Ujumuishaji: Kuishi na Ulemavu

Nchini Ujerumani, kuna karibu waja milioni nane wanaoishi na ulemavu mkubwa. Kuna aina nyingi za ulemavu. Wapo waja wenye ulemavu wa kimwili, kwa mfano waja wasioona au wanaotumia kiti cha magurudumu. Ulemavu huu mara nyingi unaweza kuonekana kwa urahisi. Pia kuna ulemavu ambao hauonekani. Kwa mfano, matatizo ya kujifunza, magonjwa sugu kama saratani au magonjwa ya afya ya akili. Wapo waja waliozaliwa na ulemavu wao. Wakati mwingine ulemavu unatokana na ajali au ugonjwa.

Audio-Player: Artikel anhören

Artikel anhören

Inklusion

Schild mit Rollstuhl vor einer Treppe © Goethe-Institut/ Simone Schirmer

Haki

Tangu mwaka 2009, Mkataba wa Umoja wa Mataifa kuhusu Haki za Waja Wenye Ulemavu unatumika nchini Ujerumani. Katika Katiba ya Ujerumani imeandikwa kwamba waja wote ni sawa. Hii inawahusu pia waja wenye ulemavu. Hakuna mja anayepaswa kubaguliwa kwa sababu ya ulemavu. Waja wenye ulemavu wanapaswa kushiriki katika maisha ya kijamii sawa na wengine. Kwa bahati mbaya, maisha kwa waja wenye ulemavu ni magumu zaidi. Ujumuishaji bado haujatimika kikamilifu kila mahali.

Msaada kutoka kwa serikali

Serikali ya Ujerumani inawauni waja wenye ulemavu. Kwa mfano, wanalipa kodi kidogo. Kuna huduma za ushauri zinazotolewa. Wanapata matibabu ya kitabibu. Wakati mwingine, gharama za kutunza watoto au msaidizi wa kazi za chengoni hulipwa. Inategemea aina ya ulemavu wa mja husika.

Ili kupata msaada kutoka kwa serikali, unahitaji kuwa na cheti cha ulemavu mkubwa. Unaweza kuomba cheti hiki katika Mamlaka ya Ustawi wa Jamii. Kwa kutumia hati hii, unaweza kutumia usafiri wa umma kama mabasi au treni za chini kwa chini bila malipo. Pia unapata kiingilio cha bure kwenye makumbusho.

Ujumuishaji kazini

Waja wenye ulemavu hupata msaada wakati wanapotafuta kazi. Wanalindwa kazini. Waajiri hawaruhusiwi kukusitisha kazi kwa urahisi. Kuna maafisa wa usawa kazini. Hawa ni waja wanaohakikisha kuwa waja wenye ulemavu hawadhulumiwi kazini.

Miundombinu

Hata waja wenye ulemavu wanapaswa kuwa na maisha mazuri. Ili hili lifanikiwe, ni muhimu waweze kujitegemea katika harakati zao mjini. Nchini Ujerumani, kuna juhudi za kuhakikisha kuwa waja wanaotegemea viti vya magurudumu wanaweza kufikia majengo ya umma. Au waweze kuingia kwa urahisi kwenye mabasi na tramu. Mara nyingi kuna njia za mteremko. Kwa bahati mbaya, hali hii haipo kila mahali. Treni za chini kwa chini mara nyingi hazijafikiwa kwa urahisi. Sio kila wakati kuna lifti.

Kwa waja wasioona, kuna mistari maalum ardhini. Mistari hii huwauni kwa vipingo vyao ili kupata njia ya kuingia kwenye jengo au kufika kwenye kituo cha basi. Taa nyingi za barabarani hutoa sauti fulani. Hii huwasaidia waja wasioona kujua wakati wa kuvuka barabara. Katika baadhi ya majengo ya umma kuna maandishi ya nukta nundu.

Pia, tovuti za intaneti zinapaswa kuwa rahisi kufikiwa. Hii inawawezesha waja wote kutumia taarifa zilizopo. Mamlaka na halmashauri hutoa taarifa muhimu kwa lugha rahisi. Wananchi wote wanapaswa kuelewa taarifa hizi. Kwa waja wenye uoni hafifu, tovuti zinahitaji kuwa na utofauti mzuri kati ya maandishi na mandharinyuma. Zaidi ya hayo, maudhui ya tovuti yanapaswa kupangwa kwa namna ambayo kifaa cha kusomea maandishi kinaweza kuyasoma yote.

Watoto wenye ulemavu

Una mtoto mwenye ulemavu au mwenye ugonjwa sugu? Mamlaka ya ustawi wa watoto na vijana katika mji wako inaweza kukuauni.

Kwa watoto wadogo, kuna huduma za uhamasishaji wa mapema. Hizi ni msaada kwa watoto kutoka kuzaliwa hadi kufikia umri wa kuanza shule. Zinalenga watoto wenye ulemavu au watoto wanaojifunza kwa kasi ndogo kuliko wengine. Kwa mfano, kuna shule ya uoni au msaada wa ukuzaji wa lugha.

Hata watoto wenye ulemavu wanaweza kuhudhuria chekechea. Kuna chekechea shirikishi. Huko, watoto wenye ulemavu na wasio na ulemavu hufunzwa pamoja. Pia kuna chekechea maalum kwa watoto wenye ulemavu pekee.

Hali ni sawa pia kwa shule. Nchini Ujerumani kuna shule maalum kwa watoto wenye ulemavu au mahitaji maalum ya elimu. Na kuna shule zenye masomo ya pamoja. Hii ina maana: watoto wenye ulemavu na wasio na ulemavu hufunzwa pamoja. Hii inatofautiana kulingana na kila jimbo la Ujerumani.

Ubaguzi

Iwapo haki haziheshimiwi, wakati mwingine inaweza kuwa ni ubaguzi. Jinsi ya kukabiliana na hali hiyo, soma katika maandishi ya Kukabiliana na Ubaguzi.

Maswali ya Mara kwa Mara

Tufuatilie