Tunasikika

Tunasikika © Goethe-Institut Tanzania

Tunasikika - Mubashara

Jukwaa jipya limeanzishwa kwa ajili ya wasanii chipukizi kufanya uwasilishaji wa muziki unaorushwa mubashara kwa njia ya mtandao.
Kwa kushirikiana na Action Music Academy kutoka Mbezi Beach Dar es Salaam, Goethe-Institut hushirikiana na wanamuziki kufikisha muziki kwa wigo mpana wa hadhira inayofikiwa kwa njia ya mtandao nchini Tanzania na nje ya mipaka yake, kila baada ya kupita Jumapili moja.
Uwasilishaji wa maudhui ya Tunasikika unatumia mfupi na papo hapo unatakiwa kujitosheleza ili kutoa changamoto kwa wasanii kufanya kilicho bora zaidi katika kile wanachoweza kutoa kwa hadhira kosoaji inayotumia intaneti na mitandao ya kijamii.
Kupitia ushirika na  Action Music Academy wasanii wanaoibuka hupokea pia mafunzo ya kitaalamu katika masomo ya sauti, piano, gitaa, gitaa la besi, ngoma, tumba, fidla, tarumbeta na uinjinia wa sauti.

Orodha ya tamasha za Tunasikika zilizopita

 • 01 Leah Ndahani na Tofa Boy - 31.05.2020
 • 02 Ng'wana Shija na Mima - Malkia wa Singeli - 28.06.2020
 • 03 Anna Kattoa na Wamwiduka Band - 12.07.2020
 • 04 Misoji Nkwabi na Hussein Masimbi - 02.08.2020
 • 05 Hokororo, na Steve DC - 27.09.2020
 • 06 Chikaya D, na Mubba - 11.10.2020
 • 07 The Ngoshaz na Ze Spirit - 08.11.2020
 • 08 Man Kifimbo na Grace Kalima - 22.11.2020
 • 09 Bahati Band - 13.12.2020
 • 10 Witiri na Soul Medication - 18.04.2021
 • 11 Harry GB na Mopao - 28.05.2021
 • 12 Upendo Manase na Vita Malulu - 22.10.2021

[Bonyeza kwenye ikoni ya Playlist Icon kutazama orodha ya kucheza]