Gebäude Jobcenter © Goethe-Institut

Kwa wahamiaji wenye viza

Kibali cha kufanya kazi

Je umetokea nje ya Umoja wa Ulaya (EU) au ukanda wa kiuchumi wa Ulaya ? Hivyo, unahitaji kibali cha kufanya kazi Ujerumani. Mataifa ya nchi za EU Romania na Bulgaria wanahitaji kibali cha kufanya kazi mpaka mwisho wa mwaka 2018, lakini sio baada ya muda huo.

Endapo umeruhusiwa kufanya kazi Ujerumani na kwa muda gani, inaonyeshwa kwenye kibali chako cha makazi.

Vyeti na Utambuzi

Je una sifa za kiufundi, shahada ya Chuo Kikuu au cheti cha shule kutoka katika nchi yako? Unatakiwa kuwa na hivi vyeti/nyaraka ambazo zimetafsiriwa na kuthibitishwa.Uthibitisho unamaanisha kuwa mamlaka rasmi imehakiki nyaraka zako na kuona kuwa ni za kweli. Mahali pazuri pakufanikishiwa jambo hili ni katika malamka iliyopo katika nchi yako. Muda mwingine sifa zako zinaweza kuwa si halali Ujerumani. Unaweza kuangalia hili jambo wakati ukiwa nchini mwako (Utambuzi wa sifa za kigeni). Unaweza kupata taarifa zaidi kupitia tovuti ya Recognition in Germany. Pia ,tazama infografiki zetu hapa.

Ein Mann bedient die Anerkennung in Deutschland Webseite auf einem Tablet © Goethe-Institut

Nafasi za kazi

Umeshapata kibali cha kufanya kazi? Hivyo, unaweza kutafuta kazi.Kuna mianya mingi sana: unaweza kutafuta kazi zinazotangazwa mitandaoni, kwenye magazeti au kwa wakala wa ajira/kitengo cha ajira. Kwa kawaida, utaona kazi za kawaida kwenye magazeti. Lakini matangazo yanaenda kwa wakati. Kuna kazi nyingi zinazotangazwa kwenye mitandao, lakini mara nyingi haziendi kiwakati. Kitengo cha ajira kitakushauri na kukutafutia kazi stahili kwa ajili yako. Lakini unaweza kwenda moja kwa moja kwenye makampuni. Muda mwingine wanakuwa na nafasi za ajira, lakini hazipo kwenye mtandao au kwenye magazeti. Muda mwingine unaweza kutafuta nafasi za ajira kwenye tovuti ya kampuni.

Pia, kuna BIZ (Kitengo cha ushauri wa kazi) katika wakala wa ajira: utaangalia matangazo ya ajira hapo pamoja na taarifa kedekede juu ya dhana za ajira na kazi.Unaweza kutuma maelezo yako mafupi hapo kwenye mtandao, hata pia katika kitengo cha ajira. Kitengo cha BIZ kinatoa huduma za ushauri wa ajira kama endapo haufahamu nini unachoweza au kutaka kufanya.

Mtawanyo wa kazi katika kampuni ni mzuri: unapata kujua kazi na unaweka mawasiliano.

Ein Mann liest Zeitung und sucht nach Stellenangeboten. © Goethe-Institut

Maombi

Maombi yako ni hatua ya kwanza katika soko la ajira. Nyaraka za maombi ni za umuhimu sana. Unatakiwa uwe na barua ya ushawishi (barau kwa kampuni), picha nzuri ya maombi, wasifu binafsi na vyeti vyako (katika kijerumani). Kitengo cha BIZ kinatoa warsha za “kuomba kazi Ujerumani’’. Unajifunza namna maombi ya kazi yanavyokuwa na namna gani ya kujiandaa kwa ajili ya mahojiano ya ajira.

Miji mingi ina huduma za ushari kwa wahamiaji. Hapa, watakusaidia kutafuta ajira na kuandika maombi ya kazi (tazama Bundesamt für Migration Bundesamt für Migration und Flüchtlinge). Ushauri maalum unapatika kwa vijana wenye umri chini ya miaka 27 kutoka kwa huduma za uhamiaji kwa vijana.

Eine Frau steht vor einem Passfotoautomaten. © Goethe-Institut

Kwa waombaji wa hifadhi

Kufanya kazi

Wakati wa miezi yao mitatu nchini ujerumani, wakimbizi hawaruhusiwi kufanya kazi. Hili linaanza katika kipindi cha udahili katika kituo cha mwanzo cha mapokezi. Baada ya miezi mitatu tu unaruhusiwa kuomba ajira. Hata hivyo, si ka kila mkimbizi aliyeomba hifadhi anaruhusiwa kufanya kazi.Wakimbizi kutoka katika nchi zenye asili ya usalama hawaruhusiwi kufanya kazi mpaka maombi yao ya hifadhi yaamuliwe.

Ungependelea kufanya kazi Ujerumani baada ya hii miezi mitatu ya mwanzo? Kwa mantiki hii, utatakiwa upate kibali kutoka Ofisi ya Udahili wa Wageni. Mwanzoni, hautakuwa na machaguzi mengi wakati wa kufanya uchaguzi wa ajira. Hata hivyo, hili linaenda kubadili urefu wa muda uliokuwepo Ujerumani.

Mara unapopewa rasmi hadhi ya ukimbizi nchini Ujerumani, unaruhusiwa kufanya kazi bila ya kizuizi chochote. Je wewe ni mwombaji mvumulivu wa hifadhi mwenye makazi ya muda mfupi wa kufukuzwa? Kwa hiyo, itakuwa katika busara ya mamlaka kama unaruhusiwa au kutoruhusiwa kufanya kazi.
 

Kutafuta ajira

Je unatafuta ajira? Basi unaweza kwenda kwenye kituo cha ajira. Kituo cha ajira kinawasaidia watu katika kutafuta ajira na wanaweza kukusaidia.

Arbeitsagentur: Jobbörse

Lakini kuna miradi pia inayowasaidia wakimbizi katika utafutaji wao wa kazi. Unaweza kupata mbadilishano kadhaa wa kazi kwenye mtandao ambapo unaweza kusajili taarifa zako.

workeer.de: Jobbörse für Flüchtlinge
jobbörse.de: Jobbörse für Flüchtlinge

Umepata kazi? Kwa mantiki hii, ofisi ya usaili wa wageni wataangalia kwanza kama hakuna mwananchi wa EU yeyote anayepatikana kujaza nafasi hii. Hili linaitwa patio la upendeleo. Kama hakuna mwananchi wa EU anayepatikana kwa kazi maalumu, utapewa kibali cha kazi. Kituo cha ajira wanatakiwa pia kutoa mtazamo wao.

Je una sifa za kiufundi au shahada? Kwa mantiki hii, nyaraka zako zinatakiwa kwanza kupitiwa na kutambuliwa. Kama nyaraka zako zinatambuliwa Ujerumani, itakuwa rahisi kupata kibali cha kazi kwa sababu hakuna pitio la upendeleo litafanyika. Kwa taarifa zaidi juu ya sifa zinazotambulika, tazama makala kwenye Shahada za chuo kikuu na mafunzo ya kiufundi.

Ujerumani kwa sasa ina uhitaji mkubwa wa mafundi wataalamu au wataalamu waliofunzwa kama vile wauguzi. Je umefunzi kwenye moja ya hizi taaluma? Kwa mantiki hii, unaweza kufanya kazi bila ya kuhitaji pitio la upendeleo.
 

Further questions? Write us via the contact form. We will forward your questions anonymously to the advisors of the youth migration services.

Contact form