TestDaF

Unafaa endapo unataka …

  • kusoma au kufanya utafiti nchini Ujerumani
  • kufanya mtihani wa lugha unaotambuliwa na vyuo vikuu na taasisi za elimu ya juu nchini Ujerumani
  • kutoa ushahidi wa uwezo wako wa Kijerumani kwa taasisi za utafiti na waajiri

TestDaF ni mtihani wa hatua ya juu wa lugha. Unajumuisha hatua za B1 hadi C1 katika ngazi ya hatua sita za uhadari zilizowekwa na Mfumo wa Pamoja wa Ulaya wa Marejeo ya Lugha (CEFR).
 
Cheti kinachotolewa baada ya kuhitimu kikamilifu seksheni zote nne za mtihani wa TestDaF kwenye hatua ya 4 ya TestDaF kitatumika ushahidi wa ustadi wa lugha unaohitajika ili kudahiliwa kuchukua somo au shahada yoyote katika chuo kikuu au taasisi ya elimu ya juu  nchini Ujerumani. Mtihani wa lugha wa TestDaF pia unaatoa ushahidi unaokubalika kimataifa kuwa ujuzi wako wa Kijerumani unakidhi kiwango cha kufanya miradi ya kisayansi na kuwa miongoni mwa wanataaluma
 
Hakuna ujuzi mahsusi unaohitajika kufanya mtihani

Unapatikana duniani kote

Mtihani wa TestDaF unaweza kufanyika katika vituo vilivyoruhusiwa tu. Hadi sasa kuna takribani vituo 450 vinavyotoa mtihani. Unaweza kuperuzi hapa chini kuona vituo vya mtihani vilivyopo Ujerumani na sehemu nyingine duniani:

Maandalizi

matini ya mazoezi

Vifaa vya mazoezi na usomaji uliopendekezwa vinapatikana hapa.

Maelezo zaidi

Mahitaji, yaliyomo katika mtihani na maelezo zaidi juu ya mtihani wa TestDaF yanapatikana hapa: