Mafunzo ya Kijerumani bila taabu
App ya kujifunza msamiati

Jifunze Kijerumani bila taabu kwa kutumia app ya kifundishi cha msamiati kutoka Goethe-Institut . Kifundishi cha msamiati cha Goethe-Institut hukusaidia kufanya mazoezi na kuboresha Kijerumani chako kwa kuongeza maneno mapya kwenye msamiati wako bila taabu

Pakua orodha za msamiati kwa ngazi tofauti za ustadi kutoka Goethe-Institut, jifunze maneno yako mwenyewe kwa kutumia the mfumo wa kadi za faharasa au tumia kadi za maneno kutoka jukwaa la mafunzo la kozi ya Kijerumani.

Mfumo wa mafunzo

Bofya “New Content” na “Find Topic” kupakua orodha za maneno zinazotolewa  na Goethe-Institut bila malipo. Ni sharti kifundishi cha msamiati  kiwe kimeunganishwa kwenye intaneti ili kiweze kutumika. Unaweza pia kutumia kifundishi kuingia na kujifunza maneno ya chaguo lako mwenyewe.

Kifundishi hukuwezesha kujifunza msamiati mpya kupitia mfumo wa kadi za faharasa wenye “visanduku” vitano. Msingi wa mfumo huu ni kwamba neno jipya litang'ang'ania kwenye kumbukumbu yako ya muda mrefu baada ya kulimaki kama “known” mara tano.

Kuunganisha kifundishi cha msamiati na jukwaa la mafunzo

Kupata mwunganisho na kozi zako kwenye jukwaa la mafunzo, ingia kwenye kifundishi na jukwaa la mafunzo kwa kubofya “User Login” na kuingiza your “My Goethe” jina tumizi and nywila.
Juu