Goethe-Zertifikat B2
Goethe-Zertifikat B2 ni mtihani wa Kijerumani kwa vijana na watu wazima. Unathibitisha kuwa watahiniwa wamepata ustadi zaidi wa kuongea lugha ya Kijerumani na unakidhi vigezo vya hatua ya nne (B2) katika ngazi ya hatua sita za uhadari zilizowekwa na Mfumo wa Pamoja wa Ulaya wa Marejeo ya Lugha (CEFR).
Kufaulu mtihani inamaanisha kuwa unaweza …
- kuelewa mambo makuu kutoka kwenye maandishi yaliyo katika lugha au mada ngumu, na pia majadiliano ya kiufundi katika eneo la utaalamu wako,
- kuwasiliana kwa kuongea bila kusita kiasi kwamba mazungumzo ya kawaida na mzungumzaji wa asili ya Kijerumani yanawezekana bila ya kuhitaji juhudi kubwa kutoka upande wowote,
- kutoa maoni yako juu ya masuala yanayoendelea katika jamii katika lugha inayoeleweka na maelezo ya kina, kuelezea msimamo wako juu ya mambo hayo na na kutaja faida na hasara kutoka maoni mbalimbali
Tarehe za mitihani
*) Bei nafuu inayoonekana inatumika ikiwa tayari ulihudhuria kozi ya Kijerumani katika taasisi ya Goethe-Institut ndani ya kipindi kisichozidi miezi sita iliyopita. Miezi hiyo sita inahesabiwa kati ya kumalizika kwa kozi na tarehe ya mtihani wa Kijerumani. Katika hali hii, bei itabadilika yenyewe kiotomatiki wakati wa mchakato wa usajili. Ikiwa hili halitafanyika, tafadhali wasiliana na idara ya kozi.