Ansicht auf ein leeres Büro mit zwei gegenüberstehenden Schreibtischen © Goethe-Institut

Marafiki

Katika siku chache za mwanzo katika mahali pako papya pa kufanyia kazi, utaweza kuwafahamu marafiki wako wapya na kazi yako. Unaweza mara kwa mara kuongea nao kawaida baada ya siku chache (tumia kijerumani cha “du”). Mambo ni tofauti pindi inapokuja kwa mkuu wako, mkuu wa kazi. Maneno rasmi hutumika kwa karibu kila mara, kwa mantiki hii- kijerumani cha “Sie” namna ya usemi. Hata hivyo, inatofautiana kulingana na kampuni. Fanya mazoezi  ya Kijerumani chako cha mahali pa kazi kwenye tovuti ya Goethe-Institut.

Haki za mwajiriwa

Ujerumani kuna sera ya ulinzi wa mwajiriwa: kampuni inatakiwa izingatie kanuni kuhusu afya na usalama wa waajiriwa. Kwa mfano, hizi hujumuisha nguo za kazi zilizoteuliwa, mapumziko ya mara kwa mara na saa za kufanya kazi. Kampuni kubwa zina bodi ya mwakilishi wa waajiriwa, baraza la kazi. Kama ukiwa na tatizo unaweza kulizungumza kwa baraza la kazi. Baraza la kazi litaongea basin a mkuu wako wa kazi.

Eine Kellnerin hat ein Tablett mit Gläsern in der Hand, im Hintergrund sind sitzende Personen zu sehen. © Goethe-Institut

Saa za kazi na mapumziko

Saa za kazi zinategemea na kazi yako. Kwa mfano , muuguzi aliyejikita hospitali unafanya kazi kwa kupokezana: muda mwingine unafanyakazi asubuhi, muda mwingine jioni au usiku. Ofisini saa zako za kazi nyingi zimepangiliwa. Unaanza asubuhi na kumaliza siku yako ya kufanya kazi baada ya saa 8 au 9. Ofisi mara nyingi zina saa chaguzi, kwa mfano una saa za kufanya kazi chaguzi. Kwa mfano unaweza kuanza saa 2 au 7 asubuhi, na kuondoka mapema au kwa kuchelewa jioni. Kila kazi ina angalau pumziko moja, mara kwa mara mapumziko kwa ajili ya chakula cha mchana cha dakika 30 au 60. Watu kwa kawaida hufanyakazi saa 38-40 kwa wiki.
Inawezekana pia kufanya kazi kwa muda wa ziada, kwa mfano , kwa asilimia hamsini. Hiyo huchukua maasa 20 kwa juma. Ikiwa una watoto au umejiajiri kwa kigezo cha muda wa ziada, hili  huwa ni chaguo moja.
 
 
Kila mwajiriwa ana kiwango maalumu cha mapumziko kwa mwaka. Unatakiwa uombe likizo yako ya mwaka na mkuu wako wa kazi lazima aipitishe. Unaweza mara kwa mara kuchukua mapumziko yako wakati ukitaka. Lakini muda mwingine huwezi kuchukua mapumziko kwa sababu kuna kazi nyingi zinazotakiwa kufanywa katika kampuni. Muda mwingine unatakiwa kuchukua likizo kwa sababu kampuni ipo kwenye mapumziko, ambapo ni hoja kwa baadhi ya kampuni kwenye krisimasi, kwa mfano. Unaendelea kupokea ujira/mshahara wako wakati wa likizo yako ya mwaka. Kama ni mgonjwa, unatakiwa umtaarifu mwajiri wako mara moja na kwenda kwa daktari. Daktari anakupatia cheti cha daktari kwa ajili ya mwajiri wako. Waajiri hawaihitaji mara kwa mara cheti cha daktari mpaka ukiwa katika likizo ya ugonjwa kwa siku tatu (tazama ukurasa wa “Afya”).

Nguo za kazi

Kwa baadhi ya kazi unatakiwa kuvaa nguo maalumu kwa kazi, kwa mfano kwenye eneo la ujenzi kukulinda na kuumia. Muda mwingine unatakiwa pia kuvaa unifomu, kwa mfano kama unafanya kazi uwanja wa ndege. Au unatakiwa uvae T-shirt yenye nembo ya kampuni yako. Hii inamsaidia mteja kuona kuwa wewe ni mwajiriwa.
Notisi - Kündigung
Kama hauwezi tena au hauna utayari wa kufanya kazi kwa kampuni, unatakiwa ukabithi notisi yako. Notisi kila mara hutolewa kwa maandishi. Na kuna muda wa notisi. Kwa kawaida muda wa notisi ni miezi 3.

Mehrere Köche arbeiten in einer Restaurantküche. Sie tragen Kopftücher und Kochjacken. © Goethe-Institut

Notisi

Kama hauwezi tena au hauna utayari wa kufanya kazi kwa kampuni, unatakiwa ukabithi notisi yako. Notisi kila mara hutolewa kwa maandishi. Na kuna muda wa notisi. Kwa kawaida muda wa notisi ni miezi 3.

Elimu ya juu

Ikiwa tayari una ujuzi au shahada na umeshafanya kazi kwa muda fulani, unaweza kujiendeleza kielimu. Utazidisha, kupanua, au kuboresha ujuzi wako .Hasa Volkhochschulen au vyuo vya elimu vya watu wazima  hutoa kozi mbalimbali.

Eine Frau sitzt an einem Tisch in ihrer Wohnung und telefoniert. Auf dem Tisch liegen Papiere und ein Laptop. © Goethe-Institut

Video International Sign

Further questions? Write us via the contact form. We will forward your questions anonymously to the advisors of the youth migration services.

Contact form