Ansicht von vorne auf einen orangenen Rettungswagen mit der Aufschrift © Goethe-Institut

Nambari muhimu zaidi kwa dharura

Nambari zote za dharura ni bure na zinaweza kupigwa bila ya fedha/ salio kwenye simu.

Polisi: 110
Polisi wanawajibika kwa dharura zote zisizo za kimatibabu, uhalifu na ajali kubwa za barabarani.
Andika jina lako na

  • Ilitokea wapi
  • Kilichotokea
  • Watu wangapi wameathirika
  • Ni majeraha gani yaliyopo
  • Subiria  maswali 
Nahaufnahme auf ein Polizeiauto von der Seite mit dem Schriftzug "Polizei" © Goethe-Institut

Idara ya zima moto/ huduma ya dharura/ uokoaji: 112
112 ni namba inayotumiwa kwa hali za kutisha za maisha kama vile mstuko wa moyo , kiharusi, au ajali kubwa.  Endapo una mashaka juu ya ukubwa wa kuumia , usisite kuwahadharisha watu wa ambulensi.  Gari hilo la ambulensi linaweza kuokoa maisha kwa dharura.

Ansicht auf das geschlossene Tor eines Feuerwehrgebäudes, durch die Fenster ist ein Feuerwehrauto sichtbar. © Goethe-Institut
 
Huduma ya dharura ya matibabu: 116117

Kwa dharura unaweza kuwapigia huduma ya dharura hata wikiendi .
Unaweza kwenda moja kwa moja kwa kituo cha dharura cha mazoezi. Vituo hivi vya dharura vya mazoezi vimeunganishwa na hospitali na hufunguliwa hadi saa nne usiku na katika sikukuu za umma.
Vinginevyo, unaweza kupiga nambari ya simu 116117. Simu hii ni bure na inapatikana nchini kote.  Hapa unaweza kupelekwa kwa daktari wa karibu.  Iwapo kutembelea nyumbani kuna hitajika , ofisi kuu itaandaa.
 
Huduma ya dharura kwa ajili ya meno: 01805/986700
Hapa mtu hupokea nambari za simu za watoa huduma na hupiga simu moja kwa moja hapa

Man sieht den oberen Teil eines grauen Gebäudes mit einem Schild, das ein rotes Kreuz auf weißem Grund zeigt. © Goethe-Institut
 
Watoto
Kimsingi, kwa watoto vigezo na nambari zilezile hutumika kama za watu wazima.
Katika kushughulikia watoto, ni muhimu pia kujua kanuni muhimu za maadili ili kutoa muamko kwa haraka na kwa usahihi. Kwanza kabisa, unapaswa umfariji mtoto baada ya kuanguka na kumtuliza. Ni muhimu kudumisha utulivu wa akili ili kumpatia huduma mtoto kwa haraka, cha zaidi usiwe na wasi wasi juu yake. Piga kwa usahihi simu za dharura kama kuna umuhimu. Boxi kamili la huduma ya kwanza linatakiwa kupatikana nyumabani ili kufunika vidonda kwa bandeji au sehemu iliyovunjika ya wazi ili kukitibu kidonda hicho kwa dawa inayopambana na vijidudu.
 
Simu ya watoto na vijana: 0800/1110333
Kwa matatizo ya watoto na vijana, wasiwasi wa tovuti na unyanyasaji wa kijinsia.
 
Simu ya wazazi: 0800/1110550
Kwa masuala ya elimu , wasiwasi juu ya tovuti, unyanyasaji wa kijinsia wa watoto na matatizo yote ambayo wazazi wanayo kuhusu watoto wao.
 
Simu ya msaada “ vurugu dhidi ya wanawake” 08000/116016
Huduma ya kitaifa ya ushauri kwa wanawake walioathirika na vurugu, mazingira yao ya kijamii na wafanyakazi wasomi. Huduma hii inapatikana bila malipo, na kutojulikana , kwa muda wote wa siku 365 kwa mwaka.
 
 
Simu ya msaada kwa wajawazito wenye uhitaji ( haijulikani na salama): 0800/4040020.
 
Simu ya ushauri: 0800/1110111

Ikiwa kuna matatizo na migogoro , k.m masuala ya ushirikiano, unyanyasaji shuleni au kazini, kupoteza kazi, ulevi, ugonjwa, upweke, migogoro na masuala ya kiroho yanaweza kupigiwa simu hapa
 
Simu ya dharura: 116116
Ili kuzuia EC na kadi  za malipo pamoja na kadi za utambulisho , k.m iwapo zimeibwa au kupotea.