Lugha ya Kijerumani

Mafanikio yako na Kijerumani.

Taasisi ya Goethe inaleta lugha ya Kijerumani duniani: tunatoa kozi na mitihani ya Kijerumani katika nchi zaidi ya 90. Unaweza kufanya mazoezi ya Kijerumani bila malipo kwa uteuzi wetu mbalimbali wa mazoezi ya mtandaoni na katika Jumuiya. Tafuta kuhusu fursa za maendeleo ya kitaaluma na nyenzo kwa walimu wa Kijerumani (DaF/DaZ).

Jifunze Kijerumani na Taasisi ya Goethe.

  • Kozi za Kijerumani

    Jifunze Kijerumani na wataalamu. Iwe Tanzania, Ujerumani au mtandaoni - sisi ni mshirika wako wa kuaminika kwa ajili ya kujifunza lugha ya Kijerumani kwa mafanikio na walimu wetu waliohitimu.

    Eine Gruppe junger Leute sitzen nebeneinander auf eine Bank. Sie lesen von Laptops und Tablets.

  • Mitihani ya Kijerumani

    Onyesha unachoweza kufanya! Mitihani yetu ya Kijerumani inayotambulika duniani kote katika ngazi ya A1 hadi C2 hutoa uthibitisho rasmi wa ujuzi wako wa lugha ya Kijerumani.

Kwa wanafunzi wa Kijerumani.

  • Fanya Mazoezi Ya Kijerumani Bila Malipo

    Katika kituo cha Goethe-Institut, unajifunza Kijerumani kutoka kwa wataalamu wenye uzoefu. Tumetengeneza nyenzo mbalimbali za kutumia bila malipo, za kukusaidia kufanya mazoezi ya Kijerumani chako – kwenye app zenye nyenzo za kujifunzia kama video, vipindi vya sauti na michezo, pamoja na mitandao ya kijamii na programu za jumuiya. Haijalishi unaongea Kijerumani kwa ustadi gani na sababu zako zozote zile za kuboresha Kijerumani chako, suala muhimu ni kwamba unaanza kufanya mazoezi – na kufurahia!

    Gruppe junger Menschen, die in die Kamera lächeln. © Goethe-Institut

Kwaajili ya walimu na taasisi za elimu.

  • Kufundisha Kijerumani.

    Tunawapa walimu wa Kijerumani programu mbalimbali za mafunzo, shughuli za madarasa yao na vifaa vya kufundishia darasa la Kijerumani lenye kutia moyo na kuhamasisha.

  • Mpango wa PASCH

    Tunawapa walimu wa Kijerumani programu mbalimbali za mafunzo, shughuli za madarasa yao na vifaa vya kufundishia darasa la Kijerumani lenye kutia moyo na kuhamasisha.

Tufuatilie