Taarifa zaidi

Kurudi kwenda Goethe-Zertifikat C1

Kila kitu kipo! Seksheni ya mtihani

Mtihani wa Goethe-Zertifikat C1 unajumuisha seksheni za kusoma, kusikiliza, kuandika na kuongea. Seksheni ya kuongea ya mtihani hufanywa katika jozi au kwa mtahiniwa mmoja. Mtihani husimamiwa na kutathminiwa kwa njia ileile duniani kote.
 

Kusoma

Unasoma maandishi yasiyokuwa riwaya, mawazo, mapitio ya vitabu na / au taarifa. Katika zoezi kama hilo, unaonesha kuwa unaweza kushughulika na kiasi kikubwa cha maandishi kwa kuyatumia na kuyatoa tena katika dondoo.

Muda: takribani dakika 70

Kuandika

Unajieleza mwenyewe kwa undani zaidi juu ya mada katika maandishi yaliyopangika vema. Utapokea maelezo katika mfumo wa michoro.

Muda: takribani dakika 80

Kusikiliza

Unasikia mazungumzo ya mdomo, mazungumzo ya simu, usaili au taarifa za redio, kuchukua maelezo na kutoa kauli.

Muda: takribani dakika 40

Kuongea

Katika sehemu ya kwanza ya mtihani, unatoa mawazo yako juu ya maandishi mafupi. Kisha unaongea na mtu unayezungumza naye kufanya uamuzi pamoja au kutafuta suluhisho.

Muda: takribani dakika 10-15

Mahitaji

Goethe-Zertifikat C1 ni mtihani wa Kijerumani kwa watu wazima.

Mitihani ya Goethe-Institut hutolewa kwa yeyote anayependa na inaweza kufanywa bila kujali umri au utaifa.
  • Umri wa chini wa miaka 16 unahitajika ili kuweza kufanya mtihani wa Goethe-Zertifikat C1.
  • Ili kufanya mtihani wa Goethe-Zertifikat C1, ni sharti mtahiniwa awe na ujuzi wa lugha ya Kijerumani unaofikia kiwango cha  ngazi ya tano ya umahiri (C1) kulingana na Mfumo wa Pamoja wa Ulaya wa Marejeo ya Lugha (CEFR).
  • Ili kufikia ngazi hii, watahiniwa wanapaswa wawe wamekamilisha vipindi  800 and 1,000 vya dakika 45 za masomo, kwa kutegemea ujuzi wake wao awali na mahitaji yao ya mafunzo.