Ein Mann sitzt auf einer Steintreppe im Freien. Er hat den Kopf nach unten gesenkt und wirkt betrübt. © Goethe-Institut
Shirika huru  la Taifa la Kupambana dhidi ya unyanyasaji ( ADS) ni mamlaka ya Ujerumani. Linasaidia watu ambao hawakupata mwanya wa  kutetea  haki zao dhidi ya ubaguzi. Matatizo yake yanaweza kupelekewa na rangi au kujikita katika ukabila, jinsia, dini au imani , ulemavu, umri au utambulisho wa jinsia. ADS inatambua uwezekano wa hatua za kisheria katika mfumo wa kanuni za kisheria kwa ajili ya ulinzi dhidi ya hasara na kutoa ushauri kwa mashirika mengine.

Ubaguzi uliojikita katika rangi , asili za ukabila ni wa kawaida sana. Ulinzi wa sheria ya usawa wa matibabu unafanyakazi kwa wote, bila kujali hadhi yao ya makazi,  yaani hata kwa wakimbizi na wageni. Inashughulikia hasa maeneo ya kazi, makazi na huduma.

Mazoea ya ubaguzi katika mchakato wa viza

Visawie? Ni chama cha mashirika mbalimbali ambayo huwataarifu watu kuhusu visa au vibali vya kusafiria. Wamejidhatiti katika utoaji wa Visa wa haki na uwazi na kutoa habari muhimu , blogu na msaada.