Usiri wa data

Kanuni za ulinzi wa Data na Ridhaa

Goethe-Institut e.V., Oskar-von-Miller-Ring, 18, 80333 Munich ("Taasisi ya Goethe" au "sisi"), kama mwendeshaji wa tovuti www.goethe.de ("Tovuti"), ni wadhibiti wa data zinazotoa utambulisho wa mtu binafsi za watumiaji ("Wewe") wa Tovuti kwa mujibu wa tafsiri ya muktadha wa Kanuni ya Pamoja ya Umoja wa Ulaya ya Ulinzi wa Data (GDPR) na sheria za Ujerumani za ulinzi wa data, lakini zaidi katika Sheria ya Shirikisho ya Ulinzi wa Data (BDSG).

Yaliyomo

 1. Matumizi ya Tovuti kwa lengo la kupata taarifa
 2. Ukusanyaji na matumizi ya data kwa lengo la kutekeleza mkataba
 3. Usajili na akaunti ya Goethe.de
  a) Data zinazokuhu na maudhui unayoweka
  b) Matangazo yanayomlenga mtumiaji
  c) Uchapishaji wa Data
  d) Mwingiliano wa data baina ya mfumo unaoratibu kozi zetu za lugha na akaunti yako ya Goethe.de
  e) Kufutwa
 4. Google reCAPTCHA na Ramani za Google
  a) Google reCAPTCHA
  b) Ramani za Google
 5. Ukusanyaji na matumizi ya data kwa malengo ya matangazo
  a) Matangazo kwa njia ya posta
  b) Jarida kwa njia ya baruapepe
 6. Vidakuzi
 7. Uchanganuzi wa mtandao
  a) Webtrekk
  b) Google(Universal) Analytics
  c) Matumizi ya uchanganuzi wa Yandex-Metrica
  d) Google Tag Manager
 8. Mitandao ya Kijamii
  a) Matumizi ya viongezi na vifaa-mkato vya Facebook, Twitter, Google+, Instagram na VKontakte kwa njia ya mtandaoni ya Shariff
  b) Matumizi ya vifaa-mkato vya Spotify na Soundcloud
  c) Kuweka na kuonesha maudhui ya mtandao wa kijamii
  d) Viongezi vya video kutoka YouTube na Vimeo
  e) Uwepo wetu kwenye mitandao ya kijamii
 9. Uhamishaji wa data kwenda kwa mhusika mwingine
  a) Uhamishaji wa data kwenda Goethe-Instituts
  b) Uhamishaji wa data kwenda kituo cha makavazi ya mtihani
 10. Usalama wa Data
 11. Haki zako na jinsi ya kuwasiliana nasi
 12. Haki ya pingamizi

Goethe-Institut inachukulia suala la ulinzi wa taarifa zako binafsi kwa umakini mkubwa. Kwa ilani hii kuhusu faragha, tunapenda kukufahamisha kwa njia ya uwazi data zinazotoa utambulisho wa mtu binafsi ("taarifa zako binafsi") tunazokusanya, kuchakata na kutumia pale unapotembelea mitandao yetu ya kijamii mtandaoni na/au unapotumia Tovuti ya Taasisi ya Goethe.  

1. MATUMIZI YA TOVUTI KWA LENGO LA KUPATA TAARIFA

Unaweza kutembelea Tovuti yetu na kutumia baadhi ya ofa tunazotoa kwa njia ya mtandao bila ulazima wa kutoa taarifa zozote binafsi. Wakati wowote unapoingia kwenye tovuti, seva ya tovuti kwa kujiendesha yenyewe hutunza kwenye nyaraka za seva data za ufikivu kama vile jina la faili ulilofungua mtandaoni, tovuti ya mwisho kutembelea, tarehe na muda wa kuingia kwenye tovuti, programu iliyotumika kuvinjari mtandaoni, kiasi cha data kilichohamishwa, anuani ya kipekee kwenye mtandao, mtoa huduma ya intaneti, nk., ambazo hutumwa na programu yako itumikayo kuvinjari mtandaoni kwa kujiendesha yenyewe. Katika wigo wa uchakataji unaofanywa kwa niaba yetu, mtoa huduma mwingine amepewa kazi kutunza na huduma ya kufanya Tovuti iweze kuonekana mtandaoni kwa niaba yetu. Mtoa huduma aliyetajwa hapa anatokea mojawapo ya nchi wanachama wa Umoja wa Ulaya au Zoni ya Kiuchumi ya Ulaya.

Kwa lengo kufupisha muda wako wa kutufikia kwa njia ya mtandao, tunatumia pia mfumo wa seva zilizopo sehemu tofauti duniani, ambazo hutumika kama njia ya kufikisha Tovuti kwa mtumiaji kupitia seva mojawapo kati ya hizo ambazo husimamiwa na mtoa huduma anayefanya kazi hiyo kwa niaba yetu ili kufanikisha mpango mzuri wa uchakataji wa data. Data za ufikivu hukusanywa pia kwa njia hiyohiyo kwenye seva za mtoa huduma.

Data zote za ufikivu hutunzwa kwa kipindi cha siku 7. Data hizi hufanyiwa tathmini ya kipekee kwa lengo la kuhakikisha utendaji mzuri wa Tovuti, uchanganuzi wa dosari na uboreshaji wa huduma tunazotoa. Matumizi ya mfumo wa kompyuta wa mtoa huduma, pamoja na mchakato uliofafanuliwa hapa, husaidia kulinda masilahi na mamlaka yetu halali katika utoaji sahihi wa huduma zetu kwa mujibu wa Ibara ya 6 (1) mstari wa 1 (f) ya Kanuni ya Pamoja ya Umoja wa Ulaya ya Ulinzi wa Data (GDPR).  

 2. Ukusanyaji na matumizi ya data kwa LENGO ya kuTEKELEZA mKaTABA

Tunakusanya data zinazotoa utambulisho wa mtu binafsi endapo unatoa taarifa hizo wakati wa kuwasiliana nasi (mf. kutumia fomu ya mawasiliano au baruapepe), pale unapofanya usajili wa akaunti ya mtumiaji ("Akaunti ya Goethe.de") au kwa kitendo cha kuweka miadi, kwa mfano unapoweka miadi ya kuchukua kozi au kufanya mtihani. Sehemu ya kujaza katika fomu huonesha aina ya data zinazokusanywa kina na taarifa ambazo ni lazima au hiyari kutoa.

Katika mazingira hayo, tunakusanya na kuchakata data ulizotoa wewe mwenyewe kwa lengo la kutekeleza mkataba husika, kwa mfano kutoa jaribio la kupima kiwango chako kulingana na kozi unazochukua za lugha au kozi ya lugha pamoja na mtihani wake unaofuatia, na kukujibu maswali unayouliza kwa mujibu wa Ibara ya 6 (1) mstari wa 1 (b) GDPR. Kwa mantiki hii unaporidhia mchakato wa uchakataji wa mkusanyiko maalumu wa data kwa mujibu wa Ibara ya 9 (2) (a) GDPR, tutakusanya data zako za afya (mf. mzio) kwa lengo mahsusi lililofafanuliwa kwako wakati wa kuridhia. 

Data zako zitakoma kutumika zaidi na kufutwa baada ya kuisha kwa muda wa lazima wa kutunza data chini ya sheria ya kodi na biashara. Pale ambapo sheria ya kodi au biashara inayolazimisha kuhifadhi data haihusiani na data za mtu binafsi, taarifa zake zitafutwa mara moja baada ya kutekelezwa kwa mkataba husika. Tofauti pekee ni pale ambapo umeridhia kuendelea kutumika kwa data zako au pale tunapokuwa na haki ya kutumia data zako kwa lengo jingine lolote linaloruhusiwa kisheria na ambalo tumekutaarifu juu yake hapa chini.

Data za akaunti yako inayohusiana na programu zetu za masomo nazo pia zitajifuta zenyewe baada ya kipindi cha miaka mitatu kupita bila kutumika.

Uhamishaji wa data kwa lengo la utekelezaji wa mkataba

Ndani ya utaratibu wa kuweka miadi ya kuchukua kozi na kufanya mtihani, data zako zako zinazotoa utambulisho wa mtu binafsi zitachakatwa katika mfumo wetu wa pamoja unaosimamia kozi za lugha, ambapo ofisi nyingine za Taasisi ya Goethe zina uwezo kuingia kwenye mfumo huo, isipokuwa pale ambapo imekatazwa kulingana na sheria za nchi husika. Hii ni kwa lengo la kukamilisha mchakato wa mkataba kwa mujibu wa Ibara ya 6 (1) mstari wa 1 (b) GDPR, pamoja na kulinda maslahi yetu mapana na halali katika kupokea taarifa stahiki na kumbukumbu sahihi za data unapoweka miadi ya kozi kwa mujibu wa Ibara ya 6 (1) mstari wa 1 (f) ya Kanuni ya Pamoja ya Umoja wa Ulaya ya Ulinzi wa Data (GDPR). Kwa mantiki hii pale ambapo data zinazotoa utambulisho wa mtu binafsi zinachakatwa katika nchi zilizo nje ya Umoja wa Ulaya au Zoni ya Kiuchumi ya Ulaya kwa lengo hili, tumekubaliana sheria zinazotumika Umoja wa Ulaya na kuzingatiwa na Taasisi za Goethe zinafaa kama hakikisho kwa mujibu wa tafsiri ya Ibara ya 46 (2) (c) GDPR kwa ulinzi wa data.

Ili kutimiza matakwa ya mkataba, tutatuma taarifa zako binafsi kwenda kampuni iliyopewa jukumu la kufikisha huduma kwa mtumiaji, kwa kuwa kufanya hivyo ni muhimu katika kufikisha bidhaa zilizoagizwa au utoaji wa wa huduma inayotarajiwa. Kulingana na aina ya malipo inayokubaliwa na mtoaji wa huduma uliyemchagua katika mchakato wa kuagiza, tutatuma data za malipo zokusanywa kwa lengo hili mahsusi kwenda benki iliyopewa dhamana ya kukusanya malipo na, endapo inakubalika, kwenda kwenye mfumo wa malipo ya mtoaji wa huduma tuliyempa kazi hiyo au kwenye huduma ya malipo iliyochaguliwa kwa ajili ya mchakato wa malipo. Katika mazingira fulani, watoaji wa huduma ya malipo waliochaguliwa pia hukusanya data hizi wao wenyewe endapo utafungua akaunti yako kupitia kwao. Katika mazingira hayo, ni sharti uingie kwenye tovuti ya mtoaji wa huduma za malipo kwa kutumia data zako za ufikivu ulizotumia katika mchakato wa kuweka miadi. Kwa msingi huo, tamko la ulinzi wa data kutoka kwa mtoaji wa huduma za malipo ndilo linahusika. Unapoagiza kitu kutoka duka letu la mtandaoni, data za malipo unazoingiza hutumwa moja kwa moja kwenda kwa mtoaji wa huduma za malipo aliyepewa kandarasi hiyo. Hatuna uwezo wa kutumia hizi data wakati wowote ule.

Kwa mantiki hii wakati mtoaji wa huduma za malipo anapochakata data zako zinazotoa utambulisho wa mtu binafsi kwa lengo la kukamilisha mchakato wa malipo, mf. mchakato wa malipo kwa njia ya kadi, kama mdhibiti kwa mujibu wa Ibara ya 4 (7) GDPR, tutakutumia taarifa ambazo mtoaji wa huduma za malipo anapaswa kuzitoa kwa mujibu wa Ibara ya 13, 14 GDPR.
Taarifa hizo zinapatikana hapa (PDF, 150 kB) zu finden.

Kama sehemu ya utekelezaji wa mkataba baina yetu na wewe, kwa mfano, kwa utoaji wa kozi za lugha, kwa nyakati fulani huwa tunatuma taarifa zako binafsi kwa mtoaji wa huduma ambaye anazichakata kwa niaba yetu na katika utaratibu wa mkataba uliopo baina ya Taasisi ya Goethe na mtoaji husika wa huduma kwa ajili ya utekelezaji mzuri wa mchakato. Mtoaji huyo wa huduma anaweza, kwa mfano, kuwa ndiye mzalishaji wa programu ya kompyuta ambayo hutumiwa na Taasisi ya Goethe katika utekelezaji wa mkataba.  

3. USAJILI NA AKAUNTI YA GOETHE.DE

Unatakiwa kufanya usajili na kutengeneza "akaunti ya Goethe.de" endapo una nia ya kutoa maoni au kuandika ujumbe, kubadilishana taarifa na watumiaji wengine, kushiriki kozi kwa njia ya mtandao, kutumia majukwaa ya mafunzo, kununua bidhaa kutoka duka la mtandaoni, kuazima vitu kidijitali na kuomba nafasi ya kushiriki kozi au kufanya mitihani au kutumia huduma zetu mtandaoni kwa lengo la rejea za maktaba (kufanya tafiti au kutoa ombi la kuwekewa vitabu, kuhuisha uanachama, nk.). Ili kujisajili, tunachakata data unazotumia kuingia kwenye akaunti yako (anuani ya baruapepe na nywila), kitendo kinachokupatia uwezo wa kutumia ofa mahsusi kutoka Taasisi ya Goethe, huduma nyingine kadri ya ridhaa yako pamoja na nchi yako na lugha unayopendelea.

  a) Data zinazokuhusu na maudhui unayoweka
Katika kuelekea kutengeneza akaunti ya Goethe.de, data ambazo tunazihitaji kwa lengo la utekelezaji wa utoaji wa ofa zetu au uhusiano wowote wa kimkataba baina yetu na wewe ndizo za lazima.

Tunakusanya na kuchakata data ulizotoa wewe mwenyewe ndani ya wigo wa utekelezaji wa mkataba wa mtumiaji kwa mujibu wa Ibara ya 6 (1) mstari wa 1 (b) GDPR ili
 • kuhakiki maombi yako ya akaunti ya Goethe.de
 • kutoa huduma bila malipo ambazo unashiriki (blogu, majukwaa, sehemu ya kutoa maoni, kujitambulisha, jumuiya za mtandaoni, majadiliano, nk.)
 • kutimiza wajibu wetu utokanao na mkataba uliopo baina yetu na wewe (utoaji wa kozi kwa njia ya mtandao, jukwaa la mafunzo na bidhaa za kidijitali kama sehemu ya mkopo, kufikishiwa bidhaa kutoka duka la mtandaoni pamoja na kuendesha kozi na mitihani, mikataba ya uazimishaji kutoka maktaba).
Unaweza kutoa kwa hiyari yako maelezo zaidi yanayokuhusu pamoja na maudhui unayoweka (hujulikana pia kama maudhui kutoka kwa mtumiaji), kama vile picha yako, maandishi katika mfumo wa blogu au ujumbe katika majukwaa, majadiliano, nk. Sehemu ya kujaza katika fomu huonesha ni data zipi hukusanywa kwa kina na taarifa zipi ni lazima na zipi ni hiyari. Tunachakata data ulizotoa kwa kwa hiyari yako kwa lengo la kulinda maslahi yetu mapana ya pamoja na anuai katika utaratibu wa jukwaa letu kwa mujibu wa Ibara ya 6 (1) mstari wa 1 (f) ya Kanuni ya Pamoja ya Umoja wa Ulaya ya Ulinzi wa Data (GDPR).  

b) Matangazo yanayomlenga mtumiaji
Kwa malengo ya kufanya matangazo, tunatumia pia data unazotoa kwenye akaunti yako ya mtumiaji kufanya ubunifu mahsusi unaomlenga mtumiaji wa tovuti yetu na ofa tunazotoa kwa njia ya intaneti, mf. ukurasa wa mtu binafsi na eneo lake la kuweka maelezo mafupi juu yake ambapo tunaweka ofa zinazokufaa. Hii husaidia kulinda masilahi na mamlaka yetu halali katika matangazo ya huduma tunazotoa kwa watumiaji kwa mujibu wa Ibara ya 6 (1) mstari wa 1 (f) ya Kanuni ya Pamoja ya Umoja wa Ulaya ya Ulinzi wa Data (GDPR).  

  c) Uchapishaji wa data
Baadhi ya data unazoingiza pale unapotumia akaunti ya Goethe.de huonekana pia kwa watumiaji wengine. Taarifa hizo zinajumuisha, kwa mfano, jina lako halisi au jina unalotumia kwenye akaunti yako, ujumbe unaotuma pamoja na tarehe na muda wa kutengeneza akaunti yako, makundi kwenye Tovuti ambapo wewe ni mwanachama, rafiki zako, orodha ya vitu ulivyosoma, nyaraka zako, ishara kuwa upo mtandaoni, viwango vyako, muda wa uanachama wako, jinsia yako na orodha ya wageni kwenye ukurasa wako. Uchapishaji wa data unatakiwa kufanyika kwa mujibu wa Ibara ya 6 (1) mstari wa 1 (b) GDPR ili kuweza kukupatia huduma za jukwaa letu ulizokubaliana nazo kimkataba.
   d) Mwingiliano wa data baina ya mfumo unaoratibu kozi zetu za lugha na akaunti yako ya Goethe.de kozi
Ili kuwezesha wasimamizi wa kozi na mitihani yetu kuona taarifa na matokeo yaliyomo kwenye akaunti ya Goethe.de, mwingiliano wa data (kuoanisha) hufanyika baina ya programu ya kompyuta inayotumika katika kozi na mitihani yetu na akaunti yako ya Goethe.de. Kwa mujibu wa Ibara ya 6 (1) mstari wa 1 (f) ya Kanuni ya Pamoja ya Umoja wa Ulaya ya Ulinzi wa Data (GDPR), hii husaidia kulinda maslahi yetu halali – katika muktadha wa mlingano wa maslahi – katika kuoanisha rekodi za data kwa lengo la kukuwezesha kuwa na udhibiti mkuu wa data unaofana pamoja na taarifa fupi juu ya kozi na mitihani uliyoomba kufanya, pia kwenye Tovuti yetu.

  e) Kufutwa
Endapo hutathibitisha usajili wako ndani ya siku 7, akaunti yako ya Goethe.de itafutwa pamoja na data ulizotoa wakati wa kujiandikisha. Unapothibitisha usajili, akaunti ya mtumiaji itatengenezwa kulingana na maelezo ya sasa. Hii haihusiki na akaunti za Goethe.de zilizotengenezwa kama sehemu ya kuagiza kutoka duka la mtandaoni. Hizi zitakuwa za kudumu isipokuwa ukiomba ziondolewe. Unaweza kufuta wakati wowote uleakaunti yako ya Goethe.de na data ulizotoa wakati wa kutumia akaunti hiyo na hili linaweza kufanyika kwa kutuma ujumbe kupitia mojawapo ya anuani zilitolewa hapa chini au kwa kutumia nyenzo inayopatikana kwenye akaunti ya mtumiaji ambayo imewekwa kwa lengo hili mahsusi.  


4. GOOGLE RECAPTCHA NA RAMANI ZA RAMANI ZA GOOGLE

  a) Google reCAPTCHA
Kwa lengo la ulinzi dhidi ya matumizi mabaya ya fomu zetu za kujaza mtandaoni pia dhidi ya ujumbe vamizi, tunatumia huduma za Google reCAPTCHA katika baadhi ya fomu kwenye tovuti hii. Ili kuthibitisha kuwa umeingiza taarifa kwa mkono, huduma hii huzuia programu vamizi zinazojiendesha zenyewe (bots) kufanya vitendo viovu kwenye tovuti. Kwa mujibu wa Ibara ya 6 (1) mstari wa 1 (f) ya Kanuni ya Pamoja ya Umoja wa Ulaya ya Ulinzi wa Data (GDPR), hii husaidia kulinda maslahi yetu halali katika ulinzi wa tovuti yetu dhidi ya matumizi mabaya na kutoa taswira nzuri ya uwepo wetu mtandaoni.

Google reCAPTCHA ni ofa kutoka Google Ireland Limited, kampuni iliyosajiliwa na kusimamiwa chini ya sheria za Ireland, ikiwa na ofisi yake rasmi Jengo la Gordon, Mtaa wa Barrow, Dublin 4, Ireland (www.google.de). Kwa mantiki hii taarifa zinapohamishwa kwenda kwenye seva za Google zilizopo Marekani na kuhifadhiwa huko, kampuni ya Kimarekani ya Google LLC inakuwa imepewa idhini chini ya Mpango unaozingatia mahitaji ya ulinzi wa data wakati wa kuhamisha taarifa binafsi baina ya Umoja wa Ulaya na Marekani (Privacy Shield). Idhini iliyotolewa hivi karibuni inaweza kuonekana hapa. Kwa msingi wa makubaliano haya baina ya Marekani na Tume ya Ulaya, Tume ya Ulaya imeweka kiwango cha kutosha cha ulinzi wa data kwa makampuni yaliyopewa idhini chini ya mpango huo. Google reCAPTCHA hutumia mfumo uliowekwa kwenye tovuti, ujulikanao kama JavaScript, kama sehemu ya uthibitisho wa mbinu zinazoruhusu uchanganuzi wa matumizi yako ya tovuti, kama vile vidakuzi. Taarifa za matumizi yako ya tovuti hii zinazokusanywa kwa mfumo unaojiendesha wenyewe, pamoja na anuani yako ya kipekee kwenye intaneti, kwa kawaida huhamishwa kwenda kwenye seva za Google zilizopo Marekani na kuhifadhiwa huko. Halikadhalika, vidakuzi vingine vinavyohifadhiwa kwenye programu itumikayo kuvinjari mtandaoni na huduma za Google hufanyiwa tathmini na Google reCAPTCHA.

Data zinazotoa utambulisho wa mtu binafsi haziwezi kusomwa au kuhifadhiwa kwenye sehemu za kujaza taarifa katika fomu husika. Maelezo zaidi juu ya sera za Google kuhusu faragha yanapatikana kupitia www.google.com/policies/privacy/.

Unaweza kuzuia Google isikusanye data zinazotokana na JavaScript au kidakuzi na data zinazohusiana na matumizi yako ya tovuti (pamoja na anuani yako ya kipekee kwenye intaneti, ) na kuzuia mchakato wa Google wa hizo data kwa kuzuia JavaScript au kukataa mpangilio wa vidakuzi kwenye programu itumikayo kuvinjari mtandaoni. Tafadhali zingatia kwamba kwa kufanya hivyo unaweza kuzuia utendaji kwa baadhi ya nyenzo kwenye tovuti yetu zilizowekwa kwa matumizi yako.

  b) Ramani za Google
Kwenye Tovuti yetu tunatumia mfumo mzima wa Ramani za Google kuonesha taarifa za kijiografia. hii husaidia kulinda masilahi na mamlaka yetu halali katika utoaji mzuri wa huduma zetu katika vituo vyetu tunapohakiki maslahi husika, kwa mujibu wa Ibara ya 6 (1) mstari wa 1 (f) wa Kanuni ya Pamoja ya Umoja wa Ulaya ya Ulinzi wa Data (GDPR)GDPR.

Ramani za Google ni ofa kutoka Google Ireland Limited, kampuni iliyosajiliwa na kusimamiwa chini ya sheria za Ireland, ikiwa na ofisi yake rasmi Jengo la Gordon, Mtaa wa Barrow, Dublin 4, Ireland (www.google.de).

Kwa mantiki hii wakati taarifa zinapelekwa kwenye seva za Google zilizopo Marekani na kuhifadhiwa huko, kampuni ya Kimarekani ya Google LLC inakuwa imepewa idhini chini ya Mpango unaozingatia mahitaji ya ulinzi wa data wakati wa kuhamisha taarifa binafsi baina ya Umoja wa Ulaya na Marekani (Privacy Shield). Idhini iliyotolewa hivi karibuni inaweza kusomwa hapa Tume ya Ulaya imeweka kiwango cha kutosha cha ulinzi wa data kwa makampuni yaliyopewa idhini chini ya mpango huo, kwa msingi wa makubaliano haya baina ya Marekani na Tume ya Ulaya. Unapoingia kwenye tovuti inayotumia Ramani za Google, seva ya tovuti ya Google kwa kujiendesha yenyewe hutunza kwenye nyaraka za seva data za ufikivu kama vile jina la faili ulilofungua, tovuti ya mwisho kuingia na tarehe na muda wa kuingia kwenye tovuti, programu itumikayo kuvinjari mtandaoni, uhamishaji wa data, kiasi cha data kilichohamishwa, anuani ya kipekee kwenye intaneti, mtoa huduma ya mtandao, nk. Unapotumia Ramani za Google, Google pia huchakata data juu matumizi ya nyenzo za ramani kutoka kwa watumiaji wa tovuti.

Maelezo zaidi kuhusujuu ya sera za Google kuhusu faragha na uchaguzi wa mpangilio unaoutaka yanapatikana kupitia https://policies.google.com/privacy.

 

5. UKUSANYAJI NA MATUMIZI YA DATA KWA MAlengo YA MATANGAZO

  a) Matangazo kwa njia ya posta
Tunayo haki ya kutumia majina na anuani yako kamili ya posta kwa lengo la kufanya matangazo yetu, mf. kukutumia ofa zinazoweza kukuvutia na taarifa juu ya bidhaa zetu kwa njia ya posa. Hii husaidia kulinda masilahi na mamlaka yetu halali katika kuwasiliana na wateja wetu kwa lengo la matangazo kwa mujibu wa Ibara ya 6 (1) (f) ya Kanuni ya Pamoja ya Umoja wa Ulaya ya Ulinzi wa Data (GDPR). Unaweza kupinga taarifa zako binafsi kuhifadhiwa na kutumika kwa malengo hayo wakati wowote ule kwa kutuma ujumbe kwenda  datenschutz@goethe.de 

  b) Jarida kwa njia ya baruapepe
Ikiwa utajisajili kupokea mojawapo ya majarida yetu, tutatumia data zinazohitajika kwa lengo hili mahsusi au data ulizotoa kwingineko ili kukutumia jarida husika kwa njia ya baruapepe kila linapotoka. Kutumiwa jarida kwa njia ya baruapepe hufanyika kwa msingi wa ridhaa yako uliyotoa kwa mujibu wa Ibara ya 6 (1) mstari wa 1 (a) GDPR. Kwa sababu za usalama, tunatumia mchakato wa kujirudia mara mbili: Tutakutumia jarida kwa njia ya baruapepe endapo tu utakuwa umethibitisha usajili wako kuhusiana na jarida hilo. Kwa lengo hili mahsusi, tutakutumia baruapepe ya kuthibitisha usajili wako kupitia kiunga kilichomo ndani yake. Hii ni kuhakikisha kwamba ni wewe pekee, kama mmiliki wa anuani ya baruapepe iliyotolewa, ndiye unaweza kupokea jarida.

Jarida linaweza kutumwa kupitia mtoaji wa huduma ambaye si Taasisi ya Goethe, na ambaye tutampatia anuani yako ya baruapepe kwa lengo hili mahsusi. Katika mazingira hayo, mchakato unatekelezwa kwa niaba yetu. Unaweza kupinga matumizi haya ya anuani yako ya baruapepe wakati wowote ule kwa kutuma ujumbe kwenda mojawapo ya anuani zilitolewa hapa chini au kupitia kiunga ambacho kimewekwa kwa lengo hili mahsusi kwenye baruapepe inayohusiana na tangazo, bila kuingia gharama yoyote isipokuwa gharama za utumaji kulingana na viwango vya msingi.

Ikiwa mtoaji wa huduma ni kampuni ya Kimarekani, daima tunahakikisha kwamba imepewa idhini kulingana na mpango unaozingatia mahitaji ya ulinzi wa data wakati wa kuhamisha taarifa binafsi baina ya Umoja wa Ulaya na Marekani (Privacy Shield). Idhini iliyotolewa hivi karibuni inaweza kusomwa hapa Tume ya Ulaya imeweka kiwango cha kutosha cha ulinzi wa data kwa makampuni yaliyopewa idhini chini ya mpango huo kutokana na makubaliano haya baina ya Marekani na Tume ya Ulaya.  

6. VIDAKUZI

Tunatumia vidakuzi kwenye kurasa kadha wa kadha ili kuifanya tovuti yetu kuwa na mvuto na ili kuwezesha matumizi ya nyenzo fulani. Hii husaidia kulinda masilahi na mamlaka yetu halali katika utoaji mzuri wa huduma zetu kwa mujibu wa Ibara ya 6 (1) mstari wa 1 (f) ya Kanuni ya Pamoja ya Umoja wa Ulaya ya Ulinzi wa Data (GDPR). Vidakuzi ni nyaraka ndogo za maandishi zinazohifadhiwa kwenye kifaa unachotumia.

Baadhi ya vidakuzi tunavyotumia hufutwa tena baada ya kumalizika kwa duru ya programu itumikayo kuvinjari mtandaoni, mf. baada ya kufunga programu yako itumikayo kuvinjari mtandaoni (vidakuzi vya duru). Vidakuzi vingine hubaki kwenye kifaa unachotumia na hutuwezesha kutambua programu yako itumikayo kuvinjari mtandaoni pale utakapoingia tena, kama ni muhimu, programu hiyo hukuwezesha kuingia kwa kujiendesha yenyewe (vidakuzi-chagizi). Endapo, kwa mfano, umefanya uchaguzi wa "Remain logged in" kwa kuweka alama ya pata pale unapoingia goethe.de, kidakuzi kitawekwa ambacho hutuwezesha kukutambua pale unapotembelea tovuti ya goethe.de katika kipindi fulani cha muda.

Unaweza kuangalia muda uliowekwa wa vidakuzi-chagizi kupitia programu yako itumikayo kuvinjari mtandaoni. Unaweza kuipa programu yako itumikayo kuvinjari mtandaoni uwezo wa kukutaarifu juu ya mpangilio wa vidakuzi na kuamua mwenyewe kuvikubali au kuvikataa katika baadhi ya mazingira au kwa ujumla wake. Programu moja itumikayo kuvinjari mtandaoni ni tofauti na nyingine kwa namna inavyoshughulikia mpangilio wa kidakuzi. Jambo hili limeelezwa kwenye orodha ya vitenda kazi vya kutoa msaada ya kila programu itumikayo kuvinjari mtandaoni, ambayo hufafanua jinsi unavyoweza kubadili mipangilio yako ya vidakuzi.

Endapo vidakuzi vinakataliwa, kuna uwezekano wa utendaji wa tovuti yetu kutokuwa mkamilifu.  

7. UCHANGANUZI WA MTANDAO

  a) Webtrekk
Tunatumia huduma za Webtrekk (www.webtrekk.com), kukusanya data za kitakwimu za matumizi ya tovuti yetu, ili kuiboresha, kuwezesha uchanganuzi wa matumizi ya tovuti yetu na kuandika ripoti juu ya shughuli za tovuti. Hii husaidia kulinda masilahi na mamlaka yetu halali katika utoaji mzuri wa huduma zetu kwa mujibu wa Ibara ya 6 (1) mstari wa 1 (f) ya Kanuni ya Pamoja ya Umoja wa Ulaya ya Ulinzi wa Data (GDPR). Vidakuzi vinaweza kutumika kwa lengo hili mahsusi. Ndani ya utaratibu wa ufuatiliaji huu, huwekwa kwenye tovuti sehemu la kuweka taarifa binafsi kwa kutumia jina la kukopa. Haya maelezo hayataunganishwa na data zinazotoa utambulisho wa mtu binafsi anayetumia jina la kukopa isipokuwa kwa ridhaa ya wazi ya mtumiaji huyo. Baada ya kusitishwa kwa lengo hili na ukomo wa matumizi yetu ya Webtrekk, data zinazokusanywa kwa kusudio hili zitafutwa.
Unaweza kuzuia matumizi ya baadaye ya kukusanya na kuhifadhi data hizi wakati wowote ule kwa kubofya kitufe hiki.Ili kuweza kutekeleza pingamizi hili wakati wa kuingia tena kwenye tovuti, uchaguzi huu utahifadhiwa kwenye kidakuzi katika programu yako itumikayo kuvinjari mtandaoni. Kufuatia pingamizi lako, kidakuzi cha kukupa uamuzi wa kujiondoa huwekwa kwenye kifaa unachotumia. Endapo utafuta vidakuzi vyako, utalazimika kubofya tena kiunga.

  b) Google(Universal) Analytics
Tovuti hii hutumia Google (Universal) Analytics kwa lengo la uchanganuzi wa tovuti, ambayo ni huduma kutoka Google Ireland Limited (www.google.de). Huduma hii husaidia kulinda masilahi na mamlaka yetu halali katika utoaji mzuri wa huduma zetu kwa mujibu wa Ibara ya 6 (1) mstari wa 1 (f) ya Kanuni ya Pamoja ya Umoja wa Ulaya ya Ulinzi wa Data (GDPR). Google (Universal) Analytics hutumia mbinu zinazowezesha uchanganuzi wa matumizi yako ya tovuti, kama vile vidakuzi. Kwa kawaida, taarifa zinazokusanywa kwa mfumo unaojiendesha wenyewe juu ya matumizi yako ya tovuti hii huhamishwa hadi seva za Google zilizopo Marekani na kuhifadhiwa huko. Kwa kubofya kitufe cha kufanya usijulikane kilichowekwa kwenye Tovuti hii, anuani ya kipekee kwenye mtandao hufupishwa kabla ya kuhamishwa kutoka nchi wanachama wa Umoja wa Ulaya au nchi nyingine ambao ni wanachama wa Mkataba wa Zoni ya Kiuchumi ya Ulaya. Ni katika mazingira machache sana ambapo anuani ya kipekee kwenye mtandao huhamishwa kama ilivyo kwenda kwenye seva za Google zilizopo Marekani na kufupishwa huko. Kimsingi anuani ya kipekee kwenye mtandao yenye utambulisho usiojulikanailiyotolewa na programu yako itumikayo kuvinjari mtandaoni katika muktadha wa Google Analytics haitaunganishwa na data nyingine za Google. Baada ya kusitishwa kwa lengo hili na ukomo wa matumizi yetu ya Google Analytics, data zilizokusanywa kwa kusudio hili zitafutwa.   

Google Ireland Limited ni kampuni iliyosajiliwa na kusimamiwa chini ya sheria za Ireland ikiwa na ofisi yake rasmi Jengo la Gordon, Mtaa wa Barrow, Dublin 4, Ireland (www.google.de).
Kwa mantiki hii wakati taarifa zinapelekwa kwenye seva za Google zilizopo Marekani na kuhifadhiwa huko, kampuni ya Kimarekani ya Google LLC inakuwa imepewa idhini chini ya Mpango unaozingatia mahitaji ya ulinzi wa data wakati wa kuhamisha taarifa binafsi baina ya Umoja wa Ulaya na Marekani (Privacy Shield). Idhini iliyotolewa hivi karibuni inaweza kusomwa hapa Tume ya Ulaya imeweka kiwango cha kutosha cha ulinzi wa data kwa makampuni yaliyopewa idhini chini ya mpango huo kutokana na makubaliano haya baina ya Marekani na Tume ya Ulaya.

Unaweza kuzuia ukusanyaji wa data zinazotolewa na kidakuzi kuhusiana na matumizi yako ya tovuti (pamoja na anuani yako ya kipekee kwenye mtandao, ) pamoja na uchakataji kwa hizi data unaofanywa na Google, kwa kupakua na kuweka katika kifaa chako kiongezi cha programu itumikayo kuvinjari mtandaoni kinazopatikana kupitia kiunga kifuatacho: https://tools.google.com/dlpage/gaoptout?hl=de

Ikiwa huhitaji kiongezi hicho, unaweza kubofya kiunga hiki ili kuzuia ukusanyaji unaofanywa na Google Analytics kwenye tovuti hii kwa matumizi ya baadaye. Kidakuzi kinachokupa uamuzi wa kujiondoa kimewekwa kwenye kifaa unachotumia. Endapo utafuta vidakuzi vyako, utalazimika kubofya tena kiunga.

  c) Matumizi ya uchanganuzi wa programu ya Yandex-Metrica
Tunatumia Yandex.Metrica, huduma ya uchanganuzi wa mtandao na ufuatiliaji wa watumiaji na uboreshaji wa tovuti kutoka kampuni ya Yandex Oy, Moreenikatu 6, 04600 Mantsala, Finland.

Yandex.Metrica inatuwezesha kuchanganua uingiaji na utokaji wa watumiaji wa tovuti yetu na maingiliano baina yao na vitenda kazi vya tovuti, ili kuelewa jinsi tovuti yetu inavyotumia pamoja na nyenzo na maudhui yenye mvuto kwa watumiaji. Hii inatuwezesha kutathmini na kuboresha nyenzo na maudhui ya tovuti yetu. Kwa kuwa matokeo ya majaribio haya yanakuwa sahihi zaidi endapo maingiliano ya watumiaji yanafuatiliwa kwa kipindi fulani cha muda (mf. watumiaji walewale wakitumia nyenzo au maudhui yaleyale kwa kujirudiarudia), vidakuzi huhifadhiwa kwenye vifaa vya watumiaji. Anuani ya kipekee ya mtumiaji kwenye intaneti nayo pia hurekodiwa, lakini ikiwa imefupishwa kwa digiti mbili. Zaidi ya hapo, data hukusanywa kwenye vifaa vya matumizi (mf. Kompyuta au simu), mifumo na programu zitumikazo kuvinjari mtandaoni, pamoja na muda wa matumizi na huduma kutoka kwenye tovuti zetu au tovuti wanazotembelea watumiaji baada ya kuondoka kwenye tovuti zetu.

Taarifa zinazokusanywa kwa msaada wa Yandex.Metrica zinachakatwa kwa niaba yetu pekee na kwa kufuata maelekezo yetu. Kwa lengo hili mahsusi, tumeingia mkataba na Yandex Oy mujibu wa Ibara ya 28 ya GDPR (https://yandex.com/legal/metrica_agreement/)

Kwa mantiki hii wakati data zinachakatwa nchi nyingine (mf.nje ya Umoja wa Ulaya au Zoni ya Kiuchumi ya Ulaya), hili itafanyika endapo tu kuna hakikisho la uzingativu wa kiwango cha ulinzi wa data kilichokubaliwa na GDPR. Halikadhalika, mkataba ambao msingi wake ni sheria za ulinzi wa data zinazotumika Umoja wa Ulaya kulingana na matakwa ya Tume ya Umoja wa Ulaya ulitiwa saini baina ya Yandex Oy na YANDEX LLC, 16 Lva Tolstogo st., Moscow, 11 902 1, Urusi, ambao ndio wahusika wa kuchakata data.

Data zinazotoa utambulisho wa mtu binafsi za watumiaji zinachakatwa kwa msingi unaozingatia maslahi yetu halali (mf. maslahi ya kuchanganua, kuboresha na kuendesha kiuchumi ofa zetu kwa njia ya mtandao, kwa mujibu wa tafsiri kutoka Ibara ya 6 (1) mstari wa 1 (f)) GDPR.

Maelezo zaidi kuhusu Yandex.Metrica, yanapatikana kwenye sera ya faragha ya mtoa huduma: https://yandex.com/legal/privacy/.

Endapo unataka kuzuia uchakataji kwa taarifa zako binafsi unaofanywa na Yandex.Metrica (kujiondoa) kwenye tovuti zote zinazotumia Yandex.Metrica, unaweza kuweka kiongezi cha programu itumikayo kuvinjari mtandaoni kwa lengo hili mahsusi:
https://yandex.com/support/metrica/general/opt-out.html

  d) Google Tag Manager
Tunatumia Google Tag Manager kuratibu huduma za matangazo zitokanazo na matumizi. Hii husaidia kulinda masilahi na mamlaka yetu halali katika kuboresha matangazo kwenye tovuti yetu kwa mujibu wa Ibara ya 6 (1) mstari wa 1 (f) ya Kanuni ya Pamoja ya Umoja wa Ulaya ya Ulinzi wa Data (GDPR). Mfumo huu wa lebo ni uwanja usiotumia vidakuzi na haukusanyi data zozote zinazotoa utambulisho wa mtu binafsi. Badala yake, huziamsha lebo nyingine, ambazo huweza kukusanya data.

Google Tag Manager ni ofa kutoka Google Ireland Limited, kampuni iliyosajiliwa na kusimamiwa chini ya sheria za Ireland, ikiwa na ofisi yake rasmi Jengo la Gordon, Mtaa wa Barrow, Dublin 4, Ireland (www.google.de).  Kwa mantiki hii wakati taarifa zinapelekwa kwenye seva za Google zilizopo Marekani na kuhifadhiwa huko, kampuni ya Kimarekani ya Google LLC inakuwa imepewa idhini chini ya Mpango unaozingatia mahitaji ya ulinzi wa data wakati wa kuhamisha taarifa binafsi baina ya Umoja wa Ulaya na Marekani (Privacy Shield). Idhini iliyotolewa hivi karibuni inaweza kusomwa hapa. Tume ya Ulaya imeweka kiwango cha kutosha cha ulinzi wa data kwa makampuni yaliyopewa idhini chini ya mpango huo kutokana na makubaliano haya baina ya Marekani na Tume ya Ulaya.

Endapo umezuia mfumo huu au kiwango cha kidakuzi, mfumo utabaki ukiwa umezuiwa kufuatilia lebo zilizomo kwenye Google Tag Manager.  

8. MITANDAO YA KIJAMII

  a) Matumizi ya viongezi na vifaa-mkato vya Facebook, Twitter, Google+, Instagram na VKontakte kwa njia ya mtandaoni ya Shariff
Vitufe pamoja na vifaa-mkato vinavyojulikana kama widgets kutoka mitandao ya kijamii hutumika kwenye Tovuti yetu.

Kwa lengo la kuongeza ulinzi wa taarifa zako binafsi unapotembelea tovuti yetu, vitufe hivi pamoja na vifaa-mkato kuonekana kwenye ukurasa vikiwa siyo sehemu kamili ya kurasa, bali hufikiwa kupitia kiunga cha HTML. Mwingiliano huu unatoa hakikisho kwamba hata baada ya kuingia kwenye ukurasa wa tovuti yetu wenye vitufe hivyo, kunakuwa bado hakujafanyika mawasiliano na seva za mtoa huduma wa mtandao husika wa kijamii.

Unapobofya mojawapo ya vitufe, ukurasa mpya wa programu yako itumikayo kuvinjari mtandaoni hufunguka na kufungua ukurasa wa mtoaji husika wa huduma, ambapo kwa mfano unaweza kubofya kitufe cha “Like” au “Share,” (hii inaweza kuwa baada ya kuingiza data unazotumia kuingia kwenye akaunti yako).

Lengo na wigo wa ukusanyaji wa data na mwendelezo wa mchakato na matumizi yake unaofanywa watoa huduma kwenye tovuti zao, pamoja na uchaguzi wa hiyari wa kushirikisha kumbukumbu zako za mawasiliano na haki zako na uchaguzi wa mpangilio unaoutaka kwa lengo la ulinzi wa faragha yako, zinapatikana kwenye sera za faragha za watoa huduma:

https://www.facebook.com/policy.php
https://twitter.com/privacy
https://help.instagram.com/155833707900388
https://vk.com/privacy/eu

    b) Matumizi ya vifaa-mkato vya Spotify na Soundcloud
Tunatumia vifaa-mkato kutoka Spotify na Soundcloud kwenye tovuti yetu kwa lengo la kupendezesha maudhui yetu. Hii husaidia kulinda maslahi yetu mapana ya utoaji wa huduma na shughuli zetu kwa njia mseto kwa mujibu wa Ibara ya 6 (1) mstari wa 1 (f) ya Kanuni ya Pamoja ya Umoja wa Ulaya ya Ulinzi wa Data (GDPR).

Unapofungua ukurasa wenye kiongezi kwenye tovuti yetu, programu yako itumikayo kuvinjari mtandaoni itawasiliana moja kwa moja na seva za Spotify au Soundcloud. Maudhui ya viongezi huhamishwa na mtoa huduma husika moja kwa moja hadi kwenye programu yako itumikayo kuvinjari mtandaoni na kuonekana kwenye ukurasa. Kupitia viongezi, watoa huduma hupokea taarifa ambayo programu yako itumikayo kuvinjari mtandaoni imechukua kutoka kwenye ukurasa wa tovuti yetu, hata kama huna eneo la kuweka taarifa binafsi au haupo mtandaoni kwa wakati huo. Taarifa hizo (pamoja na anuani yako ya kipekee kwenye mtandao) huhamishwa na programu yako itumikayo kuvinjari mtandaoni moja kwa moja hadi kwenye seva ya mtoa huduma husika na kuhifadhiwa huko.

Endapo umeingia kwenye mojawapo ya huduma zinazotolewa kwenye tovuti yetu, watoa huduma wanaweza kupeleka moja kwa moja taarifa za uwepo wako hadi kwenye eneo lako la kuweka taarifa binafsi la mtandao husika wa kijamii. Kunapotokea mwingiliano baina yako na viongezi, kwa mfano unapoperuzi maudhui, taarifa unazopokea nazo pia hupelekwa moja kwa moja hadi kwenye seva ya watoa huduma na kuhifadhiwa huko.

Taarifa inaweza pia kuchapishwa kwenye mtandao wa kijamii na kuonekana kwenye taarifa zako za mawasiliano.

Lengo na wigo wa ukusanyaji wa data na mwendelezo wa mchakato na matumizi yake unaofanywa watoa huduma kwenye tovuti zao, pamoja na uchaguzi wa hiyari wa kushirikisha kumbukumbu zako za mawasiliano na haki zako na uchaguzi wa mpangilio unaoutaka kwa lengo la ulinzi wa faragha yako, zinapatikana kwenye sera za faragha za watoa huduma:

Spotify AB: https://www.spotify.com/de/legal/privacy-policy/
SoundCloud Limited: https://soundcloud.com/pages/privacy

Endapo hutaki mitandao ya kijamii kuhusika na data zinazokusanywa kupitia tovuti yetu moja kwa moja kutoka eneo lako la kuweka taarifa binafsi kwenye huduma husika, unaweza kuzuia kabisa vifaa-mkato pamoja na viongezi vya programu yako itumikayo kuvinjari mtandaoni kufanya kazi, mf. kutumia nyenzo iitwato "NoScript" (https://noscript.net/)."   

c) Kuingiza na kuonesha yaliyomo kwenye mtandao wa kijamii
Twitter, Instagram und Facebook
Kwenye tovuti yetu, hasa kuhusiana na makala kutoka Taasisi ya Goethe, maudhui (maandishi/pisha, maoni na/au chaneli za habari) kutoka Twitter, Instagram na Facebook huweza kutumika kupitia viongezi za kijamii.

Maingiliano haya yana msingi wake kwenye Embetty (Heise Medien GmbH & Co. KG, Artikel zu Embetty). Hii hutoa hakikisho kwamba hakuna mawasiliano ya moja kwa moja baina ya mteja na huduma ya mtandao wa kijamii unaohusika. Ni pale tu kunapotokea maingiliano baina yako na maudhui (mf. unapotoa maoni, unapobofya kitufe cha LIKE), ndipo unapoingia mara moja kwenye huduma ya mtandao wa kijamii na uhamishaji wa data hufanyika. Hii inaweza kuhusisha data zifuatazo:
 • Tovuti ulizotembelea
 • Taarifa za programu itumikayo kuvinjari mtandaoni
 • Taarifa kuhusu mfumo unaoendesha kompyuta yako
 • Anuani ya kipekee kwenye mtandao

ZIMA VIONGEZI

Twitter

Einwilligung für Twitter widerrufen Einwilligung erfolgreich widerrufen

Instagram

Einwilligung für Instagram widerrufen Einwilligung erfolgreich widerrufen


Maudhui kutoka mitandao mingine ya kijamii
Halikadhalika, maudhui kutoka mitandao mingine ya kijamii (mf. Spotify na Soundcloud) yanaweza kutumika kupitia viongezi za kijamii. Kupitia viongezi vya kijamii, mawasiliano ya moja kwa moja yanaweza kuanza kwenye seva za mtandao husika, ambapo data hupelekwa kwa mtoa huduma. Hii inaweza kuhusisha data zifuatazo:
 • Tovuti ulizotembelea
 • Programu itumikayo kuvinjari mtandaoni taarifa
 • Taarifa kuhusu mfumo unaoendesha kompyuta yako
 • Anuani ya kipekee kwenye mtandao
Hii husaidia kulinda maslahi yetu mapana ya utumiaji wa njia mseto katika utoaji wa huduma na shughuli zetu kwa mujibu wa Ibara ya 6 (1) mstari wa 1 (f) ya Kanuni ya Pamoja ya Umoja wa Ulaya ya Ulinzi wa Data (GDPR).

  d) Viongezi vya video kutoka YouTube na Vimeo
Kwenye Tovuti hii, maudhui kutoka tovuti nyingine yanaonekana kupitia YouTube na Vimeo kwa lengo la usanifu shirikishi wa maudhui yetu.

YouTube inaendeshwa na Google Ireland Limited, kampuni iliyosajiliwa na kusimamiwa chini ya sheria za Ireland, ikiwa na ofisi yake rasmi Jengo la Gordon, Mtaa wa Barrow, Dublin 4, Ireland. ("Google").

Vimeo inaendeshwa na Vimeo LLC, Mtaa wa 555 West 18th, New York, New York 10011, USA.

Ili kuongeza ulinzi wa taarifa zako binafsi unapotembelea tovuti yetu, viongezi huonekana kwenye ukurasa kwa namna ambayo vinaweza kuwashwa kwa kubofya tena. Maingiliano huya hutoa hakikisho kwamba hata baada ya kuingia kwenye ukurasa wa tovuti yetu wenye viongezi, kunakuwa bado hakujafanyika mawasiliano na seva za mtandao husika wa kijamii. Ni pale tu utakapowasha viongezi ndipo programu yako itumikayo kuvinjari mtandaoni itaanzisha mawasiliano ya moja kwa moja na seva za mtandao husika wa kijamii. 

Mtoa huduma husika hupeleka maudhui ya kiongezi moja kwa moja hadi kwenye programu yako itumikayo kuvinjari mtandaoni na kuonekana kwenye ukurasa. Kupitia viongezi, watoa huduma hupokea taarifa ambayo programu yako itumikayo kuvinjari mtandaoni imechukua kutoka kwenye ukurasa wa tovuti yetu, hata kama huna eneo la kuweka taarifa binafsi au haupo mtandaoni kwa wakati huo. Taarifa hizo (pamoja na anuani yako ya kipekee kwenye mtandao) huhamishwa na programu yako itumikayo kuvinjari mtandaoni moja kwa moja hadi kwenye seva ya mtoa huduma husika (huenda Marekani) na kuhifadhiwa huko.

Kunapotokea mwingiliano baina yako na viongezi, kwa mfano kwa kubofya kitufe cha "Like", taarifa unazopokea nazo pia hupelekwa moja kwa moja hadi kwenye seva ya watoa huduma na kuhifadhiwa huko.

Pale unapowasha kiongezi, kidakuzi nacho huanza kufanya kazi kwenye programu itumikayo kuvinjari mtandaoni. Unaweza kuzima kiongezi kwa kubofya kitufe ambacho kimewekwa kwa lengo hili mahsusi. Kwa kufanya hivyo utafuta kidakuzi pia.

ZIMA KIONGEZI

Youtube

Einwilligung für YouTube widerrufen Einwilligung erfolgreich widerrufen

Vimeo

Einwilligung für Vimeo widerrufen Einwilligung erfolgreich widerrufen

Kwa upande wa video kutoka YouTube ambazo zimewekwa kwenye kwenye tovuti yetu, mpangilio wa faragha wa hali ya juu zaidi umewezeshwa. Hii ina maana kuwa hakuna taarifa itakayokusanywa na kuhifadhiwa kutoka kwa watumiaji wa tovuti na kutumwa YouTube isipokuwa pale watumiaji wanapoangalia video.

Video kutoka Vimeo ambazo zimewekwa kwenye kwenye tovuti yetu zinatumia mfumo uliounganishwa wa Google Analytics unaojiendesha wenyewe. Hatuna uwezo wa kuathiri matokeo ya uchanganuzi na hatuwezi kuyaona. Halikadhalika, kwa kujumuisha video za Vimeo, violezo vya kutoa tahadhari mtandaoni huwepo kwa lengo la watumiaji wa tovuti pale wanapoviwasha. Ili kuzuia vidakuzi fuatilizi vya Google Analytics kufanya kazi, unaweza kuchukua tahadhari ya kawaida ya kuzima Google Analytics. Kwa taarifa zaidi, angalia seksheni ya uchanganuzi wa mtandao.

Matumizi haya husaidia kulinda maslahi yetu mapana ya matumizi ya njia mseto katika utoaji wa huduma na shughuli zetu kwa mujibu wa Ibara ya 6 (1) mstari wa 1 (f) ya Kanuni ya Pamoja ya Umoja wa Ulaya ya Ulinzi wa Data (GDPR). Lengo na wigo wa ukusanyaji wa data na mwendelezo wa mchakato wake na matumizi ya data ya watoa huduma na haki zako na uchaguzi wa mpangilio unaoutaka kwa lengo la ulinzi wa faragha yako, zinapatikana kwenye sera ya faragha wa watoa huduma:

YouTube / Google: https://www.google.de/intl/de/policies/privacy/ 
Vimeo: https://vimeo.com/privacy

  e) Uwepo wetu kwenye mitandao ya kijamii
Uwepo wetu kwenye mitandao na majukwaa ya kijamii umefanywa kwa malengo ya mawasiliano bora, yenye tija, baina yetu na wateja wetu pamoja na wadau wengine. Tunatoa taarifa kuhusu bidhaa zetu kupitia mitandao hiyo.

Unapotembelea mitandao yetu ya kijamii taarifa zako binafsi zinaweza kukusanywa kwa kujiendesha zenyewe na kuhifadhiwa kwa lengo la tafiti za masoko na kutoa matangazo. Kutokana na hizi data, eneo la kuweka taarifa binafsi za mtumiaji hutengenezwa kwa kutumia jina la kukopa. Majina haya yanaweza kutumika, kwa mfano, kuweka matangazo ndani na nje ya majukwaa ambayo yanadhaniwa kuendana na maslahi yako. Kwa lengo hili mahsusi, vidakuzi hutumika kwenye kifaa unachotumia. Vidakuzi hivi hutunza kumbukumbu ya tabia na maslahi ya watumiaji. Hii husaidia kulinda masilahi na mamlaka yetu halali katika utoaji mzuri wa huduma zetu na mawasiliano yenye kuleta tija baina yetu na wateja wetu pamoja na wadau wengine tukihakiki maslahi husika, kwa mujibu wa Ibara ya 6 (1) mstari wa 1 (f) GDPR. Endapo mwendeshaji wa jukwaa husika la mtandao wa kijamii amekuomba idhini (ruhusa) ya uchakataji wa data, mf. kwa njia ya visanduku vya kuweka alama ya kukubali, msingi wa kisheria wa uchakataji wa data ni Ibara ya 6 (1) mstari wa 1 (a) GDPR.

Kwa kuwa majukwaa ya mitandao ya kijamii yaliyotajwa hapo juu yana makao yake makuu nchini Marekani, Tume ya Umoja wa Ulaya imechukua uamuzi unaofaa kwa lengo la Marekani. Hii inaturudisha kwenye mpango unaozingatia mahitaji ya ulinzi wa data wakati wa kuhamisha taarifa binafsi baina ya Umoja wa Ulaya na Marekani (Privacy Shield). Idhini iliyotolewa hivi karibuni kwa lengo la kampuni husika inaweza kusomwa hapa

Kwa taarifa za kina juu ya uchakataji na matumizi ya data ya watoa huduma kwenye tovuti zao, pamoja na hiyari ya kushirikisha kumbukumbu zako za mawasiliano na haki zako na uchaguzi wa mpangilio unaoutaka kwa lengo la ulinzi wa faragha yako, hasa hiyari juu ya uamuzi wa kujitoa, tafadhali rejelea sera za faragha za watoa huduma kupitia viunga vilivyowekwa hapa chini. Endapo bado unahitaji msaada juu ya suala hili, unaweza kuwasiliana nasi.

Facebook: https://www.facebook.com/about/privacy/     
Uwezekano wa rufaa (kujiondoa):
Facebook: https://www.facebook.com/settings?tab=ads  
 

9. UHAMISHAJI WA DATA KWENDA KWA MHUSIKA MWINGINE

  a) Uhamishaji wa data kwenda Goethe-Instituts
Mara baada ya akaunti yako ya Goethe.de kutengenezwa, maofisa kutoka Taasisi ya Goethe inayohusika, iliyopo nchi za nje, wanapewa uwezo wa kutumia data zilizohifadhiwa kwenye akaunti. Uchakataji wa data unaotokea katika mazingira haya kwa upande mmoja hufanyika kwa malengo ya uchakataji wa kiofisi wa data za mtumiaji, mf. urekebishaji/uzuiaji/uondoaji au utoaji wa majukumu na idhini ndani ya mfumo. Msingi wa kisheria wa utekelezaji wa kwa lengo la mkataba ni Ibara ya 6 (1) mstari wa 1 (f) ya Kanuni ya Pamoja ya Umoja wa Ulaya ya Ulinzi wa Data (GDPR). Zaidi ya hapo, kwa mujibu wa Ibara ya 6 (1) mstari wa 1 (f) ya Kanuni ya Pamoja ya Umoja wa Ulaya ya Ulinzi wa Data (GDPR), hii husaidia kulinda masilahi na mamlaka yetu halali ya taarifa halali na kumbukumbu sahihi za data katika mfumo wetu. Kwa upande mwingine, data za mtumiaji (katika mtindo usiotoa utambulisho wake) zinaweza kutumika kuboresha tovuti yetu. Hii husaidia kulinda masilahi na mamlaka yetu halali katika kuboresha huduma tunazotoa kwa mujibu wa Ibara ya 6 (1) mstari wa 1 (f) ya Kanuni ya Pamoja ya Umoja wa Ulaya ya Ulinzi wa Data (GDPR).

Kwa mantiki hii data zinazotoa utambulisho wa mtu binafsi zinapohamishwa kwenda Taasisi ya Goethe iliyopo nchi nyingine na isiyofuata uamuzi unaofaa uliotolewa na Tume ya Umoja wa Ulaya kwa mujibu wa Ibara ya 45 (1) GDPR, uhamishaji wa data hufanyika kwa msingi wa sheria za ulinzi wa data zinazotumika Umoja wa Ulaya zilizotungwa na Tume ya Umoja wa Ulaya kama hakikisho la kufaa kwa mujibu wa Ibara ya 46 (2) (c) GDPR. Nakala za sheria za Umoja wa Ulaja juu ya faragha zinaweza kupatikana kwenye tovuti ya Tume ya Umoja wa Ulaya kupitia https://ec.europa.eu/info/law/law-topic/data-protection/data-transfers-outside-eu/model-contracts-transfer-personal-data-third-countries_de.

FEndapo umeondolewa kwenye mtihani wa Goethe-Institut kwa sababu zulizotajwa kwenye kanuni za mtihani na kisha Goethe-Institut ikakuzuia kufanya mitihani kama sehemu ya utaratibu wa mitihani inayotolewa na Taasisi ya Goethe duniani, taarifa zako binafsi zitapelekwa kwenye vituo vya mitihani wa Taasisi ya Goethe (angalia seksheni ya 2 ya kanuni za mtihani) duniani na kwenye vituo vya mitihani vya Diploma ya Lugha Austria (ÖSD) kwa lengo la kusimamia hatua hizi (udhibiti wa uzingativu wa zuio lililowekwa la kutofanya mtihani) na kuchakatwa huko kwa lengo hili mahsusi. Jambo hili linafanyika kwa msingi wa utekelezaji wa mkataba wa pamoja juu ya utoaji wa wa mtihani kwa mujibu wa Ibara ya 6 (1) (b) GDPR. Kwa mantiki hii data zinazotoa utambulisho wa mtu binafsi zinachakatwa katika nchi zilizo nje ya Umoja wa Ulaya au Zoni ya Kiuchumi ya Ulaya, pia jambo hili linafanyika kutokana umuhimu wa uhamishaji kwa lengo la utekelezaji wa mkataba huu.

 
  b) Uhamishaji wa data kwenda kituo cha makavazi ya mtihani
Kwa lengo la kuhakiki uasilia na ubadilishaji wa vyeti, data kuhusiana na mitihani uliyofanya zitahifadhiwa na kutumiwa katika kituo cha makavazi ya mtihani (kwa ukomo wa miaka10). Jambo hili linafanyika kwa msingi wa utekelezaji wa mkataba kwa mujibu wa Ibara ya 6 (1) (b) GDPR.
 

10. USALAMA WA DATA

Tunailinda tovuti yetu na mifumo mingine kupitia hatua za kiteknolojia na kiutawala dhidi ya upotevu, uharibifu, uwezo wa kutumia, kufanyiwa mabadiliko au kutolewa kwa taarifa zako binafsi na watu wasioruhusiwa, kama vile wakati wa kutengeneza akaunti ya Goethe.de au kuingia kwenye akaunti yako tena na tena kupitia mfumo wa SSL.  

11. HAKI ZAKO NA JINSI YA KUWASILIANA NASI

Kama mhusika wa data, una haki zifuatazo:
 • kwa mujibu wa Ibara ya 15 GDPR, haki ya kuomba taarifa kuhusu data zako zinazotoa utambulisho wa mtu binafsi zilizochakatwa nasi kwa kiasi kilichoelezwa hapa;
 • kwa mujibu wa Ibara ya 16 GDPR, haki ya kudai kufanyika mara moja kwa masahihisho ya data zinazotoa utambulisho wa mtu binafsi zilizohifadhiwa nasi, zilizokosewa au kutokukamilika;
 • kwa mujibu wa Ibara ya 17 GDPR, haki ya kudai kuondolewa kwa data zako zinazotoa utambulisho wa mtu binafsi zilizohifadhiwa nasi, isipokuwa pale ambapo data hizo ni muhimu
  • kuhakikisha utekelezaji wa haki ya uhuru wa kujieleza na kupata taarifa;
  • kutimiza takwa la kisheria;
  • kwa sababu za maslahi ya umma, au
  • kudai, kutumia au kutoa utetezi kwenye madai ya kisheria
 
 • kwa mujibu wa Ibara ya 18 GDPR, haki ya kudai zuio la uchakataji wa data zako zinazotoa utambulisho wa mtu binafsi, pale ambapo
  • unatilia shaka usahihi wa data;
  • uchakataji ni kinyume cha sheria, lakini hauko radhi kuondolewa;
  • hatuhitaji tena data, lakini unazihitaji kwa lengo la kudai, kutumia au kutoa utetezi kwenye madai ya kisheria, au
  • umefungua madai ya pingamizi juu ya uchakataji kwa mujibu wa Ibara ya 21 GDPR
 • kwa mujibu wa Ibara ya 20 GDPR, haki ya kupokea data zako zinazotoa utambulisho wa mtu binafsi zilizotolewa kwetu katika muundo uliopangiliwa, uliozoeleka na unaosomeka au kuomba uhamishaji kwenda kwa mdhibiti mwingine;
 • kwa mujibu wa Ibara ya 77 GDPR, haki ya kufungua malalamiko kwenye mamlaka ya usimamizi. Kama kanuni, unaweza kuwasiliana na mamlaka ya usimamizi yalipo makazi yako au sehemu yako ya kazi au ofisi ya kampuni yako.

Endapo una maswali yoyotekuhusu ukusanyaji, uchakataji au matumizi ya data zako zinazotoa utambulisho wa mtu binafsi, kuhusu taarifa, masahihisho, zuio la uchakataji au kuondolewa kwa data pamoja na kutenguliwa kwa ridhaa zozote zilizotolewa au pingamizi kwa matumizi fulani ya data pamoja na haki ya uwezo wa kuhamisha data, tafadhali wasiliana na ofisa wa kampuni yetu ya ulinzi wa data:

Ofisa Ulinzi wa Data
Goethe-Institut e.V.
Oskar-von-Miller-Ring 18
80333 München
datenschutz@goethe.de
 

12. HAKI YA PINGAMIZI

Kwa mantiki hii wakati tunachakata data zinazotoa utambulisho wa mtu binafsi kulingana na ufafanuzi uliotolewa hapo juu ili kulinda maslahi yetu mapana na halali, unaweza kupinga uchakataji huu kwa matumizi ya baadaye. Endapo uchakataji unafanyika kwa malengo ya kufanya matangazo ya moja kwa moja, unaweza kutumia haki hii wakati wowote ule kulingana na maelezo yaliyotolewa hapo juu. Endapo uchakataji unafanyika kwa malengo mengine, una haki ya pingamizi pale tu kunapokuwa na sababu zinazotokana na hali fulani inayokuhusu.

Baada ya kutumia haki yako ya pingamizi, hatutaendelea kuchakata data zako zinazotoa utambulisho wa mtu binafsi kwa malengo hayo, isipokuwa kama tuna sababu muhimu sana za ulinzi wa uchakataji zinazopindukia maslahi yako, haki na uhuru, au endapo huduma za uchakataji zimefanyika ili kutetea haki, kudai au kujitetea dhidi ya madai ya kisheria.

Sharti hili halihusiki endapo uchakataji unafanyika kwa malengo ya kufanya matangazo. Kwa maana hiyo hatutaendelea kuchakata data zako zinazotoa utambulisho wa mtu binafsi kwa lengo hili mahsusi.