Integrationskurs Foto: © colourbox.de
Kwa wahamiaji wenye viza

Mahudhurio 

U mgeni Ujerumani na unataka kujifunza lugha? Kuhudhuria kozi shirikishi itakusaidia kwa hilo. Kama hauongei Kijerumani au unaongea kidogo, mahudhurio ni ya lazima, kwa maneno mengine unatakiwa kufanya kozi shirikishi.

Ausländeramt (Ofisi ya uhamiaji) wanakupatia cheti cha ustahiki na orodha ya watoaji wa kozi, kwa maneno mengine ni shule za lugha. Basi unaweza kuipata shule ya lugha katika eneo lako na kujisajili hapo.

Unaweza pia kupata anuani ya watoaji wa kozi wote shirikishi chini ya anuani muhimu ongozi. Hapo unaweza kutafuta watoa kozi walio karibu na eneo lako Ujerumani. Basi utatafuta matokeo pamoja na taarifa kama vile anuani au namba ya simu kwenye ramani.

Tathmini ya ngazi ya lugha, masomo na mtihani wa mwisho  

Pindi umejisajili na mtoaji wa kozi unafanya tathmini ya kiwango cha lugha. Hii inawawezesha kutafuta kozi ipi inakufaa. Gharama kwako ni 1.20 Euro kwa somo. Kama hauna pesa nyingi, hauhitajiki kulipa na/au gharama zako za usafiri zitalipwa. Kozi shirikishi inajumuisha kozi ya lugha na kozi elekezi.

Kozi ya lugha inajumuisha masomo 600. Hapa utajifunza lugha pamoja na vipengele vya maisha ya kila siku, kama vile ununuzi, nyumba, watoto, vyombo vya habari, burudani, shule na kazi, au miadi na daktari.

Mwishoni unafanya mtihani wako wa mwisho (“Jaribio la Lugha ya Kijerumani kwa Wahamiaji”; DTZ). Baada ya mtihani unatunukiwa “Cheti cha kozi shirikishi”. Utaweza baadae kuongea, kusoma na kuandika kwa Kijerumani mpaka ngazi ya kiwango cha A2 au B1. Waajiri wengi wanataka kuona hiki cheti. Muda mwingine unaihitaji kwa ajiri ya mamlaka kama vile ofisi ya uhamiaji. Kama unataka kuomba uraia, kwa maneno mengine kama unataka kuwa raia wa Ujerumani, “Cheti cha kozi shirikishi” ni cha msaada pia kuwa nacho.

Ikoje kama usipofaulu mtihani wa mwisho? Basi unaweza kurudia masomo 300. Na vile vile  unaweza kufanya tena mtihani.

Baada ya  kozi ya lugha utafanya kozi ya mwongozo. Kozi ya mwongozo ina masomo 100. Hapa utajifunza mambo mengi kuhusu mfumo wa sheria , historia na utamaduni.  Masuala muhimu pia yana  thamani  au kwa kuishi pamoja katika jamii.

Mwishoni unafanya mtihani ambao unahusu “kuishi Ujerumani“.

Kozi maalumu

Kuna kozi maalumu kwa vijana wadogo mpaka umri wa miaka 27, kozi shirikishi ya vijana. Inakusaidia kama unataka kufanya mafunzo ya ufundi. Taarifa zinapatikana kutoka kwa Bundesamt für Migration und Flüchtlinge.

Kwa baadhi ya miji, kozi maalumu zinatolewa pia, kama vile kozi zilizolengwa kwa wanawake tu, kozi za kusoma na kuandika au kozi za matuzo ya watoto. Uliza kwenye shule ya lugha.

Kwa watafutaji wa hifadhi

Ushirikishi: Kujifunza kijerumani

Pindi unapotunukiwa hifadhi, utaruhusiwa kushiriki katika kozi shirikishi. Kabla ya hili, hakuna haki iliyopo kwa kozi kama hiyo. Lakini kuna upekee:

Watafutaji wa hifadhi wenye matarajio mazuri ya kubaki nchini wanaweza kuomba kozi shirikishi. Matarajio ya kubaki nchini yanatazamwa vizuri kwa mtafutaji wa hifadhi mwenye kibali cha muda mfupi cha makazi. Taarifa muhimu kuhusu masharti haya tofauti yanapatikana kwenye tovuti ya Ofisi Kuu kwa ajili ya Uhamiaji na Wakimbizi (BAMF):

Kozi shirikishi kwa waombaji wa hifadhi

Unataka kuanza kusoma Kijerumani hivi punde? Kwa mantiki hii, wakimbizi wana machaguzi mbali mbali. Watoto lazima wahudhurie shule Ujerumani. Hii inafanyika kwa watoto na vijana ambao wameshakusanya maombi yao ya hifadhi, ili mradi hawajahudhuria shule kwa miaka tisa. Shuleni, watapewa utangulizi wa lugha ya kijerumani na utamaduni. (tazama “Mfumo wa shule”).
Lakini watu wazima, wanaweza kuanza kujifunza kijerumani wakati wakisubiri uamuzi wa maombio yao ya hifadhi. Vituo vingi vya wakimbizi vina walimu wa kujitolea ambao wanaotoa masomo ya kijerumani bure.


Integrationskurse für AsylbewerberIntegrationskurse für Asylbewerber

Maswali yanayo ulizwa mara kwa mara

Kozi shirikishi inachukua muda gani?

Kozi shirikishi kwa vijana inachukua muda gani?

Wapi naweza kufanya kozi shirikishi?

Kama sihitaji kufanya kozi shirikishi, Je, Kuna ulazima wa kuifanya?

Je ninatakiwa kufanya kozi shirikishi?

Je napaswa kufanya mtihani wa mwisho?

Siwezi kuhudhuria kozi , kwa mfano kwa sababu siko vizuri au mtoto wangu anaumwa, nitafanya nini?

Je naweza kubadili mtoa kozi?

Nini ninahitaji kwa ajli ya kozi?

Je naweza kupumzika?

Kwa nini sio kila watafutaji wa hifadhi wanafanya kozi shirikishi?

Kwa maswali zaidi wasiliana na mshauri wa huduma za uamiaji kwa vijana.

Ushauri wa mtandaoni