Njama za uwongo
“Zitaondoa tabasamu usoni mwako”

Hofu ya kupoteza udhibiti hufanya watu wana uelekeo mkubwa zaidi wa hatari ya kukumbwa na athari za dhana za njama. Jambo hili linatokea wakati wa janga la korona: washiriki katika yaliyoitwa maandamano ya usafi mjini Berlin wakionesha upinzani dhidi ya hatua za serikali za kukabiliana na janga.
Hofu ya kupoteza udhibiti hufanya watu wana uelekeo mkubwa zaidi wa hatari ya kukumbwa na athari za dhana za njama. Jambo hili linatokea wakati wa janga la korona: washiriki katika yaliyoitwa maandamano ya usafi mjini Berlin wakionesha upinzani dhidi ya hatua za serikali za kukabiliana na janga. | Picha (maelezo): © picture alliance/Marc Vorwerk/SULUPRESS.DE

Watu wana uelekeo mkubwa zaidi wa hatari ya kukumbwa na athari za  dhana za njama pale wanapohofia kupotea kwa udhibiti wa hali, na kufanya janga la korona kuwa kimbunga halisi. Katika mahojiano,  mwanasayansi ya kisiasa na mwanaharakati wa masuala ya intaneti Katharina Nocun anaeleza jinsi gani tunapaswa kufanya pale tunapokutana na watu wanaochangamkia nadharia za njama.

Bi. Nocun, wewe na mwandishi mwenzako Pia Lamberty mlichapisha kitabu kwa jina la “Vigezo vya Uwongo. Jinsi Nadharia za Njama Zinavyoathiri Kufikiri Kwetu” mwezi Aprili 2020. Lakini badala ya nadharia za njama, mmeziita “njama za uwongo” au “fikira”. Kwa nini?
 

Nadharia ni dhana ya kisayansi. Tunakisia kwamba watetezi hawatakawia kuiondoa au kuizingatia upya nadharia pale inapothibitika kuwa haipo sahihi. Hata hivyo, hiki siyo kitu ambacho waunga mkono wa nadharia za njama wanachofanya. Njama ya uwongo ni simulizi la makubaliano ya siri baina ya mtu mmoja mmoja au makundi linalochukuliwa kuwa na nguvu. Wanaodaiwa kuwa wala njama wamejaliwa vipaji na uwezo fulani.  Hata hivyo, masimulizi mithili ya hayo  yanaweza pia kuyalenga makundi ya kijamii yenye mahitaji maalumu na yanayobaguliwa, kama vile simulizi la Balaa Jeusi la mauaji ya kikatili ya halaiki ya Wasemiti katika Zama za Kati. Sifa nyingine ya msingi ni kwamba wala njama wanashutumiwa kwa kuwa na dhamira ovu na kutafuta kuwadhuru wengine kwa kudhamiria.

Katharina Maria Nocun ni mwanaharakati wa masuala ya intaneti na mwandishi wa habari pendwa. Anaandika katika blogu kupitia kattascha.de na hutengeneza vipindi vya sauti "Denkangebot". Kitabu chake cha kwanza  "Die Daten, die ich rief" (Data ambazo Nilizoziita) kilichapishwamwaka 2018. Kitabu chake " Fake Facts. Wie Verschwörungstheorien unser Denken bestimmen“ (Vigezo vya Uwongo. Jinsi Nadharia za Njama Zinavyoathiri Kufikiri Kwetu) kilichapishwa na Quadriga mwaka 2020. Katharina Maria Nocun ni mwanaharakati wa masuala ya intaneti na mwandishi wa habari pendwa. Anaandika katika blogu kupitia kattascha.de na hutengeneza vipindi vya sauti "Denkangebot". Kitabu chake cha kwanza "Die Daten, die ich rief" (Data ambazo Nilizoziita) kilichapishwamwaka 2018. Kitabu chake " Fake Facts. Wie Verschwörungstheorien unser Denken bestimmen“ (Vigezo vya Uwongo. Jinsi Nadharia za Njama Zinavyoathiri Kufikiri Kwetu) kilichapishwa na Quadriga mwaka 2020. | Picha: © Miriam Juschkat Kwa hiyo tunawezaje kujua kwamba  kwa kweli siyonjama?
 
Kuna njama halisi, bila shaka. Katika demokrasia, ni muhimu kufuatilia kwa karibu shughuli ambazo idara za usalama na serikali zinafanya, kinachotokea katika siasa na uchumi. Kigezo cha kufikia maamuzi ni ama ninaweza kuthibitisha madai yangu kwa ukweli na vidokezo sahihi, au endapo ninaogelea tu katika dhana fungwa ya mitazamo, maadili, masimulizi na matarajio kutoka katika dunia iliyotuzunguka. Kuna tofauti kati ya kujadili nadharia tete na kuwa mfuasi wa imani ya mtu mwingine.  
 
Ni wakati gani hasa watu wanakuwa na uwezekano mkubwa wa kuamini katika njama?
 
Watu wanapohisi kama udhibiti wa hali ni unateleza kutoka kwao – pale wanapopoteza ajira, kwa mfano, wakati wa mageuzi makubwa ya kisiasa au janga linapoikumba dunia – wana kawaida ya kuamini njama za uwongo. Hivi ndivyo tafiti zimeonesha. Hapo njama ya uwongo inaweza kutumika kama aina ya kuziba pengo. Siyo lazima kumpa mwenye kuamini mitazamo au matarajio chanya, bali huwapatia hisia kwamba kuna muundo, mpango, na wahusika dhahiri wenye hatia wa kuwanyooshea kidole.  
 
Ni yapi baadhi ya masimulizi yaliyozoeleka?
 
Kuna njama za uwongo nyingi sana zinazozunguka katika fani ya utabibu kwa mfano. Watu wanaodai kwamba chanjo ni hatari mara kwa mara wananukuu dhana za njama kama uthibitisho. Baadhi ya masimulizi haya yanasema kwamba kuna njama ya mamilioni ya madaktari kutoka duniani kote walioungana kwa dhamira ya kuidhuru dunia. kuhusuHili siyo suala la vigezo vinavyoaminika kuwa kweli; halina uhusiano wowote na uhalisia. Hata hivyo, husababisha baadhi ya watu kutowaamini madaktari, hivyo badala yake wanaweza kuishia kwa watenda miujiza hata pale wanapokuwa mahtuti. Mitazamo kama hiyo inayopingana na sayansi inaweza kusababisha kifo.
 
Je, intaneti inachochea mienendo kama hiyo?
 
Kuna dhana potofu iliyozoeleka kwamba intaneti ndiyo kitu cha kwanza kuzipa shime njama za uwongo. Hata hivyo, wakati wa utawala wa Nazi, walio wengi miongoni mwa watu waliamini uongo uliotokana nanjama ya kimataifa dhidi ya Wayahudi, na vivyo hivyo katika masimulizi dhahiri ya  njama dhidi wa Wasemiti. Huu ulikuwa ndio msimamo wa  serikali na ilifundishwa hivyo mashuleni. Kulikuwa hakuna intaneti nyakati hizo. Japo ni ukweli kwamba njia mpya za habari na mawasiliano zimefanya jambo kuonekana zaidi na bila shaka ni rahisi zaidi kutengeneza na kusambaza kwa haraka masimulizi hayo kidijitali.
 
Ni kwa vipi aina hii ya mtazamo wa kidunia imekuwa halisi sana kwa watu?
 
Watu wanaochangamkia njama za uwongo wanaichukulia dunia kwa aina fulani tofauti. Wengi miongoni mwetu tuna ubaguzi linapokuja suala la mtaalamu: tuna kawaida ya kuamini watu tunaodhani ni wataalamu zaidi kuliko tunavyoamini wengine. Tafiti zimeonesha kwamba waumini wa njama za uwongo wana ‘ubaguzi’ wa chini linapokuja suala la mtaalamu, na katika mifano mingi wanawamini hata jirani zaidi kama ambavyo wangemwamini mtaalamu anayetambulika kimataifa.
 
Tunapaswa kufanya nini na dhana za njama kwenye intaneti?
 
Ni muhimu kutuma mara moja kauli ya kanusho au masahihisho  kwenye mitandao ya kijamii na katika vikundi vya majadiliano. Tunatakiwa kuwa ma msimamo dhahiri dhidi ya kauli za ubaguzi wa rangi na dhidi wa Wasemiti na kusema “imetosha!” Jambo hili kwa kweli ni  muhimu, kwa sababu njama za uwongo nazo pia hutumika kuchochea chuki dhidi ya watu, jambo linaloweza kuwa na matokeo mabaya sana. Mara nyingi ukimya hutafsiriwa kama kukubaliana.
 
Unamaanisha nini hasa unaposema “matokeo mabaya sana”?
 
Wengi miongoni mwa wauaji wenye mrengo mkali wa kulia – mjini Hanau na Halle na pia katika mji wa Christchurch (New Zealand) – waliamini hadithi za njama na walizitumia kuhalalisha kufanya mauaji. Imeoneshwa kwamba njama za uwongo ni kiini cha kumasisha watu wenye mrengo mkali wa kulia. Tunapaswa kulitazama jambo hili kama tatizo la kimfumo linalotakiwa kupewa uzito wake. Njama huwalenga watu kwa kudhamiria. Sasa tunaona jambo hili kupitia korona. Wanasayansi wanaopokea vitisho vya kifo wana utayari mdogo wa kuongelea jambo hilo hadharani. Kwa kufanya hivyo hawasaidii au kukoleza mdahalo wa kitaalamu, wa pande zote.
 
Tunapaswa kufanya nini endapo marafiki wanaanza ghafla kuonesha imani kama hizo?
 
Vigezo vya ukaguzi wa habari unaweza kusaidia – kunazipo taarifa za kweli nzuri sana kwa vipengele vyote vya korona. Mazungumzo binafsi yanaweza pia kuwa na tija, na kufika mwenyewe, kuuliza, “Unaendeleaje?” Licha ya hayo, tunajua kwamba hisia ya kupoteza udhibiti husababisha baadhi ya watu  kuanza ghafla kuamini jambo ambalo vinginevyo huwa hawana kawaida ya kuliamini.  
 
Kuna uwezekano mkubwa kiasi gani wa kuwafikia watu walioshawishiwa kabisa kwa njama?
 
Ni vigumu kufanya mawasiliano yenye tija na watu ambao tayari wameanguka katika kina kirefu cha hii dunia yenye usambamba wa taarifa na imani katika njama za kisayansi au habari. Vigezo vya ukaguzi wa habari hutoka kwa watu, ambao watu hao wenye kuamini, huamini kuwa ni sehemu ya njama. Katika hatua hii, vituo vya ushauri hupendekeza kujaribu maswali kama: “Umekagua? Kwa nini unadhani kituo hiki cha habari ni kinaaminika kuliko kile?” – na hivyo kuwasukuma kuhoji dhana zao. Kinadharia, kufanya hivi husaidia kuzima au kupooza misimamo mikali. Mara nyingi imani katika njama moja huanzisha imani katika njama nyingine, na katika hatua fulani huu huishia katika mtu kujifungua mtazamo wa kidunia unaoelezewa kama akili inayopambanua kila jambo kiwepesiwepesi.
 
Halafu kuna kipengele cha wendawazimu, ambao huchukulia njama za uongo kama burudani kwao.  
 
Watu wanapenda kuchekelea moshi unaoonekana nyuma ya roketi, unaoemekana kuachilia sumu zenye madhara kwetu, badala ya moshi wa ndege ya kawaida usioonekana. Hata hivyo, siyo furaha kwa mtoto ambaye haruhusiwi kutoka nje mara tu baada ya moshi huo kuonekana angani kwa sababu wazazi wao wanaamini jambo hilo. Wanaishi katika hofu isiyokwisha. Awali, watu daima hufurahia kusikia hadithi za njama zenye mvuto wa juu, lakini huwa siyo hivyo baada ya mazungumzo juu ya usuli na madhara ya habari hizo. Zitaondoa tabasamu usoni mwako ukifikiria kwa makini.
 
Ni mahali gani ambapo watu wanaohitaji ushauri – wa kushughulika na watu au jamaa walioathirika – wanapoweza kupata msaada?
 
Kwa sasa watu wengi sana wamegeukia kwenye vituo vya taarifa vinavyoegemea imani fulani, kwa kuwa makundi ya kiimani husambaza njama za uwongo kuwafanya waumini wao kuwa watiifu na kuendelea kuwakamata kwa hila. Kituo kinachohamahama cha Ushauri dhidi ya Msimamo Mkali wa Mrengo wa Kulia pia hutoa ushauri juu ya masuala haya. Kwa bahati mbaya, kuna vituo vichache sana na vilivyopo vinahitaji kuboreshwa. Tunahitaji pia ufadhili bora kwa vyama vinavyofanyia kazi suala hili.
 
Taasisi za serikali zifanye nini?
 
Mashule yanapaswa kujumuisha kimfumo mada hii katika mitaala. Haitachukua muda vijana watakutana na jambo hii na wanapaswa kujifunza namna ya kutambua masimulizi ya njama na namna ya kushughulika nayo. Elimu ya saikolojia ni muhimu pia: endapo unajua kwamba unakabiliwa na hatari ya kukumbwa na athari za hali hii au ile, inaweza kuimarisha uelewa binafsi juu yako mwenyewe hivyo unaamua kungoja usiku upite kabla ya kuchangia mawazo yako kwenye majadiliano mtandaoni. Binafsi, ningependa kuona mpango mkuu na mkakati kutoka serikalini – na fedha zaidi za utafiti