Uwezo wa kiakili wa kompyuta na Sheria
Ni kitu gani roboti aruhusiwe kufanya?

Itakuwaje endapo anafanya kosa? Roboti “Pepper” mwenye mwonekano na tabia mithili ya mwanadamu anafanya kazi katika makazi ya kutoa matunzo kwa wagonjwa mjini Erlenbach.
Itakuwaje endapo anafanya kosa? Roboti “Pepper” mwenye mwonekano na tabia mithili ya mwanadamu anafanya kazi katika makazi ya kutoa matunzo kwa wagonjwa mjini Erlenbach. | Picha (maelezo): © picture alliance / REUTERS / Kai Pfaffenbach

Uwezo wa kiakili wa kompyuta hufanya maisha yetu kuwa rahisi zaidi kwa njia nyingi. Lakini ni nani wa kuwajibika pale kanuni za kimahesabu za kompyuta na maroboti yanapofanya makosa?

Tunakutana na aina mbalimbali za uwezo wa kiakili wa kompyuta kila mahali katika maisha yetu ya kila siku na sasa ni wazi kwamba uwezo huo unaendelea kufanana na sisi wanadamu zaidi na zaidi kwa vigezo vya uwezo wake - leo hii kanuni za kimahesabu za kompyuta haziwezi tu kuwa za kimantiki, bali za kibunifu pia. Maroboti hujifundisha yenyewe mambo mapya. Jambo hili lina maana gani katika mazingira ya kisheria? Je, roboti anaweza kuwa na haki na wajibu kama mwanadamu?
Nani wa kulaumiwa pale gari linalojiendesha lenyewe linapofanya kosa? Maswali kama haya kuhusiana na jinsi ya kushughulika na uwezo wa kiakili wa kompyuta yanaendelea kutoa changamoto zaidi na zaidi kwa wanasheria pamoja na serikali. Nani wa kulaumiwa pale gari linalojiendesha lenyewe linapofanya kosa? Maswali kama haya kuhusiana na jinsi ya kushughulika na uwezo wa kiakili wa kompyuta yanaendelea kutoa changamoto zaidi na zaidi kwa wanasheria pamoja na serikali. | Picha: © picture alliance/dieKLEINERT/Markus Grolik Wanamaadili, wanasheria pamoja na serikali wanatumia muda mwingi sana kufikiri juu ya maswali yanayofanana na hili, kwa sababu ni kawaida kufanya makosa, na sasa kama inavyoonekana, siyo tu kwa mwanadamu. Programu zinazojiendesha zenyewe hufanya maamuzi yake yenyewe, na ambayo nyakati fulani yanaweza kuwa maamuzi mabovu – hata kanuni bora kabisa za kimahesabu za kompyuta haziwezi kuhakikisha ulinzi dhidi ya jambo hilo. Mfano mmoja wa jambo hili ni gari linalojiendesha lenyewe. Kama ilivyo kwa watumiaji wote wa barabara, kanuni fulani hazina budi kufuatwa. Kinyume na wanadamu, gari linaweza kuwekewa mfumo wa kuhakikisha kwamba hakuna kishawishi cha kukimbia zaidi ya ukomo wa mwendo au kuchukua uamuzi wa hatari wa kuyapita magari yaliyo mbele yake. Hata hivyo, itakuwaje pale watumiaji wengine wa barabara watakapofanya makosa? Kwa mfano, pale baiskeli itakapoingia barabarani kwa ghafla. Jaribu kujenga picha ya gari, likichepuka ghafla upande na uwezekano wa kuwahatarisha watembea kwa miguu. Je, gari liwekewe mfumo wa kufanya maamuzi ya hatari? Au gari liachiwe lenyewe kuamua? Na endapo uamuzi mbovu unafikiwa – nani atawajibika?

Je, uwezo wa kiakili wa kompyuta unaweza kuchukuliwa sawa na mtu au chombo chenye wajibu wa kisheria?

Kwa ajili ya kujenga msingi wa kisheria kwa masuala magumu kama hayo katika ngazi ya awali, Bunge la Ulaya lilipendekeza mwaka 2017 kwamba mashine zenye uwezo wa kiakili zilipaswa kupatiwa hadhi ya kuitwa “mtu wa kielektroniki” ambaye – kama ilivyo kwa watu na makampuni –angetambuliwa  kama mtu au chombo chenye wajibu wa kisheria. Hata hivyo, watafiti wa uwezo wa kiakili wa kompyuta na washauri wa masuala ya kisheria hawakuwa na shauku ya kipekee kuhusiana na wazo hili. Katika barua ya wazi kwenda Kamisheni ya Umoja wa Ulaya, wataalamu 250 waliongea wazi kupinga wazo hilo. Ni wazo linatokana na dhana potofu kwamba swali la dhima ya kisheria haliwezi kujibiwa pale maroboti yanayojiendesha yenyewe yanapofanya maamuzi mabovu. Hali hii ya uelewa potofu ilisababishwa na udanganyifu wa maroboti katika riwaya za sayansi na mihemko katika matangazo kwa vyombo vya habari, inasemwa ndani ya barua hiyo. Wizara ya Mambo ya Kiuchumi na Nishati ya Shirikisho la Ujerumani (BMWi) nayo pia haioni hitaji la kutengeneza hadhi ya kisheria ya “mtu wa kielektroniki”. Maswali ya kisheria  yaliyoibuliwa na mashine zenye uwezo wa kiakili yanaweza kupatiwa ufumbuzi kupitia mfumo uliopo wa kisheria, wizara ilitamka ndani ya nyaraka za matokeo ya tafiti kuhusiana na suala la uwezo wa kiakili wa kompyuta na sheria katika muktadha wa Mapinduzi ya 4 ya viwanda. “Mifumo ya uwezo wa kiakili wa kompyuta haijafikia bado kiwango cha kujisimamia yenyewe ambacho kingefutilia mbali uhusiano wake na tabia ya mwanadamu.” Kwa hiyo ni lazima kwa wanadamu kuendelea kuwa na wajibu kwa the matokeo ya kutumia uwezo wa kiakili wa kompyuta. Licha ya yote hayo, wajibu hauwezi kirahisi tu kubambikiwa mashine zisizo na uhai au programu za kompyuta.

Roboti kama muasisi?

Kwa upande mwingine, kunaswali la nani anapaswa kunufaika pale uwezo wa kiakili wa kompyuta unapozalisha mali bunifu. Suala hili siyo jipya kabisa. Mapema sana miaka ya  mwanzoni mwa 1960, maroboti waliotumika kupaka rangi yaliibua maswali yanayofanana na hayo. Kazi walizotengeneza, hata hivyo, zilitokana zaidi na kanuni za kimahesabu za kompyuta zisizokuwa na mpangilio maalumu ambazo kwa njia yoyote ile haziwezi kulinganishwa na akili ya mwanadamu. Hata hivyo, ndani ya miaka kumi iliyopita, uwezo wa kiakili wa kompyuta unaonekana “kufikia ngazi mpya ya maendeleo”, kama wizara ilivyosema katika nyaraka zake. Leo hii roboti anaandika muswada mzima wa filamu na kutunga vipande vya muziki. Ni vigumu kulinganishwa na kanuni za kuchorachora tu bla mpangilio za miaka hiyo ya nyuma. Je, kwa maana hiyo, roboti anaweza kuwa mtunzi? – muasisi?
 
Wanasheria hupenda kurejelea mfano kutoka kwenye ulimwengu wa wanyama. Mwaka 2008, mpigapicha wa the Uingereza, David J. Slater, alikabidhi kamera yake kwa nyani anayeitwa Naruto, ambaye alijipiga picha iliyopata umaarufu miaka mitatu baadaye na kusambaa duniani kote. Shirika la kutetea haki za wanyama, Peta, lilijaribu to kufungua madai, kwa niaba ya Naruto, kudai mapato yaliyotokana na picha hiyo. Madai hayo  yalifuatiwa na kesi ya kisheria iliyochukua miaka kadhaa, ambayo iliunguruma nchini Marekani. Mwaka 2017, Slater alikubali kufanya mapatano nje ya mahakama na aliahidi kutoa kwa Peta robo ya mapato ambayo yangepatikana kutokana picha ya Naturo ya kujipiga mwenyewe. Hata hivyo, Mahakama ya Rufaa ya San Francisco ilipinga mapatano hayo. Kesi ya kisheria ilitupiliwa mbali kwa msingikwamba Naturo mwenyewe hakuwa na kauli yoyote katika mapatano hayo na kwamba lengo kwa wakati wote lilikuwa ni kuweka tu mfano wa kurejelea. Kwa kuongezea, Peta alilazimika kumlipa mpigapicha gharama zake za ada za kisheria. Slater alitambuliwa kama muasisi wa picha hiyo. Baadaye aliifungulia madai bendi ya Ujerumani, Terrorgruppe, kwa kutumia picha hiyo kwenye jalada la rekodi idhini. Ofisi ya Hakimiliki ya Marekani ilitamka kwamba hakimili inaweza kutolewa tu kwa wanadamu na kwa hiyo siyo kwa wanyama– au maroboti.
 
Kwa sasa, mahakama na serikali haziwaondolei watu wajibu wao juu ya uwezo wa kiakili wa kompyuta ambao wameutengeneza, hata endapo uvumbuzi wao unageuka na wenyewe unakuwa wavumbuzi. Haki na wajibu vinabakia kwa watumiaji wa uwezo wa kiakili wa kompyuta au kwa wale ambao wanauendesha. Sheria ya Uingereza ya Hakimiliki ya Usanifu na Udhibiti wa Kuiga ilikuja na uamuzi huu huko nyuma mwaka 1988 pale kompyuta za awali za majumbani zilipoibua maswali yanayofanana na yale yanayoibuliwa na “roboti mwenye kujifunza” leo hii. Kamisheni ya Umoja wa Ulaya nayo pia inaonekana kukubaliana na wazo hili. Teknolojia haina budi kutumika daima katika kutoa huduma kwa mwanadamu na kuambatana na haki zinazohitajika, ilitamkwa kwenye mawasiliano kuhusiana na taswira ya mustakabali wa kidijitali wa Ulaya, mwezi Februari 2020