Auf einem Bild, das von einem Kind gemalt wurde, sind Wörter in verschiedenen Sprachen zu sehen. © Goethe-Institut

Kila mwaka watu wengi kutoka katika mataifa mengine wanakuja kuishi ujerumani, zaidi ya asilimia ishirini (20%) ya watu wanaoishi ujerumani wanatoka katika utamaduni mwingine wengi ni wamahiri wa lugha nyingi hawazungumzi lugha yao ya kwanza tu, lakini kuzungumza lugha moja nyingine ya pili au zaidi pia. Watu wengine wanaokuja kuishi ujerumani wanajifunza kijerumani kama lugha ya kigeni au lugha ya pili. Kuzungumza lugha ya nchi husika au kanda wanayoishi (hii inajulikana kama lugha ya asili/mama) inarahisisha kuwasiliana na wanajamii na kupata uelewa juu ya mtindo wa maisha yao.

Manufaa ya umahiri wa uzungumzaji wa lugha nyingi

Uwezo wa kuzungumza lugha mbalimbali ni ujuzi muhimu katika dunia ya leo, mipaka baina ya mataifa yanafunguliwa sana kwa sasa zaidi ya kipindi cha nyuma, na watu wengi wanahamia katika nchi nyingine. Mtu anayezungumza lugha yake ya asili pamoja na lugha nyingine ana fursa nyingi, kazini, katika mazingira binafsi, wanaweza kuwaunganisha watu wanaotokea katika tamaduni tofauti, watu wenye uwezo wa kuzungumza lugha zaidi ya moja wana ujuzi wa tamaduni tofautitofauti. Hivyo wanaweza kuitazama mifumo ya maisha ya watu katika mitazamo tofauti. Watoto wengi katika familia za wahamiaji wanaokulia ujerumani kwa kawaida hujifunza lugha ya wazazi wao (lugha asilia) tokea wanapozaliwa. Sambamba na lugha wanajifunza pia juu ya utamaduni na desturi za taifa au wazazi wao. Wanajifunza pia kijerumani kwa kupitia michezo na mawasiliano yao na watoto wengine na watu wazima. Kwa mfano kindagate na shuleni watoto hawa wanakuza umahiri wa kuzungumza lugha nyingi (lugha mbili).

Umuhimu wa lugha ya kijerumani 

Kwa watu wazima wanaoishi ujerumani, ni muhimu kujifunza kijerumani ili kuweza kuwasiliana na watu wanao wazunguka, kuzungumza lugha ya jamii husika pia inasaidia sana katika maingiliano kwa watoto, ujuzi wa lugha ya kijerumani ni muhimu pindi wanapokwenda katika shule za kijerumani.

Upokeaji na utumiaji 

Tunapojifunza lugha, upokeaji na utumiaji zina umuhimu mkubwa sana “upokeaji” na lugha ambayo mtu husikia na kuisoma. Watu wanahitaji mawasiliano ya mara kwa mara na lugha, kimtizamo katika matukio halisi ya shughuli mbalimbali katika maisha. Upokeaji wa lugha unatakiwa uwe wa kiwango cha juu kwa maneno mengine, inatakiwa itokee kwa mzungumzaji wa lugha mama. Kusoma kwa umakini vitabu teule kwa kwa sauti kwa watoto ni vizuri zaidi kwa upokeaji wao wa lugha.

Utumiaji pia ni muhimu sana “utumiaji” inamaanisha lugha mtu anayoizalisha mathalani kuzungumza au kuandika. Ni msingi kwa watu kuweza kutumia lugha, kuzungumza lugha vyema, nafasi nyingi ya kufanyia mazoezi kwa vitendo katika maisha halisi inahitajika uzungumzaji na uandikaji ni muhimu na njia fanisi ya kufanyia mazoezi ya lugha.

Kama utazungumza lugha yako ya asili badala ya kijerumani na mtoto wako au watoto nyumbani, kuna vitu vingi utahitajika kuvifanya ili kukuza ujuzi wa lugha.

Lugha ya familia ni muhimu 

Katika familia nyingi, mama na baba huzungumza lugha moja katika familia nyingi za wahamiaji lugha hiyo sio kijerumani. Hivyo basi watoto kujifunza lugha ya familia ni vizuri kuzungumza nyumbani kwa namna hii, watoto huanzisha hisia za karibu ya mahusiano na lugha hiyo na utamaduni wa asili.

Lugha ya asili (lugha ya kwanza au lugha ya familia) inayozungumzwa na watoto na watu wazima siku zote husaweresha (huwasilisha) taarifa za kitamaduni, desturi na thamani vile vile. Familia hazitakiwi kuacha lugha zao za asili, badala yake wanatakiwa waendelee kukizunzumza nyumabani na watoto wao na familia zao. Na ni muhimu hasa kwa watoto kuzungumza Lugha yao ya kwanza vizuri. Uelewa mzuri wa lugha ya kwanza ni hatua nzuri ya kufikia kiwango cha juu cha utalii katika lugha nyinginezo katika miji mikubwa kuna wamahili wengi (watu wenye uwezo wa kuzungumza lugha mbili kifasaha) na pia watu wenye ujuzi wa kuzungumza lugha tatu, chekechea kwa watoto walio katika mafunzo au elimu ya kabla ya kuanza shule.

Vor einer Weltkarte hängt ein Wandkalender auf Burmesisch mit deutschen Notizen. © Goethe-Institut

Mtu mmoja - lugha moja 

Kama baadhi ya familia baba na mama hawazungumzi lugha moja hapa wazazi wengi hutumia mbinu ya “mtu mmoja - lugha moja”. Hii inamaanisha kuwa kila mzazi huzungumza lugha yake na mtoto. Lugha ya familia kwa maneno mengine, lugha ambayo wazazi wawili na motto huzungumza wanapokuwa pamoja. Wakati mwingine huweza kuwa lugha mojawapo kati ya lugha mbili za wazazi (ya mama au baba) lakini muda mwingine yaweza kuwa ni lugha ya tatu ambayo wazazi wote huzungumza kiustadi.

Kuwalea watoto kuwa wamahiri wa uzungumzaji wa lugha nyingi kipi cha msingi 

Tunapowalea watoto kuwa wazunguimzaji wa lugha. Ni muhimu kwa wazazi kuwa na hisia thabiti na lugha yao. Chaguo sahihi bila shaka ni kwa mama au baba kuzungumza na motto kwa lugha mama (lugha ya kwanza). Kama kuna lugha ya familia hii inapaswa siku zote kuzungumza nyumbani kama motto hataki kuzungumza lugha hiyo hawapaswi kulazimishwa kufanya hivyo. Mara nyingi hii huwa ni hatua to ambayo hupita wazazi pale wanapokuwa katika mazungumzo, kuona kuwa baba na mama wana mtazamo chanya juu ya lugha yao inawahamasisha watoto kujifunza lugha ya mzazi/wazazi pia.

Kuendeleza ujuzi wa watoto kwa lugha yao ya kwanza ni muhimu sana lakini pia inaendeleza maarifa yao ya lugha yao ya asili.

Vituo vingi vinatoa msaada na usaidizi juu ya mambo yanayohusiana na elimu ya umahiri wa lugha nyingi, miji mingi na manispaa zina ofisi au idara zinazoshughulika na masuala ya maingiliano ya tamaduni tofautitofauti, wafanyakazi wake wana uelewa wa kutosha juu ya lugha na program za kitamaduni zinazopatikana na kuweza kutoa ushauri wenye manufaa. Taasisi binafsi pia zinatoa huduma hii ya ushauri. Pia kuna mawakala wengi wanaofanya kazi katika maeneo tofautitofauti ya umahiri wa uzungumzaji wa lugjha nyingi na utofauti wa kitamaduni. Uchunguaji wa mtandaoni kwa kutumia maneno kama “vituo vya ushauri wa mwingiliano wa kitamaduni” au ushauri wa umahiri wa lugha nyingi inatoa taarifa za msingi sana na vyanzo vya habari hizo.

Kuendeleza ujuzi wa lugha ya kijerumani kwa watoto 

Kila mji ujerumani ina sheria zake, program na mikakati ya kuendeleza ujuzi wa watoto wa ujerumani juu ya lugha ya kijerumani kabla ya shule na wakati wa shule. Watoto wanaokosa ujuzi wa kijerumani wanaweza kupata msaada katika program za maendeleo ya lugha kama vile kozi za maandalizi na madarasa ya kuwasaidia ujerumani. Pia kuna vituo vingi vya ushauri vinavyotoa msaada na taarifa endapo watoto watahitaji msaada zaidi wa kujifunza kijerumani.

Kuendeleza lugha ya asili

Ujuzi wa lugha ya kwanza kwa watoto unaweza kuendelezwa zaidi nyumbani na pia katika muktadha wa shuleni ili kukuza ustadi wa watoto katika lugha ya familia, wazazi hawana budi kuwasomea watoto wao mara kwa mara kuwaimbia nyimbo na kucheza nao michezo mbalimbali na watoto wao, watoto pia wanaweza kuwasiliana kwa simu au kwa njia ya video na wanafamilia. Kama wanajua familia nyinginezo zinazozubgumza lugha moja na wao na yenye tamaduni sawia watoto wanaweza kucheza pamoja na kuzungumza lugha yao ya asili.

Washauri wengi na vyama vinavyotoa programu za kimaendeleo katika lugha za kifamilia kwa watoto wenye umri ea kwenda shule, katika madarasa haya watoto hufanyia mazoezi uandikaji na usomaji katika lugha yao ya kwanza na kujifunza juu ya mitindo ya maisha na desturi za nchi zao za asili. Katika baadhi ya miji ya ujerumani programu za maendeleo katika lugha asili zinapatikana pia katika shule kuu hii inajulikana kama maelekezo ya ziada ya lugha mama.

Kuna taarifa nyingi mitandaoni juu ya vyama vingi na mashirika yanayo wasilisha lugha maalumu tamaduni za kijamii na kuendeleza makundi ya michezo. Vilabu vya michezo na matukio ya kijamii kwa mfano wanawapa watoto na wazazi nafasi ya kutumia lugha ya familia au lugha ya asili mara kwa mara katika matukio halisi katika matukio ya kimaisha.

 

Video International Sign

Further questions? Write us via the contact form. We will forward your questions anonymously to the advisors of the youth migration services.

Contact form