Masharti

VIGEZO VYA MATUMIZI

kutoka Goethe-Institut e.V. (“Taasisi ya Goethe”) kwa matumizi ya goethe.de (“Tovuti”)

YALIYOMO

  1. Wigo na maudhui ya mkataba
  2. Usajili na muundo wa mkataba
  3. Huduma za Taasisi ya Goethe
  4. Wajibu wa Mtumiaji na kanuni zinazosimamia
  5. Hatua zinazochukuliwa katika ukiukaji wa kanuni; marufuku jukwaani
  6. Ridhaa ya haki ya matumizi
  7. Hakikisho la wajibu wa kisheria
  8. Vigezo na kutenguliwa kwa mkataba
  9. Mabadiliko ya vigezo vya matumizi
  10. Uchaguzi wa sheria
 

1. WIGO NA MAUDHUI YA MKATABA

Kwa kuzingatia matumizi ya Tovuti hii, na uhusiano baina ya “Mtumiaji” na Taasisi ya Goethe (kama mwendeshaji wa Tovuti) Vigezo vya Matumizi vifuatavyo vinatumika. Mtumiaji anakubaliana na hivi Vigezo vya Matumizi mara tu anapofanya usajili.

Maudhui ya mkataba huu ni matumizi ya Tovuti, bila malipo, kama jukwaa la taarifa na mawasiliano (“Huduma”). Kozi za mafunzo kwa njia ya masafa zinazotolewa kwa kulipia ada ni maudhui tofauti ya Vigezo na Masharti ya Biashara.

 

2. USAJILI NA MUUNDO WA MKATABA

Ni sharti kufanya usajili kabla ya matumizi ya huduma za Tovuti kwa mtu binafsi. Wakati wa usajili, ni sharti Mtumiaji kutoa maelezo ya kweli na hupewa taarifa za kanuni za ulinzi wa data na hutakiwa kutoa ridhaa yake kwa mujibu wa sheria ya ulinzi wa data. Kufuatia usajili, Mtumiaji hupokea baruapepe yenye kiunga cha kuthibitisha. Katika muda ule ambapo Taasisi ya Goethe hufungua akaunti ya Mtumiaji, papo hapo Mtumiaji wa Tovuti huingia makubaliano yenye kuwa na athari kwake.

Mtumiaji hawezi kutoa madai ya haki ya kufunguliwa kwa akaunti. Haki zisizo na ukomo za Taasisi ya Goethe kama mmiliki na mhifadhi ndizo zitatumika. Kwa msisitizo, Taasisi ya Goethe na watendaji na waratibu wake watakuwa na haki ya kuwaondoa watumiaji fulani.

Mtumiaji hawezi kuruhusu watu wengine kutumia taarifa zake zinazomwezesha kuingia kwenye Tovuti na, kama mmiliki wa akaunti kwenye Tovuti, anawajibika katika kuilinda akaunti hiyo dhidi ya matumizi yasiyofaa. Kwa sababu hii, Mtumiaji anabeba wajibu wa kuhakikisha data zake za ufikivu zinakuwa siri na kuzilinda dhidi ya kuingiliwa na watu wengine. Hairuhusiwi kutumia majina ya chapa za bidhaa zinazolindwa kwa mujibu wa sheria au majina halisi ya watu au taasisi nyingine kama jina la Mtumiaji.

Mtumiaji anaweza kusitisha matumizi yake ya Huduma wakati wowote, na anaweza kufuta usajili wake na data za usajili kwa sababu yoyote ile. 

 

3. HUDUMA ZA TAASISI YA GOETHE

Katika wigo wa hivi Vigezo vya Huduma, Taasisi ya Goethe inaruhusu Mtumiaji kusoma na kutuma maudhui kwenye Tovuti na kuwasiliana na watumiaji wengine. Kwa lengo hili, Taasisi ya Goethe humpa Mtumiaji jukwaa lenye vitenda-kazi mbalimbali vya kijamii, bila malipo, kwa kadri inavyoweza kufanya hivyo kiufundi na kibiashara.

Taasisi ya Goethe itafanya jitihada kuhakikisha Huduma zake zinapatikana bila ya kukatika kwa kadri inavyowezekana. Taasisi ya Goethe haiwajibiki kutoa Huduma zaidi ya zile zilizotajwa. Kwa msisitizo, Mtumiaji hawezi kutoa madai ya haki ya upatikanaji wa daima au utoaji usio na kasoro wa Huduma. 

Taasisi ya Goethe ina haki ya kufanyia marekebisho, kuongeza, kuingilia au kusitisha wakati wowote vipengele vyote vinavyohusiana na mtu binafsi katika Huduma zake, kwa kutoa au kutokutoa taarifa kwa Mtumiaji, kwa muda au moja kwa moja, kitu kinachoweza kupelekea kufutwa kwa akaunti zilizopo za Mtumiaji na/au Maudhui ya Mtumiaji.

 

4. WAJIBU WA MTUMIAJI NA KANUNI ZINAZOSIMAMIA

Mara tu anapofanya usajili, Mtumiaji huchukuliwa kuwa anakubali kwamba kwa wakati wote atatoa maelezo yanayohusiana na utambulisho wake kwa kuzingatia ukweli, wakati uliopo na ukamilifu wa maelezo yake kadri inavyotakiwa katika fomu ya usajili na haitampasa wakati wowote ule kuidanganya Taasisi ya Goethe au watumiaji wengine kuhusiana na utambulisho wake.

Kwa kuchapisha maudhui kwenye Tovuti, Mtumiaji huchukuliwa kuwa anatoa hakikisho kwamba yeye ni mmiliki wa haki zote zinazohitajika kwa lengo hili. Mtumiaji anakubali kwamba hatachapisha kitu chochote kwenye Tovuti ambacho kinakiuka maadili katika jamii au sheria halali. Mtumiaji, kwa msisitizo, anakubali kwamba hatachapisha kitu chochote,

  • ambacho uchapishaji wake utapelekea viashiria vya jinai au ukiukaji wa sheria,
  • ambacho kinaingilia hakimiliki, sheria ya chapa za kibiashara au sheria ya ushindani,
  • ambacho kinaingilia haki za watu wengine za ulinzi wa data (mf. uchapishaji wa ujumbe binafsi bila ya kupata ridhaa ya mtumaji husika),
  • ambacho maudhui yake yanakashifu, hayana ukweli, yana chochea ubaguzi wa rangi au ubaguzi wa aina nyinginezo, yana athari mbaya kwa vijana au ponografia,
  • chenye tangazo, ambalo pia linajumuisha picha au viunga vilivyo au visivyokuwa na maandishi juu yake kwenye sahihi ya kidijitali au kitu chenyewe.
Kwa kuongezea juu ya wajibu uliotajwa, watumiaji watapaswa kwa wakati wote kufuata kanuni za ujumla za umiliki na kuchukuliana kwa kuheshimiana, na hawawezi kutumia Huduma kutishana, kusumbuana, kuumizana kwa namna fulani, kuhadaa au kuharibu hadhi au biashara za watumiaji au watu wengine.

Pale ambapo Mtumiaji ni shahidi katika tukio lolote la lukiukaji wa hivi Vigezo vya Matumizi uliofanywa na Mtumiaji mwingine, ni sharti kwake kuwataarifu watendaji kwa njia ya baruapepe kupitia anuani kdf@goethe.de.

 

5. HATUA ZINAZOCHUKULIWA KATIKA UKIUKAJI WA KANUNI; MARUFUKU JUKWAANI

Katika tukio la ukiukaji au pale ambapo ushahidi wa kimazingira unatosheleza kushuku ukiukaji wa wajibu uliotajwa kwenye kifungu cha 4 hapo juu, Taasisi ya Goethe inaweza, kwa hiyari yake yenyewe, kuchukua hatua zifuatazo kwa Watumiaji:

  • kufutwa au kufanyiwa marekebisho maudhui yaliyotumwa na Mtumiaji, ikiwa ni pamoja na pale ambapo, kwa uamuzi wa Taasisi ya Goethe, yataonekana kukiuka sheria au kwenda kinyume na maadili katika jamii,
  • kupewa onyo au onyo la maandishi,
  • kuwekewa mipaka ya matumizi ya Huduma,
  • kuzuiwa kwa muda au moja kwa moja kupata huduma,
  • kusitishwa kwa Makubaliano na Mtumiaji na kufutwa kwa data na maudhui yote ya huyo Mtumiaji, ikiwa ni pamoja na kutekeleza hatua hii mara moja na bila kutoa kwanza taarifa ya onyo.

Mtumiaji ataifidia Taasisi ya Goethe na hawezi kuiwajibisha dhidi ya madai yote ya watu wengine yaliyotolewa na hao watu wengine ambayo msingi wake unatokana na ukiukaji wa taratibu uliofanywa na Mtumiaji; wajibu uliotajwa kwenye kifungu cha 4 hapo juu. Mtumiaji anakubali kwamba atashirikiana na Taasisi ya Goethe kwa nia njema kwa kuwasilisha taarifa na nyaraka zitakazosaidia kujitetea dhidi ya madai kama hayo. Mtumiaji atafidia pia gharama za Taasisi ya Goethe kwa ajili ya utetezi wa kisheria. Hii itafanyika bila kuathiri haki nyingine za Taasisi ya Goethe na madai mengine ya fidia za gharama.

 

6. RIDHAA YA HAKI YA MATUMIZI 

Hakimiliki kwa upande wa maudhui yaliyotumwa, kiasi cha kufikia uwezo wa kulindwa na sheria ya ulinzi wa hakimiliki, itabaki kuwa halali ya Mtumiaji husika. Hatahivyo, kwa kitendo cha kutuma maudhui kwenda goethe.de, Mtumiaji anaipa Taasisi ya Goethe haki ya

  • kufanya maudhui hayo kuonekana moja kwa moja kwenye Tovuti (pamoja na tafsiri yake katika lugha nyingine),
  • kurudufu na kusambaza kazi katika machapisho (pamoja na tafsiri yake katika lugha nyingine),
  • kuhamisha maudhui ndani ya Tovuti na kuyaunganisha na maudhui mengine,
  • kuyafanyia marekebisho au kufuta baadhi ya sehemu zake pale inapofaa kulingana na kifungu cha 5.

Mtumiaji hatakuwa na haki juu ya kufutwa au kufanyiwa marekebisho kwa yaliyowekwamaudhui yaliyotoka kwake.

 

7. HAKIKISHO NA WAJIBU WA KISHERIA

Taasisi ya Goethe haitoi hakikisho la kuwa sahihi, kukamilika, kuaminika, kutoka kwa wakati na kutumika kwa maudhui inayotoa bila malipo au maudhui yaliyotumwa na Watumiaji, na wala maudhui hayo hayawasilishi mtazamo wa Taasisi ya Goethe. Maudhui ya Mtumiaji yenye ukiukaji wa sheria yatafutwa mara moja pale Taasisi ya Goethe itakapogundua ukiukaji wa sheria.

Mtumiaji hatakuwa na haki ya madai ya kufidiwa gharama dhidi ya Taasisi ya Goethe, wawakilishi wake kisheria na mawakala wanaofanya kazi kwa niaba yake, isipokuwa kama ilivyoelezwa hapa chini. Isipokuwa hapa ni madai ya gharama ambayo msingi wake ni hakikisho au ahadi iliyotolewa na Taasisi ya Goethe, madai ambayo msingi wake ni madhara kwa maisha, kiungo cha mwili au afya, madai ambayo msingi wake ni Product Liability Act, na madai ya kufidiwa gharama ambayo msingi wake ni ukiukaji wa wajibu wa kutekeleza mkataba. Wajibu kutekeleza mkataba ni majukumu ambayo utekelezaji wake unahitajika ili kufikia malengo ya mkataba. Ilani hii ya uwajibikaji wa kisheria katika msingi huohuo halijumuishi uwajibikaji wa kisheria kwa hasara ambazo msingi wake ni ukiukaji wa makusudi au uzembe wa hali ya juu wa mtoa huduma, wawakilishi wake kisheria au mawakala wanaofanya kazi kwa niaba yake.

 

8. VIGEZO NA KUTENGULIWA KWA MKATABA

Makubaliano haya hayana ukomo wa muda na yanaweza kusitishwa na upande wowote bila ya hitaji la kuzingatia tarehe yoyote ya ukomo wa muda kwa maandishi (mf. kwa njia ya baruapepe). 

Kufuatia ukomo wa mkataba huu, Taasisi ya Goethe itakuwa na haki lakini bila kushurutishwa ya kufuta maudhui yaliyowekwa na Mtumiaji. Mtumiaji hatakuwa na haki ya madai ya kupewa maudhui yaliyowekwa naye.

Kunapotokea sababu ya kuchukua hatua, kwa msisitizo, pale ambapo msingi wake ni ukiukaji wowote wa wajibu unaosomeka kwenye kifungu cha 4, Taasisi ya Goethe itakuwa na haki kuzuia mara moja upatikanaji wa huduma kwa Mtumiaji na kusitisha mkataba bila kutoa kwanza taarifa ya onyo. Katika mazingira hayo, Mtumiaji husika anaweza kufanya usajili tena endapo tu kabla ya kufanya hivyo atakuwa amepata ridhaa ya maandishi kutoka Taasisi ya Goethe.

 

9. MABADILIKO YA VIGEZO VYA MATUMIZI

Taasisi ya Goethe ina haki ya kufanyia mabadiliko hivi Vigezo vya Matumizi bila ya hitaji la kueleza msingi mabadiliko hayo. Taasisi ya Goethe itamtaarifu Mtumiaji ndani ya muda mwafaka juu ya mabadiliko yaliyofanyika wakati wa Mtumiaji kutembelea tena Tovuti baada kufanyika mabadiliko, na itaomba ridhaa ya Mtumiaji kwenye mabadiliko ya Vigezo vya Matumizi. Pale ambapo Mtumiaji hataweka pingamizi, itachukuliwa kwamba Vigezo vya Matumizi vimekubaliwa. Pale ambapo Mtumiaji ataweka pingamizi, uanachama wa Mtumiaji utasitishwa.

 

10. UCHAGUZI WA SHERIA

Kwa upande wa uhusiano wa mkataba baina ya Taasisi ya Goethe na Mtumiaji, sheria za Shirikisho la Jamhuri ya Ujerumani zitatumika. Kwa upande wa watumiaji wa kawaida, uchaguzi huu wa sheria utatumika tu kwa kiwango ambacho hakitamnyima mtumiaji huyo ulinzi unaotolewa kwake na sheria ya ulinzi wa mtumiaji ambayo ni lazima katika nchi ambayo yeye ni mkazi wa siku zote.

Juu