Usafiri

Straße in einer Stadt mit Straßenbahnen und Bus © Goethe-Institut/ Gina Bolle

Waja wengi nchini Ujerumani hutembea kwa miguu au huendesha baiskeli. Hili ni jambo la siha na pia linanufaisha mazingira. Kuna njia nyingi za waendao kwa miguu na za baiskeli. Katika vitongojii na miji midogo, unaweza kufikia sehemu nyingi kwa miguu. Waja wengi nchini Ujerumani huenda madukani, kazini au kuwatembelea wandani kwa kutumia baiskeli.

Audio-Player: Artikel anhören

Artikel anhören

Mobilität

Kwa miguu na kwa baiskeli

Pale ambapo hakuna njia ya baiskeli, waja wazima hulazimika kuendesha barabarani. Watoto walio na umri wa hadi miaka 8 sharti waendeshe baiskeli kwenye njia ya waendao kwa miguu wakiwa mjini au mahali palipo na makaazi. Watoto hadi miaka 10 wanaruhusiwa kutumia njia ya waendao kwa miguu. Kuna sheria za barabarani: kwa mfano, ukivuka taa ikiwa nyekundu au ikiwa taa ya baiskeli yako imeharibika, polisi wakikutia machoni, utatozwa faini – yaani adhabu ya pesa.

Kwa usafiri wa umma

Katika miji, kuna usafiri wa umma kama vile treni za juu ardhini, treni za chini ya ardhi, tramu (huko Ujerumani Kusini zaitwa Tram) na mabasi. Karibu kila mji una mpango wa simu kwa usafiri huu. Unaweza kununua tiketi kwa urahisi kupitia mpango huo. Pia kuna mashine za tiketi katika vituo vya reli na vituo vya magari. Vituoni, tiketi pia zinapatikana kwa njia ya kaunta. Wakati mwingine unaweza kununua tiketii ndani ya basi au tramu.

Katika miji mingi, sharti uthibitishe tiketi yako. Kuna mashine za kufanya hivyo. Mara nyingi unaingiza tiketii kwenye sehemu ya mashine, na mashine itatia muhuri wa tarehe na saa. Katika baadhi ya miji, tiketi huwa tayari zina muda wa matumizi ulioandikwa. Hizi huhitaji uthibitisho tena.

Unaweza pia kununua tiketi ya siku moja, ya juma, ya mwezi au ya mwaka. Kama unasafiri mara kwa mara ukitumia usafiri wa umma, hili huwa nafuu zaidi. Watoto, wanagenzi wa shule, wanagenzi wa vyuo na wazee mara nyingi hupata punguzo. Wanalipa bei ya chini. Waja wenye ulemavu mara nyingi husafiri bure.

Katika vituo vya mabasi na vituo vya reli, kuna ratiba za safari. Ratiba huonyesha mabasi au treni itang'oa nanga saa ngapi na kuelekea wapi? Unaweza pia kuangalia ratiba hizo kwenye tovuti za kampuni za usafiri au kupitia programu kwenye simu.

Kawaida, vituo vya reli havina vizuizi mlangoni. Unaweza kuingia moja kwa moja. Hata hivyo, sharti uwe na tiketi halali. Katika mabasi na treni, ukaguzi wa tiketi huaandaliwa ghafla mara kwa mara. Ukitiwa mbaroni kama huna tiketi, utatozwa faini.

Katika miji mingi mikubwa, kuna pikipiki na baiskeli za umeme zinazoweza kukodishwa. Unahitaji programu ya simu ili kuzitumia. Malipo hufanyika kwa kila safari. Unaweza kutumia programu hio kutafuta kama kuna chombo kilicho karibu nawe na kuanza safari papo hapo. Ukifika unakoenda, unakiweka tu mahali salama. Hii huauni hasa pale ambapo hakuna kituo cha usafiri wa umma karibu.

Tikiti ya Ujerumani

Unasafiri mara kwa mara kwa usafiri wa umma au unazuru maeneo mbalimbali nchini Ujerumani? Basi tiketi ya Ujerumani inakufaa. Kwa euro 49 kwa mwezi (kuanzia 2024), unaweza kutumia mabasi yote, tramu, treni za chini na juu ya ardhi na treni za maeneo ya karibu. Tiketi hii haitumiki kwa mabasi ya masafa marefu, wala treni za IC-/EC- au ICE. Kwa hizo, unahitaji tiketi ya ziada. Tiketi ya Ujerumani hutolewa kwa njia ya usajili wa kila mwezi. Maana yake ni kuwa: utanunua tiketi mwezi mmoja na utapokea tiketi mpya bila ya mkono wa mja mwezi unaofuata. Kwa hivyo, unalipia euro 49 kila mwezi. Ukihitaji kusitisha, lazima uifute kabla ya tarehe 10 ya mwezi husika.

Kwa gari

Waja wengi wanaoishi vitongojini hutumia magari yao binafsi. Hii ni kwa sababu mara nyingi hakuna au kuna usafiri wa umma mchache sana. Hata mijini, baadhi ya waja hutumia magari. Katika miji kuna maegesho ya barabarani na ya majumba ya kuegesha: alama za barabarani huonyesha wapi pa kuegesha. Mara nyingi, unalazimika kulipa. Si rahisi kila mara kupata sehemu ya kuegesha.

Katika miji mingi, kuna huduma za kugawana magari. Kupitia mpango wa simu, unaweza kukodisha gari. Kwa mfano, kama ungependa kwenda matembezi ya familia. Malipo hufanyika kwa kila kilomita au kwa muda ulioutumia. Kugawana magari ni nafuu zaidi kuliko kuwa na gari lako binafsi.

Ukilitumia gari, sharti uzifahamu sheria za barabarani za Ujerumani. Ni sharti ufahamu alama mbalimbali zinamaanisha nini na pia kasi inayoruhusiwa. Sharti uwe na leseni ya kuendesha gari kila wakati. Kwa gari lako binafsi, unahitaji hati ya usajili wa gari. Polisi wanaweza kukuuliza hayo wakati wa ukaguzi. Unahitaji leseni kutoka Ujerumani au kutoka nchi nyingine ya Umoja wa Ulaya.

Nchi yako haimo katika Umoja wa Ulaya? Basi sharti ugeuze leseni yako ndani ya miezi sita ya kwanza ya kukaa Ujerumani. Anza mchakato huo upesi iwezekanavyo. Unaruhusiwa kuendesha gari kwa leseni yako ya awali kwa muda wa miezi sita tu. Jisajili katika ofisi ya leseni ya eneo lako. Umeshindwa kubadilisha leseni ndani ya muda huo na bado ungependa kuendesha gari? Basi utahitaji kufanya upya mtihani wa udereva nchini Ujerumani.

Safari

Ungependa kusafiri kwenda miji mingine ya Ujerumani au hata nje ya nchi? Unaweza kutumia treni, ndege au basi.

Waja wengi husafiri ndani ya Ujerumani kwa kutumia treni. Kwenye njia nyingi, huduma hutolewa na Deutsche Bahn (DB). Katika maeneo mengine kuna watoa huduma wengine. Akraba zilizo na watoto husafiri kwa bei nafuu kupitia Deutsche Bahn. Watoto wanaosafiri na wazazi au mzazi mmoja husafiri bure hadi umri wa miaka 14. Tiketi za treni huwa ghali ukichelewa kuzinunua. Tumia punguzo la bei nafuu. Ukihifadhi mapema, tiketi ni nafuu zaidi. Tiketi ya Ujerumani inatumika kwa treni za maeneo ya karibu za DB. Safari kwa treni hizi huchukua muda mrefu zaidi ikilinganishwa na treni za ICE.

Vituo vya mabasi ya masafa marefu hupatikana karibu na vituo vya reli katika miji mingi. Mabasi haya husafiri kwenda miji mbalimbali nchini Ujerumani na barani Ulaya. Ukihifadhi mapema, tiketi ni za bei nafuu zaidi. Mabasi haya ni ya starehe na mara nyingi huwa na mtandao wa WiFi.

Nchini Ujerumani kuna viwanja kadhaa vya ndege vya kimataifa. Kwa visiwa vya Bahari ya Kaskazini na Bahari ya Baltiki, pia kuna meli kubwa zinazofika huko.

Maswali Ya Mara kwa Mara

Tufuatilie