Nini cha kufanya wakati wa dharura?
Audio-Player: Artikel anhören
Artikel anhörenMWND Notfall
00:00
00:00
00:00
Polisi: 110
Polisi wanawajibika kwa dharura zote zisizo za kimatibabu, uhalifu na ajali kubwa za barabarani. Andika jina lako na
- Ilitokea wapi
- Kilichotokea
- Watu wangapi wameathirika
- Ni majeraha gani yaliyopo
- Subiria maswali
Watoto
Kimsingi, kwa watoto vigezo na nambari zilezile hutumika kama za watu wazima.
Katika kushughulikia watoto, ni muhimu pia kujua kanuni muhimu za maadili ili kutoa muamko kwa haraka na kwa usahihi. Kwanza kabisa, unapaswa umfariji mtoto baada ya kuanguka na kumtuliza. Ni muhimu kudumisha utulivu wa akili ili kumpatia huduma mtoto kwa haraka, cha zaidi usiwe na wasi wasi juu yake. Piga kwa usahihi simu za dharura kama kuna umuhimu. Boxi kamili la huduma ya kwanza linatakiwa kupatikana nyumabani ili kufunika vidonda kwa bandeji au sehemu iliyovunjika ya wazi ili kukitibu kidonda hicho kwa dawa inayopambana na vijidudu.
Simu ya watoto na vijana: 0800/1110333
Kwa matatizo ya watoto na vijana, wasiwasi wa tovuti na unyanyasaji wa kijinsia.
Simu ya wazazi: 0800/1110550
Kwa masuala ya elimu , wasiwasi juu ya tovuti, unyanyasaji wa kijinsia wa watoto na matatizo yote ambayo wazazi wanayo kuhusu watoto wao.
Simu ya msaada “ vurugu dhidi ya wanawake” 08000/116016
Huduma ya kitaifa ya ushauri kwa wanawake walioathirika na vurugu, mazingira yao ya kijamii na wafanyakazi wasomi. Huduma hii inapatikana bila malipo, na kutojulikana , kwa muda wote wa siku 365 kwa mwaka.
Simu ya msaada kwa wajawazito wenye uhitaji ( haijulikani na salama): 0800/4040020.
Simu ya ushauri: 0800/1110111
Ikiwa kuna matatizo na migogoro , k.m masuala ya ushirikiano, unyanyasaji shuleni au kazini, kupoteza kazi, ulevi, ugonjwa, upweke, migogoro na masuala ya kiroho yanaweza kupigiwa simu hapa
Simu ya dharura: 116116
Ili kuzuia EC na kadi za malipo pamoja na kadi za utambulisho , k.m iwapo zimeibwa au kupotea.