosoaji mkali. Jürgen Zimmerer, mwanahistoria wa Hamburg, anaona mkazo unaowekwa kwenye utafiti wa chimbuko la kitu kama mkakati wa kukawiza  maazimio muhimu ya kisiasa. Anahofia jambo hili linaweza kuhamasisha “kujisahaulisha makusudi mambo ya kikoloni” badala ya kuongoza mhadhara unaohitajika kwa umma. “Kushughulika na urithi wa kikoloni wa Ulaya ni mmoja kati ya midahalo mikubwa, kama siyo mkubwa kuliko yote, wa utambulisho katika zama zetu,” Zimmerer anaandika. Badala ya utafiti wa asili za kitu, anatoa wito wa kuwatua watu mzigo wa kutoa uthibitisho, akipendekeza makusanyo ya kikoloni ndiyo yatoe uthibitisho kuwa vitu yanayoviliki vilitwaliwa kisheria. Kinyume na hapo, vitu vya kibunifu vinavyoongelewa vichukuliwe moja kwa moja kuwa viliibwa.

Ufaransa inaweza kuongoza njia

Serikali ya Ujerumani  pia ni inapata shinikizo kutoka kwa Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron, ambaye yupo tayari kufikia makubaliano baina ya nchi yake na mataifa ya Kiafrika juu ya kurudishwa kwa mali za kikoloni zinazotunzwa nchini Ufaransa. Rais huyo alivutiwa kwa sehemu fulani na kazi ya Bénédicte Savoy, mwanahistoria wa sanaa wa Kifaransa  anayefundisha katika Chuo Kikuu cha Ufundi  cha Berlin, na mchumi Felwine Sarr. Ndani ya ripoti ya tume, walimtia moyo Macron kufuatilia mchakato wa kuwarudishia wenyewe moja kwa moja sanaa zote zilizoibwa.
 
Madai ya Savoy pia yanatoa mwangwi unaosikika ndani ya kumbi za Berlin. Hapa ndipo ulipo utata wa Jukwaa la Humboldt. Makumbusho hii italeta pamoja makusanyo ya vitu vya sanaa visivyotoka Ulaya; na vinavyotoka Asia vya Taasisi ya Urithi wa Utamaduni wa Kijeruma inayohifadhi  makumi ya maelfu ya vitu vya kibunifu ambazo asili yake inatiliwa shaka, na kuvionesha katika jumba lililojengwa upya jiji. Mwaka 2017, Savoy alijiuzulu nafasi yake katika Bodi ya Ushauri ya  Jukwaa la Humboldt kuonesha upinzani, kiasi fulani ikiwa ni kwa sababu ya kukosekana uwazi na kupuuzwa kwa utafiti wa chimbuko la kitu.