Upatikanaji wa haraka :

Nenda moja kwa moja kwenye maudhui (Alt 1) Nenda moja kwa moja kwenye ngazi ya pili ya urambazaji (Alt 3)Nenda moja kwa moja kwenye ngazi ya kwanza ya urambazaji (Alt 2)
AFROYOUNGADULT LogoGoethe-Institut Johannesburg

Call for submissions
AFROYOUNGADULT

Chuo cha Goethe inawakilisha #AFROYOUNGADULT: Mashindano ya kutafuta Kijana Mwandishi kutoka Africa

AFROYOUNGADULT

Chuo cha Goethe inawakilisha #AFROYOUNGADULT: Mashindano ya kutafuta Kijana Mwandishi kutoka Africa

Kituo cha Utamaduni cha Ujerumani (Goethe-Institut) inakaribisha wanaopenda kuwa waandishi wenye umri wowote wa kuandika hadithi kwa vijana (13 - 19 years) kutuma hadithi zao zenye maneno 3000 hadi 5000 kwa lugha za Kiswahili, Kiingereza au Kifaransa.

Jopo la majaji watachagua hadithi nzuri na kuwaalika waandishi wa hadithi hizo kuhudhuria mafunzo yatakayo fanyika mwezi Februrari 2019 sehemu mbalimbali barani Afrika.

Hadithi zitakazo shinda wakati wa mafunzo haya zitachapishwa kwenye jarida. Jarida hiyo itapatikana kwa lugha za Kiswahili, Kiingereza na Kifaransa na kutambulishwa kwenye Tamasha ya Ake 2019 Lagos, Nigeria.


UPDATE 1 march 2019

Goethe-Institut Sub Sahara Afrika  ina furaha kutangaza hadithi fupi za Vijana zilizochaguliwa pamoja na waandishi wake, ambazo ni matokeo ya warsha zilizofanyika katika miji minane ya Afrika mwezi wa Februari. Hadithi zilichaguliwa na jopo la majaji lililojumuisha waandishi, wanaharakati wa usomaji na muhimu kabisa, wasomaji Vijana kutoka barani kote.
Zukiswa Wanner, mratibu wa mradi huu alikuwa na haya ya kusema juu ya mchakato huo, “Tulipopata wazo na kuitisha miswada, tulitegemea labda tungeweza kupata hadithi nzuri 10 au 12 kwa ajili ya kitabu cha mkusanyo wa hadithi hizo zinazolenga wasomaji wenye umri kati ya miaka 13-19 ambalo ni rika lisilotiliwa maanani sana katika fasihi yetu. Kwa msaada wa wasomaji Vijana waliokuwa sehemu ya uamuzi, tumeweza kupata hadithi fupi 17 za Vijana, ongezeko kubwa zaidi ya matarajio yetu. Hadithi hizi kutoka bara kongwe duniani lililosheheni vijana zinajumuisha visa tofauti toka vile vya vile vinavyoonesha jinsi Afrika nyingine ilivyo, kama kumwona kijana akiwa katikati ya vita na mafumbo juu kifo hadi kwenye maswali ya nafsi juu ya familia, urafiki na uhusiano wa kimapenzi. Pamoja na utofauti mpana wa dhamira zake, kitu kimoja kinachofanana juu ya hadithi hizi ni kutumia kwake sauti ya kijana inayofahamika kwao au kwa yeyote aliyewahi kuwa kijana. Ni sauti shupavu kwa wakati fulani, zenye mashaka wakati mwingine, lakini zenye kuutambua ulimwengu unaozizunguka.”
 
Hongera kwa washindi 17:
Asiedu Benneh – Summer School
Chinelo Enemuo – The Hunter
Fatma Shafii – Safarini
Howard Meh-Buh - Oubliette
Justin Clement – Burden
Kelvin Nonvignon Adantchede – Elxa
Kofi Berko – The Sun is White
Lukorito Wafula Jones – Pepo la Zehara
Laurence Gnaro – Naka, La Guerriere Lama
Merdi Mukore – Cornee Noire, Iris Blanc
Precious Colette Kemigisha –Water Birds on The Lake Shore
Priscillar Matara – Last Places
Raoul Djimeli –Premiere fois pour les nulles
Sabah Carrim – Tara’s Hair
Shamin Chibba – The Year of Failure
Tamanda Kanjaye – A Change in Sleeping Arrangements
Yamikani Mlangiza – Forever Hers
 

KWA TOLEO YA SASA HIVI, januari 3 2019

Goethe-Institut yafurahia kutangaza *uteuzi* wa waandishi wa miji nane ya Afrika ya warsha za Vijana kutoka Afrika kutoka 11-15 Februari (isipokuwa ya Lagos ambayo itafanyika 4-8 Februari kwa sababu ya uchaguzi). Kulikuwa na mawasilisho ya nakala 435 kutoka kote bara la Afrika na ughaibuni. Kati ya nakala hizo, wawezeshaji wetu wa warsha walichagua 52 ambao hadithi zao zinaweza kuboreshwa kupitia warsha kwa matayarisho ya uteuzi za hadithi zitakazochapishwa katika kusanyiko la maandishi kwa kitabu chetu ijayo.

Ili kuhakikisha kutokuwa na ubaguzi, majina ya washiriki yaliondolewa kutoka kwa hadithi kabla ya kutumwa kwa wawezeshaji wetu wa warsha. Aidha, tulijaribu tuwezavyo kuzuia wawezeshaji wa warsha kushiriki katika uteuzi wa hadithi katika miji ambayo watawezesha warsha. Kwa mfano, mwezeshaji wa warsha ya Lagos alisoma na kuchagua hadithi za warsha ya Accra ilhali mwezeshaji wa warsha ya Johannesburg Mohale Mashigo alichagua hadithi za warsha ya Nairobi. Huu mtindo ulifuatwa isipokuwa katika warsha ya miji ya Dakar, Lome na Dar es Salaam. Katika miji miwili ya kwanza, mwezeshaji wa warsha ya Lome Edwige Dro na mwezeshaji wa warsha ya Dakar Richard Ali Mutu kwa pamoja walichagua washiriki kumi wa miji hiyo mbili mtawalia. Katika mji wa mwisho, Elias Mutani ambaye ni mwezeshaji wa warsha ya Dar es Salaam alichagua washiriki wote wa Swahili. Kutobagua kwake na kujitahidi kuchagua hadithi bora zaidi `yaonekana vizuri katika uchaguzi wake ya washiriki zaidi kutoka Kenya kuliko nchi yake asili, Tanzania.

“Inaridhisha kuwa Goethe-Institut inaongoza katika kuhakikisha hadithi za kubuniwa ya Vijana inapatikana barani kupitia mradi huu. Pia inafurahisha zaidi kuona shauku ya waandishi wengi katika bara, na nakala iliyowasilishwa ya mtu mwenye umri mdogo ikiwa ya mwanafunzi wa miaka 13 kutoka Kenya. Kupitia mradi huu ya Vijana kutoka Afrika, tunatarajia sio tu kusanyiko la maandishi kwa kitabu ambacho Vijana kote Afrika watahusiana nayo na kufurahia, bali pia iwezeshe watu zaidi waandike katika mtindo huu wa hadithi ili tuweze kuwa na hadithi ya kubuniwa tofauti ya Vijana kwa hadithi fupi na ndefu kwa vile tunafanya hadithi fupi na riwaya ya watu wazima,” mtunza Zukiswa Wanner alisema.
 

WASHIRIKI WALIOCHAGULIWA KWA WARSHA, MADA ZA HADITHI NA WAWEZESHAJI WA WARSHA

 
DAR ES SALAAM warsha ikiwezeshwa na Elias Mutani
Adui Yangu - Amos Nandasaba (Kenya)
Arudi Shuleni - Jackline Kasanga (Tanzania)
Fadhaa ya Marejeo - Mungai Mutonya (Kenya)
Hukumu - Wafula Wakoko (Kenya)
Mtaka cha Mvunguni -Karangae Chaga
Pepo La Zehara - Jones Lukorito (Kenya)
Safarini - Fatma Mohamed (Kenya)
 
DAKAR warsha ikiwezeshwa na Richard Ali Mutu
Dangereuse Escapade – Jocelyn Tchetche Tendop (Kamerun)
Deux Femmes, Trois ages – Nina Wade (Senegal)
Cornee Noir, Iris Blanc - Merdi Muintshe Mukore (Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo)
Le Vide L’Histoire – Jocelyn Danga (Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo)
Viatique d’une Sokhna – Elhadji Amadou Ngom Dieye (Senegal)
 
LOME warsha ikiwezeshwa na Renee Edwige-Dro
La Dame en Toyota – Sadlay Hounyeme (Benin)
Abih Selassie – Simon Cardin Neyeng (Kamerun)
Le Prix d’un Plat de Riz – Kelvin Adantchede (Benin)
Le Labyrinthe des Complexes- Manuella Mayugo (Kamerun)
La Maison des Noces – Raoul Djimeli (Kamerun)

ACCRA warsha ikiwezeshwa na Mamle Wolo
Blood and Fire - Kwesi Woode (Ghana)
The Sun is White - Kofi Benko (Ghana)
A Memory of a Lesser God (Ghana)
The Beauty Ceremony - Akwasi Addai (Ghana)
Living from October the Third - Emmanuel Lindsay (Ghana)
Summer School - Asiedu Benneh
 
JOHANNESBURG warsha ikiwezeshwa na Mohale Mashigo
The Healer and the Extra - Maria Chichava (Msumbiji)
Daddy Loves Us - Peter Nawa (Zambia)
The Year of the Failure - Shamin Chibba (Afrika Kusini)
Tara's Hair - Sabah Carrim (Morisi)
The Last Places - Priscillar Matara (Botswana)
Coronation - Catherine Jarvis (Afrika Kusini)
Her World - Fiske Serah Nyirongo (Zambia)
 
KIGALI warsha ikiwezeshawa na Zukiswa Wanner
Cry, Oh My Soul - Alain Jules Hirwa (Rwanda)
Within the Shadows - Precious Collette Kemigisha (Rwanda)
Homecoming - Daniel Nuwamanya (Uganda)
Going to Sancturary - Paul Kisakye (Uganda)
A Change in Sleeping Arrangements - Tamanda Kanjaye (Malawi)
A Love of Her Dream - Yamikani Mlangiza (Malawi)
 
LAGOS warsha ikiwezeshwa na William Moore
The Hunter - Chinelo Enemuo (Nigeria)
Oubliette - Howard Meh-Buh (Kamerun)
The Witches' Camp - Chioma Iwunze-Ibiam (Nigeria)
The Red Dream - Musih T. Xaviere (Kamerun)
This is Not for Allah to Decide - Okechi Okeke (Nigeria)
Ebiye - Justin Clement (Nigeria)
Girl of My Dreams - Olakitan Aladesuyi (Nigeria)
Of Little, Beautiful Broken Things - Ernest Ogunyemi (Nigeria)
 
NAIROBI warsha ikiwezeshawa na Kinyanjui Kombani
 To Seek Gold Dust - Dennis Mugaa (Kenya)
Savannahs & The Sun - Selam Teslam (Kenya)
The Jinni Girl - Mango Joyce Nawiri (Kenya)
Moving to Kakamega - Gloria Mwaniga (Kenya)
Twist of Fate - Valerie Tonya Kidarisi (Kenya)
The Girl with Black and White Hair - Caroline Biegon (Kenya)
Only Good Christian Girls Live Here - Ruth Kenyah (Kenya)
 
Kuuliza maswali, tuma barua pepe kwa  afroyoungadult@gmail.com 

Tarehe muhimu:

Kutuma hadithi: Septemba 1 hadi Novemba 20 2018

Kutangaza waliochaguliwa kuhudhuria mafunzo: Januari 3 2019

Mafunzo: Februari 11-15 2019 (Kumbuka: Watakao tuma Hadithi zao ni kwa wale ambao wataweza kusafiri kwenda kwenye vituo vya mafunzo kama ilivyo onyeshwa kwenye orodha za miji zitakazo fanyika mafunzo)

Vituo vya mafunzo:

Kwa Kiswahili - Dar es Salaam, Tanzania

Kwa Kifaransa - Lome, Togo na Dakar Senegal

Kwa Kiingereza - Accra, Ghana; Kigali, Rwanda; Lagos, Nigeria; Nairobi, Kenya; Johannesburg, Afrika Kusini


AYA authors on other platforms

Stomaching soiled adult diapers © Shamin Chibba

Shaming Chibba: Stomaching soiled adult diapers

Shamin Chibba speaks about the desolate state of elder care in South Africa.

Changing the ‘African’ Attitude to Pets During the COVID-19 Lockdown © Precious Colette Kemigisha

Precious Colette Kemigisha: Changing the ‘African’ Attitude to Pets During the COVID-19 Lockdown

Precious Colette Kemigisha writes about the relationship between pets and families during lockdown in Africa

Juu