Jemand arbeitet an einer Werkbank. Man sieht ein Lineal, einen Messschieber und Klebeband. © Goethe-Institut
Kwa wahamiaji wenye viza

Mahafali na cheti 

Katika nchi ya ujerumani unaweza ukapata kazi nzuri kama una degree au elimu ya ufundi. Unatakiwa uwe umemaliza ufundi na umepata cheti.je una cheti kutoka katika nchi yako? Kiwe kimetafsiriwa na kimethibitishwa.

In einer Küche eines Restaurants arbeiten verschiedene Menschen. © Goethe-Institut

Mafunzo ya ufundi mchakato 

Unatakiwa kuwa na kiwango cha Hauptschue kwa mafunzo ya ufundi. Bila ya kuwa na cheti ni vigumu kjiunga na mafunzo ya ufundi. Katika nchi ya ujerumani mafunzo ya ufundi ni muhimu na hutolewa hata kwa fani nyingi. Unaweza kujifunza ujuzi kwa kupitia uzoefu wa mafunzo kwa vitendo katika shirika. Na pia kwenda kwenye shule za biashara. Huko uatajifunza kanuni kwa nadharia. Kwa fani hiyo. Pia utakuwa na masomo ya kawaida machache kama vile kijerumani, siasa, na michezo.

Unaweza kufanya mafunzo kwa vitendo katika kampuni. Utfanya kazi kwa muda wa masaa 3 au 4 kwa wiki katika kampuni na kuhudhuria mafunzo ya biashara kwa muda wa masaa 8 au 12 kwa muda wa wiki moja. Au utatumia majuma machache kwenye kampuni na majuma machache kwenye mafunzo ya biashara. Unaweza kupata kufanya mafunzo kwa vitendo kwenye kampuni mbalimbali, mara nyingi katika kampuni zenye wataalamu. Kutafuta sehemu zenye vyuo vya ufundi stadi ni sawa na kutafuta kazi. Pia utume maombi (tazama ”kutafuta kazi") utakuwa ukilipwa kiasi cha pesa ukiwa ukifanya mafunzo ya ufundi stadi katika kampuni.

Fanya mazoezi ya Kijerumani chako kwa ajiri ya mahali pa kazi katika tovuti ya Goethe-Institut.

Finding work


wa mafunzo kwa vitendo

Mafunzo ya ufundi hudumu kwa muda wa miaka 2 au 3. Lakini vitendo hupatikana katika utaalamu unaweza kujifunza kwa haraka Zaidi, kwa mfano utunzaji wa watoto,kuwatunza wazee,urembo au upambaji. Unaweza pata kutoka kwa mawakala wa ajira  katika mji au jiji lako.

Auf dem Bild ist eine Bibliothek mit Tischen, an denen man sitzen und arbeiten kann, zu sehen. © Goethe-Institut

Shahada 

Kama una  Abitur/ kidato cha sita au sifa nyingine za kujiunga na chuo unaweza kusoma chuo kikuu. Kama una kiwango cha Fachabitur unaweza kujiunga na vyuo vya ufundi (Fachhochschule; FH). Shahada katika vyuo vya ufundi ni mara nyingi ni ya vitendo Zaidi kuliko vyuo vikuu vya kawaida. Wanafunzi wa elimu ya juu nchini ujerumani (uni na FH) ni lazima ujue kijerumani. kama kijerumani sio lugha yako ya asili,lazima uonyeshe umahiri wako katika lugha ya kijerumani. Kwa kawaida unatakiwa kuwa na “Deutsche Sprachprüfung für den Hochschulzugang” (mtihani wa lugha ya kijerumani kwa ajili ya udahili wa chuo kikuu; DSH) au TestDaf (mtihani wa lugha ya kijerumani kama lugha ya kigeni).

Katika majimbo shirika mengine  ni lazima ulipie kwa ajili ya mafunzo ya shahada, na mengine hakuna malipo. Unaweza kupata taarifa Zaidi kutoka studieren.de. ada za chuo hutofautiana. Unalipa kati ya 150€ na 700€ kwa muhula(miezi 6).

Kunaweza pia kuwa na mahitaji mengine kama vile kiwango mahususi cha wastani wa alam ( numerus clausus). Unaweza kupata taarifa kuhusu jambo hili katika chuo husika.
Ada ya masomo hutegemeana na jimbo .  Programu za awali za shahada na uzamili ni bure katika vyuo vya serikali. Gharama ya utawala, umoja wa wanafunzi na tiketi ya semista zinatolewa kwa kila semista. Taarifa zinaweza kupatikana kwenye www.studieren.de au www.studis-online.de.

Kwa shahada ya kwanza unahitajika kusoma mihula 6 hadi 8. Na baada ya mihula mingine 2 hadi 4 zaidi unaweza kufanya shahada ya uzamili. Kila mji/jiji lina vitengo vya ushauri wa kitaaluma (BIZ). Unaweza kupata BIZkupitia kwa mawakala wa ajira katika mji wako. Hapa unaweza ukashauriwa masomo ya elimu ya ufundi, shahada na masomo mengine ya elimu ya juu.

Kwa waombaji wa hifadhi

Mafunzo ya ufundi 

Kipindi cha miezi mitatu ya kwanza nchini ujerumani,wakimbizi ambao wameshawasilisha vibali vyao hawaruhusiwi kufanya kazi. Mara baada ya miezi mitatu, wanaruhusiwa kufanya mafunzo ya ufundi. Hata hivyo sio wote waliowasilisha vibali vyao wanaruhusiwa kufanya kazi. Wakimbizi ambao waliotoka katika nchi zenye amani hawaruhusiwi kufanya kazi hadi taratibu za kupata hifadhi zimekamilika.

Kuanza kusoma mafunzo ya ufundi stadi haimaanishi kuwa umeruhusiwa kuishi ujerumani. Kibali cha makazi kitaongezwa kwa kipindi Fulani.

Wakimbizi wenye vibali vya muda watafanya kazi mpaka watakapokamilisha taratibu, kama hatua Fulani zitafikiwa. Mtu binafsi wanaoishi kwa muda mfupi, pia watafanya kazi kwa makubaliano maalumu.

Taarifa muhumu zinazotokana na makubaliano hutolewa kwenye tovuti ya maafisa uhamiaji na wakimbizi (BAMF):

Shahada za chuo kikuu 

Je, unataka kusoma chuo kikuu nchini ujerumani? Hii ni rahisi kwa wakimbizi wanaotoka katika nchi washirika. Ingawa makubaliano hutofautiana kati ya nchi wanachama na vyuo. Kwa kawaida, huitaji shahada nzuri na yenye ufanisi ya ujerumani (C1). Ili uweze kujisajili kwa shahada unatakiwa uwe na vigezo vinavyohitajika. Ingawa vyuo vingi vinatoa ofa maalumu kwa wakimbizi. Ofisi shirika ya uhamiaji na wakimbizi  hutoa taarifa juu ya jambo hili.

Utambuzi wa vigezo na nyaraka 

Vigezo maalumu vinhitajika ili uweze kuanza mafunzo ya ufundi au elimu ya juu. Vigezo vinatakiwa kuhakikiwa kwa vyeti au nyaraka. Pamoja na nyaraka kutoka katika nchi yako, sifa hizo zinaweza kutambulika nchini ujerumani. Ingawa si kila kigezo kitatambulika nchini ujerumani. Hii inahitaji uhakiki wa ziada.

Je una sifa za elimu ya mafunzo ya ufundi au una shahada? Katika hatua hii nyaraka zako zinapaswa kuhakikiwa ili zitambuliwe.kama hauna nyaraka yoyote, utafanya mtihani wa utimilifu. Katika hili utapata maelekezo kazini, utasailiwa, na kuifanya jaribio. Ingawa mwanya huu haupo katika nchi washirika.

Je, unahitaji msaada wa utambuzi of sifa zako? Tafadhali wasiliana na ofisi za uhamiaji na wakimbizi (BAMF). Wana simu ambazo unaweza kuwapigia.


+49 30-1815-1111

Recognition of foreign qualifications in Germany
 

Wapi naweza soma mafunzo ya ufundi?

Lini nitaanza mafunzo ya ufundi?

Natakiwa kwenda kwenye shule ya biashara?

Je msaada wa kifedha unapatikana kwa ajili ya kusoma shahada?

Je vyeti vyangu vinaweza kutambulika?

Nawezaje kupata utarajali nikiwa kama mtafutaji wa hifadhi?

Further questions? Write us via the contact form. We will forward your questions anonymously to the advisors of the youth migration services.

Contact form