Goethe-Zertifikat A2: Fit in Deutsch

Unafaa endapo unataka

  • kufanya mtihani wa Kijerumani kwa vijana kati ya miaka 12 hadi 16
  • kuonesha kuwa una kiwango cha msingi cha uelewa wa Kijerumani 
  • kuthibitisha kuwa umefaulu kufika hatua A2
  • kupata cheti rasmi kinachotambulika kimataifa

Goethe-Zertifikat A2: Fit in Deutsch ni mtihani wa Kijerumani kwa vijana kati ya miaka 12 hadi 16. Unathibitisha kuwa mtahiniwa ameweza kupata maarifa ya msingi ya stadi wa lugha na unakidhi vigezo vya hatua ya pili (A2) katika ngazi ya hatua sita za uhadari zilizowekwa na Mfumo wa Pamoja wa Ulaya wa Marejeo ya Lugha (CEFR).

Kufaulu mtihani inamaanisha kuwa unaweza …

  • kuelewa na kutumia sentensi na maneno ya kawaida ya kila siku,
  • kueleweka unapoongea katika mazingira yanayohitaji kutoa na kupokea taarifa nyepesi juu ya mambo yaliyozoeleka
  • kuelezea historia yako na elimu yako, mazingira yaliyokuzunguka kwa karibu na mambo mengine yanayohusu mahitaji yako, kwa njia rahisi

Maandalizi

Matini ya mazoezi

Mitihani ya mfano na matini ya kufanyia majaribio ambazo ni rahisi kutumia kukusaidia mtandaoni vinapatikana hapa

Maelezo zaidi

Mahitaji, yaliyomo katika mtihani na maelezo zaidi juu ya mtihani wa Goethe-Zertifikat A2: Fit in Deutsch yanapatikana hapa: