Erste Schritte in Deutschland Foto: © colourbox.de
Kwa wahamiaji wenye viza

Hati ya kusafiria na Viza 

Kwa ajili ya kusafiri kwenda Ujerumani, unahitaji hati ya kusafiria halali na nyaraka nyingine halali ambazo zinathibitisha utambulisho wako.Utahitaji hati ya kusafiria baadae pindi utakapoenda kudahiliwa katika mamlaka.Wakazi wa nchi nje ya Umoja wa Ulaya (EU) wanahitaji pia viza.

Unaweza kuomba viza katika ubalozi wa Ujerumani nchini mwako. Je, umeshapata tayari mkataba wa ajira UJerumani, au una wanafamilia wanaoishi hapo? Basi, itakuwa rahisi kupata viza. Unaweza kupata taarifa kutoka Federal Foreign Office.
Wananchi kutoka EU au nchi yoyote iliyopo katika Ukanda wa Kiuchumi wa Ulaya hawaitaji viza.
 

Ofisi ya Udahili wa Wakazi na Kibali cha makazi 

Ukiwa Ujerumani unatakiwa ujisajili katika Einwohnermeldeamt (Ofisi ya udahili wa wakazi) katika mji au jiji lako la makazi. Baadae, unatakiwa uende kwa Ausländeramt (Ofisi ya uhamiaji). Hapo utapatiwa hati ya makazi. Ni kadi inaonyesha hadhi yako ya makazi. Inaonyesha muda gani unaruhusiwa kubaki Ujerumani na kama unaruhusiwa kufanya kazi.

Je, unahitaji kutembelea ofisi, lakini huwezi kuzungumza kijerumani vizuri? Basi, unaweza kumwomba mkalimani. Ni yule ambaye anaweza kuongea kijerumani na lugha yako na atakusadia kuwasiliana.
.

Kozi shirikishi 

Kama hauwezi kuongea kijerumani vizuri sana, basi unaruhusiwa kufanya kozi shirikishi. Muda mwingine, unatakiwa kufanya kozi shirikishi. Utajifunza kijerumani kizuri katika kozi. Na utapatiwa taarifa muhimu kuhusu maisha ya Ujerumani. Ofisi ya Uhamiaji itakupatia kwa ajili ya kozi na itakwambia wapi utaweza kufanya kozi. Unaweza kuisoma zaidi kwa kufuata kiungo cha kozi shirikishi.
 

Kutafuta ajira na mafunzo ya kiufundi 

Hatua ifuatayo ni kutafuta kazi. Ulishasoma tayari taaluma hiyo nchini mwako, au ulishawahi kuwa chuo kikuu? Basi, unatakiwa kuwa na nyaraka zilizotafsiriwa na kuthibitishwa.Uliza wapi unaweza kuifanya katika wakala wa ajira. Wakala wa ajira watakusaidia kutafuta ajira.Kama bado hauna taaluma au sifa za kuondoka shule, unatakiwa uende pia kwa wakala wa ajira. Watakupatia ushauri wa kazi. Watakusaidia kama hauna uhakika juu ya aina ya kazi ungependelea kufanya au ungeweza kuifanya.Wakala wa ajira watakupatia taarifa kuhusu mafunzo na kozi. Unaweza kupata taarifa zaidi katika ukurasa wa Utafiti wa kitaaluma na  mafunzo ya ufundi.
 

Watoto na Shule 

Watoto kuhudhuria shule. Msajili mtoto wako katika shule. Jugendamt (ofisi ya vijana) katika mji/jiji lako inaweza kukusaidia. Soma zaidi katika kurasa zifuatazo: elimu ya wali na mfumo wa shule.
 

Bima 

Baadhi ya mipango ya bima ni muhimu sana hasa bima ya afya, bima ya pensheni na bima ya huduma (tazama ukurasa wa bima). Kama una kazi, utahakikishiwa moja kwa moja mipango hii (tazama ukurasa wa kuanza kazi). Na unahitaji akaunti ya sasa katika benki (tazama akaunti ya benki na fedha).
 

Kwa waombaji wa hifadhi

Taratibu za hifadhi

Umekuja Ujerumani kudai hifadhi? Hii taarifa ni muhimu kwa maombi yako ya hifadhi.

Kwanza, udahiliwe katika kitengo cha mwanzo cha mapokezi.Kutoka katika kitengo cha mwanzo cha mapokezi, unaweza kupangiwa malazi tofauti katika moja ya majimbo 16 shirikishi. Pindi utakapofika katika kitengo cha mapokezi ulichopangiwa, unaweza kukusanya maombi ya hifadhi katika moja ya matawi ya ofisi shirikishi kwa ajili ya uhamiaji na wakimbizi (BAMF). Hatua ya kupata hifadhi inaweza kuchukua miaka miwili au zaidi.

Maombi

Unatakiwa ukusanye maombi yako ya hifadhi binafsi kwa ofisi kuu kwa ajili ya uhamiaji na wakimbizi (BAMF). Utapokea taarifa ya miadi ya maombi yako au miadi itaonyeshwa katika ubao wa matangazo katika kitengo cha mwanzo cha mapokezi. Kupata tawi la BAMF la karibu nenda.

Katika tawi la BAMF, taarifa zako binafsi zitanaswa.Kama ni mkubwa kuliko miaka 14, alama zako za vidole na picha zitachukuliwa.Hii ni kwa ajili ya kuanzisha kwamba haya ni maombi yako ya kwanza ya hifadhi.

Zaidi ya hayo, utaulizwa kuhusu njia yako ya safari ambayo itaamua kama Ujerumani itawajibika au kutowajibika kwa ajili ya madai yako ya hifadhi. Kwa mfano, kama alama zako za vidole zilichukuliwa katika nchi nyingine, Ujerumani haitachunguza maombi yako ya hifadhi, na utarudishwa nchi inayowajibika kwa ajili ya dai lako.Kwa hiyo, mamlaka zitachunguza nchi ipi ya EU inawajibika kwa ajili ya maombi yako ya hidfadhi. Kwa hali yoyote, hii itakuwa nchi ya kwanza kuingia. Hii ni kwa mujibu wa makubaliano ya Dublin.

Kama Ujerumani inawajibika kwa ajili ya madai yako ya hifadhi, maombi yako yatashughulikiwa Ujerumani.

Punde si punde maombi yako ya hifadhi yakishakusanywa, utapokea kibali cha makazi. Kibali cha makazi kitakupatia makazi ya kisheria Ujerumani kwa kipindi cha mchakato wa hifadhi. Katika baadhi ya majimbo shirikishi, hiki kibali cha muda mfupi cha makazi kimejikita kwa baadhi ya maeneo. Hii inamaanisha kwamba hautaweza kuondoka eneo lako ulilopangiwa au jimbo shirikishi wakati wa miezi mitatu ya mwanzo ya makao yako.

Kila mwombaji wa hifadhi amepangiwa meneja wa dharura. Hii inamaanisha, kama unakusanya maombi ya hifadhi kama familia, utakuwa na mameneja mbalimbali wa dharura. Kwa sababu hii ya msingi, urefu wa mchakato wa maombi unaweza kutofautiana kwa wanafamilia.

Mahojiano ya Maombi

Kila mwombaji wa hifadhi anatakiwa ahudhurie binafsi mahojiano ya hifadhi. Kila maombi yanachunguzwa kutokana na umuhimu wake. Muamuzi kutoka BAMF na mkalimani wapo katika mahojiano ya hifadhi.

Hatimaye, ni muhimu kuelezea hadithi ya mtu binafsi kuliko kufafanua hali ya ujumla ya nchi yake.

Kama una ushahidi kuwa ulishawahi kuteswa, kwa mfano kwa siasa, dini au sababu nyingine, unatakiwa kuleta ushahidi huo katika mahojiano ya hifadhi. Mwishoni mwa mahojiano, utapokea nakala ya rekodi ya mahojiano. Unatakiwa uwe na rekodi hii iliyotafsiriwa katika lugha yako na kusaini kama una uhakika kuwa kila kitu kimerokodiwa ipasavyo. Ni vigumu sana kufanyia marekebisho ya taarifa za awali.

Uamuzi

Utapokea barua itakayokutaarifu juu ya maamuzi ya maombi yako ya hifadhi. Barua itatatja sababu nyuma ya uamuzi. Endapo maombi yako yamekataliwa, barua pia itakutaka uondoke ujerumani. Kwa minajiri hii, utatakiwa uonde Ujerumani, vinginevyo utahamishwa. Hata hivyo, una haki ya kukata rufaa ya kukataliwa kwa maombi yako. Wakati ukifanya hivyo, inashauriwa kutafuta msaada wa mwanasheria au kituo cha msaada.

Kukubalika 

Umetunukiwa hadhi ya ukimbizi au hifadhi? Kwa hali hii, unaruhusiwa kukaaa Ujerumani  angalau kwa miaka mitatu. Baada ya miaka hii, unaweza kupokea hati ya makazi ya kudumu. Kama umetunukiwaq hifadhi mbadala ya kitaifa au ya kimataifa (kwa mwaka mmoja), unaweza kupokea makazi ya kudumu baada ya miaka mitano au saba.

Waombaji wa hifadhi wenye vyeti vya Duldung, makazi ya muda mfupi wa kuhamishwa, unapaswa uombe tena kuongezewa kwa kila miezi mitatu. Makazi ya muda mfupi wa kuhamishwa sio hadhi ya makazi, ambayo inamaanisha kuwa unapaswa kuondoka nchini na kwamba kwa sheria, unaweza kuhamishwa muda wowote kama sababu za makazi yako ya muda mfupi wa kuhamishwa zinaonekana kukatishwa.Watu waliokakaa Ujerumani kwa muda mrefu kwa misingi ya makazi ya muda mfupi ya kuhamishwa na ambao wamechangamana haswa (kuhudhuria shule, kupokea mafunzo ya kiufundi, kusoma kijerumani), wanaweza kupokea hadhi ya makazi. Kwa taarifa zaidi, tafadhali wasiliana na vitio vya ushauri vilivyopo karibu yako.

Kukataliwa 

Kama unatoka kwenye nchi zinazoitwa nchi salama au unatafuta hifadhi kwa sababu za kiuchumi, mpango wako wa kupewa hadhi ya hifadhi au kutambulika kama mkimbizi sio nzuri.
Ombi lako lilikataliwa? Kwa mantiki hii una machaguzi mbalimbali: ama uondoke Ujerumani au uanze mchakato wa kukata rufaa. Kwa mchakato wa kukata rufaa, inashauriwa kutafuta msaada wa mwanasheria au kituo cha ushauri. Haya makataa lazima yazingatiwe.

Maswali yanayoulizwa mara kwa mara

Nchi zipi zipo kwenye umoja wa Ulaya?

Nchi zipi zinamilikiwa na Ulaya katika eneo la uchumi?

Naweza kuendesha Ujerumani nikiwa na Leseni yangu ya udereva?

Je una maswali mengine kuhusu mada ya viza na uhamiaji?

Siielewi hii barua muhimu, nani anaweza kunisaidia na ugumu wa nyaraka na urasimu Ujerumani?

Ni huduma gani nitazipata mimi kama mtafutaji wa hifadhi?

Mshauri wangu katika huduma za kijamii/wakala wa ajira ananitenda vibaya .Nifanyaje?

Kwa maswali zaidi wasiliana na mshauri wa huduma za uamiaji kwa vijana.

Ushauri wa mtandaoni