Seitliche Ansicht auf einen jungen Mann der vor einem Schild an einem Gebäude mit der Auschrift © Goethe-Institut

 Inafanyaje kazi?

Je, unatafuta watoa kozi shirikishi ofisi ya uhamiaji au huduma za ushauri kuhusu uhamiaji katika mji wako nchini Ujerumani? Utapata anuani katika kipengele hiki. Ingiza msimbo wa mji unaoishi nchini Ujerumani, au nenda chini yake kisha bonyeza  . Halafu utawaona watoa kozi shirikishi wote, ofisi za uhamiaji na watoa huduma za ushauri kuhusu uhamiaji. Hufahamu anuani ya posta? Basi andika jina la mji unaoishi.

Je una swali au tatizo? Unahitaji majibu au maelekezo? Katika kipengele cha ushauri utapata watu watakaokusaidia. Washauri hawa watafahamu majibu ya swali lako, au watafahamu wapi utakapopata msaada.

Vipi kama hauhitaji kwenda kwenye eneo la ushauri peke yako? Basi waweza kwenda na mtu kama vile mume au mke, mpenzi au mtu mwingine. Vituo vingi vya ushauri pia wanaruhusu uweze kuwapigia simu. Hapo washauri watajibu swali lako kwa njia ya simu. Pia kuna huduma za ushauri wa mtandaoni, unaweza kuuliza swali lako kwa njia ya barua pepe.

Huduma za ushauri hazitaji majina: washauri wanajadili tu maswali na matatizo yako pamoja nawe. Hawaruhusiwi kumwambia mtu meingine yeyote maswali na matatizo yako. Ushauri vilevile huwa wa upande wowote: washauri huhitaji kukusidia wewe. Unaweza kuwaambia vitu vya siri. Hakuna haja ya kuogopa. Mara nyingi huduma za ushauri ni bure pia. Hutakiwi kulipia msaada wowote unaoupata. Wakati mwingine wanaweza kukusaidia papo hapo lakini mara pengine utatakiwa kuwajulisha kabla.
 

Je, kuna huduma zozote maalum za ushauri  kwa ajili yangu?

Huduma maalum za ushauri zipo kwa ajili ya wahamiaji. The migrationsberatungfur erwachsene Zuwanderer (MBE) (Ushauri wa uhamiaji kwa wahamiaji watu wazima) na Jugengmigrationsdiente (JDM) (Huduma za uhamiaji kwa vijana) ni za siri, za upande wowote na za bure. MBE itawasaidia wahamiaji wote walio  watu watu wazima na JDM itawasaidia vijana wenye umri kati ya miaka 12 na 27 na wazazi wao. Hapo washauri huzungumza lugha mbalimbali. Vipi kama mshauri hazungumzi lugha yako na wewe huwezi vizuri Kijerumani? Hapo mkalimani atakusaidia. Yeye anazungumza lugha zote mbili.
 

Nitawauliza nini washauri?

JDM na MBE watakusaidia maswali na matatizo yako yote kuhusu kuishi Ujerumani. Kwa mfano nitaishi Ujerumani kwa muda gani kwa viza yangu? Nitapata wapi msaada iwapo nina matatizo ya kifamilia? Nitajifunza wapi Kijerumani? Nitapata wapi malazi? Naweza kufanya kazi Ujerumani? Nitapata wapi kazi? Nitafanyeje ikiwa nina tatizo la kifedha? Nitafanyeje ikiwa ninaumwa? Nani atakayenisaidia ikiwa nina mtoto? Nitapata wapi leseni ya udereva? Tiketi gani ya treni niniyotakiwa kuwa nayo? Ni wapi ambapo vyeti vyangu vitathibitishwa?. Kwa umahususi JDM  pia husaidia kwa maelekezo mashuleni na katika mifumo ya mafunzo ya ufundi.


Tayari niko Ujerumani. Nitapataje huduma ya ushauri?

Tayari uko Ujerumani na unajaribu kuwasiliana huduma za ushauri wa uhamiaji? Unaweza kupata anuani ya huduma za ushauri wa uhamiaji (MBE au JDM) karibu na eneo lako, chini ya kichwa anuani muhimu (important addresses) kisha utaona matokeo na taarifa kama vile anuani na namba ya simu kwenye ramani.


Bado niko nchini  kwangu. Je, kuna huduma yoyote ya ushauri ninayoweza kuwasiliana nayo?

Unatafuta kituo cha ushauri kabla ya kuwasili Ujerumani? Kuna huduma ya ushauri mtandaoni kukidhi hilo. Bonyeza tovuti ushauri wa mtandaoni (online advice). Utapata taarifa zaidi hapo.