Ein Fahrrad mit zwei Körben ist gefüllt mit Einkäufen. © Goethe-Institut

Manunuzi kwa bidhaa za kila siku 

Kuna Supamaketi katika miji yote ya ujerumani na pia katika baadhi ya vijiji. Unaweza kupata mahitaji mengi ya muhimu kwa ajili ya kutosheleza mahitaji yako ya kila siku. Mikate na nyama, maziwa ya mgando na chokoleti ,vifaa ya kusafishia nyumba na karatasi za chooni. Kwa kawaida Supamaketi zinafunguliwa kuanzia saa moja asubuhi hadi saa mbili jioni. Unahitaji kununua chakula kisafi? Miji mingi ina masoko ya wiki mara moja au mara mbili kwa wiki. Kwa kawaida huwa ni jumapili. Kwenye masoko ya wiki unaweza kununua matunda, mboga za majani na vibobezi vya kanda husika.

Unaweza kupata nyama safi na nyama baridi buchani (inajulikana kama Metzgerei ujerumani ya kusini). Unaweza kununua mikate kwa waokaji. Baadhi ya waokaji, bucha na manunuzi madogo madogo kwa ajili ya chamcha chako. Kwa kawaida yanakuwa wazi mpaka saa 12:00 au 12:30 jioni. Masoko ya wiki kwa kawaida yanakuwa wazi kuanzia asubuhi hadi mchana. Maduka yote yanafungwa siku ya jumapili.

Auf einem Tisch liegen in einem Beutel verschiedene Gemüsesorten, Obst und andere Einkäufe © Goethe-Institut

Huduma za kila siku 

Kma hutaki kuondoka kutoka nyumbani kwako kwenda dukani, unaweza kutumia huduma za kuagiza. Unaweza kuwapigia watu wa huduma za kuagiza au kujaza fomu kwenye intaneti. Kisha atakuletea pizza au maji ya madini mpaka nyumbani kwako. Ijapokuwa huduma hii inagharimu kuliko kwenda kununua mwenyewe bidhaa hizi dukani. Vijiji vingi havina maduka, lakini wafanyabiashara wa mawasiliano wanakuwepo mara kwa mara kwa ajili ya huduma. Wanauza vyakula, maji na bidhaa za kila siku.
 

Maduka maalumu na intaneti 

Kama unataka kununua kabati, kompyuta au jozi za viatu kwa mfano unaweza kwenda kwenye stoo ya idara husika au duka maalumu kwa bidhaa hizo. Maduka haya maalumu makubwa yanakuwa na bidhaa tofauti tofauti. Kwa mfano kuna maduka ya samani, ya vifaa vya umeme ama maduka ya viatu. Muda wa kufungua  kwa kawaida huwa ni kuanzia saa 12:30 asubuhi hadi saa 2 jioni.

Siku hizi unaweza kupata vitu vingi sana kwenye intaneti. Kwa kawaida unatakiwa kusubiri kwa siku kadhaaa kabla ya bidhaa zako kukufikia nyumbani kwako.

In einem Möbelhaus sieht man ein eingerichtetes Wohnzimmer mit verschiedenen Möbeln zum Verkauf. © Goethe-Institut

Malipo 

Namna mbalimbali za malipo zinatumika Ujerumani. Unaweza kulipa kwa pesa taslimu popote pale. Kama una akaunti ya benki au benki ya uhifadhi utapewa kadi ya malipo ya EC na mara nyingi kadi ya malipo (Masta kadi au viza) pia. Katika baadhi ya supamaketi, stoo za idara maalumu na maduka maalumu unaweza kulipa kwa kutumia kadi ya malipo.

Kwenye intaneti utalipa kwa kutumia kadi ya malipo, lakini pia malipo ya moja kwa moja. Kama unahitaji kulipa malipo ya moja kwa moja unatakiwa kuingiza taarifa za akaunti mtandaoni. Kisha Pesa itatolewa kotoka kwenye akaunti yako, kama unatumia Ankara unaweza kuhamisha pesa pesa zako kutoka kwenye akaunti yako.

Eine Person zieht eine Kreditkarte aus einem Geldbeutel. © Goethe-Institut
 

Bei, waranti na bidhaa za mabadilishano

Muda mwingine unaweza ukakubaliana na mwenye duka au unaponunua vitu vya gharama kubwa unaweza kuomba kupunguziwa gharama kwa sheria ya uhakikisho wa bidhaa. Lakini sio kawaida kupandisha bei ya bidhaa kwa wateja.

Umenunua kitu chenye kasoro? Basi una miaka miwili ambapo unaweza kurudisha bidhaa hiyo mpya kwa mujibu wa sheria za uhakikisho kisha utapewa bidhaa nyingine mpya. Au utarudisha bidhaa hiyo kisha utarudishiwa pesa yako. Au utatakiwa kulipa kidogo. Kwa bidhaa zilizotumiwa, ni miezi 12. Muda mwingine bidhaa zinakuwa na waranti. Endapo bidhaa kama runinga ikavunjika wakati wa waranti itatengenezwa bila malipo au utapewa bidhaa mpya. Kipindi cha udhamini ni miezi 12-24 kutoka tarehe ya ununuzi.

Baadhi ya duka pia zinatoa nafasi ya kubalisha bidhaa. Kama haujapenda bidhaa unaweza kuirudisha. Pesa yako itarudishwa. Kwenye intaneti au maduka makubwa na maduka makubwa ya uhifadhi inawezekana siku zote kubadilishana ndani ya siku 14. Kwa hili unahitaji kuonesha risiti au Ankara (maelezo ya malipo). Ni vigumu kubadilishana bidhaa katika ofa maalumu.

Video International Sign

Further questions? Write us via the contact form. We will forward your questions anonymously to the advisors of the youth migration services.

Contact form