Goethe-Zertifikat A1: Start Deutsch 1

Unafaa endapo unataka

  • kuomba nafasi ya usaidizi wa nyumbani nchini Ujerumani
  • kutoa ushahidi juu ya stadi za lugha unaohitajika ili kupata visa ya kuungana na mume au mke nchini Ujerumani
  • kuthibitisha kuwa umefaulu kufika hatua A1
  • kupata cheti rasmi kinachotambulika kimataifa

Goethe-Zertifikat A1: Start Deutsch 1 ni mtihani wa Kijerumani kwa watu wazima. Unathibitisha kuwa mtahiniwa ameweza kupata maarifa ya msingi ya stadi wa lugha na unakidhi vigezo vya hatua ya kwanza (A1) katika ngazi ya hatua sita za uhadari zilizowekwa na Mfumo wa Pamoja wa Ulaya wa Marejeo ya Lugha (CEFR).

Kufaulu mtihani inamaanisha kuwa unaweza …

  • kufanya mawasiliano rahisi endapo mtu unayeongea naye anazungumza polepole na anasikika vizuri
  • kuelewa maneno yaliyozoeleka na yayotumiwa kila siku pamoja na sentensi nyepesi (mf. taarifa zako binafsi na familia yako au kununua kitu dukani, kazi na mazingira yaliyokuzunguka kwa karibu),
  • kujitambulisha mwenyewe na kuwatambulisha wengine, pia kuwauliza wengine maswali, mf. wanakaa wapi, wanamjua nani au wana nini

Maandalizi

Matini ya mazoezi

Mitihani ya mfano na matini ya kufanyia majaribio ambazo ni rahisi kutumia kukusaidia mtandaoni vinapatikana hapa

Maelezo zaidi

Mahitaji, yaliyomo katika mtihani na maelezo zaidi juu ya mtihani wa Goethe-Zertifikat A1: Start Deutsch 1  yanapatikana hapa: