Umoja wa Ulaya (EU)

Umoja wa Ulaya (EU) ni kundi la mataifa mengi yaliyo barani Ulaya. Ni jumuiya ya ushirikiano. Katika eneo lenye zaidi ya kilomita za mraba milioni nne, wanaishi takribani watu milioni 450. Kwa sasa, EU ina nchi 27 ambazo ni wanachama . Zinataka amani, ushirikiano na ustawi kwa waja wote barani Ulaya. Lengo lao ni kuhakikisha kuwa kila Mwana-Ulaya ana maisha mazuri. EU inalenga kufanya aushi kuwa bora, salama na rahisi zaidi. EU inaauni nchi kushirikiana katika kutatua matatizo, kufanya biashara, na kuishi kwa kufuata kanuni za pamoja.

Audio-Player: Artikel anhören

Artikel anhören

Die Europäische Union

Europäische Flagge © Goethe-Institut/ Gina Bolle

Utawala

Kuna lugha 24 ambazo ni rasmi. Nyaraka na taarifa zote za EU zimeandikwa kwa lugha hizi. Ili EU iweze kufanya kazi vizuri, kuna taasisi za natija kama vile: Bunge la Ulaya, Tume ya Ulaya, Baraza la Umoja wa Ulaya na taasisi nyingine.

Historia

EU ilianzishwa baada ya Vita vya Pili vya Dunia. Ujerumani na nchi nyingine tano zilianzisha jumuiya ya kwanza ya Ulaya mwaka wa 1951. Walitaka kujenga uchumi imara barani Ulaya. Tangu wakati huo, EU imebadilika. Tangu mwaka 2002, kuna sarafu ya pamoja inayoitwa euro. Katika nchi 20 za EU, waja hutumia euro kama fedha yao ya kawaida.

Malengo na Maadili

EU ni jumuiya yenye maadili ya pamoja. Miongoni mwa maadili haya ni amani, demokrasia, uhuru na usawa kwa waja wote. Maadili hutufundisha kutofautisha lililo sahihi na lililo baya. Hutuauni kufanya yaliyo sahihi.

Malengo ya EU ni pamoja na: kulinda mazingira na kuimarisha uchumi. Waja wote waishio Ulaya wanapaswa kuwa na aushi bora. Waja wote wanapaswa kutekelezewa mambo kwa usawa, bila kujali jinsia yao, asilia au dini yao.

Katika EU, kuna ofisi ya usawa wa haki. Ofisi hii huhakikisha kuwa kila mja anapewa haki sawa. Hakuna mja anayepaswa kubaguliwa, iwe ni kwa sababu ya asili, dini, jinsia au maumbile maalum. Ofisi ya usawa huauni waja. Taarifa na ushauri hutolewa kwa lugha mbalimbali.

Uhamaji ndani ya EU

Waja walioko ndani ya Umoja wa Ulaya wanaweza kusafiri kwa urahisi kutoka nchi moja hadi nyingine. Ikiwa unatoka katika nchi ya EU, unaweza kusafiri kwa uhuru ndani ya mataifa ya EU. Unaweza pia kuishi, kufanya kazi au kusoma katika nchi nyingine ya EU.

Unatoka katika nchi isiyo ya EU? Basi wewe ni raia wa nchi ya tatu. Na wewe unaweza kusafiri, kuishi na kufanya kazi ndani ya EU. Lakini kuna masharti maalum. Kwa mfano, unahitaji kibali cha ukaazi kwa ajili ya nchi moja maalum ya EU. Unapaswa kuwa umeishi huko kwa miaka kadhaa na kujimudu kimaisha. Ndipo unaweza kuomba kibali hicho. Ukiwa nacho, unaweza pia kuhamia nchi nyingine ndani ya EU.

Tufuatilie