Ein Wohnhaus mit vielen Wohnungen ist zu sehen. Vor dem Haus steht ein blühender Baum. © Goethe-Institut

Unatafuta malazi 

Je unatafuta malazi? Magazeti mengi yana sehemu maalumu ya kutangaza juu ya malazi, kwa kawaida huwa ni kwa siku za ijumaa na jumamosi. Unaweza kupata pia habari za makazi katika tovuti za magazeti. Pia kuna tovuti maalumu kwa ajili ya mali.Ofisi ya makazi katika mji wako unaweza pia kukupatia msaada wa kukutafutia makazi. Katika baadhi ya mikoa ni rahisi kupata makazi lakini katika mikoa mingine ni vigumu sana kupata malazi. Kwa sababu hiyo,mawakala wa miji wanaweza kukusaidia na kama watakupatia makazi huna budi kuwalipa. Kwa kawaida mawakala hupokea kodi ya miezi mitatu kama kamisheni.

Ein Schlüsselbrett mit vielen Schlüsseln hängt im Eingang einer Wohnung. © Goethe-Institut

Kodi na amana 

Kwa kawaida matangazo huwa yanafafanua kiasi cha kodi unachostahili kulipa kwa ajili ya malazi. Kodi baridi inajumuisha malipo yote ya ziada. Kodi joto ni kile unachomlipa mwenye nyumba kila mwisho wa mwezi.

Kwa kawaida maghorofa yanakuwa na samani kamili. Kunakuwepo na jiko na vitu vingine vya mpangaji wa kipindi cha nyuma aliyekuwa akiishi katika ghorofa hiyo,Kama vile friji ambayo unapaswa kuilipia. Hizi zinajulikana kama malazi.

Mara nyingi wenye nyumaba hutaka wapangaji kulipia amana. Hii inatakiwa isizidi thamani ya malipo baridi. Wapangaji hurudushiwa amana yao pindi wamuapo kuhama. Iwapa unataka kutazama kama kodi ya nyumba ipo juu sana unaweza kutazama “Mietspiegel” na jina la mji wako.

Mwanzoni mwa mwaka ni vigumu kuweza kujua ni kiasi gani cha maji, umeme au gesi utakayokwenda kutumia, hivyo unapaswa kulipia malipo ya awali ya kila mwezi kisha mwishoni mwa mwaka unaweza kurudishiwa kiasi Fulani cha pesa au kulipia Zaidi.

Ein Stromzähler hängt im Keller einer Wohnung. © Goethe-Institut

Makubaliano ya upangaji

Taarifa zote kuhusiana na kodi na amana yanapatikana katika makubaliano ya mpangaji. Pia inakueleza kama unahitajika kurepea nyumba kipindi unapohitaji kuhama. Pia inakupa taarifa juu ya ilani (kanuni za nyumba) wakati uishipo katika nyumba hiyo. Na pindi uhamiapo kwa kawaida unatakiwa kusaini fomu ya makabidhiano. Fomu hii inasaidia kuonyesha endapo kitu chochote katika ghorofa ni kibovu, hivyo itawasaidia wewe na mwenye nyumba kujua kwamba haukuwa wewe uliyekivunja au kukiharibu. Soma makubaliano ya mpangaji na fomu ya makabidhiano kwa umakini kabla ya kutia sahihi.

Kanuni za mwenye nyumba

Hautaki mgogoro na jirani yako? Zingatia kanuni za nyumba. Kwa kawaida saa nne usiku hadi saa moja asubuhi ni muda tulivu, pia kuanzia saa saba mpaka saa tisa mchana ni mida ya mapunziko ya mchana. Kwa maana nyingine hupaswi kupiga kelele mida hii. Jumapili na siku za sikukuu kunakuwepo na ukimya siku nzima. Ujerumani kuna mapipa ya takataka na mbao, matunda na taka mboga na takakata nyinginezo. Unapaswa kuweka glasi,bati na vifaa vya umeme visivyofaa katika chombo maalumu. Utakuta kanuni nyinginezo katika nyumba utakayokwenda kupangisha. Kwa mfano je, unaruhusiwa kufuga mbwa au paka ndani kwako? Ama je unapaswa kusafisha ukumbi au lami nje ya nje yenu?

Eine Person putzt ein Treppenhaus in einem Wohnhaus. © Goethe-Institut

Video International Sign

Further questions? Write us via the contact form. We will forward your questions anonymously to the advisors of the youth migration services.

Contact form