Telefonieren Foto: © colourbox.de
Kwa wahamiaji wenye viza

Kufanya maawasiliano kwa njia ya simu kwa kutumia simu kadi kutoka ujerumani kwenda nchi nyingine ni ngumu. Kadi nyingi katika nchi ya ujerumani hazifanyi kazi, na kupiga simu kwa kadi za simu za nje ni gharama sana.

Kuna njia tofauti za kupiga simu katika nchi ujerumani. Hii ni orodha yenye taarifa ya watoa huduma tofauti tofauti:

Handytarife.de: Overview of mobile communication providersHandytarife.de: Overview of mobile communication providers

Mkataba wa simu ya mkononi 

Chaguo mojawapo na ambalo linawezekana ni mkataba wa simu. Hata hivyo hii inahitaji akaunti ya benki na taarifa za utambulisho za ujerumani kwa njia hii, watoa huduma wanaangalia kama mteja anaweza kulipa bili zake. Tahadhari: husisaini mkataba ambao hujauelewa. Badala yake, muulize mtu ili akuasidie maana yake au tafsiri yake. Kwa kawaida mkataba wa simu hudumu kwa muda wa miaka miwili. Mara nyingi ni vigumu kuvunja mkataba kabla ya wakati/muda. Malipo ya bili lazima yafanyike kila mwisho wa mwezi katika kipindi cha mkataba. Zingatia! Kama utapenda kubadili mtoa huduma na kwenda kwa mtoa huduma mwingine yakupasa usubiri hadi ule wa kwanza uwe umeisha ndani ya muda sahihi inatakiwa kufanyika miezi mitatu kabla ya mkataba, vinginevyo mkataba unaweza kurudia upya tena kwa mwaka mmoja au miwili.

Kadi ya malipo ya kabla 

Chaguo jingine ni kununua kadi ya malipo ya kabla. Kadi hizi hupatikana kwa gharama nafuu pia hupatikana mara nyingi katika maduka makubwa, vituo vya kuuzia mafuta, au kwenye kioski. Hii pia inahusu kusaini mkataba.Pindi inapoamilishwa unatakiwa  kuthibitisha jina, anwani na tarehe ya kuzaliwa. Ili kufanya hivyo unapaswa kuonyesha pasipoti yako, kadi ya utambulisho au picha rasmi ya ID katika duka. Muda mwingine unahitaji kibali cha makazi.

Je, umeshanunua kadi ya malipo ya kabla kutoka kwenye maduka ya simu moja kwa moja? Ambapo ni rahisi kuhuisha kadi yako kwenye duka. Hapa pia unaweza ukapata msaada. Umeshawahi kununua kadi ya malipo ya kabla ndani, kwa mfano: kwenye maduka makubwa?

Kisha unaweza kithibitisha utambulisho wako kwa njia ya utambuzi wa video katika smartphone yako, komypyuta bapa au kwenye kamera pembuzi katika kompyuta).

Mara kadi itakapohuishwa, unatakiwa kuongeza salio. Salio hutumika katika kupiga simu, kutuma ujumbe na kutafuta mitandao. Kadi kwa mfano: maduka makubwa, vituo vya kuuzia, na kwenye vioski. Kuna mchakato mrefu wa jinsi ya kuongeza salio kwenye kadi. Kuongeza salio, weka namba hizi kwenye simu.

Je, unataka kuwasiliana kimataifa kutoka ujerumani? Katika hili, tegemea kulipa ada ya senti 15, hata kama kwa maongezi ya muda mfupi. Kupiga simu Syria, Eritrea na nchi za Balkani ni gharama sana. Na hii ni orodha ya viwango vya kupiga simu kimataifa kutoka makampuni tofauti tofauti ya mitandao ya simu.

Wakati mwingine inawezekana kununua ushuru fulani wa ziada  ambapo unapokea kiasi fulani cha dakika za bure kwa simu za kimataifa.
 

Taarifa ya simu 

Simu zenye kadi ya malipo ya kabla pia hutumika katika kutafuta mitandao. Hata hivyo hufanya kazi haraka unapoongeza salio. Hivyo ni rahisi kununua kifurushi kinachofaa ajili ya simu. Hii itakusaidia kutumia mtandao wa simu kwa muda Fulani kwa bei ya kudumu au kununua kiasi fulani cha data .

WLAN

Kama unataka kutafuta mtandao Fulani bure, unaweza kutumia mtandao wa WLAN. Sehemu nyingi zinazotoa huduma za mitandao, maktaba, na maeneo yenye majengo ya umma  wanatoa huduma hiyo ya Mtandao wa WLAN bure. Je, ungependa kutumia mtandao wa WLAN bila malipo katika maeneo unayoishi? Tovuti ya “Freie Hotspots” itakusaidia kupata eneo la umma ambalo unaweza kupata huduma hiyo.

Public WLAN networks in GermanyPublic WLAN networks in Germany
Kwa ajili ya waombaji wa hifadhi

Kupiga simu ndani ya ujerumani kwenda nchi nyinginea inaweza kupelekea matatizo. Kadi nyingi za simu zinashindwa kufanya kazi katika nchi ya ujerumani, na kupiga simu inaatumia gharama kubwa.
Kuna njia nyingi za kupiga simu kutoka ujerumani. Hii ni orodha ya taarifa ya watoa huduma tofauti tofauti

Stiftung Warentest: Information on providers

Mkataba wa simu ya mkononi 

Chaguo mojawapo na ambalo linawezekana ni mkataba wa simu.hata hivyo hii inahitaji akaunti ya benki na taarifa za utambulisho za ujerumanikwa njia hii, watoa huduma wanaangalia kama mteja anaweza kulipa bili zake. Tahadhari: husisaini mkataba ambao hujauelewa. Badala yake, muulize mtu ili akuasidie maana au tafsiri yake.

Kadi ya simu ya malipo ya kabla 

Kadi ya simu ya malipo ya kabla ni utatuzi wa matatizo kwa wakimbizi. Hununuliwa kwa bei nafuu katika maduka makubwa, vituo vya kuuzia mafuta na kwenye vioski. Hii pia huitaji kusaini mkataba. Hata hivyo, ili kuweza kuwa na kadi ni inayofanya kazi unahitajika uwe na anuani. Je, bado hujasaliwa ujerumani? Katika miezi mitatu ya mwanzo baada ya kuwasili ujermani, unaweza kutoa maelezo ya mahali ambapo umepokelewa kwa mara ya kwanza. Mara baada ya kubadili makazi, ni muhimu kumjulisha mtoa anuani mpya. Na kama hujatoa taarifa kuhusu anuani yako mpya utatumiwa ujumbe. Kama hutotoa majibu kwa mtoa huduma wako kwa muda wa siku 14, simu kadi yako itafungiwa. Je, umewahi kukaa katika mapokezi ya awali Zaidi ya miezi mitatu? Na mwisho wa muda unaweza kuongezwa.

Je, umewahi kununua kadi ya simu ya malipo ya kabla kutoka kwenye maduka ya watoa huduma ? Halafu na ukaweza kuhuisha kadi yako moja kwa moja kutoka kwenye duka. Hapa pia unaweza kupata msaada. Je, umewahi kununua kadi ya malipo ya kabla ndani, mfano: kwenye maduka makubwa? Na kadi ya simu kuweza kufanya kazi kwenye simu.

Mara kadi ya simu inapofanya kazi, inatakiwa kuongeza salio. Na salio linakuwezesha kupiga simu, kuandika ujumbe, na kutafuta mitandao. Kama utahitaji salio Zaidi unaweza kununua kadi ya kuongeza. Pia kadi za kuongeza salio unaweza kupata katika maduka yanayouza kadi za simu. Kuna namba nyingi katika kadi ya kuongeza salio. Kwa salio unalipia kadi kabla  ingiza namba hizi kwenye simu yako ya mkononi.

Stiftung Warentest: Mobile phone tariffs for refugees

Wakati mwingine inawezekana kununua ushuru fulani wa ziada  ambapo unapokea kiasi fulani cha dakika za bure kwa simu za kimataifa.
 

Taarifa ya simu 

Simu zenye kadi ya malipo ya kabla pia hutumika katika kutafuta mitandao. Hata hivyo hufanya kazi haraka unapoongeza salio. Hivyo ni rahisi kununulia kifurushi kinachofaa kwa ajili ya simu. Hii itakusaidia kutumia mtandao wa simu kwa muda Fulani kwa bei ya kudumu au kununua kiazi fulani cha data.

WLAN

Kama unataka kutafuta mtandao Fulani bure, unaweza kutumia mtandao wa WLAN. Sehemu nyingi zinazotoa huduma za mitandao, maktaba, na maeneo yenye majengo ya umma wanatoa huduma hiyo ya mtandao wa WLAN bure. Je, ungependa kutumia mtandao wa WLAN bila malipo katika maeneo unayoishi? Tovuti ya “Freie Hotspots” itakusaidia kupata eneo la umma ambalo unaweza kupata huduma hiyo.

Public WLAN networks in Germany

Baadhi ya malazi ya wakimbizi pia hutoa WLAN ya bure.