Ein Bräutigam steckt seiner Braut den Ehering an den Finger. © Goethe-Institut

Nyaraka 

Katika nchi nyingi watu huoana katika ofisi zilizosajiliwa. Hizi ni ndoa zinazotambulika na taifa. Hivi ndivyo mambo yalivyo ujerumani, pia unaweza kuoa au kuolewa kanisani. Ndoa za kanisani zinachukua nafasi kwa umaarufu zaidi baada ya ndoa za ofisini.

Je ungependa kuoa au kuolewa ujerumani? Basi unahitaji kujisajili katika ofisi zilizosajiliwa kwenye eneo unaloishi au makazi yako. Unahitajika kuwa na baadhi ya taarifa kama kadi yako ua usajili, kitambulisho chako, viza au cheti chako cha kuzaliwa. Je wewe na mwenzi wako mna watoto pamoja? Basi kama ndivyo unahitaji pia kuleta taarifa za kimaandishi za watoto hao. Unahitajika kuwa na taarifa hizi zikiwa zimetafsiriwa katika lugha ya kijerumani zinahitaji kusajiliwa na mwandishi wa hati za sheria kuonesha kuwa tafsiri zipo sahihi, anatakiwa kuthibitisha tafsiri kama umeoa au kuolewa utapatiwa taarifa mpya za kimaandishi kutoka katika ofisi ya usajili, cheti cha ndoa, kama unapenda pia unaweza kusajili familia yako, yenye taarifa juu ya familia yako.

Tangu tarehe 1, oktoka 2017, wanandoa wa jinsia moja Ujerumani wanaweza kuoa au kuolewa kwa haki zote na wajibu. Hili linamaanisha , kwa mfano, kwamba  wanaweza kulea watoto kama wanandoa wa jinsia tofauti, ikiwa wanakidhi vigezo vya muhimu.

Es sind zwei Bräute zu sehen, die die gleichgeschlechtliche Ehe eingehen. © Goethe-Institut
Uliolewa au kuoa katika nchi yako ulipotoka? Kama ndivyo utapewa cheti cha ndoa hukohuko. Nyaraka hii ni cheti chako cha ndoa cha nchi yako ya kigeni. Inaweza pia kutambulika katika ofisi ya msajili ujerumani

Maadhimisho ya harusi 

Watu wengi wanafanya hafla kubwa kusherekea harusi yao. Bibi harusi mke, mara nyingi huvaa shela nyeupe za harusi. Wanandoa wengi pia hununua pete za harusi katika harusi  bwana harusi , mume huvishwa pete kutoka kwa mke wake, na mke huvishwa pete kutoka kwa mume wake.

Unaweza kupata taarifa zaidi juu ya mada ya “ndoa ya kimataifa“ inaweza kupatikana katika tovuti ya “ofisi ya mashirikisho ya kigeni”( Federal  foreign Office website).

Taarifa kuhusu “utaratibu wa uhamiaji wa wanandoa” kwa maneno mengine unapokuja ujerumani kuishi na mumme wako au mke wako yaweza kupatikani katika tovuti ya “BAMF”.

Ein weiß geschmückter Saal mit Hochzeitsdeko ist zu sehen. © Goethe-Institut

Utengano na talaka

Kwa sababu kadha wa kadha wanandoa wanaweza kuchagua kujitenga au talaka. Hasa kama watoto wameathirika na inaelekea katika ulipaji wa pesa ya kujikimu kutoka kwa yule mwenye kipato kikubwa, Basi hapa ushauri unaweza kuwa wa manufaa. Vituo vya ushauri nasaha vinaweza kusaidia sehemu fulani na maswali ya kisheria.

Video International Sign

Further questions? Write us via the contact form. We will forward your questions anonymously to the advisors of the youth migration services.

Contact form