Colourful books stand in a row on a shelf. © Jamie Grill/Jamie Grill via Getty Images

A

die Ablehnung, die Ablehnungen (Kukataliwa)
Wakati wa taratibu za hifadhi, mamalaka zinaangalia kama mwombaji wa makazi anaweza kubaki au la. Uamuzi hasi unatakiwa uchukuliwe  katika kipindi cha taratibu za hifadhi, mwombaji wa hifadhi atapokea kukataliwa. Kama inafaa, anatakiwa basi kondoka nchini. Kwa mantiki ya kukataliwa, inawezekana kumuona mwanasheria au ofisi ya ushauri na kukata rufaa dhidi ya uamuzi.

die Ablöse (Makazi)
Vipi endapo unapohamia kwenye manzili na mpangaji aliyepita ameacha dhamani zake hapo? Mara nyingi unatakiwa kuzilipia. Hii inajulikana kama makazi. Kwa kawaida, inapatikana kwenye dhamani kubwa na nzito, kama vile kabati. Au kwa dhamani za jikoni, kama vile jiko au jokofu.

das Abschiebehindernis, die Abschiebehindernisse (Marufuku ya kufukuzwa, marufuku za kufukuzwa)
Marufuku ya kufukuzwa ni sababu muhimu kwa nini mwaombaji wa hifadhi haweze kurudishwa nchini mwake. Mfano wa marufuku ya kufukuzwa ni ugonjwa uliokithiri au vita kwenye nchi ya nyumbani.

die Abschiebung, die Abschiebungen (Kuhamishwa)
Inatakiwa uamuzi hasi ufanyike kuhusu ombi la hifadhi, mtu anapaswa kuondoka Ujerumani kwa makataa yaliyoonyeshwa kwenye taarifa ya kukataliwa. Mtu akishindwa kuzingatia wajibu huu, anaweza kuhamishwa kwa lazima. Hii inamaanisha kwamba atachukuliwa na polisi na kurudishwa katika nchi ya asili au kwenye boda ya nchi nyingine. Matokeo ya kuhamishwa ni kwamba atazuiliwa kuingia Ujerumani kwa zaidi ya miaka mitano.

der Abschluss, die Abschlüsse (Sifa, sifa)
Mwishoni mwa kozi, mafunzo au shule, ni muhimu kufanya mtihani. Kama mtu akifaulu mtihani, wanapata sifa. Kuna aina kadha wa kadha za sifa Ujerumani. Sifa ni muhimu kama mtu anataka kufanya kazi au kusoma. Hata hivyo, sio kila sifa zinamfaa mtu kwa kila aina ya kazi au kila kozi za masomo.
 
die Abschlussprüfung, die Abschlussprüfungen (Mtihani wa mwisho)
Mtihani au jaribio mwishoni mwa kozi ya kujifunza au mafunzo ya ufundi. Mwishoni mwa kozi shirikishi unafanya “Jaribio la Lugha ya Kijerumani kwa wahamiaji” (DTZ). Wanafunzi wa kozi shirikishi wanatakiwa kufanya huu mtihani wa mwisho. Taarifa zaidi: BAMF.



der Allgemeinarzt/die Allgemeinärztin, die Allgemeinärzte (Daktari bingwa)
Daktari wa matatizo yote ya kiafya. Kama unaumwa unaenda kwanza kwa DB wako. Kama DB wako hawezi kusaidia, anakuandikia rufaa kwa mshauri wa kitaalamu.

der Alphabetisierungskurs, die Alphabetisierungskurse (Kozi ya kusoma na kuandika )
Kozi kwa watu wasiweza kusoma na kuandika. Kuna kozi maalum shirikishi zinazojumuisha elimu ya kusoma na kuandika. Hii kozi shirikishi inajulikana kama Kozi ya kusoma na kuandika na kwa kawaida inadumu kwa masaa 960.

die Anerkennung, die Anerkennungen (Utambuzi)
Kwa minajili ya uamuzi chanya kuhusu ombi la hifadhi, kuna machaguzi mbalimbali kwa matakwa ambayo BAMF inaweza fikia uamuzi.

Mwombaji anatakiwa kupatiwa hadhi ya ukimbizi au anatakiwa kupewa haki ya kutambuliwa, atapokea kibali cha makazi. Hii inadumu mwanzoni mwa miaka mitatu. Baada ya  hii, ofisi shirikishi itaangalia kibali tena. Wakati wa angalio jipya, kibali cha makazi aidha kitaondolewa au kibali cha kudumu cha makazi kitatolewa.  Yule anayetambulika kwa kupewa haki ya ulinzi kama tegemezi , atapokea kibali cha makazi ambacho kinadumu mwanzoni mwa mwaka mmoja. Inaweza pia kuongezwa kwa muda wa miaka miwili. Baada ya miaka saba, endapo kama mahitaji yamekidhi, kibali cha makazi ya kudumu kitatolewa.

Marufuku ya kufukuzwa inatakiwa iwepo, mwombaji atapewa kibali cha makazi. Hii inadumu angalau kwa mwaka mmmoja na inaweza kuongezwa baadae. Utoaji wa kibali cha makazi ya kudumu inawezekana chini ya mahitaji yanayofanana ambayo yanaombwa kwa ulinzi tegemezi

die Anerkennung ausländischer Abschlüsse (Utambuzi wa sifa ngeni)
Ujerumani kuna kazi mbalimbali ( kwa mfano daktari, mwalimu) ambapo utaweza kufanya kazi tu kama una sifa stahiki. Kufanikisha utambuzi huu, mafunzo ya ufundi na sifa za taaluma za wahamiaji zinaangaliwa. Sifa zinazitangatiwa pamoja na ushabihiano wake na kijerumani, halafu utaruhusiwa kutumia sifa hii kufanya kazi katika taaluma hii Ujerumani vile vile. Kwa taarifa zaidi : BAMF au anerkennung-in-deutschland.de



die Anhörung, die Anhörungen (Kusikia, masikizi)
Kusikia ni sehemu muhimu ya taratibu ya hifadhi. Inaunda msingi wa uamuzi kuhusu ombi la hifadhi. Mwombaji anatakiwa kuonekana mwenyewe katika kusikia. Kusikia sio umma. Muamuzi wa BAMF atakuwepo pia, mkalimani na , kama akiombwa, mtu msaidizi. Huyu mtu msaidizi anaweza kuwa mwanasheria, rafiki au mtu kutoka ofisi ya ushauri kwa mfano,  lakini sio mtu wa taratibu ya hifadhi yeye mwenyewe.
Mtu masaidizi anatakiwa asajiliwe na BAMF mbeleni.
Wakati wa kusikia, mwombaji anatakiwa aelezee hatima yake ya mateso, kwa mfano sababu za kwa nini zilimfanya kukimbia nchi yake. Hivyo, ni umuhimu wa juu kwamba hali binafsi ielezewe na sio hali ya jumla ya nchi yako ya asili. Mtu anatakiwa kuwa na uthibitisho ( makala za magazeti, picha, nyaraka nyingine), hivi vinatakiwa kwa hakika kuoneshwa.

die Anschlussgebühr, die Anschlussgebühren (Tozo ya kuunganishwa)
Hii ni mojawapo ya tozo ya nje ilipwayo katika kuanza mkataba. Pindi ulipapo, unaweza kuanza kupiga simu.

der Ansprechpartner/die Ansprechpartnerin, die Ansprechpartner (Mtoa taarifa)
Endapo kuna maswali maswali na matatizo, mtu ana nafasi ya kumuona mtoa taarifa. Mtoa taarifa anatoa msaada kama kuna maswali au matatizo. Kwa kawaida, mtu hupatikana katika sehemu fulani ya mawasiliano.

der Arbeitgeber, die Arbeitgeber (Mwajiri)
Huyu anweza kuwa kampuni, kwa mfano. Ni mwajiri wa watu wanaofanya kazio pale. Muda mwingine unaweza kupata mssada wa kifedha, kwa mfano kwa ajili  ya nyaraka andishi za ombi la kazi. Kila mji una wakala wa ajira. Unaweza kumpata wakala wa ajira hapa: www.arbeitsagentur.de


der Arbeitnehmer, die Arbeitnehmer (Mwajiriwa)
Unafanya kazi kwenye kampuni na wewe ni mwajiriwa wa kampuni hiyo? Basi wewe ni mwajiriwa.

die Arbeitnehmervertretung, die Arbeitnehmervertretungen (Bodi ya mwakilishi wa mwajiriwa)
Bodi ya mwakili wa mwajiri inawakilisha maslai ya waajiriwa wa kampuni. Kama una matatizo na mwajiri wako, basi unaweza kutafuta msaada kutoka kwa bodi ya mwakilishi wa mwajiriwa. Inapatanisha kati ya waajiriwa na mwajiri. Kuna baraza la kazi au baraza la wafanyakazi. Kwa mfano Kampuni yoyote yenye ukubwa fulani ina baraza la kazi. Pia, kuna vyama vya ushirika ambavyo vipo kwa kujitegemea kwenye kampuni.
 
 
die Arbeitserlaubnis, die Arbeitsgenehmigung, die Arbeitsgenehmigungen(Kibali cha kazi)
Unataka kufanyakazi Ujerumano lakini hutokei katika nchi za umoja wa ulaya(EU)?.Basi unahitaji kibali cha kazi. Wananchi wa  nchi za EU  Romania na Bulgaria wanahitaji pia kibali cha kazi mpaka mwisho wa 2013, lakini sio baada ya hapo. Taarifa zaidi:  www.arbeitsagentur.de

 
die Arbeitslosenversicherung, die Arbeitslosenversicherungen (Bima ya ukosefu wa ajira)
Kama mwajiriwa akipoteza kazi yake, hii bima inalipa uwiano wa mshahara wake kwa mwaka. Waajiriwa wote wana bima ya ukosefu wa ajira . Gharama za sera hufanywa kwa sehemu na mwajiri.

der Arbeitsvertrag, de Arbeitsverträge (Mkataba wa ajira)
Kama upo kwenye ajira ya kudumu utapewa mkataba wa ajira. Ina sheria zote zinahusiana na ajira yako. Kwa mfano: ajira yako inajumuisha majukumu yapi? Unalipwa kiasi gani? Unatakiwa kufanya kazi masaa mangapi kwa wiki? Mapunmziko mangapi unapata? Wewe na mwajiri wako mnasaini mkataba.

die Arbeitsunfähigkeit (Kutokuwa na uwezo wa kufanya kazi)
Huu ni wakati huwezi kufanya kazi. Kwa mfano kama ni mgonjwa au baada ya ajali.

das Arbeitsverbot, die Arbeitsverbote (  Marufuku ya kazi, kazi za marufuku.)
Marufuku ya kazi inamaana kwamba mtu haruhusiwi kufanya kazi kwa muda fulani. Hii inaonyeshwa kwenye karatasi za makazi ( kwa mfano kibali cha makazi ya muda mfupi au uvumilivu).
 
der Arbeitsvertrag, de Arbeitsverträge (Mkataba wa ajira)
Kama upo kwenye ajira ya kudumu utapewa mkataba wa ajira. Ina sheria zote zinahisiana na ajira yako. Kwa mfano: ajira yako inajumuisha majukumu yapi? Unalipwa kiasi gani? Unatakiwa kufanya kazi masaa mangapi kwa wiki? Mapunmziko mangapi unapata? Wewe na mwajiri wako mnasaini mkataba.
 
das Asyl, die Asyle (Hifadhi)
Watu wenye maslai na malengo yanayoendana hukaa pamoja katika vyama au klabu. Kwa mfano, unaweza kucheza mpira na wengine katika klabu ya mpira, au kufanya muziki pamoja katika muziki wa kijamii.

der Asylantrag, die Asylanträge (Ombi la hifadhi, maombi ya hifadhi)
Mtu angependelea kupata ulinzi Ujerumani kama mgeni, ni muhimu kukusanya maombi ya hifadhi. Inaweza tu kufanya maombi hayo Ujerumani.Maombi ya hifadhi yanatakiwa yafanywe binafsi katika ofisi ya shirika la shirikisho Ujerumani la uhamiaji na wakimbizi(Bundesamt für Migration und Flüchtlinge - BAMF).Baadhi ya maswali yataulizwa, miongoni mwao kuhusiana na njia ya kusafiria. Hata hivyo, sababu za hadhi ya mkimbizi hazitajadiliwa katika muda huu. Hili litafanyika katika kusikia. Kwa kufuata kusikia, BAMF wataangalia maombi na kisha watatafanya maamuzi kama mkimbizi atatambuliwa au la. Katika hali za kipekee, maombi ya hifadhi yanaweza kufanywa kwa kuandikwa kwa mkono.

der Asylberechtigte, die Asylberechtigten (Mtu aliyepewa haki ya hifadhi, watu waliopewa haki ya hifadhi).
Mtu aliyepewa haki ya hifadhi alikuwa anatambulika na BAMF  katika taratibu za hifadhi. Mtu aliyepewa haki ya hifadhi,kibali cha makazi kwa miezi mitatu atapatiwa mwanzoni.
der Asylbescheid, die Asylbescheide (Taarifa ya hifadhi, taarifa za hifadhi)
Uamuzi kuhusu maombu ya hifadhi yanaonyeshwa kwenye taarifa ya hifadhi. Kwa hiyo, hadhi ya hifadhi inaelezewa katika taarifa ya hifadhi. Uamuzi unachapishwa katika lugha ya asili ya mwombaji, maelezo kwa kijerumani.

Asylbewerber, die Asylbewerber (Mwombaji wa hifadhi, waombaji wa hifadhi)
Mwombaji wa hifadhi ni mtu ambaye aliyefanya maombi ya hifadhi.

das Attest, die Atteste (Cheti cha matibabu)
Unaumwa na hauwezi kufanya kazi? Basi unahitaji kwa kawaida cheti cha matibabu cha mwajiri wako. Ni kipande cha karatasi unachopewa na daktari wako. Inaonyesha kwamba u mgonjwa na huwezi kufanya kazi. Watoto muda mwingine huhitaji cheti cha matibabu kwa ajili ya shule.

die Aufenthaltserlaubnis, die Aufenthaltserlaubnisse (Kibali cha makazi, vibali vya makazi)
Kwa kuwa na kibali cha makazi, mwombaji wa hifadhi anaweza kubaki Ujerumani kwa muda fulani. Kutegemea kama mwombaji wa hifadhi ameshapewa hadhi ya kulindwa, muda wa uhalili wa kibali cha makazi utatofautiana. Kwa mfano, mtu atapokea kibali cha makazi kama watapokea utambuzi kama mtu aliyepewa hifadhi au hadhi ya ukimbizi. Hii basi ni halali kwa miaka mitatu. Mtu aliyepewa ulinzi tegemezi atapokea kibali cha makazi kwa muda wa mwanzo wa mwaka mmoja. Hii pia inapatikana endapo marufuku ya kukatazwa imehakikishwa. Ukiwa na kibali cha makazi, mtu anakuwa na haki na majukumu mbali mbali.

die Aufenthaltsgestattung, die Aufenthaltsgestattungen (Kibali cha makazi cha muda mfupi, vibali vya vya makazi vya muda mfupi)
Kibali cha muda mfupi cha makazi kinathibitisha mwombaji kuwa yupo Ujerumani kisheria  kwa kipindi cha taratibu za hifadhi. Kibali cha makazi cha muda mfupi sio cheo cha makazi au kibali cha makazi. Kwa mujibu wa hizi, kuna vikwazo.

der Aufenthaltsstatus (Hadhi ya makazi)
Hadhi ya makazi inadhibiti kwa mfano muda gani unaruhusiwa kukaa Ujerumani

der Aufenthaltstitel, die Aufenthaltstitel (Kibali cha makazi)
Kibali cha makazi kinajumuisha taarifa kuhusu muda gani unaruhusiwa kukaa Ujerumani , kwa mfano, au kama unaruhusiwa kufanya kazi Ujerumani. Kama una kibali cha makazi upo Ujerumani kisheria. Hili linaweza kuchukua muundo wa viza.

die Aufnahmeeinrichtung, die Aufnahmeeinrichtungen(Kituo cha mapokezi, vituo vya mapokezi)
Tazama kituo cha mapokezi ya mwanzo.
Kituo cha mapokezi ( pia: malazi ya wakimbizi) ni sehemu ambapo wakimbizi wanapata makazi awali. Vituo vya mapokezi vinaweza kutofautiana.
Kwa kawaida, malazi hayo ni zaidi ya mtu mmoja. Hapa, ni muhimu kutumia kwa pamoja chumba. Muda mwingine, manzili itatolewa.

die Ausbildung, die Ausbildungen (Mafunzo ya kiufundi)
Ni mafunzo ya kiufundi, mtu hupata ujuzi na uwezo katika neneo fulani. Inawezekana k ufanya mafunzo ya kiufundi katika shule ya jimbo, chuo kikuu au kwenye kampuni. Mwishoni mwa mafunzo ya kiufundi, ni muhimu kufanya mtihani. Basi mtu hupata sifa. Mafunzo kazi ni aina maamlumu ya mafunzo ambapo mtu hujifunza kazi za vitendo.

das Ausländeramt, die Ausländerämter (Ofisi ya uhamiaji)
Pia inajulikana kama Ausländerbehörde ( mamlaka ya uhamiaji). Hapa ni ambapo unaenda wakati ukifika kwanza UJerumani, lakini pia kama viza yako inaelekea kuisha muda wake na unatakiwa kuomba kuongezewa.
Mtu yeyete  kwenye ukumbi wa mji atakwambia ofisi ya uhamiaji ipo wapi.

die Ausländerbehörde, die Ausländerbehörden (Mamlaka ya uhamiaji)
Pia inajulikana kama Ausländeramt ( ofisi ya uhamiaji). Hapa ni ambapo unaenda unapofika kwanza Ujerumani, lakini pia kama viza yako inaelekea kuisha muda wake na unatakiwa kuomba kuongezewa.

die Ausreise, die Ausreise (Kuondoka)
Kuonda inamaana kuwa mtu anaondoka mchi ambayo yupo. Muda mwingine, kuondoka kuna lazimishwa.Hii inamaanisha kuwa mtu haondoki nchini kwa hiari. Mfano wa kuondoka kwa kulazimishwa ni kuhamishwa

das Auswärtige Amt (Ofisi ya mambo ya nje)
Pia inajulikana kama Außenministerium. Ofisi ya mambo ya nje ya Ujerumani ni sehemu ya serikali. Wajibu wake ni siasa ya Ujerumani ya mambo ya nje na Ulaya. Hii inamaanisha ina uhusiano na nchi nyingine na mashirika  ya kimataifa. Unaweza kupata taarifa kuhusu kusafiri kuelekea Ujerumani kutoka ofisi ya mabo ya nje.

der Ausweis, die Ausweise (Nyaraka au utambulisho)
Hii nyaraka inathibitisha utambulisho wako. Mifano ya nyaraka za utambulisho ni kadi yako ya utambulisho binafsi au hati ya kusafiria. Lakini leseni yako ya udereva ni nyaraka ya utambulisho pia.

Glossar Sprungnavigation

Glossar Sprungnavigation

B

der Bankeinzug, die Bankeinzüge(Malipo ya moja kwa moja)
Kama ukinunua kitu kwa malipo ya moja kwa moja, muuzaji anaweza kupunguza pesa kwenye akaunti yako. Hii inamaanisha unamhidhinisha kuchukua pesa kwenye akaunti yako. Hakuna tozo zozote kwa hili kama akaunti yako  ipo katika benki nchini Ujerumani. Unaweza kulipa kwa malipo ya moja kwa moja kama ukiagiza bidhaa kwenye mtandao, lakini unaweza pia kulipa kwa sera za bima na kufanya malipo ya mwezi.
 
das Bargeld (Fedha taslimu)
Fedha za noti na sarafu ni taslimu. Unaweza kulipa popote kwa pesa taslimu.
 
die Beglaubigung, beglaubigen(Uthibitisho, kuthibitisha)
Mhimili maalum unaangalia nyaraka na kuziwekea stampu kuthibisha kuwa ni za kweli.
 
die Behörde, die Behörden (Wakala wa serikali , mawakala wa serikali)
Wakala wa serikali ni taasisi ya nchi ambayo inatimiza majukumu yaliyobainishwa na sheria. Kwa hiyo, inaongoza serikali.
 
der Benutzername, die Benutzernamen (Jina la mtumiaji)
Hili ni jina unalojisajili wakati unapotumia tovuti au tarakishi.
 
die Beratung (Ushauri)
Katika kipindi cha ushauri unaweza kuomba ushauri katika mada mbali mbali kutoka kwa wataalamu. Taarifa zaidi: Getting Help
 
der Bereitschaftsdienst, die Bereitschaftsdienste (Huduma za matibabu ya simu)
Unahitaji daktari nje ya masaa- jioni, wakati wa usiku au wikiendi? Kama ni hivyo, unaweza kuwasiliana na huduma za matibabu ya simu. Namba ya simu inafanana kwa UJerumani nzima: 116117. Kwa dharura, usitumie namba hii lakini piga simu ya huduma ya gari la wagonjwa namba 112. Ni namba hiyo inatumika Ujerumani nzima.
 
die Berufsausbildung (Mafunzo ya kiufundi)
Hiii ni pindi unapojifunza kazi. Kwa kawaida mafunzo ya kiufundi hujumuisha sehemu mbili: shule ya biashara na kufanyakazi katika kampuni. Mafunzo ya kiufundi kwa kawaida huchukua miaka 2 na 3.5. Hiyo inategemeana na kazi, lakini pia katika sifa zako za kumaliza shule. Kama una Abitur, mafunzo ya kozi mara nyingi huweza kuwa mafupi.
 
das Berufsinformationszentrum; BIZ (Kituo cha ushauri wa ajira)
Hapa wafanyakazi wanakushauri kuhusu vipengele vyote vya ajira . Tazama: www.arbeitsagentur.de


 
die Berufsoberschule, die Berufsoberschulen (Chuo cha utaalamu)
Unaweza kufanya sifa za juu za kiwacho cha kumaliza shule hapa. Unaweza kwenda chuo cha cha  utaaluma mara baada ya kumaliza mafunzo ya ufundi.
 
die Berufsschule, die Berufsschulen (Shule ya biashara)
Shule ya biashara ni kipengele cha mafunzo ya ufundi. Hapa unajifunza maudhui ya kitaalamu kulingana na taaluma yako. Hata pia, vifaa kutoka nyanja nyingine. Una masomo 8 mpaka 12 kwa wiki. Unatumia masaa yaliobakia kufanya kazi kwenye kampuni. Au unataka kuzuru mafunzo: utatumia wiki chache katika shule ya biashara, halafu unatumia wiki chache kufanya kazi kwenye kampuni.Kwa baadhi ya taaluma nyingine, unatumia mwaka mmoja kwenye shule ya biashara na baadae unatafuta nafasi ya mafunzo ya ufundi kwenye kampuni. Shule ya biashara haigharimu chochote. Unatakiwa ulipie vifaa tu, kama unavyofanya katika shule za kawaida.
 
die Bewerbung, die Bewerbungen (Maombi)
Unataka kuomba ajira katika kampuni? Basi , unatakiwa uandike maombi ya kazi: kwa kawaida hii inajumuisha barua ya ushawishi, wasifu binafsi yenye picha , na vyeti vyako. Sehemu ya pili ya maombi ya ajira ni mahojiano: mwaliko wa kukutana na mwajiri kama maombi yaliyoandikwa yalikuwa mazuri. Taarifa zaidi zinapatikana kutoka kwa employment agency.


die Bewerbungsunterlagen (Nyaraka za maombi)
Hizi zinajumuisha: barua ya ushawishi, kwa maneno mengine ni barua kwa kampuni. Inaeleza kwa nini unataka kazi na kwa nini unafaa kwa hiyo kazi. Pia, hizi nyaraka zinajumuisha picha, wasifu wako binafsi(lahajedwali linaloonyesha sifa zako) na vyeti vyako.
 
die Botschaft, die Botschafte (Ubalozi)
Ubalozi ni kama ubalozi. Ni uwakilishaji wa  nchi katika nchi nyingine. Unaweza kutafuta zaidi kuhusu Ubalozi wa Ujerumani kutoka www.diplo.de

 
die Broschüre, die Broschüren (Kipeperushi, vipeperushi)
Taarifa zilizochapishwa ambazo zinapatika ili uweze kuzichukua.
 
Brutto (Jumla)
Ujira/mshahara wa jumla ni kiasi cha jumla. Unatakiwa ulipe kodi yako na bima kutoka kwa hii. Kiasi kinachobakia ni kiasi kilichobaki baada ya makato
 
das Bundesland, die Bundesländer (Jimbo shirikishi)
Majimbo shirikishi 16 (Bundesländer) kutoka Jamuhuri ya Shirikisho la Ujerumani. Kwa kawaida, nchi shirikishi ni eneo kubwa sana kama vile Bavaria , Hesse au Kaskazini mwa Rhine Magharibi mwa Phalia. Lakini baadhi ya miji huunda jimbo shirikishi katika haki zao, kwa mfano Berlin na Hamburg. Kila nchi shirikishi ina serikali yake (Landesregierung) pamoja na bunge (Landtag). Serikali ya jimbo inaweza kuamua baadhi ya vitu kwa kujitegemea kama vile elimu, mambo yanayohusu utamaduni. Lakini maamuzi mengi muhimu yanafanywa na serikali kuu, kwa maneno mengine , serikali ya Ujerumani nzima.
 
der Bundestag (  Serikali kuu ya Ujerumani)
Bundestag ni bunge la Ujerumani. Vyama vipi vipo kwenye bunge? Hiyo inaamuliwa na watu katika uchaguzi.
 
das Bußgeld, die Bußgelder (Faini)
Dhani kuwa unatembea kwa kupita kwenye taa nyekundu? Au unaendesha baiskeli yako kwenye njia ya waenda kwa miguu? Au kunywa pombe na kuendesha gari lako? Kama polisi akikukamata, utatakiwa kulipa faini. Muda mwingine ni Euro 5 au 10 tu. Lakini muda mwingine ni nyingi zaidi. Muda mwingine utapoteza hata leseni yako ya udereva. Hiyo inamaanisha hauruhusiwi kuendesha gari kwa wakati maalumu.
 

Glossar Sprungnavigation

Glossar Sprungnavigation

C

D

der Dauerauftrag, die Daueraufträge (Amri ya msimamo)
Amri ya msimamo ni aina fulani ya uhamishaji katika benki. Mara nyingi, unalipa kodi kwa kupitia amri ya msimamo: unaweka bayana tarehe ( kwa mfano siku ya kwanza ya mwezi) na unawapa namba ya mwenye nyumba. Halafu benki inahamisha kodi na kuipeleka kwenye akaunti ya mwenye nyumba katika tarehe ile ile kila mwezi.
 
die Deutsche Sprachprüfung für den Hochschulzugang/TestDAF (Mtihani wa Lugha ya Kijerumani wa
Ruhusa ya Kuingia Chuo Kikuu/ Mtihani wa Lugha wa Kijerumani kama Lugha ya Kigeni)
Kama unataka kusoma kwa ngazi ya shahada katika chuo kikuu au chuo cha ufundi, kwa kawaida unatakiwa kuzuingumza kijerumani cha hali ya juu na kufaulu moja ya hii mitihani. Unaweza kufanya mtihani mara kwa mara pindi ukiwa katika nchi yako ya asili. Taarifa zaidi: :



www.testdaf.de

der Deutschtest für Zuwanderer; DTZ (Jaribio la Lugha ya Kijerumani kwa Wahamiaji)
Huu ni mtihani wa mwisho katika kozi shirikishi. Unafanya mtihani mwishoni mwa kozi shirikishi. Hii inathibitisha kuwa unaweza kuongea/kuandika kijerumani kwa ngazi ya A2 au B1.
 
das duale System (Mfumo wa uwili)

Ujerumani inafanyakazi katika mfumo wa uwili kwa mafunzo ya ufundi. Kwa maneno mengine mafunzo ya ufundi yanajumuisha sehemu mbili: vitendo na nadharia. Unajifunza sehemu ya vitendo kwa uzoefu wa mikono katika kampuni. Unafanaya kazi pale kama mwanafunzi na unalipwa pesa au ujira  kidogo.Unaenda katika shule ya biashara kujifunza nadharia.

Glossar Sprungnavigation

Glossar Sprungnavigation

E

die EC-Karte, die EC-Karten (Kadi ya EC)
Unapewa kadi ya EC kama una akaunti katika benki ya mtaa mkubwa /benki za vikoba. EC inasimama kwa ajili ya pesa taslimu ya kieletroniki’’. Kwa hiyo unaweza kulipa kieletroniki kwa kadi ya EC, kwa mfano katika maduka mengi makubwa, stoo za kiidara na maduka ya kitaalamu. Maduka madogo ( duka la kuoka mikate, bucha, muuzaji wa simu) wanachukua pesa taslimu tu. Unaweza pia kutumia kadi ya EC kupata pesa kutoka ATM.
 
die Eheberatung, die Eheberatungen (Cheti cha ndoa  )
Kama una matatizo katika ndoa yako, unweza kwenda kwenye kituo kinachotoa ushauri wa ndoa na ushauri wa familia. Watakusaidia, mshauri mara nyingi ni mwanasaikolojia, huongea na wapenzi wawili. Kila mtu anafanya kazi pamoja kufuta na kutatua tatizo.
 
die Einbürgerung, einbürgern (Uraia)
Hii inamaanisha kuwa unapata utaifa wa Ujerumani.
 
der Einstufungstest, die Einstufungstests (Tathmini ya ngazi ya lugha)
Hili ni jaribio linalotangulia kozi. Shule inaweza kuona upo vizuri kiasi gani. Unafanya jaribio kabla ya kozi shirikishi. Shule ya lugha wanapima ujuzi wako wa kijerumani. Hii inamaanisha kwamba unaweza kuanza kozi kulingana na ngazi yako mwenyewe. Muda mwingine unaweza kufanaya jaribio wakati unapojisali wa kozi shirikishi
 
das Einwohnermeldeamt, die Einwohnermeldeämter (Ofisi ya ya usajili wa wakazi)
Unahamia mji mpya? Basi unatakiwa kujisajili hapa. Kufanya hili unaenda kwenye ofisi ya usajili wa wakazi. Unatakiwa uwe na hati ya kusafiria halali au nyaraka mbadala ambazo zinazothibitisha utambulisho wako.
 
die elektronische Lohnsteuerkarte, die elektronischen Lohnsteuerkarten (Kadi ya kodi ya mapato ya kieletroniki)
Pindi unapoanza kazi, unatakiwa umpe  mwajiri wako namba yako ya kodi. Unaweza kuipata kutoka ofisi ya fedha. Inajulikana pia kama kadi ya kodi ya mapato ya kieletroniki. Mwajiri wako anaitumia hii ilikuhesabu kodi yako. Anapunguza kiasi kutoka kwenye ujira/mshahara wako na anailipa kwenye ofisi ya fedha. Kadi za kodi ya mapato ni kadi halisi zilizotengenezwa kwa karatasi, lakini sasa kila kitu kinafanyika kieletroniki katika tarakishi.
 
der Elternabend, die Elternabende (Jioni ya wazazi)                       
Kuna jioni za wazazi katika nyakati mbali mbali ndani ya mwaka. Unaweza kupata taarifa kuntu kuhusu shule, kuzungumzia siku za mapumziko na safari kishule. Na unaweza kuwafahamu wazazi wengine.
 
das Elterngespräch, die Elterngespräche (Mashauriano ya wazazi)
Miadi na mwalimu shuleni. Atakwambia kuhusu maendeleo ya kitaaluma  na tabia ya mtoto wako shuleni.
 
die Elternvertretung, die Elternvertretungen (Mwakilishi wa wazazi)
Hawa ni wazazi wanaofanya kazi pamoja na chekechea au shule. Mwakilishi wa wazazi anachaguliwa na wazazi wote. Mwakilishi wa wazazi anawasaidi wanafunzi wenye miradi, kwa mfano. Muda mwingine wansaidia kukarabati madarasa au kutengeneza bustani shuleni.
 
die Elternzeit (Likizo ya uzazi)
Wazizi kwenye ajira ya kudumu wanaweza wakachukua likizo ya uzazi: mpaka mtoto akiwa na miaka mitatu  aidha mama au baba anaweza kukaaa nyumbani na kumuangalia mtoto. Inawezekana pia kwa wazazi wote wawili kuchukua likizo ya uzazi. Baada ya miaka 3 wanaweza kurudi kwenye kampuni. Wanalipwa posho ya uzazi kwa miezi ya mwanzo 12.
Ni asilimia 67% ya mshahara baada ya makato uliopokewa awali ( pesa unayopokea kwenye akaunti yako). Lakini baada ya hapo hakuna ujira/mshahara wowote unaolipwa kipindi cha likizo ya uzazi.
 
der Ethikunterricht (Elimu ya maadili)
Katika majimbo mengi ya shirikisho wanafunzi wanaweza kuchagua kati elimu ya dini na elimu ya maadili. Berlin, wanafunzi wote wanatakiwa kuhudhuria masomo ya maadili. Hauhitaji kuwa katika dini mahususi kufanya hili: unajifunza kuhusu dini mbali mbali na kuhusu filosofi.
 
die EU, die Europäische Union (Umoja wa Ulaya)
EU ni muungano wa kiuchumi na kisiasa kati ya nchi za ulaya. Kwa sasa, kuna nchi 27 . Hizi nchi zina kanuni kuu kama vile uhuru, usawa, demokrasia. Na wana soko kuu kwa ajili ya bidhaa na nguvu kazi zao. Wananchi wa moja ya nchi za EU wanaweza kuishi na kufanaya kazi katika nchi yoyote ndani ya EU. Pia, nchi 17 zina sarafu moja, Euro.
 
der Europäische Wirtschaftsraum (Eneo la kiuchumi la ulaya)
Hizi ni nchi zote za Umoja wa Ulaya(EU) vile vile Iceland, Liechtenstein na Norway.

Glossar Sprungnavigation

Glossar Sprungnavigation

F

das Fachabitur (Astashahada ya shule ya ufundi)
Hii ni sifa ya cheti cha kumaliza shule. Unafanya astashahada ya shule ya ufundi kwenye shule ya biashara au shule/chuo cha kitaalamu cha ufundi (Berufsfachschule, Fachakademie au Berufsoberschule). Au kupitia masomo ya mbali kwenye chuo cha ufundi. Zipo aina mbili za Fachabitur.: Fachhochschulreife na Fachgebundene Hochschulreife. Astashahada itakupa sifa kusoma katika vyuo fulani.
 
die Fachhochschule, die Fachhochschulen (Chuo cha ufundi)
Hili ni kama chuo kikuu, lakini imekitwa zaidi kivitendo. Kuna vyuo vya ufundi ambavyo vimejikita katika uhandisi, elimu ya jamii na utaalamu wa kisanaa. Kusoma katika chuo cha ufundi , unahitaji kwa kawaida Abitur au Fachabitur.
 
die Fachoberschule, die Fachoberschulen (Shule za kitaalamu)
Baada ya Realschule unaweza kuhudhuria shule ya kitaalamu. Hii shule imekitwa kwa mafunzo. Kwa mfano, kuna shule zinazobobea kwenye uhandisi au kazi za kijamii. Wanafunzi huhudhuria shule ya kitaaluma kwa miaka 2, katika mkondo wa 11 na 12. Kuna masomo ya vitendo na nadharia  na muda mrefu wa uzoefu wa kazi, kwa mfano kwenye kampuni. Mwishoni mwa kozi hii unaweza kufanya shahada katika chuo cha ufundi.
 
die Fahrscheinkontrolle, die Fahrscheinkontrollen (Uangalizi wa tiketi)
Mwanaume au mwanamke atakuomba tiketi kwenye basi, tram , metro au kwenye reli za mji, au kwenye treni. Kama hauna tiketi, utatakiwa kulipa faini.
 
der Fahrzeugschein, die Fahrzeugscheine (Nyaraka ya usajili wa gari)
Pia hujulikana kama Zulassungsbescheinigung. Hii ni nyaraka iliyosheheni taarifa zote kuhusu gari. Kwa mfano , kufanya( Fiat, VW…), namba ya usajili , mtu anayeendesha gari( mmiliki wa gari). Nyaraka pia hujumuisha taarifa zote za kiufundi kuhusu gari. Unaweza kupata nyaraka  ya usajili wa gari kutoka kwa mamlaka ya usajili wa gari. Hapa ni ambapo unaposajili gari. Unatakiwa ubebe nyaraka ya usajili wa gari muda wote. Lakini hupaswi kuiacha kwenye gari. Kama gari likiibwa, unahitaji nyaraka ya usajili wa gari kwa ajili ya polisi.
 
das Familienstammbuch, die Familienstammbücher (Daftari la familia)
Unapewa daftari la familia pindi unapofunga ndoa. Lina taarifa kuhusu familia, kwa mfano: wazazi wako ni nani? Wanatokea wapi? Lipi jina lako kabla ya kuolewa? Wapenzi wa wazazi wako ni nani? Mpenzi wako ametoka wapi? Una watoto?
 
die Filiale, die Filialen (Tawi)
Hizi ni ofisi za benki kubwa za mtaa na benki za vikoba katika miji mingi Benki nyingi zina ofisi kuu na matawi mengi.
 
die Flatrate, die Flatrates (Kiwango sawia)
Hiyo ni bei- haijalishi muda gani uliotumia kwenye simu au mtandao.
 
die Förderschule, die Förderschulen (Shule za kitaalamu)
Watoto wasioweza kusoma vizuri au ni wasomaji wa taratibu huenda kwenye shule maalumu.
 
der Führerschein, die Führerscheine (Leseni ya dereva)
Kama unaendesha gari, HGV au pikipiki , basi unahitaji leseni ya dereva. Hii nyaraka inaonyesha kuwa umeruhusiwa kuendesha gari , HGV au pikipiki.                                                                                                                          

Glossar Sprungnavigation

Glossar Sprungnavigation

G

die Ganztagsschule, die Ganztagsschulen (Shule zote za siku)
Watoto wanaweza kukaa siku nzima katika shule hii, kwa kawaida mpaka saa 8 au saa 9 mchana. Wanapewa chakula cha mchana na kusaidiwa kufanya kazi zao za nyumbani. Na wanafunzi wanaweza kuchukua kozi maalumu, kwa mfano kujifunza vifaa vya muziki, kufanya michezo au au mchezo wakuigiza. Shule zote za siku za serikali hazigharimu kitu chochote, lakini unatakiwa kulipa ada ya shule kwa shule  zote binafsi za siku.
 
die Garantie, die Garantien (Garantii)
Umenunua kifaa ( kama vile Runinga) na sasa imevunjika? Kwa mantiki hii, una garantii ambayo inamaanisha kwamba unaweza kuirudisha dukani. Duka au mtengenezaji anawajibika kukupa kifaa kingine au kulipia matengenezo. Garantii ni halali tu kwa wakati maalum ( kwa ujumla ni mwaka mmoja, lakini muada mwingine ni miaka kadhaa).
 
die Gebühreneinzugszentrale (GEZ)
Kwa kutumia redio na runinga-hata kupitia tarakishi- inagharimu kitu fulani. Unatakiwa ujisajili na GEZ na kuwalipa.
 
die Geburtsurkunde, die Geburtsurkunden (Cheti cha kuzaliwa)
Nyaraka yenye taarifa kuhusu kuzaliwa kwa mtoto: jina la mtoto, jinsi(mvualana au msichana), tarehe na mahali pa kuzaliwa, majina ya wazazi. Cheti cha kuzaliwa kinatolewa na ofisi ya usajili.
 
das Gehalt, die Gehälter OR der Lohn, die Löhne (Mshahara)
Hii ni pesa ambayo unalipwa kila mwezi kama mwajiriwa mwenye kazi ya kudumu.Unalipwa mshahara wako kama unaumwa au upo mapumzikoni. Mshahara wa jumla unajulikana kama mshahara wa jumla. Unatakiwa ulipe kodi na bima nje ya hilo. Unaobakia ni mshahara wako baki.
 
die Gesamtschule, die Gesamtschulen (Shule ya mchanganyiko)
Hii ni kuunganika kwa Hauptschule, Realscchule and Gymnasium  katika shule moja.Watoto wanachua kozi zinazotofautiana ugumu. Kam mtoto hayupo vizuri katika hesabu , basi atahudhuria kozi yenye uwezo mdogo. Kama mtoto yupo vizuri katika kiingereza , basi atachukua kozi ngumu. Katika shulu ya mchanganyiko , ni rahisi kabisa kuhama kutoka shule moja hadi nyingine. Lakini hazipatikana mahala pote.

die Gewährleistung, die Gewährleistungen ( Dhamana)
Hii ni haki ya kurudisha bidhaa mbaya kwa muuzaji ( kwa mfano idara ya stoo). Unapewa bidhaa mpya au unaweza kurudishwa pesa yako. Unaweza pia kuongea na muuazaji na mkajadiliana juu ya bei ndogo. Ni vizuri kama nado ukiwa na stakabadhi lakini hauihitaji sana.
 
Gewerbeamt, die Gewerbeämter (Ofisi ya vibali vya biashara)
Unataka kuanzisha kampuni yako mwenyewe? Au kufungua duka, mgahawa au Café? Basi unahitaji leseni ya biashara. Unaweza kuipata kutoka kwenye ofisi ya vibali vya biashara.
 
der Gewerbeschein, die Gewerbescheine (Leseni ya biashara)
Je unataka kuanzisha kampuni? Au kufungua duka, mgahawa au café?Basi, unahitaji leseni ya biashara. Unaweza kuipata kutoka ofisi ya leseni za biashara.Unahitaji nyaraka zifuatazo: hati yako ya kusafiria, kibali chako cha makazi na muda mwinginecheti cha kibalio cha polisi. Leseni ya biashara inagharimu kati ya Euro 20 na 60.
 
die Gewerkschaft, die Gewerkschaften(Chama cha wafanyakazi)
Haya ni mashirika ambayo huwakilisha maslai ya waajiriwa.
 
das Girokonto, die Girokonten (Akaunti ya sasa)
Hii ni ni akaunti muhimu ya benki kwa matumuzi ya siku hadi siku. Kwa mfano mshahara wako, pensheni na faida ya mtoto wako zinalipwa kwenye akaunti hii. Na unaweza kulipa bili nyingi kupitia akaunti hii.
 
die Grundgebühr, die Grundgebühren (Malipo ya msingi)
Hizi ni ada ambazo zinatakiwa kulipwa kila mwezi.

Glossar Sprungnavigation

Glossar Sprungnavigation

H

der Hauptschulabschluss (Cheti cha mwisho cha shule kutoka Hauptschule)
Pindi unapomaliza Hauptschule, unafanya cheti cha mwisho cha shule kutoka Hauptschule. Ambayo ni darasa la 9 (miaka 15-16) Baadhi ya majimbo shirikishi pia yana cheti cha kufuzu cha mwisho cha shule(Quali), mtihani mwishoni mwa darasa la 9. Sio lazima kuwa na Quali, lakini  anakusaidia kutafuta nafasi ya mafunzo ya ufundi Ujerumani.
 
die Hausordnung, die Hausordnungen (Sheria za nyumbani)
Sheria za nyumbani zinadhibiti namna ambayo wakazi jengo huishi pamoja. Kwa mfano, sheria: mmoja wa wakazi anatakiwa kusafisha ngazi mara moja kwa wiki. Sheria nyingine inaweza kuwa: watoto wanaweza kucheza kwenye nyasi mbele ya jengo, lakini sio gereji. Sio sheria zote za nyumba ni sawa. Sheria za nyumbani hutolewa kwa kawaida pamoja na makubaliano ya upangaji.
 
die Hebamme, die Hebammen (Mkunga)
Mkunga ni daktari. Amefunzwa ili kuwaandaa  wanawake kujifunguaa na kuwasidia wakati wakujifungua na baada. Anakusaidia maswala yote yanayohusu mtoto wako na anajibibu maswali yako.
 
das Heimatland, die Heimatländer (Nchi ya nyumbani, nchi za nyumani)
Hii ni nchi ambayo kwayo mtu kwa asili hutokea. Hati ya kusafiria inaonyesha nchi gani mtu ametokea, kwa mfano nchi ipi wamezaliwa na wana uraia upi.
 
die Heiratsurkunde, die Heiratsurkunden OR die Eheurkunde, die Eheurkunden( Cheti cha ndoa )
Kama ukifunga ndoa, basi utapewa nyaraka na ofisi ya usajili. Hiko ni cheti chako cha ndoa. Kuna maneno mawili kwa hilo katika kijerumani: Heiratsurkunde” na “Eheurkunde”.
 
das Herkunftsland, die Herkunftsländer (Nchi ya asili, nchi za asili)
Hii ni nchi ambayo mtu kwa asili hutokea. Hati ya kusafiria inaonyesha mtu ametokea nchi gani, kwa mfano nchi gani wamezaliwa na wana uraia upi.
 
das sichere Herkunftsland, die sicheren Herkunftsländer (Nchi salama uliyotokea , nchi salama ulizotokea)
Watu wanaotoka kutoka kwenye nchi zinazojulikana kama nchi salama, ni vigumu kutambulika kama waombaji wa hifadhi Ujerumani. Nchi salama kwa sasa zinajumuisha, nchi za Ulaya(EU), Bosnia and Herzegovina, Serbia, Macedonia, Ghana, Senegal, Morocco, Algeria and Tunisia.

die Hochschulzugangsberechtigung, die Hochschulzugangsberechtigungen (Haki ya upatikanaji wa chuo kikuu, haki za upatikanaji wa vyuo vikuu)
Ili kusoma chuo kikuu Ujerumani , haki ya upatikanaji wa chuo kikuu inahitajika. Mtu hupata haki ya upatikanaji wa chiuo kikuu katika kupata sifa fulani kutoka shuleni. Kwa kuwa na haki ya upatikanaji wa chuo kikuu, inawezekana kusoma katika chuo kikuu chochote Ujerumani. Hata hivyo, Haiwezekani muda wote kusoma kila somo. Kwa baadhi ya masomo, daraja fulani linahitajika.
 
der Hort (Kituo cha kulea watoto baada ya shule)
Watoto wanaweza kukaa hapa baada ya kutoka shule kama wazazi wanafanya kazi. Muda mwengine, wanaweza kwenda pale hata kabla ya kwenda shule. Watotot wanapewa chakula cha machana katika kituo cha kulea watoto baada ya kutoka shule, vile vile kuwasaidia kazi zao za nyumbani.Kwa kawaida watoto wanaweza kukaa happ mpaka saa 8 au 9 mchana.
 

Glossar Sprungnavigation

Glossar Sprungnavigation

I

der Immobilienmakler/Makler, die Immobilienmakler/Makler (Wakala wa nyumba)
Unahitaji msaada kutafuta manzili? Wakala wa nyumba( ambao wanajulikana kama dalali) wanaweza kukusaidia katika ada.
 
die Impfung, die Impfungen (Chanjo)
Magonjwa mengi yanasababishwa na bakteria au virusi. Chanjo ni pindi daktari anapokupa bakteria au virusi wale wale lakini katika muundo dhaifu sana. Chanjo inasababisha kingamwili kujizalisha. Kingamwili hulinda watu dhidi ya bakteria na virusi. Hawataweza tena kupata

Glossar Sprungnavigation

Glossar Sprungnavigation

J

das Job-Center (Kituo cha kazi)
Hapa wanakusidia kutafuta kazi sahihi. Unaweza kupata matangazo ya kazi ya aina zote za ajira hapa. Muda mwingine unaweza kupata msaada wa kifedha, kwa mfano kwa gharama ya nyaraka andishi ya ombi la kazi. Kila mji una kituo cha kazi; tafuta yako kwenye



das Jugendamt, die Jugendämter
Das Jugendamt hilft Kindern und Jugendlichen und ihren Eltern. Es gibt zum Beispiel eine psychologische Beratung bei Problemen in einer Familie. Manchmal sind die Probleme so groß, dass ein Kind nicht mehr in der Familie bleiben kann. Dann sucht das Jugendamt eine andere Familie, die das Kind für einige Zeit zu sich nimmt. Jugendämter haben oft auch Kindergärten/Kitas. In jeder Stadt ist ein Jugendamt. 

Glossar Sprungnavigation

Glossar Sprungnavigation

K

die Kaltmiete, die Kaltmieten (Kodi ya baridi)
Hii ni kodi ukiondoa sitima. Tozo za matumizi hujumuisha viwango vya maji, usafishaji wa ngazi za jumuiya na ukusanyaji wa taka taka. Kileta joto na umeme unaweza kujumuishwa katika tozo hizi, lakini hutofautiana. Muulize mwenye nyumba kipi kinajumuishwa kwenye tozo za matumizi, kipi unatakiwa kulipa mwenyewe. “Kodi baridi” zikijumuishwa pamoja na tozo za matumizi hujulikana kama “kodi ya joto”,
 
der Kaufvertrag, die Kaufverträge (Mkataba wa mauzo)
Kama unanunua bidhaa ya ghali kama vile gari, wewe na muuzaji mnasaini nyaraka inayojulikana kama mkataba wa mauzo. Ni rekodi ya taarifa za ununuzi wako, kama vile bei, tarehe ya kununua n.k
 
die Kaution (Amana)
Mpangaji analipa amana kwa mwenye nyumba wakati anapohama kwenda kwenye malazi mapya. Mwenye nyumba anaweza kutumia pesa hiyo kwa dharura, kwa mfano kama mpangaji halipi kodi. Kwa kawaida, mwenye nyumba hurudisha pesa kwa mpangaji pindi anapohama. Amani sawa ya upeo wa miezi 3 ya kodi ya baridi.
 
die Kinderbetreuung, die Kinderbetreuungen (Uleaji wa watoto)
Umeshapata ajira na sasa unahitaji mtu wa kumwangalia mtoto wako. Kuna machaguzi kadha wa kadha: kwa ujumla, walio chini ya miaka 6 wanaenda kwenye kituo cha kulea watoto au chekechea.Kwa watoto wadogo(chini ya miaka 3), kuna chekechea zinapatikana. Au unaweza kuweka mipango binafsi na mwangalizi wa mtoto. Unaweza kumpeleka mtoto wako asubuhi kwa mwangalizi wa watoto na kumchukua mchana au jioni.
 
der Kindergarten, die Kindergärten (Chekechea)
Watoto wapo pamoja na wengine katika kundi. Watoto wenye umri wa miaka 3 na 6 wanaenda chekechea. Watoto wanajifunza kutoka kwa watoto wa zamani na kutoka kwa walezi. Chekechea nyingi zina eneo la kuchezea kwa nje. Chekechea ya siku zote inajulikana pia kama “kita ( Kituo cha malezi ya watoto) .
 
die Kinderkrippe, die Kinderkrippen (Chekechea)
Uanzishwaji wa watoto wenye miezi michache mpaka miaka 3
 
die Kindertagesstätte (Kita), die Kindertagesstätten (Kitas) (Kituo cha kulea watoto)
Hii ni kama chekechea : watoto wanaweza kukaa hapa siku nzima, kwa kawaida mpaka saa 10 au 11 jioni.
 
der Kredit, die Kredite (Mkopo)
Unataka kununua kitu fulani lakini huna peasa ya kutosha? Basi unaweza kuchukua mkopo kutoka benki, kwa mfano. Benki inakupa kiasi cha fedha kwa muda maalumu. Halafu unatakiwa uilipe pesa kwa riba.                                              
die Kreditkarte, die Kreditkarten (Kadi ya malipo)
Unaweza kulipa pasipo kuwa na pesa taslimu kwa hii kadi. Sio maduka yote yanachukua kadi za malipo.Pindi unapofanya manunuzi mkondoni , unaweza mara kwa mara kulipa kwa kadi ya malipo, vivyo hivyo kwa treni na ndege.
 
die Kündigung, die Kündigungen (Notisi)
Kama ukitaka kusitisha mkataba, unatakiwa utoe notisi. Taarifa hii inatakiwa iandikwe.
 
die Kündigungsfrist, die Kündigungsfristen (Arbeit)) (Muda wa notisi – kazi  )
Kama hutaki kufanya kazi tena kwenye kampuni, unatakiwa ukabidhi notisi. Kwa kawaida unatakiwa utoe notisi ya miezi 3. Kama mwajiri anataka kusitisha ajira yako, anatakiwa pia akupe notisi ya miezi 3. Pia, kuna kufukuzwa kwa papo hapo bila ya notisi. Kwa mantiki hiyo, mwajiriwa anatakiwa kuondoka haraka, kwa mfano kama hataki kufanya kazi.                                                                                                                   
 
die Kündigungsfrist, die Kündigungsfristen (Wohnung) (Muda wa notisi-malazi)
Mpangai anatakiwa kumtaarifu mwenye nyumba kwa maandishi kama anadhamiria kuhama. Kwa kawaida ni miezi 3 kabla hajaondoka. Inatakiwa ifanyike mara kwa mara mwanzoni mwa mwezi. Mwenye nyuma anatakiwa pia kutoa notisi ya muda wa miezi 3 au zaidi.
 
der Kursträger, die Kursträger (Mtiaji wa kozi)
Hizi ni shule za lugha zinazotoa kozi shirikishi.Unaweza kupata taarifa kutoka shule ya lugha au mtandaoni. Mtafuate mtu aliyekaribu nawe katika tovuti ya eneo ya kozi shirikishi ya BAMF .

Glossar Sprungnavigation

Glossar Sprungnavigation

L

der Landtag, die Landtage (Bunge la nchi)
Jamhuri shirikishi ya Ujerumani imegawantika katika majimbo shirikishi 16. Kila jimbo lina bunge lake. Bunge la nchi linaitwa Landtag.
 
die Landtagswahl, die Landtagswahlen (Uchaguzi wa bunge la nchi)
Wanachama wa bunge wanachaguliwa kila baada ya miaka 4 au 5. Hawa ni wanasiasa katika Landtag kwenye jimbo shirikishi.
 
der Lebenslauf, die Lebensläufe (Wasifu binafsi)
Wasifu binafsi unajumuishwa katika nyaraka za maombi yako wakati unapotafuta kazi. Wasifu wako binafsi unajumuisha kwa mfano jina lako, kazi, sifa na uzoefu wowote wa kazi ujuzi maalum( tarakishi? Lugha za kigeni….)



der Lohn, die Löhne (Mshahara)
Hii ni pesa ambayo unalipwa kila mwezi kama mwajiriwa mwenye kazi ya kudumu.Unalipwa mshahara wako kama unaumwa au upo mapumzikoni. Mshahara wa jumla unajulikana kama mshahara wa jumla. Unatakiwa ulipe kodi na bima nje ya hilo. Unaobakia ni mshahara wako baki.
 

Glossar Sprungnavigation

Glossar Sprungnavigation

M

die Meldebescheinigung, die Meldebescheinigungen (Kadi ya usajili)
Nyaraka inayoonyesha anuani yako. Unapata kadi ya usajili kutoka kwa ofisi ya usajili wa wakazi au ukumbio wa mji katika mji ambao unaishi. Kitu unachohitaji ni hati yako ya kusafiria. Kadi ya usajili inagharimu kwa kawaida Euro 5.
 
der Mietspiegel (Kiwango cha kukodisha)
Kiwango cha kukodisha ina wastani wa kodi za makazi katika mji fulani.
 
der Mietvertrag, die Mietverträge (Makubaliano ya upangaji)
Unapanga manzili? Kama ni hivyo, utapewa nyaraka inayojulikana kama makubaliano ya upangaji. Wewe na mwenye nyumaba mnatakiwa msaini makubaliano. Hiyo inakufanya kuwa mpangaji.
 
die Migrationsberatung, die Migrationsberatungen (Huduma ya ushauri wa uhamiaji, huduma za ushauri wa uhamiaji)
Watu wanaopanga maisha katika nchi mpya wanaweza kupata taarifa kutoka kwa huduma ya ushauri wa uhamiaji. Endapo kuna matatizo na maswali, mtu anaweza kuwasiliana na huduma ya ushauri wa uhamiaji. Wanaweza kukupatia masaada kama kuna hali mpya na isiyojulikana. Unaweza kupata huduma ya ushauri wa uhamiaji karibu nawe katika “safari yangu kuelekea Ujerumani “ hapa:



der Minijob/450-Euro-Jobs, die Minijobs/450-Euro-Jobs (Kazi ya ziada )
Kazi ya ziada ni pindi haulipi kodi na unapata upeo wa Euro 450. Unapata moja kwa moja bima ya afya na bima ya pensheni, lakini haijumuishwi kwa wasiokuwa na ajira. Kazi za ziada zinapatikana katika nyanja mbalimbali, kama vile msaada wa kazi za nyumbani, mfanyakazi wa ofisini au dereva. Unaweza kupata kazi ya ziada kupitia kituo cha kazi, kwenye gazeti na kwenye mtandao.

der Mitgliedsbeitrag, die Mitgliedsbeiträge (Mchango wa uanachama, michango ya uanachama)
Katika vyama vingi, ni muhimu kulipa mchango wauanachama. Hiki ni kiasi taslimu cha mwezi au cha mwaka ambacho kinatakiwa kulipwa ili kuweza kushriki katika shughuli za chama.
 
der Mutterschutz (Ulinzi wa kisheria kwa wakina mama wanaofanya kazi)
Hizi ni sheria za kumlinda mama mjamzito na wamama wenye kazi ya kudumu. Sheria muhimu sana ni: mwan ya kuzaliwa. Waanawake haruhusiwi kufanya kazi kwa kipindi fulani kabla na baada ya kuzaliwa kwa mtoto wake. Ujerumani ni wiki 6 kabla ya kuzaliwa na angalau wiki 8 baada ya kuzaliwa. Wakati wa muda huu mwanamke anaendelea kupokea ujira/mshahara wake. Kuna kazi nyingine ambapo mwanamke haruhusiwi kufanya kazi kwa kipindi chote cha ujauzito. Hii inapatikana hasa kwa kazi ambazo unafanya kazi na kemikali dutu.
 

Glossar Sprungnavigation

Glossar Sprungnavigation

N

die Nebenkosten(Tozo za matumizi)
Hizi tozo zinajumuishwa kwenye bei ya kodi ya malazi ( kodi baridi). Kwa mfano, viwango vya maji, umeme kwenye maeneo ya kijamii kama vile ngazi na pishi, ukusanyaji wa takataka, kebo ya runinga. Muda mwingine chombo cha kutoa joto na umeme zinajumuishwa, lakini mara kwa mara zinalipwa tofauti.
 
Netto (net)
Ni mshahara/ujira ukitoa kodi na bima.
 
die Niederlassungserlaubnis, die Niederlassungserlaubnisse (Kibali cha makazi ya kudumu, vibali vya makazi ya kudumu)
Kama mtu ana kibali cha makazi ya kudumu, anaruhusiwa kukaa au kuishi daima Ujerumani. Kwa kawaida , kibali cha makazi ya kudumu kinapatikana kama mtu alikuwa na kibali cha makazi kwa miaka mitatu au mitano na hapokei faida yoyote. Ni muhimu pia kwamba mtu aongee kijerumani vizuri na ana utambuzi wa awali.
 
der Notdienst, die Notdienste (Huduma za dharura)
Waganga na famasia ambao wanafanya kazi jumamosi/jumapili na usiku. Kama ukihitaji msaada wa haraka, waganga na famasia hawa wapo hapo kwa ajili yako.

Glossar Sprungnavigation

Glossar Sprungnavigation

O

P

das Parkhaus, die Parkhäuser (Ugeshaji wa gari kwenye ghorofa)
Miji mingi ina uegeshaji wa magari kwenye ghorofa kwa sababu hakuna nafasi ya kutosha kuegesha gari kwenye mtaa. Kuna ghorofa mbali mbali ambazo unaweza kuegesha gari lako. Kuna tozo ya kuegesha magari hapo. Kwa kawaida, unaegesha gari lako kwenye hifadhi ya gari na unalipa unapoondoka. Kama gari likiegeshwa kwenye ghorofa tu kwa muda mfupi, haigharimu sana. Kama ukiliacha hapo kwa muda mrefu, unalipa zaidi.
 
die Partei, die Parteien (Chama)
Chama cha siasa ni kikundi cha watu wenye matumaini na malengo mamoja. Chama kinatumaini kufanya au kuchochea maamuzi kwa niaba ya nchi. Ni muhimu kwa nchi ya kidemokrasia kwamba kuna vyama mbali mbali vya kisiasa.
 
der Pass, die Pässe (Hati ya kusafiria)
Hii nyaraka inathibitisha utambulisho wa mtu. Hati ya kusafiria ina taarifa binafsi ( jina, umri, ….) na utaifa.  Unahitaji hati ya kusafiria katika nchi yako mwenyewe, kwa mfano kama ukienda kwenye mamlaka. Na unahitaji hati ya kusafiria kusafiri nchi nyingine. Mara nyingi hati ya kusafiria ina taarifa nyingine, kama vile taarifa juu ya viza yako au hadhi ya makazi.
 
das Passwort, die Passwörter (Neno la siri)
Hili ni neno la kodi ya siri kwa kujisajili kwenye tovuti au kwenye tarakishi. Unatakiwa mara kwa mara uitumie pindi unapoingiza jina lako la ktumia. Inalinda taarifa zako binafsi.
 
das polizeiliche Führungszeugnis (Cheti cha kibali cha polisi)
Hii ni nyaraka inayotolewa na mamlaka. Inaonyesha kama una rekodi ya polisi. Waajiri wengi wanataka kuona cheti cha kibali chako cha polisi.
 
das Praktikum, die Praktika (Kazi kwa vitendo)
Kama umependezwa na kazi fulani, unaweza kufanya kazi kwa vitendo kwa mfano katika kampuni au kliniki. Unachangia katika kazi, na unaweza kujifunza mwenyewe kazi katika njia hiii. Kwa kawaida hupokei pesa yoyote wakati wa kazi kwa vitendo. Kipindi cha kazi kwa vitendo hutofautiana kutegemeana na kazi na kampuni.
 
die Probezeit (Kipindi cha kujaribu)
Kwa kawaida una kipindi cha kujaribu wakati ukianza kazi mpya. Wakatika wa kipindi cha kujaribu, wewe na mwajiri manweza kusitisha mkataba kwa notisi pungufu. Wakati wa kipindi hiki mwajiri anakuangalia kwa karibu sana. Anaamua kama akuache kwenye kampuni baada ya kipindi cha kujaribu. Na unaamua kama unataka kuendelea kufanyakazi hapo. Kipindi cha kijaribu kinaweza kuwa mpaka miezi 6.
 
die Provision, die Provisionen (Kamisheni)
Unakodi au unanunua manzili kupitia wakala wa nyumma? Kama ni hivyo, Unatakiwa umlipe wakala kwa huduma hizi. Hii tozo inajulikana kama kamisheni.

Glossar Sprungnavigation

Glossar Sprungnavigation

Q

Uthibitisho wa uzoefu wa kazi
 (die Qualifikationsanalyse, die Qualifikationsanalysen)
Katika uthibitisho wa uzoefu wa kazi, inaangaliwa kama mtu anafaa kwa kazi fulani. Kwa kawaida uthibitisho huu upo katika cheti au katika nyaraka nyingine. Cheti hiko unakipata pindi ukimaliza masomo.
Bado unaweza kufanya uthibitisho wa uzoefu kazini kama haujapata cheti. Hii husaidia katika mazungumzo au itaangaliwa pia kwenye kazi.

Glossar Sprungnavigation

Glossar Sprungnavigation

R

die Rechnung, die Rechnungen(Ankara)
Umenunua kitu na hujaliwa kwa hicho moja kwa moja? Basi unaweza kuwa umeitolea Ankara, kwa mfano kama ukifanaya manunuzi mtandaoni. Basi unahamisha pesa moja kwa moja kutoka kwenye akaunti yako kwenda kwenye akaunti ya kampuni. Kwa kawaida, hakuna tozo za ziada kwa hilo.
 
der Religionsunterricht (Elimu ya dini)
Hili ni somo kwenye shule. Kwa kawaida, ni mafundisho kwa imani za waprotestant na wakatoliki. Katika nchi nyingine shirikishi kuna elimu ya dini katika ukristo wa waorthodox, uyahudi,au hata ubuddha. Kwa waislamu shule nyingi zina mafundisho ya kiislamu kwa kitakishi au kiarabu. Elimu ya dini siyo ya lazima kwa watoto. Hivyo haimaanishi kuwa wana kipindi cha kuwa huru ingawa- kwenye majimbo mengi wanatakiwa kuhudhuria masomo ya maadili badala yake, ambayo inamaanisha kuwa wanafundishwa kuhusu filosofia.
 
die Rentenversicherung, die Rentenversicherungen (Bima ya pensheni)
Kwa kawaida , Ujerumani watu hufanya kazi mpaka umri wa miaka 67. Baada ya hapo wanastaafu. Mpaka kustaafu kwao, watu wanalipa uwiano wa mshahara wao kwenye mpango wa bima ya pesheni kila mwezi. Pindi unapostaaafu, unapokea uwiano wa mshahara wako wako wa awali kila mwezi kutotoka kwenye mfuko wako wa pensheni. Waajiriwa wana mpango wa bima ya pensheni. Mwajiri analipa sehemu ya gharama hizi. Kama sio mwajiriwa, unaweza kuchukua sera binafsi ya pensheni. Watu wengi wana mpango wa pensheni kisheria( inayoendeshwa na nchi) vile vile sera binafsi.
 
das Rezept, die Rezepte (Maelekezo)
Kuna dawa za aina nyingi ambayo unaweza kununua kwenye duka la dawa bila ya maelekezo. Kwa baadhi ya dawa unahitaji nyarika iliyotolewa na daktari. Hii nyaraka ni maelekezo.

Glossar Sprungnavigation

Glossar Sprungnavigation

S

das Schulgeld (Ada ya shule)
Unailipa tu katika shule binafsi, katika shule binafsi unaalipa mara kwa mara pesa nyingi ya masomo.
 
die Schulpflicht (Jukumu la shule)
Ujerumani, ni lazima kuhudhuria shuleni. Hii inamaanisha kuwa watoto na vijana wanatakiwa wahudhurie shule angalau miaka tisa mpaka umri fulani. Hii imetolewa na sheria.
 
die Schwangerschaftsberatung, die Schwangerschaftsberatungen (Ushauri wakati wa ujauzito)
Hiki ni kituo ambacho unaweza kupata ushauri juu ya mambo yote yahusuyo mimba.Kuna vituo kama hiki katika miji mingi. Daktari wako wa uzazi anaweza kukwambia mara nyingi wapi unaweza kuipata, au anaweza kukushauri.
 
die selbständige Arbeit (Ajira binafsi)
Hauna mwajiri. Wewe ni bosi mwenyewe.
 
das Sonderangebot, die Sonderangebote (Ofa maalumu)
Baadhi ya maduka yanauza biza zao kwa viwango maalumu kwa muda mfupi. Hizi bidhaa zinajulikana kama ofa maalumu. Kwa kawaida unapata ofa maalumu kwa haraka dukani. Mara nyingi hupatikana mlangoni.
 
das Sozialamt, die Sozialämter (Ofisi ya usalama wa jamii, ofisi za usalama wa jamii)
Ofisi ya usalama wa jamii ni mamlaka. Kama mtu anahitaji msaada wa kifedha, ofisi ya usalama wa jamii itaangalia kama mtu anakidhi mahitaji ili kupata faida.
 
die Sozialleistung, die Sozialleistungen (Faida)
Watu wanaohitaji msaada wa kifedha wanaweza kuomba faida kutoka ofisi ya usalama wa jamii kwa kuzingatia hali fulani. Kwa msaada huu, wanaweza kuishi katika malazi bora. Bima zao za afya zinajumuishwa na wanaweza kutafuta ajira.
 
die Sozialversicherung, die Sozialversicherungen (Bima ya jamii)
Hii inajumuisha bima ya afya, bima ya pensheni, bima ya ajali na bima ya matunzo.
 
die Sozialwohnung, die Sozialwohnungen (Makazi ya kijamii)
Hili ni aina ya makazi amabayo ni bei nafuu kukodi kuliko malazi ya kawaida. Unaweza kukodi makazi ya kijamii kama una kipato cha chini. Kwa hili, unahitaji cheti cha ustahiki cha makazi ya jamii . Kwa kawaida inapatikana kutoka mamlaka ya manispaa au ofisi ya makazi.
 
die Sparkasse, die Sparkassen (Benki za akiba)
Sparkasse ni kama benki. Lakini siyo binafsi, ni sehemu ya jamii au mji.
 
das Sparkonto, die Sparkonten (Akaunti ya akiba)
Hii ni akaunti ya muda mrefu. Hauwezi kuitumia kuhamisha pesa ( kama vile kodi yako: kwa hilo, unatumia akaunti yako ya sasa). Unalipwa riba nyingi kwenye  pesa za akaunti ya akiba kuliko kwenye akaunti ya sasa. Kwa ujumla,pesa kwenye akaunti kwa muda mrefu , hilo ni jambo la akaunti ya sasa.

die Spielgruppe, die Spielgruppen (Kikundi cha mchezo)
Hapa ni ambapo wanafunzi huwa pamoja na kucheza. Mama na baba zao kwa kawaida hukaa nao. Muda mwingine mtu mzima mwingine anaongoza kundi na kucheza na watoto.
 
die Sprachförderung (Msaada wa lugha)
Watoto wanajifunza kuongea kijerumani vizuri kupitia michezo maalum, hadithi na nyimbo. Mara nyingi kuna msaada maalum wa lugha kwenye chekechea na vituo vya malezi (Kita) vya watoto wakigeni.
 
der Sprachtest, die Sprachtests (Jaribio la lugha)
Watoto mara nyingi hufanya jaribio kwenye chekechea/ kituo cha malezi (Kita). Wanaweza kutathmini namna gani mtoto amekwisha na umilisi wa lugha.
 
die staatliche Schule, die staatlichen Schulen (Shule ya jimbo)
Ujerumani shule nyingi zinendeshwa na jimbo. Haulipi ada , ni bure.
 
das Standesamt, die Standesämter (Ofisi ya usajili)
Unataka kufunga ndoa? Una mtoto? Unataka kutalikiana? Basi unatakiwa uende ofisi ya ysajili kwenye mjio wako.
 
die Studiengebühren (Ada)
Hii ni pesa unayolipa unapohudhuria chuo kikuu au chuo cha ufundi (FH). Kuna ada katika baadhi ya majimbo shirikishi, lakini kiwango hutofautiana.
 
das Studium (Shahada ya chuo kikuu  )
Unahitaji kuwa na shahada kwa baadhi ya taaluma, kama vile mhandisi au mwalimu. Unaweza kusoma kwenye chuo kikuu au chuo cha ufundi.
 

Glossar Sprungnavigation

Glossar Sprungnavigation

T

das Tagesgeldkonto, die Tagesgeldkonten (Akaunti ya fedha ya siku)
Hii akaunti sio kwa matumizi ya kila siku kama akaunti ya sasa. Kama una pesa zozote za ziada unaweza kuzitunza kwenye akaunti ya fedha ya siku. Benki hulipa kiwango kikubwa cha riba kwenye akaunti ya fedha ya siku kuliko kwenye akaunti ya sasa au akaunti ya akiba. Unaweza kutoa pesa kwa taarifa fupi pia.
 
die Tagesmutter, die Tagesmütter (Mwangalizi wa watoto)
Waangalizi wa watoto wanawaangalia watoto majumbani kwao. Kuna waangalizi wa watoto wa kiume. Watoto kadhaa huhudumiwa mara nyingi na mwangalizi wa watoto. Waangalizi wa watoto wanatakiwa wawe wamepata mafunzo mahususi na unatakiwa kuwalipa.
 
die Teilnahmeberechtigung für den Integrationskurs (cheti cha ustahiki kwa kozi shirikishi)
Hii ni nyaraka ambayo unatakiwa kusajili katika kozi shirikishi. Kwa kawaida unaipata kutoka ofisi ya uhamiaji katika mji ambao unaishi. Wananchi wa EU wanaweza kufanya kozi shirikishi pia, lakini wanatakiwa kuomba kwa BAMF.



die Teilzeitarbeit(Kazi ya muda wa ziada)
Una kazi ya kudumu, lakini hufanyi kazi massa 8 kwa siku, haufanyi kazi sana- labda saa 4 kwa siku. Wanawake wenye watoto wadogo mara nyingi hufanya hivyo. Unaweza kufanya kwa ziada katika kampuni nyingi.


Kiwango cha mshahara rasmi (der Tariflohn, die Tariflöhne)
Katika kazi nyingi, wafanyakazi hulipwa katika kiwango fulani cha mshahara. Kiasi hiki cha mshahara kimejadiliwa na waajiri na vyama vya wafanyakazi. Mshahara katika kazi hizi haupaswi kuwa chini kuliko kiwango cha mshahara rasmi.

Glossar Sprungnavigation

Glossar Sprungnavigation

U

das Übergabeprotokoll, die Übergabeprotokolle (Orodha)
Umekodisha manzili na unataka kuhamia.Lakini kitu fulani kwenye manzili kimevunjika . Wewe na mwenye nyumba mnatakiwa kuinakili kwenye orodha, ambayo mnatakiwa msaini.
 
die Überweisung, die Überweisungen (Rufaa ( kwa dakatari) )
Unaumwa na unahitaji nushauri wa kitaalamu wa kimatibabu? Daktari wako wa jumla atakupa nyaraka inayojulika kama rufaa ili uweze kumuona mtaalamu.
 
die Überweisung, die Überweisungen (Uhamishaji)
Benki inatuma pesa kutoka akaunti moja hadi nyingine. Kwa mfano kulipa kodi ya malazi yako. Pesa inahitajika iende moja kwa moja kutoka kwenye akaunti yako hadi kwenye akaunti ya mwenye nyumba. Unaijulisha benki, na watahamisha pesa kwenda kwenye akaunti ya mwenye nyumba.
 
der Umtausch (Kubadilishana au kurudi)
Umenunua kitu na ungependa kukirudisha? Katika maduka mengi, unaweza kurudisha bidhaa kwa malipo tena. Hii inamaanisha unarudishiwa pesa. Muda mwingine, haurudishiwi pesa yako, lakini unaweza kuchagua kitu kingine kutoka kwenye duka. Hiyo inajulikana kama kubadilishana. Mara nyingi, hauwezi kurudisha bidhaa za ofa maalumu.
 
die Unterrichtsstunde, die Unterrichtsstunden (Somo)
Somo katika kozi shirikishi linadumu kwa dakika 45.
 
der Urlaub (Mapumziko)
Una idadi maalum ya siku za mapumziko kila mwaka. Ujira/mshahara wako bado unalipwa kipindi cha mapumziko yako. Unatakiwa uongee na mkuu wako wa kazi , lini unaweza kupata mapumziko. Ujerumani watu kwa kawaida hufanya kazi siku 5 za wiki. Kwa hiyo, kama unataka kuchukua mapumziko ya wiki  ( kutoka jumatatu mpaka jumapili) unahitaji likzo ya siku 5.

Glossar Sprungnavigation

Glossar Sprungnavigation

V

die Verbraucherzentrale, die Verbraucherzentralen (Kituo cha ushauri wa mteja)
Hiki ni kituo cha taarifa kwa wateja. Mteja ni mtu ambaye ananunua kitu.Kituo cha ushauri wa mteja kinatoa taarifa kuhusu bidhaa mbalimbali na kinasidia juu ya matatizo ya kisheria( kwa mfano, kama umenunua bidhaa ambayo imebadilika na kuwa mbovu  na duka linakataa kuichua. Kwa mantiki hii, kituo cha huduma ya mteja inaweza kusaidia.)
 
der Verein, die Vereine (Chama)
Watu wenye maslai na malengo yanayoendana hukaa pamoja katika vyama au klabu. Kwa mfano, unaweza kucheza mpira na wengine katika klabu ya mpira, au kufanya muziki pamoja katika muziki wa kijamii.
 
die Verfassung, die Verfassungen (Katiba)
Katiba ni nyaraka. Inabeba sheria muhimu na kanuni za nchi: Namna gani nchi inavyopangwa? Haki na wajibu upi wananchi wanao katika nchi?....Katiba ya Ujerumani inaitwa Grundgesetz.
 
die Versicherung, die Versicherungen (Bima)
Unalipa pesa ya sera ya bima kila mwezi au kila mwaka kwa hali fulani. Hii inamaanisha unapewa bima kwa hiii hali. Kwa mfano ugonjwa: unalipa malipo ya mwezi kwa ajili ya bima yako ya afya. Basi u mgonjwa na unahitaji kumuona daktari.  Kwa hali hii kampuni ya bima ya afya hulimlipa daktari, sio wewe.
 
das Visum, die Visa (Viza)
Unaruhusiwa kusafiri nchi tofauti tofauti ukiwa na viza. Unaweza kuomba viza kwenye ubalozi wa  nchi.
 
die Volkshochschule, die Volkshochschulen (Kitengo cha elimu ya watu wazima)
Watu wazima na vijana wenye umri wa 16+ wanaweza kuchua kozi katika kitengo cha watu wazima. Kozi hazigharimu sana. Unaweza kujifunza lugha ikiwemo Kijerumani-Kupigaji picha , kutengeneza vito, kucheza, kuchora na zaidi. Pia, kuna kozi zilizojika katika taaluma kama vile

der/die Vorgesetzte, die Vorgesetzten (Mkuu wa kazi )
Mkuu wako wa kazi ni kiongozi wako bora, mkuu wa kazi anawajibika kwako na kazi yako kipindi cha masaa ya kufanya kazi. Anasema kazi gani utapangiwa na namna unatakiwa kuifanya. Kwa kawaida mkuu wako wa kazi ana mkuu wake wa kazi pia.

die Vorsorgeuntersuchung, die Vorsorgeuntersuchungen (Kuangalia afya zuizi )
Hujumuisha maangalio 10 ya mara kwa mara ya  watoto yanayofanywa na daktari wa watoto. Ni bure. Angalio la kwanza ni mara baada ya kuzaliwa, la mwisho ni kabla mtoto hajaanza shule.
 
das Vorstellungsgespräch, die Vorstellungsgespräche (Mahojiano ya kazi)
Umeomba kazi ? Mwajiri anapendezwa na ombi lako? Basi atapendelea kukufahamu na kupata maelezo zaidi kuhusu wewe. Anakualika kwenye mahojiano. Unaweza kupata taarifa za jumla kuhusu mahojiano ya kazi kutoka kwa wakala wa ajira au kituo cha kazi.

Glossar Sprungnavigation

Glossar Sprungnavigation

W

der Wochenmarkt, die Wochenmärkte (Soko la wiki)
Miji mingi ina masoko mara moja au mara mbili kwa wiki. Ni katika sehemu ya soko kuu au katika jengo kubwa. Wauzaji wengi ni wa kawaida, sokoni unaweza kupata matunda freshi na mbogamboga za majani, vile vile maziwa na jibini, samaki na nyama. Muda mwingine unaweza kununua nguo hapa.
 
der Wohlfahrtsverband, die Wohlfahrtsverbände (Shirika la ustawi, mashirika ya ustawi)
Shirika la ustawi huhusu haki za jamii Ujerumani. Kuna mashirika ya ustawi katika jamii ndogo ndogo lakini pia katika miji  mikubwa. Watu wengi hufanyakazi hapa kwa kujitolea. Kwa mfano, wanatoa msaada kwa wakimbizi. Kama mkimbizi ana maswali, anaweza kuwasiliana na shirika la ustawi la karibu. Hapa, anaweza kupata taarifa muhimu na msaada endapo kuna matatizo.
 
das Wohngeld (Faida ya makazi)
Ni kodi ya manzili ya kawaida nyingi zaidi kuliko unavyoweza kuimudu? Kama ni hivyo, ofisi ya makazi inaweza kusaidia, kwa mfano kwa kukupa faida ya makazi au kukupatia makazi ya jamii. Ofisi ya makazi itajibu pia maswali mengine yoyote unayoweza kuwanayo kuhusu malazi.
 
das Wohnungsamt, die Wohnungsämter ( Ofisi ya makazi)
Kodi ya manzili ya kawaida ni kubwa kuliko unavyoweza kumudu? Kama ni hivyo, ofisi ya makazi inaweza kusaidia, kwa mfano kwa kukupa faida ya makazi au kukupa makazi ya kijamii. Ofisi ya makazi itajibu pia maswali mengine yoyote unayoweza kuwa nayo kuhusu malazi.

Glossar Sprungnavigation

Glossar Sprungnavigation

X

Y

Z

das Zahlungsmittel, die Zahlungsmittel (Njia ya malipo)
Kuna njia tofauti tofauti za malipo: kwa mfano fedha taslimu, kuhamisha pesa katika benki, kadi ya EC , kadi ya malipo na Ankara.
 
das Zeugnis, die Zeugnisse (cheti)
Vyeti vinajumuishwa katika nyaraka zako za maombi wakati unatafunza kazi. Unaweza kuwa vyeti vinavyotoa kumbukumbu ya kazi. Vintoa maelezo ya ajira yako ya zamani. Na kuna vyeti vya shule na chuo kikuu: Nyaraka rasmi zinatolewa na shule yako au chuo kikuu chako. Kama una vyeti kutoka nchi yako mama , unatakiwa kuwa navyo vikiwa vimetafsiriwa na kuthibitishwa.
 
die Zinsen (Riba)
Una pesa kwenye akaunti yako? Basi utalipwa fedha kiasi na benki kila mwezi. Hiyo inaitwa riba. Umechukua mkopo kwenye benki? Basi unatakiwa uilipe benki kiasi cha fedha kila mwezi kwa hilo. Hiyo ni riba vile vile.
 
die zweisprachige Schule, die zweisprachigen Schulen (Shule za lugha mbili)
Masomo yapo kwa lugha 2, kwa kawaida ni Kijerumani na lugha nyingine.
 

Glossar Sprungnavigation

Glossar Sprungnavigation