Wohnen Foto: © colourbox.de
Kwa wahamiaji wenye viza

Unatafuta malazi 

Je unatafuta malazi? Magazeti mengi yana sehemu maalumu ya kutangaza juu ya malazi, kwa kawaida huwa ni kwa siku za ijumaa na jumamosi. Unaweza kupata pia habari za makazi katika tovuti za magazeti. Pia kuna tovuti maalumu kwa ajili ya mali.Ofisi ya makazi katika mji wako unaweza pia kukupatia msaada wa kukutafutia makazi. Katika baadhi ya mikoa ni rahisi kupata makazi lakini katika mikoa mingine ni vigumu sana kupata malazi. Kwa sababu hiyo,mawakala wa miji wanaweza kukusaidia na kama watakupatia makazi huna budi kuwalipa. Kwa kawaida mawakala hupokea kodi ya miezi mitatu kama kamisheni.

Kodi na amana 

Kwa kawaida matangazo huwa yanafafanua kiasi cha kodi unachostahili kulipa kwa ajili ya malazi. Kodi baridi inajumuisha malipo yote ya ziada. Kodi joto ni kile unachomlipa mwenye nyumba kila mwisho wa mwezi.

Kwa kawaida maghorofa yanakuwa na samani kamili. Kunakuwepo na jiko na vitu vingine vya mpangaji wa kipindi cha nyuma aliyekuwa akiishi katika ghorofa hiyo,Kama vile friji ambayo unapaswa kuilipia. Hizi zinajulikana kama malazi.

Mara nyingi wenye nyumaba hutaka wapangaji kulipia amana. Hii inatakiwa isizidi thamani ya malipo baridi. Wapangaji hurudushiwa amana yao pindi wamuapo kuhama. Iwapa unataka kutazama kama kodi ya nyumba ipo juu sana unaweza kutazama “Mietspiegel” na jina la mji wako.

Mwanzoni mwa mwaka ni vigumu kuweza kujua ni kiasi gani cha maji, umeme au gesi utakayokwenda kutumia, hivyo unapaswa kulipia malipo ya awali ya kila mwezi kisha mwishoni mwa mwaka unaweza kurudishiwa kiasi Fulani cha pesa au kulipia Zaidi.

Makubaliano ya upangaji

Taarifa zote kuhusiana na kodi na amana yanapatikana katika makubaliano ya mpangaji. Pia inakueleza kama unahitajika kurepea nyumba kipindi unapohitaji kuhama. Pia inakupa taarifa juu ya ilani (kanuni za nyumba) wakati uishipo katika nyumba hiyo. Na pindi uhamiapo kwa kawaida unatakiwa kusaini fomu ya makabidhiano. Fomu hii inasaidia kuonyesha endapo kitu chochote katika ghorofa ni kibovu, hivyo itawasaidia wewe na mwenye nyumba kujua kwamba haukuwa wewe uliyekivunja au kukiharibu. Soma makubaliano ya mpangaji na fomu ya makabidhiano kwa umakini kabla ya kutia sahihi.

Kanuni za mwenye nyumba

Hautaki mgogoro na jirani yako? Zingatia kanuni za nyumba. Kwa kawaida saa nne usiku hadi saa moja asubuhi ni muda tulivu, pia kuanzia saa saba mpaka saa tisa mchana ni mida ya mapunziko ya mchana. Kwa maana nyingine hupaswi kupiga kelele mida hii. Jumapili na siku za sikukuu kunakuwepo na ukimya siku nzima. Ujerumani kuna mapipa ya takataka na mbao, matunda na taka mboga na takakata nyinginezo. Unapaswa kuweka glasi,bati na vifaa vya umeme visivyofaa katika chombo maalumu. Utakuta kanuni nyinginezo katika nyumba utakayokwenda kupangisha. Kwa mfano je, unaruhusiwa kufuga mbwa au paka ndani kwako? Ama je unapaswa kusafisha ukumbi au lami nje ya nje yenu?
Kwa watafuta hifadhi

Umekuja ujerumani kutafuta hifadhi? Pindi ukamilishapo taratibu utatakiwa kukusanya maombi yako ya hifadhi kisha utapangiwa karibu na kituo cha mapokezi. Inaweza tokea pia ukapangiwa katika mji shirikisho tofauti na ule uliopangiwa mwanzoni kwa namma nyingine hii inatokana na nchi yako utokapo na idadi ya watu ambao wamekwisha kupangiwa katika kituo husika cha mapokezi ya awali.

Mara nyingi vituo vya awali vya mapokezi huwa ni shuleni, kumbi za muziki na majumba mengine yaliyo wazi. Yanaweza kuwa na vitanda katika vyumba vikubwa, kantini na Daktari. Majumba haya mara nyingi huwa yanakuwa yamezungushiwa uzio na kulindwa na makampuni binafsi ya ulinzi. Utapatiwa mavazi, vifaa vya usafi wa mazingira na milo mitatu kwa siku. Utasajiliwa katika kituo cha mapokezi cha awali. Hii inamaanisha kuwa data zako binafsi zitachukuliwa na utapatiwa kadi maalumu ya haki ya makazi japo hii siyo maombi yako ya hifadhi.

Mwanzoni itakuwa vigumu kuamua ni wapi pakuishi ujerumani. Katika miezi mitatu ya kuwepo kwako ujerumani, hutaruhusiwa kuondoka katika eneo lako la mji shirikisho uliopangiwa kuishi. Ni pindi tu baada ya kumalizika kwa miezi hii mitatu ndipo utakaporuhusiwa kutembelea miji mingine ya shirikisho.

Utabakia katika kituo chako cha mapokezi cha awali kwa muda wa miezi sita, katika miezi hizi utahamishwa katika manispaa tofautitofauti ndani ya mji shirikisho. Hii inamaanisha kuwa utapangiwa upya malazi tofauti. Muda mwingine unaweza hamishiwa katika makazi ya makundi ya watu huko wakazi ni lazima washirikiane chumba. Utaishi katika makazi hayo mpaka pale maombi yako ya hifadhi yatakapoamuliwa. Ni muhimu hasa kuwafahamisha ofisi ya shirikisho ya uhamiaji na wakimbizi anuani ya makazi yako pindi uhamishwapo makazi ili taarifa muhimu ziweze kukufikia.

Unatokea katika kinachojulikana Kama nchi asilia? Kwa sababu hii unatakiwa kubakia katika kituo chako cha awali cha mapokezi mpaka maombi yako ya hifadhi yatakapoamuliwa. Hutakiwi kuondoka katika eneo ulilopangiwa au mji shirikisho.

Wakati wa mchakato wako wa maombi ya uhifadhi utakapokamilika na kuthibitishwa kupewa ruhusa ya makazi, upo huru kuamua ni wapi  ungelipenda kuishi ujerumani, ijapokuwa utaruhusiwa kuondoka katika mji shirikisho endapo tu haupokei ufadhili wowote wa taifa. Pia inatambulika kama ufadhili wa hifadhi za jamii, japokuwa hili linaweza kuchukua mwaka mmoja au Zaidi. Unaweza kutafuta ghorofa mwenyewe na faili la maombi au unaweza kutafuta msaada wa kutafutiwa. Kwa namna hii manispaa ya maeneo husika itakutafutia ghorofa kwa ajili yako. Unaweza kupata taarifa Zaidi katika ofisi ya mipango ya wahamiaji na wakimbizi.

Je, una cheti cha “muda cha makazi” cheti cha makazi ya muda mfupi, kama ndivyo kwa kawaida huruhusiwi kupangiwa upya ndani ya ujerumani.
 


 

Napata shida kupata malazi. Wapi naweza pata msaada?

Malazi katika eneo langu ni ghali mno. Siwezi kumudu. Wapi nitapata msaada?

Nimepata malazi lakini sina hakika kama makubaliano ya upangaji yako sahihi. Wapi nitapata msaada?

Nimehamia kwenye makazi yangu mapya. Nifikirie nini tena?

Kwa maswali zaidi wasiliana na mshauri wa huduma za uamiaji kwa vijana.

Ushauri wa mtandaoni