Burudani

Menschen an einem Flussufer © Goethe-Institut

Kule Ujerumani kuna fursa nyingi za kutumia muda wa burudani. Mijini kuna nafasi zaidi. Mijini kuna utamaduni mwingi, kwa mfano maonyesho ya jukwaani, vyumba vya makumbusho na tamasha. Pia kuna mikahawa na maduka mengi. Na kuna vyombo vya usafiri wa umma. Hata hivyo, aushi ni ghali zaidi mjini. Kuna kelele nyingi na mazingira ya asili si mengi.

Audio-Player: Artikel anhören

Artikel anhören

Freizeit

Jiji na Mashambani

Mashambani au katika miji midogo, nafasi za burudani si nyingi sana. Lakini aushi ya huko ni tulivu zaidi. Kuna mazingira ya asili ya kutosha na nafasi kubwa. Hakuna kelele nyingi wala uchafu. Nyumba na manyumba mara nyingi huwa na bustani. Gharama za makazi ni nafuu.

Taarifa kuhusu fursa za burudani hupatikana kwenye tovuti ya mji au eneo unakoishi.

Utamaduni

Unapenda utamaduni? Katika miji mingi kuna makumbusho, maonyesho, sinema, maonyesho ya jukwaani, tamasha na hafla nyinginezo. Sinema nyingi huonyesha filamu za kimataifa katika lugha yake ya asili (OV), mara nyingi zikiwa zimenukuliwa. Miji na maeneo mengi huwa na ratiba ya matukio mtandaoni. Unaweza kuchunguza mtandaoni kuona nini kipo.

Katika maktaba au maktaba za miji, unaweza kudurusu vitabu, kusikiliza muziki na kuangalia filamu bila malipo au kwa ada ndogo. Unahitaji kujisajili katika maktaba ya mji wako. Mara nyingi utahitaji cheti cha makazi. Unaweza pia kukopa vitabu, filamu na diski tambazi: unaenda navyo chengoni na kuvirudisha baadaye.

Bustani na Mazingira Asilia

Unapenda kwenda ziara? Mazingira ya asilia ni sehemu nzuri ya kupumzika. Kila mji una hifadhi na bustani. Waweza kutembea, kucheza au kufanya mandhari humo. Wakati wa kiangazi, hifadhi huwa na waja wengi. Waja hufanya mazoezi huko pia. Unaweza kuchana mbuga, kucheza kandanda, pingpong au kufanya mazoezi ya mwili. Karibu hifadhi zote kingilio ni bure.

Kwa watoto kuna maeneo mengi ya kuchezea. Katika bustani za mimea, unaweza kuona mimea maalum. Wanyama kutoka sehemu mbalimbali za dunia hupatikana katika mbuga za wanyama. Bustani za mimea na mbuga kwa kawaida huwa na ada. Zaidi ya hayo, kuna maziwa, misitu au milima katika maeneo mengi. Huenda unaishi karibu na bahari. Ukiwa mjini, unaweza kwenda matembezi ya ziari. Wakati wa kiangazi, unaweza kwenda ziwani kupiga mbizi.
 

Kupata Marafiki

Unajisikia vizuri na marafiki. Ni vizuri kutumia wakati wako wa bure pamoja. Unaweza kukutana na watu na kupata marafiki wapya nchini Ujerumani. Kuwa wazi na kuonyesha nia. Fanya mambo mengi katika wakati wako wa bure. Kuwa na subira. Wakati mwingine inachukua muda kidogo.

Mwanzoni, jamii ya watu kutoka nchi yako inaweza kukuauni. Unaweza kuwapata kwenye mitandao ya kijamii. Kuna vikundi vingi vya waja wenye mapenzi au mambo ya pamoja. Pia kuna mashirika ya wahamiaji. Uliza katika kituo cha ushauri. Miji mingi ina mikutano au matukio ya kimataifa. Huko, unaweza kuzungumza na waja kutoka nchi mbalimbali.

Una watoto? Basi utakutana na wazazi wengine mara kwa mara, kwa mfano shuleni au katika kitengo Cha chekechea. Kupitia watoto, tayari mna mada ya pamoja. Amkua majirani zako. Wakati mwingine, kuna masoko ya mitaani, sherehe za mitaa au mikutano ya majirani.

Kazini, kuna hakika kuwa wenzako ni wazuri. Mnaweza kuzungumza wakati wa mapumziko au mkutane baada ya kazi, kwa mfano kwa matembezi au kinywaji. Hapo ndipo usahibui huanza.

Katika darasa la lugha, utapata waja waliowasili Ujerumani hivi karibuni . Labda utapata wandani wapya hapo. Pia kwenye michezo unaweza kukutana na watu. Michezo hufurahisha zaidi ukiwa na kundi. Katika miji mingi, kuna vikundi vinavyokutana hifadhini wakati wa kiangazi kufanya mazoezi pamoja. Au unaweza kujiunga na chama.

Vyama, Vilabu na Vyuo vya Watu Wazima

Kuna vyama vingi vya michezo nchini Ujerumani. Wewe na watoto wako mnaweza kucheza kandanda, kupiga mbizi, kucheza dansi au kufanya mazoezi ya viungo. Mnaweza kufanya michezo pamoja na wengine. Kuna pia vyama vingine na vilabu. Katika chama, watu hukutana kwa lengo na mapenzi ya pamoja. Kwa mfano kuna vyama vya muziki, vilabu vya vijana, vilabu vya kupika au vya kompyuta. Kuna vyama vya waja wazima na vya vijana.

Katika maeneo mengi, kuna vyuo vya waja wazima. Hapo kuna kozi hasa kwa waja wazima, kwa mfano kozi za lugha, dansi, kompyuta au michezo. Pia kuna kozi za michezo katika vyuo hivi.

Kwa wazazi na watoto, mara nyingi kuna matoleo ya bure. Kwa watoto wadogo, katika baadhi ya maeneo, kuna vikundi vya michezo.

Utamaduni wa Chakula

Kama ilivyo sehemu nyingine duniani, Wajerumani wanapenda chakula kizuri. Kuna vyakula maalum vinavyopatikana tu Ujerumani au katika sehemu fulani tu za nchi hiyo. Karibu kila Mjerumani anajua kuhusu Weißwurst na Brezen – hivi ni vyakula vya kawaida kutoka Bavaria. Kaskazini mwa Ujerumani, waja hula samaki wengi.
Lakini chakula kule Ujerumani pia ni cha kimataifa. Kuna mikahawa ya aina mbalimbali. Katika miji mikubwa, kuna uchaguzi mkubwa sana. Unaweza kula chakula cha Kivietinamu, Kihindi, Kiitaliano, Kituruki au Kiethiopia.

Waja nchini Ujerumani pia hufurahia kukaa na wandani katika vikao vya kahawa na keki. Wakati wa kiangazi, watu huketi nje zaidi.

Maswali Ya Mara kwa Mara

Tufuatilie