Nahaufnahme auf einen Tisch im Freien mit einem Getränk darauf. Man sieht einen Arm einer Person, die ein Smartphone bedient. © Goethe-Institut

Kufanya maawasiliano kwa njia ya simu kwa kutumia simu kadi kutoka ujerumani kwenda nchi nyingine ni ngumu. Kadi nyingi katika nchi ya ujerumani hazifanyi kazi, na kupiga simu kwa kadi za simu za nje ni gharama sana.

Kuna njia tofauti za kupiga simu katika nchi ujerumani. Hii ni orodha yenye taarifa ya watoa huduma tofauti tofauti:

Mkataba wa simu ya mkononi 

Chaguo mojawapo na ambalo linawezekana ni mkataba wa simu. Hata hivyo hii inahitaji akaunti ya benki na taarifa za utambulisho za ujerumani kwa njia hii, watoa huduma wanaangalia kama mteja anaweza kulipa bili zake. Tahadhari: husisaini mkataba ambao hujauelewa. Badala yake, muulize mtu ili akuasidie maana yake au tafsiri yake. Kwa kawaida mkataba wa simu hudumu kwa muda wa miaka miwili. Mara nyingi ni vigumu kuvunja mkataba kabla ya wakati/muda. Malipo ya bili lazima yafanyike kila mwisho wa mwezi katika kipindi cha mkataba. Zingatia! Kama utapenda kubadili mtoa huduma na kwenda kwa mtoa huduma mwingine yakupasa usubiri hadi ule wa kwanza uwe umeisha ndani ya muda sahihi inatakiwa kufanyika miezi mitatu kabla ya mkataba, vinginevyo mkataba unaweza kurudia upya tena kwa mwaka mmoja au miwili.

Ein Mann lehnt an einem Laternenpfahl und telefoniert mit seinem Handy. © Goethe-Institut

Kadi ya malipo ya kabla 

Chaguo jingine ni kununua kadi ya malipo ya kabla. Kadi hizi hupatikana kwa gharama nafuu pia hupatikana mara nyingi katika maduka makubwa, vituo vya kuuzia mafuta, au kwenye kioski. Hii pia inahusu kusaini mkataba.Pindi inapoamilishwa unatakiwa  kuthibitisha jina, anwani na tarehe ya kuzaliwa. Ili kufanya hivyo unapaswa kuonyesha pasipoti yako, kadi ya utambulisho au picha rasmi ya ID katika duka. Muda mwingine unahitaji kibali cha makazi.

Je, umeshanunua kadi ya malipo ya kabla kutoka kwenye maduka ya simu moja kwa moja? Ambapo ni rahisi kuhuisha kadi yako kwenye duka. Hapa pia unaweza ukapata msaada. Umeshawahi kununua kadi ya malipo ya kabla ndani, kwa mfano: kwenye maduka makubwa?

Kisha unaweza kithibitisha utambulisho wako kwa njia ya utambuzi wa video katika smartphone yako, komypyuta bapa au kwenye kamera pembuzi katika kompyuta).

Mara kadi itakapohuishwa, unatakiwa kuongeza salio. Salio hutumika katika kupiga simu, kutuma ujumbe na kutafuta mitandao. Kadi kwa mfano: maduka makubwa, vituo vya kuuzia, na kwenye vioski. Kuna mchakato mrefu wa jinsi ya kuongeza salio kwenye kadi. Kuongeza salio, weka namba hizi kwenye simu.

Je, unataka kuwasiliana kimataifa kutoka ujerumani? Katika hili, tegemea kulipa ada ya senti 15, hata kama kwa maongezi ya muda mfupi. Kupiga simu Syria, Eritrea na nchi za Balkani ni gharama sana. Na hii ni orodha ya viwango vya kupiga simu kimataifa kutoka makampuni tofauti tofauti ya mitandao ya simu.

Wakati mwingine inawezekana kununua ushuru fulani wa ziada  ambapo unapokea kiasi fulani cha dakika za bure kwa simu za kimataifa.

In einem Geschäft hängen viele verschiedene SIM-Karten von verschiedenen Anbietern auf einer Verkaufsstange. © Goethe-Institut
 

Taarifa ya simu 

Simu zenye kadi ya malipo ya kabla pia hutumika katika kutafuta mitandao. Hata hivyo hufanya kazi haraka unapoongeza salio. Hivyo ni rahisi kununua kifurushi kinachofaa ajili ya simu. Hii itakusaidia kutumia mtandao wa simu kwa muda Fulani kwa bei ya kudumu au kununua kiasi fulani cha data.

Ein Mann sitzt vor einem Café und nutzt sein Smartphone. © Goethe-Institut

WLAN

Kama unataka kutafuta mtandao Fulani bure, unaweza kutumia mtandao wa WLAN. Sehemu nyingi zinazotoa huduma za mitandao, maktaba, na maeneo yenye majengo ya umma  wanatoa huduma hiyo ya Mtandao wa WLAN bure. Je, ungependa kutumia mtandao wa WLAN bila malipo katika maeneo unayoishi? Tovuti ya “Freie Hotspots” itakusaidia kupata eneo la umma ambalo unaweza kupata huduma hiyo.

Video International Sign

 

Further questions? Write us via the contact form. We will forward your questions anonymously to the advisors of the youth migration services.

Contact form