Maadhimisho ya " Mein Weg nach Deutschland ". Miaka 10 ya usaidizi wa kuwasili Ujerumani

Miaka 70 ya uzoefu katika kujenga madaraja ya kitamaduni kati ya mataifa – Goethe Institut ipo kwa ajili hiyo. Tunaelewa jinsi ujenzi huu wa madaraja ya kitamaduni unavyofanya kazi na vipi mazungumzo na ufikiaji wa lugha mpya hufanya kazi. Na tunafanya kazi zaidi nchini kuliko watu wengi wanavyofikiria.

" Mein Weg nach Deutschland " ilianza miaka 10 iliyopita kwa msaada wa wanandoa waliohamia Ujerumani wakati wa kipindi cha mpito kutoka nchi yao ya asili hadi kuwasili hapo Ujerumani. Hivi sasa tovuti hio ni sehemu ya mradi wa "Ushirikiano wa awali na usimamizi wa mpito - kuhakikisha mchakato wa uhamiaji unafanyika kwa mafanikio", ambao unalenga raia wapya waliohamia kutoka nchi ya tatu wanaokuja Ujerumani kwa sababu za kitaaluma au za kibinafsi.

Kwa msaada wa tovuti ya "Mein Weg nach Deutschland" tumekuwa tukiwarahisishia wahamiaji wapya kuanza maisha Ujerumani kwa miaka 10 sasa. Tunakusaidia kwa taarifa kuhusu kuishi na kufanya kazi Ujerumani katika lugha 30, matoleo ya mazoezi ya Kijerumani bila malipo na anwani za vituo vya ushauri. Kwenye "Mein Weg nach Deutschland" kila kitu kipo katika sehemu moja.


Sie möchten mit uns in Kontakt treten? Sie haben Fragen oder Anmerkungen? Dann schreiben Sie uns eine E-Mail an: mwnd@goethe.de