Kumbukumbu Potofu
Kilichotokea kwa Mandela

Kumbe alikuwa bado ana nguvu na uwezo wa kufanya kazi licha ya umri wake mkubwa! Wakati picha hii inachukuliwa mwaka 1990, Nelson Mandela alitakiwa awe tayari amekufa kitambo kirefu kabla, endapo tunategemea taarifa kutoka katika kumbukumbu za wengi miongoni mwa watu wa hirimu yake. Hicho kilidhaniwa kuwa kifo chake ndicho kilichosababisha kuibuka kwa dhana ya kumbukumbu potofu za pamoja - Kilichotokea kwa Mandela.
Picha (maelezo): © picture alliance/dpa/empics

Bila kujali kwamba ni suala la kuamini mtu fulani amefariki tokea kitambo, ingawa mtu huyo bado ana afya njema kabisa, au suala la kuimba maneno ya wimbo kwa kutumia maneno yasiyokuwa sahihi – pale ambapo watu wengi katika umoja wao wanakumbuka mambo kidanganyifu, tunaongelea Kilichotokea kwa Mandela. Yawezekana jambo hili kamwe lisitokee kwako, sawa? Kwa kupitia mifano yetu unaweza kugundua kama upo au haupo sahihi.
 

“Nini? Bado yupo hai?” Sentensi hii husikika sana na mara nyingi sana katika siku hizi, iwe ni kwenye sherehe ya familia au katika sehemu ya kinywaji. Kwa kujibu, unatikisa tu kichwa chako taratibu na bila papara unapiga funda la kahawa yako. Sasa inakuwa ni jambo linalozoeleka zaidi na zaidi kwa mtu kukumbuka tukio ambalo kwa hakika halikutokea kwa namna wanavyolikumbuka. Kitu hiki, kwa kweli, ni kumbukumbu potofu, lakini siyo kwamba jambo hili hutokea tu kwa mtu mmoja mmoja. Halaiki yote inaweza pia katika umoja wake kukumbuka mambo kidanganyifu – na dhana hii inakwenda kwa jina la Kilichotokea kwa Mandela.

Imepewa jina hilo kutokana na kigezo kwamba watu wengi walifikiri kwamba Nelson Mandela alikuwa tayari amefariki akiwa gerezani. Jambo ambalo siyo kweli. Mandela aliachiwa huru kutoka gerezani mwaka 1990 na alikuwa Rais wa Afrika Kusini kuanzia mwaka 1994 hadi 1999, hadi alipofariki kutokana na nimonia tarehe 5 Desemba 2013, akiwa amezungukwa na ndugu wa karibu wa familia. Wasomaji wadadisi wanaweza kuwa tayari wamegundua kwamba kuna kipindi cha miaka 23 kati ya iliyodhaniwa kuwa tarehe ya kifo na tarehe halisi ya kifo. Habari za kifo cha Mandela zilipotangazwa kupitia vyombo vya habari, watu wengi walipata mshtuko – na hata walidhani kwamba walikuwa wanakumbuka kuona kipindi cha mazishi yake kwenye televisheni.

Majimbo yasiyohesabika ya marekani

Japokuwa inasikika kama kitu cha ajabu, ni dhana inayotambulika na hisia na iliyoonea sana kiasi kwamba watu wengi sana hukumbuka kidanganyifu uzoefu mbalimbali kwa namna ya kawaida. Kuna mifano ya jambo hili kutoka kila nchi na utamaduni. Iwe ni muziki, filamu au watu maarufu – hakuna anayesalimika dhidi ya “Kilichotokea kwa Mandela”.

Chukulia mfano wa wimbo mashuhuri wa mahadhi ya ballad “Sisi ni Machampioni” wa bendi ya Queen, kwa mfano. Kila mwenye kufahamu maandishi, anaweza kuimba sambamba na bendi au kutoa sauti ya mvumo, iwe ni katika mchezo wa soka au sehemu ya kinywaji wanapopiga wimbo huo. Na namna tunavyosubiria mwishoni mwa wimbo pale ambapo unahama kuelekea kwenye kilele chake, tunasimama bega kwa bega kando ya kila mmoja na kujiweka tayari kwa ajili ya kuimba mstari wa mwisho – “Sisi ni machampioni ... wa dunia!” Hivyo ndivyo inavyokuwa, au siyo?
Endapo hiyo ndiyo njia hasa unayoitaka - Freddie Mercury aliendelea na tamati bandia iliyoongezewa kwenye wimbo wa “Sisi ni Machampioni” na pamoja na mashabiki katika maonesho mubashara alichapuka na kibwagizo “..wa dunia!” Endapo hiyo ndiyo njia hasa unayoitaka - Freddie Mercury aliendelea na tamati bandia iliyoongezewa kwenye wimbo wa “Sisi ni Machampioni” na pamoja na mashabiki katika maonesho mubashara alichapuka na kibwagizo “..wa dunia!” | Picha (maelezo): © picture alliance/Photoshot Hapana, hivyo sivyo njia inavyopaswa kuwa. Maneno “… wa dunia!” zaidi yakififia kwenye ombwe, kwa sababu kwenye toleo la asili wimbo huo humalizika tu kwa maneno “sisi ni machampioni” na hakuna maneno mengine zaidi. Hata hivyo, mwimbaji Freddie Mercury anaonekana kuwajali mashabiki wake pale ambapo alifanya maonesho ya wimbo huo katika matukio mubashara kwa kuimba sambamba pamoja na mashabiki na kuongeza maneno kidogo mwishoni ili kwamba mashabiki kamwe wasibaki peke yao wakati kuimba sehemu ya mwisho ya wimbo. Kwenye kipindi cha tano cha mfululizo wa tamthiliya ya ya Star Wars, Darth Vader hasemi, “Luke, mimi ni baba yako,” kama wengi wanavyodhani. Pale ambapo kijana Skywalker anaposema kwamba Darth Vader alimuua baba yake, Vader anajibu, “Hapana, Mimi ni baba yako.”
“Luke, mimi ni baba yako.” Err, hapana - mashabiki kindakindaki wa Star Wars waliishia wao wenyewe kudanganyika. Darth Vader alimjibu Luke: “Hapana, Mimi ni baba yako.” “Luke, mimi ni baba yako.” Err, hapana - mashabiki kindakindaki wa Star Wars waliishia wao wenyewe kudanganyika. Darth Vader alimjibu Luke: “Hapana, Mimi ni baba yako.” | Picha (maelezo): © picture-alliance/Mary Evans Picture Library Mfano mwingine wa kukumbuka kidanganyifu uzushi wa kifo cha Mandela ni kifo cha mwigizaji David Soul, anayejulikana pia kama Hutch aliyeigiza mfululizo wa filamu za uhalifu unaojulikana kama Starsky & Hutch. David Soul bado ni mcheshi mwenye siha njema. Ukweli ni kwamba, sasa ana umri wa miaka 77, lakini mara ya mwisho kusimama mbele ya kamera ilikuwa ni mwaka 2013.

Au pia mfano mwingine maarufu – kuna majimbo mangapi nchini Marekani?

A. 50                B. 51                C. 52

Unaweza kuapa ukidai kuwa kuna majimbo 52? Hata hivyo jibu sahihi ni A. Nchi ya Marekani inaundwa na majimbo 50, majimbo ya Hawaii na Alaska yalijiunga baadaye sana, na kuongeza idadi kutoka majimbo 48 yalikuwepo hapo kabla. Kuna dhana potofu iliyoenea sana unayopaswa kuikumbuka katika duru ijayo ya chemsha pamoja na wenzako. Yamkini kasoro inatokana na watu wengi kuamini kwamba Puerto Rico na Washington, DC  ni majimbo ya Marekani (Puerto Rico ni himaya tu ya Marekani, Washington, DC ni  wilaya tu), au ni kutokana na watu kutazama sana Star Trek (katika mfululizo wa tamthiliya ya The Royale ambapo bendera ya Marekani ilipepea ikionekana kuwa na nyota 52) – hatuwezi kujua kwa hakika.

Muungwana mwenye miwani ya Jicho Moja

Mchezo wa Chemsha Bongo wenye asili yake nchini Kanada. Mchezo mzuri wa kuwavutia watu kupitia maarifa yako, hasa pale ambapo unapocheza na familia ya mwenzi wako – hata kama utawanyima raha kidogo washiriki wake wote. Kwa nini usitengeneze pesa kidogo na kumchota akili mama mkwe mtarajiwa katika mchezo wa Monopoly – unanunua nyumba tatu huko Mayfair, unangoja kwa muda kidogo ukiwa na Mjomba Pennybags Tajiri (mwanaume mleta bahati katika mchezo wa Monopoly mwenye miwani ya jicho moja), na kisha ukavuna pesa nyingi kutoka kwenye biashara yenye faida kubwa. Pengine ni kwa sababu ya jina lala mchezo huo ambalo kwa Kiswahili linamaanisha Ukiritimba ndiyo kitu kinachokufanya moja kwa moja unamfikiria mwanaume muungwa aliyevalia barabara akiwa na miwani ya jicho moja – lakini hii miwani ya jicho moja kwa kweli hiapo. Vichepuko fulani ndani ya vichwa vyetu huongezea miwani ya jicho moja kwenye jicho la mwanaume mleta bahati wa Monopoly. Kwa kuongezea juu ya hapo, ukiachilia koti lenye mkia, fimbo ya kutembelea na mustachi wake maridadi, hana sifa nyingine au vigezo vyovyote vya kuwa mleta bahati. Katika baadhi ya michoro, hana hata fuko lililojaa pesa – lakini sote tunaujua mchezo wa Monopoly, kwa bahati mbaya utajiri huwa ni kwa muda tu.
Hakina, mwanaume wa Monopoly huvaa miwani ya jicho moja. Au pengine sivyo? Hakina, mwanaume wa Monopoly huvaa miwani ya jicho moja. Au pengine sivyo? | Picha (maelezo): © picture alliance/The Advertising Archives Pia kuna mfano mzuri sana kwa vijana wa kileo – ambao hawapendi kutazama nyuma katika zama za zamani za Pokémon. Fikiria jinsi tulivyotumia fedha nyingi sana kununulia kadi za mchezo, wanasesere wanyama wenye manyoya laini, michezo ya video. Kitu cha muhimu kuliko yote kilikuwa ni kuwepo kwa Pikachu juu ya kila kitu! Hata hivyo ni upi hasa ulikuwa mwonekano wa Pikachu? Mashavu mekundu, mkia wenye manyoya yanayochomachoma na mistari myeusi kwenye kishungi cha  mkia huo? Hapana, kwa bahati mbaya hakuwa na mistari myeusi kwenye mkia wake – Pikachu alikuwa tu na vishungi vyeusi kwenye masikio yake. Hata hivyo watu wengi wanamwona akiwa na kishungi cheusi kwenye mkia wake.

Vishungi vyeusi kwenye masikio yake, lakini mkia wa njano - Pikachu naye pia mara nyingi hukumbukwa kidanganyifu. Vishungi vyeusi kwenye masikio yake, lakini mkia wa njano - Pikachu naye pia mara nyingi hukumbukwa kidanganyifu. | Picha (maelezo): © picture alliance/United Archives/IFTN Ubongo siyo sawa na kifaa cha Kompyuta chenye kazi ya kutunza kumbukumbu

Kuna mifano mingi sana mithili ya Kilichotokea kwa Mandela duniani kote. Ni mahali gani hasa inapotoka na namna gani inavyotokea havijafanyiwa utafiti wa kutosha. Kwa kiasi kikubwa mwelekeo wa kuielezea dhana hii umejikita katika njama -zinazotokana na nadharia bandia zinazoongelea dunia mbili tofauti.

Kigezo, hata hivyo ni kwamba, ni rahisi kuurubuni ubongo wa mwanadamu. Vichwa vyetu havifanyi kazi kama kifaa cha kompyuta chenye kazi ya kutunza kumbukumbu – hatuwezi kila mara kupata  kumbukumbu tunazohitaji, achilia mbali kukumbuka kila kitu. Ukweli na vigezo vinavyoaminika kuwa vya kweli hufifia kirahisi sana. Na jinsi ilivyo ni rahisi kupandikiza kumbukumbu potofu kichwani kwako kwa kuuliza maswali ili upate majibu unayoyataka au kupindisha hadithi. Hata hivyo jinsi ambavyo mamilioni ya watu hufikia kwenye dhana potofu inayofanana, nalo ni swali jingine