In einem offenen Geldbeutel sind Münzen, Geldscheine und Kreditkarten zu sehen. Der Geldbeutel liegt auf einer Zeitung. © Goethe-Institut

Akaunti

Kama unaishi au kufanya kazi Ujerumani, unatakiwa kuwa na akaunti ya benki. Unaweza ukafungua akaunti yako katika mitaa mikubwa yenye benki au benki ya akiba (Sparkasse). Benki nyingi na benki za akiba zina matawi. Kuna benki nyingine unaweza kutumia tu kwa njia ya mtandao. Kwa kawaida unapaswa kulipa pesa kwa ajili ya akaunti benki, ada. Mara nyingi akaunti za benki ni bure kwa shule na wanafunzi wa vyuo vikuu. Kuna aina mbali mbali za akaunti: ukiwa na salio benki unaweza tu kutoa pesa kwenye akaunti ambayo ulishaweka. Ukiwa na akaunti ambayo unaweza ukatoa Zaidi ya salio ulilo nalo (Dispo) unaweza ukatoa pesa hata kama akaunti yako haina pesa. Benki zinaweza kukukopesha pesa hadi kufikia kiasi fulani. Lakini unapaswa kurejesha kiasi cha pesa ulichochukua pamoja na riba. Mara nyingi riba huwa ni kubwa.

Kufungua akaunti - Kontoeröffnung

Je unataka kufungua akaunti? Unaweza ukafanya hivyo kwenye tawi lolote. Lakini benki/benki ya akiba mara nyingi huangalia kitambulisho chako hivyo unapaswa kuonesha kitambulisho chako ama hati ya kusafiria.

Benki nyingi zinakuruhusu kufungua akaunti kwa njia ya mtandao au kwa njia ya posta. Unaweza ukatumia kitambulisho cha posta kwa hili: benki watakutumia fomu. Utachukua karatasi hizo na kitambulisho au hati ya kusafiria na unakwenda katika ofisi ya posta pamoja navyo. Unaweza ukajitambulisha huko. Wakati mwingine unalazimika kutumia kitambulisho cha usajili kwa ajili ya kufungua akaunti pia.

Ein Mann sitzt an einem Laptop und tätigt eine Online-Überweisung. © Goethe-Institut

Malipo ya moja kwa moja ya benki - Überweisung

Unatakiwa kuwa na akaunti ya muda kwa ajili ya kodi na mshahara: mwajiri wako anatakiwa kukulipa mshahara wako kwa kukuwekea pesa benki. Mara nyingi unapaswa kulipa gharama za makazi kwa kupitia benki. Unaweza ukatengeneza mfumo wa malipo yako ya mara kwa mara kupitia benki. Kwa malipo mengine utapata fomu kupitia benki, karatasi ya malipo. Kiasi gani cha pesa unataka kulipa? Nani ni mpokeaji wa hizo pesa? Unatakiwa kuandika taarifa hizi kwenye karatasi ya malipo. Na baadaye utairejesha karatasi ya malipo benki. Je! Unataka kulipa malipo kupitia mtandao? Unapofungua akaunti yako, waeleze unataka kufanya huduma za kibenki kwa njia ya mtandao ama kwa njia ya kawaida.

Tangu mwaka 2004, njia za malipo ya SEPA katika nchi 34 za ulaya ( kama ilivyo mwezi Julai 2018) ili kuhamisha fedha ( Euro) iwezekanavyo. IBAN inawakilisha nambari ya akaunti na kodi ya benki ya BIC. Kwa mfano, IBAN na BIC zinaweza kupatikana kwenye kadi yako ya EC.

Eine Person zieht eine Kreditkarte aus einem Geldbeutel. © Goethe-Institut

Kadi ya EC na kadi ya malipo – EC-Karte und Kreditkarte

Utapewa kadi ya EC kwenye akaunti yako ya muda.kama utapenda, unaweza pia kuwa na kadi ya malipo (mfano: MasterCard, Visa). Mara nyingi benki hutuma kadi ya EC na/au kadi ya malipo kwa njia ya posta. Unapaswa kusaini kadi hizi.siku chache baadae utapokea namba za siri kwa njia ya posta, Unatakiwa kuikumbuka namba ya siri. Unaweza kutoa pesa kwenye mashine zote za kutolea pesa kwa kutumia kadi ya EC. Ili ufanikishe ili unatakiwa kuwa na namba ya siri. Unaweza ukalipa kwa kutumia kitambulisho cha malipo kwenye baadhi ya maduka na kwa njia ya mtandao. Unaweza kulipa kwa pesa taslimu kwenye tawi lako la benki.

Ikiwa umepoteza kadi yako EC au kadi ya malipo au imeibiwa, unatakiwa uzuie kadi zako haraka iwezekanavyo:
Simu ya dharura: 116116

Riba

Utakuwa ukilipwa riba kutoka benki kutokana na akiba iliyopo kwenye akaunti yako. Utapokea kiasi kidogo cha riba kwenye akaunti yako ya muda. Kama unataka kutunza pesa, unaweza ukafungua huduma za kibenki za kudumu au akaunti ya akiba. Pia utakuwa ukilipwa kiasi kidogo cha riba  kuliko ile ya kwenye akaunti ya muda.
 

Video International Sign

Further questions? Write us via the contact form. We will forward your questions anonymously to the advisors of the youth migration services.

Contact form