Eine Demonstration mit vielen Menschen ist zu sehen. Im Vordergrund sieht man eine Regenbogenfahne. © Goethe-Institut
Katiba ya ujerumani inajulikana kama sheria ya msingi. Katiba inajumuisha sheria halali za nchi pamoja na utawala wa kisiasa kwa jamuhuri ya shirikisho ya ujerumani, kwa mfano katiba inaweka wazi kuwa ujerumani ni nchi ya kidemokrasia. Hii inamaanisha kuwa haki ya kushiriki katika siasa, kwa mfano katika vyama, mipango, miungano na vyama vya siasa.

Vyama vya siasa vina ajenda na malengo mbalimbali. Vyama vikuu vya siasa ni SPD (Social democratic party), CDU (Christian democratic union), Bündnis 90/The green party, FDP (Free democratic party),  AfD (Alternative for Germany) na Die Linke (chama cha mrengo wa kushoto). Mbali na haya kuna vyama vinginevyo vingi vidogo.

Eine Demonstrationen zum Klima ist zu sehen. Viele Plakate werden in die Luft gehalten. © Goethe-Institut

Katiba pia inajumuisha haki na majukumu ya watu ujerumani. Jukumu la msingi ni kuhudhuria shule ya lazima. Watoto na vijana wadogo ujerumani wanatakiwa kwenda shuleni. Kisha kuna utozwaji wa kodi. Kila mtu anayeingiza kipato anapaswa kulipa kodi. Na wajibu wa kulitimiza kwa mujibu wa sharia: Kila mmoja anapaswa kutii sheria.


Na hizi ni haki za msingi Zaidi:

Utu wa mwanadamu: Ni lazima uwaheshimu watu.

Haki ya usawa: Watu wote wana haki ya usawa. Kwa mfano wanaume na wanawake wana haki sawa.

Usawa katika sharia: Watu wote ni sawa katika sharia.

Haki ya uhuru wa kujieleza: Watu wanaweza kusema wanavyofikiri.

Uhuru wa kusanyiko: Watu wanaruhusiwa kukutana katika makundi.

Haki ya kuhama: Watu wote wanaruhusiwa kuishi na kuamua wapi pa kuishi.

Haki ya kufanya kazi: Watu wanaruhusiwa kuchagua shughuli zao za kufanya.

Haki nyinginezo inajumuisha ulinzi wa ndoa na familia, haki ya kupiga kura na uhuru wa dini.

    
Haki ya kupiga kura inasema kwamba watu ujerumani wana ruhusiwa kupiga kura. Na wanaruhusiwa kuchaguliwa pia, Uchaguzi ni sharti iwe siri, ya jumla na huru. Kuna uchaguzi wa ulaya, chaguzi za bunge, chaguzi za taifa na chaguzi za serikali za mitaa. Kwa kawaida umri wa kupiga kura ni kuanzia miaka 18 na Zaidi. Katika baadhi ya mashirikisho ya miji (Majimbo) unaweza kupiga kura katika uchaguzi wa serikali za mitaa ukiwa na umri wa miaka 16 na uchaguzi wa wabunge ni sharti uwe na umri wa miaka 18 ili kuweza kupiga kura.

Katika maeneo mengi kuna kamati za halmashauri shirikishi. Kwa kawaida huchaguliwa na wahamiaji. Kamati za halmashauri shirikishi kwa kawaida hufanya kazi kwa maslahi ya kisiasa ya wahamiaji. Wanawasaidia pia kuwapa maelekezo kwa maswali yao na kutatua matatizo. Dhumuni la kazi hii ni kuimarisha namna wahamiaji na wajerumani wanavyoishi pamoja.

Das Innere einer christlichen Kirche ist zu sehen. © Goethe-Institut

Uhuru wa kidini unamaainisha kila mmoja yupo huru kuchagua dini zao na kuzitumiakia. Karibia robo ya watu wa ujerumani hawana dini rasmi. Wajerumani wengi ni wakristo, kwa namna nyingine ni wakatoliki waroman au waprotestanti. Sikukuu nyingi za kikristo kama vile krisimasi na pasaka ni sikukuu za umma. Hii ina maana kwamba watu wengi hawafanyi kazi katika siku hizi. Lakini wanachama wa dini nyinginezo pia wapo ujerumani. Shule zinatoa elimu ya dini ya kikatoliki na kiprotestatnti. Katika baadhi ya shule masomo ya kidini pia yanapatikana kama wakristo, othodoksi, kiyahudi au dini ya mafundisho ya kiislamu. Wazazi wanaweza kuamua endapo watoto wao wapate elimu gani ya kidini.

Ujerumani mvuto wa kimapezi kwa mtu fulani unaweza kufanyika hadharani. Hii inamaanisha kwamba mapenzi ya jinsia moja, mbili na watu wasio kuwa na utambulisho wa kiume au kike au ambao wapo katikati ni sehemu ya maisha ya kila siku kama wapenzi wa jinsia tofauti. Harakati za LGBTQ zina jukumu la umuhimu Ujerumani. Hii ni jumuiya ya wasagaji,mashoga, wapenda jinsia mbili kimapenzi( kiume na kike), watu wenye jinsia ya kike au kiume lakini akili inamsadikisha kuwa yeye ni wa jinsia tofauti na mabaasha au wasenge. Wanalindwa Ujerumani. Kwa mfano, alama ya harakati ya LGBT ni bendera ya upinde wa mvua.
 
Tangu tarehe 1, oktoba 2017 wanandoa wa jinsia moja Ujerumani wanaruhusiwa kuoa au kuolewa kwa haki zote na wajibu. Hii inamaanisha kwamba, kwa mfano, wanaweza kuwalea watoto kama wanandoa wa jinsia tofauti kama wakikidhi masharti muhimu.

Menschen sitzen vor einem Cafe in der Sonne. Ein Mann in einem Rollstuhl ist zu sehen. © Goethe-Institut
 
Kama haki zisipozingatiwa, inaweza kuwepo wakati mwingine ubaguzi. Angalia sehemu hii kwenye tovuti yetu.
 
 

Video International Sign

Further questions? Write us via the contact form. We will forward your questions anonymously to the advisors of the youth migration services.

Contact form