Kursteilnehmende machen eine Wortübung auf dem Tisch. Zu sehen sind Wortkarten und Lehrbücher. © Goethe-Institut

Mahudhurio 

U mgeni Ujerumani na unataka kujifunza lugha? Kuhudhuria kozi shirikishi itakusaidia kwa hilo. Kama hauongei Kijerumani au unaongea kidogo, mahudhurio ni ya lazima, kwa maneno mengine unatakiwa kufanya kozi shirikishi.

Ausländeramt (Ofisi ya uhamiaji) wanakupatia cheti cha ustahiki na orodha ya watoaji wa kozi, kwa maneno mengine ni shule za lugha. Basi unaweza kuipata shule ya lugha katika eneo lako na kujisajili hapo.

Unaweza pia kupata anuani ya watoaji wa kozi wote shirikishi chini ya anuani muhimu ongozi. Hapo unaweza kutafuta watoa kozi walio karibu na eneo lako Ujerumani. Basi utatafuta matokeo pamoja na taarifa kama vile anuani au namba ya simu kwenye ramani.

Der Ablauf eines Integrationskurses ist auf einem Whiteboard schematisch dargestellt. © Goethe-Institut

Tathmini ya ngazi ya lugha, masomo na mtihani wa mwisho  

Pindi umejisajili na mtoaji wa kozi unafanya tathmini ya kiwango cha lugha. Hii inawawezesha kutafuta kozi ipi inakufaa. Gharama kwako ni 2.29 Euro kwa somo. Kama hauna pesa nyingi, hauhitajiki kulipa na/au gharama zako za usafiri zitalipwa. Kozi shirikishi inajumuisha kozi ya lugha na kozi elekezi.

Kozi ya lugha inajumuisha masomo 700. Hapa utajifunza lugha pamoja na vipengele vya maisha ya kila siku, kama vile ununuzi, nyumba, watoto, vyombo vya habari, burudani, shule na kazi, au miadi na daktari.

Mwishoni unafanya mtihani wako wa mwisho (“Jaribio la Lugha ya Kijerumani kwa Wahamiaji”; DTZ). Baada ya mtihani unatunukiwa “Cheti cha kozi shirikishi”. Utaweza baadae kuongea, kusoma na kuandika kwa Kijerumani mpaka ngazi ya kiwango cha A2 au B1. Waajiri wengi wanataka kuona hiki cheti. Muda mwingine unaihitaji kwa ajiri ya mamlaka kama vile ofisi ya uhamiaji. Kama unataka kuomba uraia, kwa maneno mengine kama unataka kuwa raia wa Ujerumani, “Cheti cha kozi shirikishi” ni cha msaada pia kuwa nacho.

Ikoje kama usipofaulu mtihani wa mwisho? Basi unaweza kurudia masomo 300. Na vile vile  unaweza kufanya tena mtihani.

Baada ya  kozi ya lugha utafanya kozi ya mwongozo. Kozi ya mwongozo ina masomo 100. Hapa utajifunza mambo mengi kuhusu mfumo wa sheria , historia na utamaduni.  Masuala muhimu pia yana  thamani  au kwa kuishi pamoja katika jamii.

Mwishoni unafanya mtihani ambao unahusu “kuishi Ujerumani“.

Ein Kursteilnehmer ist im Klassenzimmer zu sehen. © Goethe-Institut

Kozi maalumu

Kuna kozi maalumu kwa vijana wadogo mpaka umri wa miaka 27, kozi shirikishi ya vijana. Inakusaidia kama unataka kufanya mafunzo ya ufundi. Taarifa zinapatikana kutoka kwa Bundesamt für Migration und Flüchtlinge.

Kwa baadhi ya miji, kozi maalumu zinatolewa pia, kama vile kozi zilizolengwa kwa wanawake tu, kozi za kusoma na kuandika au kozi za matuzo ya watoto. Uliza kwenye shule ya lugha.

Video International Sign

Maswali yanayo ulizwa mara kwa mara

Further questions? Write us via the contact form. We will forward your questions anonymously to the advisors of the youth migration services.

Contact form