Kufundisha Kijerumani

Dhamira ya Goethe-Institut ni kukuza utamaduni wa Kijerumani na kuendeleza ufundishaji na ujifunzaji wa Kijerumani kama lugha ya kigeni. Tumejitolea kutoa mafunzo ya hali ya juu ya maendeleo ya kitaaluma kwa walimu na vifaa vya kufundishia bila malipo ili kufanya kujifunza Kijerumani kuwa jambo la kufurahisha na rahisi.

Maendeleo ya kitaaluma.

Kwaajili ya masomo yako.

Tovuti ya kuingilia kwaajili ya walimu wa DaF.

Deutschstunde

Deutschstunde ni tovuti ya kuingilia kwaajili ya kufundishia Kijerumani kama lugha ya kigeni, mafunzo ya hali ya juu na lugha ya majarida. Mawasiliano na walimu wengine kupitia jamii za wenyeji yako umbali wa mibofyo michache tu.

  • Maktaba ya dijitali.

    Deutschstunde Katika ‘Onleihe’ utapata aina mbalimbali za vifaa vya Kijerumani kama lugha ya kigeni, vitabu vya kufundishia, vitabu vya kielektroniki na vitabu vya sauti vya kujifunza lugha na utamaduni wa Kijerumani.

  • Kusoma kumerahisishwa.

    Kwa wanafunzi wa Kijerumani kutoka viwango vya lugha B2 na C1 (vya Mfumo wa Marejeleo ya Lugha wa Pamoja wa Ulaya), tunapendekeza kazi zifuatazo za fasihi ya kisasa ya Kijerumani katika Onleihe, (maktaba yetu ya kidijitali ya bure).

Mawasiliano

Ushirikiano wa Kijerumani kama Lugha ya Kigeni unasaidia walimu wa Kitanzania, shule na taasisi katika kufanikisha ufundishaji wa lugha ya Kijerumani. Tunatoa mafunzo kwa walimu wa Kijerumani, kuanzia warsha za siku moja hadi semina za wiki kadhaa. Pia tunatoa mawazo na vitendea kazi vya kuhamasisha ujifunzaji wa Kijerumani pamoja na muhtasari wa vifaa vya kisasa vya kufundishia.

Tufuatilie