Schulsystem Foto: © colourbox.de
Kwa wahamiaji wenye viza

Gharama za lazima na mahudhurio shuleni 

Mahudhurio shuleni ni lazima katika nchi ya ujerumani. Watoto wanapaswa kuhudhuria shule kwa muda wa miaka 9. Baadhi ya majimbo, mahudhurio shuleni ni lazima  hii ni pamoja na wale watoto wenye mazaingira magumu. Mwaka wa masomo huanza mwezi wa nane (8) au wa tisa (9) na huendelea hadi mwezi wa sita (6) au wa saba (7), hii ni kulingana na jimbo husika. Mara nyingi watoto hupelekwa katika shule zinazofadhiliwa na serikali. Hakuna mtu anayelipa ada. Kuna gharama ndogo kwa ajili ya kutoa nakala, kununulia vifaa mbalimbali. Katika shule binafsi unatakiwa kulipa ada. Mtoto wako anahitaji ufadhili maalumu wa Ujerumani?  Basi wasiliana na shule moja kwa moja.
 

Aina za shule 

Kuna aina tofauti za shule. Watoto wote wenye umri kuanzia miaka 6 au 7 wanahudhuria elimu ya msingi. Baada ya miaka 4 wanafunzi wanaendelea na elimu ya sekondari. Kuna utofauti mkubwa katika shule za sekondari. Shule za msingi nyingi hushauri kuhusu shule ambayo mtoto wako anaweza kwenda wakati anapokuwa tayari kwenda kuanza. Kuna shule za Hauptschule (sekondari za ufundi: 5-9th daraja), katika shule hizi unaweza kufanya Hauptschlabschluss ukapata cheti mwishoni mwa masomo au kama mtu amefuzu na ana vigezo vya kuendelea anaweza kuendelea na masomo. Katika Hauptschule kuna masomo kwa vitendo kama vile useremala/uhunzi au uchoraji. Kiwango cha juu cha elimu hii ni Reaschule (hatua ya sekondari ya kati, daraja la 5-10th), katika hatua hii utafanya Realschulabschuss (diploma. Shule za sekondari). Baada ya Hauptschule au Realschule unaweza kujifunza utaalamu. Baada ya hapo kuna Gymnasium (shule za lugha; hadi daraja la 12th). Hapa unaweza kufanya Abitur, na baadaye ukafuzu na kwenda kujiunga na chuo kikuu. Katika hatua ya Gymnasium mara nyingi unajifunza lugha za kigeni 2 au 3, kama vile kiingereza na kifaransa.

Katika majimbo mengine wana Gesamtschule (shule za ufahamu). Hizi zinajumuisha Hauptschule, Realschule, na Gymnasium katika jingo moja. Endapo mwanafunzi anataka kuhama shule mfano kutoka Hauptschule na kwenda Realschule, ni rahisi. Kuna uwezekano wa kubadili shule kama zipo tofauti, lakini sio moja kwa moja. Kila jimbo lina shule zinazotumia lugha mbili, shule maalumu,wataaluma wa taaluma na vyuo vya ufundi.

Maelezo ya kina zaidi yanaweza kupatikana katka infografiki zetu.
 

Muda wa shule 

Shule nyingi humaliza vipindi wakati wa mchana (saa 8 au 9 mchana). Baaada ya masomo watoto wanaweza kwenda kwenye vituo vya kulelea watoto.watakaa hapo kwa muda wa mchana. Huko watapewa chakula na kusaidiwa mazoezi ya nyumbani. Lakini katika vituo hivyo vya kulelea watoto hulipiwa. Shule za kutwa zinaongezeka sana. Wanafunzi hutumia muda mwingi kwenye hizi shule,kwa kawaida hadi saa 10 au 11 za jioni.

Masomo shuleni 

Wanafunzi hujifunza masomo mbalimbali wakiwa shuleni. Pamoja na somo la PE. Katika shule za msingi somo hili halifundishwi kwenye makundi ya kijinsia. Kwa hiyo wavulana kwa wasichana wanafanya PE pamoja. Pia kuna somo la kuogelea. Shule nyingi zina vipindi vya dini ya kikristo. Lakini unaweza usisome kipindi cha dini, na ukahudhuria vipindi vingine vya ziada. Maadili hutolewa kama mbadala, na baadhi ya shule kuna vipindi vya ziada kama dini zingine (Mfano, dini ya kiislamu na kiyaudi).

Ikiwa mtoto wako ana shida katika somo  fulani shuleni, anaweza akapata msaada wa masomo ya ziada.  Aidha kwa mwalimu binafsi wa masomo ya ziada au shule . Maranyingi, masomo ya ziada huwa ni ya bei nafuu kidogo.
 

 

Shughuli za ziada 

Kwa kawaida wanafunzi huenda safari za kimasomo mara moja kwa mwaka.mara nyingi huwa ni siku 3-5. Darasa hufanya matembezi katika miji na mahali mbalimbali kwa pamoja. Hii pia huwa kama mazoezi kwa vitendo. Kwa kufanya hivi inamsaidia mwanafunzi kujifunza kuhusu historia, utamaduni na asili. Shule pia huwa na matamasha. Ambapo matamasha haya huwapa wanafunzi fursa za kushiriki kwa wanafunzi na kuwa mfano kwa wengine.

Wazazi 

Kila shule ina mwakilishi wa wazazi – ambaye anafanya kazi pamoja na walimu shuleni. Kuna jioni ya wazazi mara nyingi katika kila mwaka. Ambapo muda huo wazazi wapewa taarifa kutoka kwa walimu, na pia wanapata fursa za kufahamiana. Pia ni wakati maalumu wa kuwasiliana na walimu kwa ajili ya kupanga ratiba za kukutana na wazazi katika muda binafsi. Huu ni muda wa mazungumzo baina ya wazazi na walimu husika. Hii pia hufanyika endapo kuna tatizo shuleni. Au kama mzazi anahitaji kujua maendeleo ya mtoto wake shuleni.

Kwa waombaji wa hifadhi

Shule 

Suala la elimu katika nchi ya ujerumani ni la lazima.hii ina maana kwamba watoto wanapaswa kupelekwa shule kwa muda wa miaka 9. Watoto wa wakimbizi nao wanatakiwa kwenda shule lakini wanasubiri kwa kipindi cha wiki kadhaa kabla ya kwenda shule. Kipindi cha kusubira kinategemeana na jimbo husika. Mara nyingine huchukua muda wa wiki chache, lakini kwa kawaida inaweza kuchukua hadi miezi sita. Sharti ni kwamba hutakiwi kuendelea kukaa katika eneo la mapokezi. Mara unaenda kuishi katika eneo ambalo linakuhusu, watoto wako wanaweza kwenda shule.

Ukiwa katika kambi unaweza pata msaada kutoka kwenye ofisi za usajili [Einwohnermeldeamt]. Mtu utakayewasiliana naye atawasiliana na shule unayostahili kwenda. Baada ya hapo utaweza kwenda shule na pia kuonana na walimu.

Watoto na vijana ambao hawajui kuongea lugha ya kijerumani wanaanza kwa kukwa katika darasa tofauti ambako watajifunza lugha na utamaduni wa kijerumani. Hivi hujulikana kama masomo ya ukaribisho au masomo ya mpito yaliyopangwa ili kufanya mwanzo rahisi katika shule ya kijerumani. Walimu watakuwa na furaha kutoa msaada na kujibu maswali.

Kuhudhuria shule ni bure kwa watoto wa wakimbizi. Kama watoto wako wanatakiwa kuchukua basi kuelekea shule, kwa mfano, hawatakiwi kulipa. Chakula cha mchana cha shule, ziara, vitabu, penseli na notpad ni bure. Shule itazilipa. Kuapata msaada wa kifedha wa aina hii utatakiwa kujaza nyaraka mbalimbali. Unaweza kupata taarifa zaidi kwenye ukumbi wako wa mji.
 

Je, natakiwa kumsajili mtoto wangu shuleni?

Lini mtoto wangu anatakiwa kwenda shule?

Naweza kuwafundisha watoto wangu nyumbani?

Wanasoma muda kiasi gani kwa siku?

Mtoto wangu anapenda kwenda chuo kikuu. Shule ipi akasome?

Sisi ni wageni Ujerumani na mtoto wangu hawezi kuongea Kijerumani. Anaweza kusoma shule za Kijerumani?

Naweza kuchagua shule?

Mtoto wangu anaweza kwenda shule kwa kutumia basi la shule?

Mtoto wangu atapewa kitu chochote cha kula?

Kwa maswali zaidi wasiliana na mshauri wa huduma za uamiaji kwa vijana.

Ushauri wa mtandaoni