Fanya Mazoezi Ya Kijerumani Bila Malipo
Katika kituo cha Goethe-Institut, unajifunza Kijerumani kutoka kwa wataalamu wenye uzoefu. Tumetengeneza nyenzo mbalimbali za kutumia bila malipo za kukusaidia kufanya mazoezi ya Kijerumani chako – kwenye app zenye matini ya kujifunzia hadi video, vipindi vya sauti na michezo, pamoja na mitandao ya kijamii na programu za jumuiya. Haijalishi unaongea Kijerumani kwa ustadi gani na sababu zako zozote zile za kuboresha Kijerumani chako, suala muhimu ni kwamba unaanza kufanya mazoezi – na kukifurahia!