Auf einem Tisch steht eine Tüte mit dem Apotheken-Symbol. Daneben stehen verschiedene Medikamente, Handtücher und eine Wärmflasche. © Goethe-Institut
Kwa wahamiaji wenye viza

Nini cha kufanya kama unaumwa? 

Katika matukio ya magonjwa madogo madogo kama vile magonjwa ya sababishwayo na baridi, kichwa unaweza kununua dawa katika maduka ya dawa. Lakini madawa mengi yanapatikana kwa maelekezo kutoka kwa mtaalamu wa afya maelezo hayo hayana budi kuandikwa na madaktari kisha waweza kutumia maelezo hayo ya daktari kujipatia dawa katika maduka ya dawa za binadamu na unapaswa kulipia gharama za dawa hizo. 

Maduka ya dawa siku zote kufunguliwa kuanzia jumatatu hadi ijumaa saa 2: 00 asubuhi hadi 12:30 jioni. Jumamosi wanafunga saa saba mchana katika baadhi ya miji maduka haya hufunguliwa mpaka saa 2:00 usiku. Pia kuna huduma ya dharura kwa jumamosi au jumapili na wakati wa usiku.

Eine Person liegt krank im Bett. Auf dem Nachttisch sind Taschentücher, Nasenspray, Medikamente und eine Tasse Tee zu sehen. © Goethe-Institut

Kumuona daktari 

Unahisi kuumwa Sana? Jambo la msingi ni kuweka mpango wa kukutana na GIP. Mtoto wake hayupo sawa? Kama ndivyo nenda Kwa daktari wa watoto. Kwa kawaida unaweza kumuona daktari kuanzia jumatatu hadi ijumaa lakini kuna muda wa ziada kwa huduma ya madaktari kwa siku za jumamosi na jumapili na nyakati za usiku.

Kama una makubaliano ya kuonana na daktari unahitaji kuwa na kadi ya bima ya kampuni yako, mara ya kwanza ya kukutana na daktari unahitaji kujaza dodoso na taarifa zako binafsi na taarifa juu ya kuugua kwako/ugonjwa wako pindi utakapomaliza kusajiliwa utahitajika kusubiri katika chumba cha kusubiria. Watakuita kwa kutumia jina lako, mara nyingi inachukua dakika chahe lakini yaweza chukua pia saa moja au Zaidi.

Katika chumba cha ushauri, Daktari hukuuliza maswali ya awali katika hatua hii unapaswa kuelezea dalili za ugonjwa wako kwa uwazi: nini kinachouma? Imeuma kwa muda gani? Ulishawahi kuwa na maumivu haya hapo mwanzo? Baada ya kuuliza maswali hayo daktari atakufanyia uchunguzi. baada ya hapo atatoa hitimisho/utambuzi). Atakuambia ni ugonjwa gani ulionao.

Hutakiwi kulipa ili kumuona daktari kama una bima  halali. Unatakiwa kulipa kwa huduma binafsi za ziada. Daktari wako atakushauri.

Taarifa ya ugonjwa na mtaalamu   

Baada ya kufanyiwa uchunguzi, daktari atakuandikia taarifa ya ugonjwa wako. Mara nyingi atakupatia maelekezo ya dawa, pia pengine waweza pewa maagizo ya kukutana tena na daktari kwa ajili ya uchunguzi ujao au GP atakuelekeza kwa mtaalamu mwingine, mtaalamu huyo atakupatia uchunguzi wa kina. Kwa mfano, kwa dakari wa sikio, pua na koo, mifupa au mwanajikolojia/daktari wa wanawake. Kwa hili utapokea uhamisho, ili daktari wa familia yako ataarifiwe. Mtaalamu humchunguza tena.

Uchunguzi wa kimatibabu

Ili kuzuia ugonjwa yaani kutokuwa mgonjwa wakati wote, au kutambua mapema, kuna uchunguzi wa kuzuia. Baadhi ya uchunguzi una madai ya kisheria, mengine unatakiwa ulipe mwenyewe. Kwa watoto, kuna kinachojulikana kama U-uchunguzi unaowasaidia katika maendeleo yao.Pia kuna chanjo dhidi ya magonjwa ya kuambukizwa kama vile surua, kifaduro, kikohozi, matubwitubwi.

Kuanzia umri wa miaka 35, kuna upimaji wa mapema wa kutambua magonjwa ya figo na moyo, ugonjwa wa kisukari na kansa. Pia, kwa wanawake kuna vipimo vya  kugusa maziwa.

Kuna vipimo maalumu kulingana na jinsia, umri, magonjwa ya kifamilia au mimba. Hasa kwa ajili ya kusafiri, lakini pia kwa maisha ya Ujerumani baadhi ya chanjo zinaweza kupendekezwa. Ongea na daktari wako kuhusu hili.

Nambari muhimu zaidi kwa dharura

Nambari zote za dharura ni bure na zinaweza kupigwa bila ya fedha/ salio kwenye simu.

Polisi: 110
Polisi wanawajibika kwa dharura zote zisizo za kimatibabu, uhalifu na ajali kubwa za barabarani.
Andika jina lako na

  • Ilitokea wapi
  • Kilichotokea
  • Watu wangapi wameathirika
  • Ni majeraha gani yaliyopo
  • Subiria  maswali 
Nahaufnahme auf ein Polizeiauto von der Seite mit dem Schriftzug "Polizei" © Goethe-Institut

Idara ya zima moto/ huduma ya dharura/ uokoaji: 112
112 ni namba inayotumiwa kwa hali za kutisha za maisha kama vile mstuko wa moyo , kiharusi, au ajali kubwa.  Endapo una mashaka juu ya ukubwa wa kuumia , usisite kuwahadharisha watu wa ambulensi.  Gari hilo la ambulensi linaweza kuokoa maisha kwa dharura.

Ansicht auf das geschlossene Tor eines Feuerwehrgebäudes, durch die Fenster ist ein Feuerwehrauto sichtbar. © Goethe-Institut
 
Huduma ya dharura ya matibabu: 116117

Kwa dharura unaweza kuwapigia huduma ya dharura hata wikiendi .
Unaweza kwenda moja kwa moja kwa kituo cha dharura cha mazoezi. Vituo hivi vya dharura vya mazoezi vimeunganishwa na hospitali na hufunguliwa hadi saa nne usiku na katika sikukuu za umma.
Vinginevyo, unaweza kupiga nambari ya simu 116117. Simu hii ni bure na inapatikana nchini kote.  Hapa unaweza kupelekwa kwa daktari wa karibu.  Iwapo kutembelea nyumbani kuna hitajika , ofisi kuu itaandaa.
 
Huduma ya dharura kwa ajili ya meno: 01805/986700
Hapa mtu hupokea nambari za simu za watoa huduma na hupiga simu moja kwa moja hapa

Man sieht den oberen Teil eines grauen Gebäudes mit einem Schild, das ein rotes Kreuz auf weißem Grund zeigt. © Goethe-Institut
 
Watoto
Kimsingi, kwa watoto vigezo na nambari zilezile hutumika kama za watu wazima.
Katika kushughulikia watoto, ni muhimu pia kujua kanuni muhimu za maadili ili kutoa muamko kwa haraka na kwa usahihi. Kwanza kabisa, unapaswa umfariji mtoto baada ya kuanguka na kumtuliza. Ni muhimu kudumisha utulivu wa akili ili kumpatia huduma mtoto kwa haraka, cha zaidi usiwe na wasi wasi juu yake. Piga kwa usahihi simu za dharura kama kuna umuhimu. Boxi kamili la huduma ya kwanza linatakiwa kupatikana nyumabani ili kufunika vidonda kwa bandeji au sehemu iliyovunjika ya wazi ili kukitibu kidonda hicho kwa dawa inayopambana na vijidudu.
 
Simu ya watoto na vijana: 0800/1110333
Kwa matatizo ya watoto na vijana, wasiwasi wa tovuti na unyanyasaji wa kijinsia.
 
Simu ya wazazi: 0800/1110550
Kwa masuala ya elimu , wasiwasi juu ya tovuti, unyanyasaji wa kijinsia wa watoto na matatizo yote ambayo wazazi wanayo kuhusu watoto wao.
 
Simu ya msaada “ vurugu dhidi ya wanawake” 08000/116016
Huduma ya kitaifa ya ushauri kwa wanawake walioathirika na vurugu, mazingira yao ya kijamii na wafanyakazi wasomi. Huduma hii inapatikana bila malipo, na kutojulikana , kwa muda wote wa siku 365 kwa mwaka.
 
 
Simu ya msaada kwa wajawazito wenye uhitaji ( haijulikani na salama): 0800/4040020.
 
Simu ya ushauri: 0800/1110111

Ikiwa kuna matatizo na migogoro , k.m masuala ya ushirikiano, unyanyasaji shuleni au kazini, kupoteza kazi, ulevi, ugonjwa, upweke, migogoro na masuala ya kiroho yanaweza kupigiwa simu hapa
 
Simu ya dharura: 116116
Ili kuzuia EC na kadi  za malipo pamoja na kadi za utambulisho , k.m iwapo zimeibwa au kupotea.
 

Sera mbalimbali za bima 

Kila mtu anaishi kwenye matatizo: matatizo hayo ni kama ugonjwa au kutokuwa na uwezo wa kufanya kazi ( kutoweza kufanya kazi kabisa). Katika mazingira kama hayo,unaweza pata gharama za ziada bila matarajio, unaweza ukakata bima: utakuwa ukilipa pesa katika kampuni ya bima kila mwezi au kila mwaka. Katika matukio ya ugonjwa au kutokuwa na uwezo wa kufanya kazi kabisa, kampuni ya bima hukulipa pesa. Baadhi ya bima ni za lazima nchini ujerumani: kila mmoja anapaswa kuingia kwenye makubaliano. Bima zinginine ni za hiari:unaweza ukawa na bima kama ukipenda.

Bima za lazima 

Bima ya muhimu na ya lazima  ni bima ya afya,bima ya mafao na bima ya kutokuwa na ajira au kazi. Bima ya afya hulipwa tu unapomtembelea daktari au kupata huduma za kitabibu. Bima ya kutokuwa na ajira utapata kwa mwaka kama utakuwa umepoteza kazi na bado hujapata kazi nyingine. Bima ya mafao ni ya lazima kwa mwajiriwa: utapokuwa mzee na hauwezi kufanya kazi kabisa. Maelezo ya bima ya mafao itakulipa pesa kwa ajili ya kuendelea na maisha. Je una mwajiri? Kwa hivyo huwezi ukajilipia. Bima ya afya na bima ya jamii. Mwajiri wako atakulipia nusu nzima ya bima zote. Kama una gari au pikipiki, unatakiwa pia kuwa na bima ya vyombo vya usafiri. Utafanyaje kama umepata ajali na gari nyingine ikaharibika? Bima ya vyombo vya usafiri itakulipia kwa ajili ya matengenezo, au gharama zinazolingana na uharibifu huo.

Ein Auto hat in der deutliche Kratzer in der Tür. © Goethe-Institut

Bima za hiari 

Bima ya muhimu na ya lazima ni bima ya dhamana ya vitu, bima ya nyumba na vitu vyake na bima ya maisha. Umewahi kuharibu kitu cha mtu mwingine? Na kampuni ya bima ya dhamana ya vitu ikalipa. Bima ya nyumba na vitu vyake hufidiwa kama vimeharibika, mfano matukio kama ya mafuriko.na bima ya maisha itafidia pindi utakapokufa. Kwa mfano pesa inaweza ikafidiwa kwa watoto.

Kuna bima nyingine mbalimbali. Bima binafsi za ajali kwa mfano utafidiwa pindi utakapopata ajali nje ya masaa ya kazi. Bima ya halali ya kujikinga ni kwa ajili ya msaada wa kisheria, kwa mfano kumkodisha mtaalamu wa sheria. Malipo kwa ajili ya dhamana ya bima, bima kwa ajili ya safari, na bima kwa ajili ya tahadhari vyote vinapatikana. Ila kuwa makini na aina ya bima unayoitaka. Hoja ni kwamba kila aina ya bima inagharimu kiasi cha pesa.

Kwa waombaji wa hifadhi

Katika tukio la ugonjwa 

Katika hali ya tahadhari, wakimbizi wanaosubiri majibu ya maombi yao ya makazi wanaweza kumuona daktari. Hivyo ni kwa mujibu wa sheria. Kabla ya kwenda kumuona daktari unapaswa kuomba vocha maalumu ya bima ya afya katika ofisi za ustawi wa jamii. Tafadhali chukua vocha hii na ombi lako la kuonana na daktari ili ustawi wa jamii uweze kukulipia gharama ya matibabu. Muda mwingine daktari anaweza kukuagiza dawa, chukua maelekezo ya dawa nenda nayo duka la dawa ili kupatiwa dawa zako, gharama zinalipwa na ustawi wa jamii. Wanawake wajawazito au wamama wenye watoto wanapatiwa msaada maalumu na taifa.

Kama umeishi ujerumani kwa zaidi ya miezi 15 hauhitaji tena vocha ya bima ya afya unapohitaji kumuona daktari, ustawi wa jamii utalipa kwa namna sawa kama bima za afya zinavyolipa. Hata ivyo kiwango cha uchunguzi hufanikiwa. Ofisi ya ustawi wa jamii haitalipia miwani na gharama za usafiri za kumfikia daktari taratibu zaweza kutofautiana na watoto.

Ujerumani kila mtu mwenye bima ya afya pia anayo kadi ya bima ya afya. Katika miji shirikisho ya Hamburg na Bremen, kila mkimbizi pia hupewa kadi ya bima ya afya, kadi hii ina maanisha hautahitaji tena vocha ya bima ya afya na unaweza kwenda moja kwa moja kumuona daktari. Hata hivyo hii haimaanishi kwamba una bima ya afya, ofisi ya ustawi wa jamii italipia kiwango cha fedha cha uchunguzi.

Matatizo ya kisaikolojia

Hivyo hivyo pia ndivyo inavyotumika katika matatizo ya kisaikolojia: mwanzoni unaweza kumuona daktari kwa dharura. Hata hivyo miji mingi ina vituo vya ushauri vinavyoweza kutoa msaada. Daktari anaweza kukwambia wapi unapoweza kupata msaada pia.

 

Wapi naweza kumpata daktari wa jumla (GP) karibu na ninapoishi?

Naweza kwenda moja kwa moja kwa mbobevu au mtaalamu?

Ni vipi naweza kumpata daktari wa dharura katika maeneo yangu?

Nawezaje kupata kadi ya afya?

Nitafanyaje ikiwa naumwa na siwezi kwenda kazini?

Nawezaje kumpata daktari anayeongea lugha yangu ya asili?

Nini tofauti kati ya shughuli za kitabibu na hospitali?

Je, ninatakiwa kulipia kiasi gani kwa bima ya afya na bima ya mafao?

Kampuni yangu inatakiwa kulipia chochote kwa ajili ya bima yangu ya afya na bima ya mafao. Je, ninapataje fedha hizo?

Ninapata fedha nyngi na na bima ya afya kisheria ni ghali sana. Je kuna mbadala?

Ninaweza kupata wapi kampuni ya bima ya mafao?

Nikizeeka mradi wa bima ya mafao utanilipa. Je nitapokea fedha nyingi kama ninazopokea sasa?

Bima ya gari hulipia iwapo nitaharibu gari lingine. Je, iwapo nitaharibu gari langu mwenyewe katika ajali?

Ninatafuta sera ya bima kwa mbwa wangu. Aina gani ya bima ni nzuri?

Nina maswali mengi kuhusu mada ya bima. Nani anaweza kunisaidia?

Further questions? Write us via the contact form. We will forward your questions anonymously to the advisors of the youth migration services.

Contact form