Bima

Auto mit Schaden an hinterer Türe © Goethe-Institut/ Gina Bolle

Kila mja anaweza kuugua au kupoteza kazi. Pia mambo mengine yanaweza kutokea. Hivyo tunaishi kwa hatari. Hatari hizi zinaweza kuwa za gharama kubwa. Madamu hii, kuna bima. Kwa mfano, zinakulipa sehemu au gharama zote unapopata ajali.

Audio-Player: Artikel anhören

Artikel anhören

Versicherungen

Bima Mbalimbali

Bima sharti ifungwe mapema. Unafanya mkataba na kulipa pesa kila mwezi au mara moja kwa mwaka kwa kampuni ya bima.

Baadhi ya bima ni za sharti nchini Ujerumani. Kila mja sharti awe na bima hizo. Hizo bima huwa na kanuni maalum. Bima nyingine ni za hiari: Unaweza kuwa nazo kama unataka

Bima ya Kijamii

Ujerumani ina mfumo mzuri wa usalama wa kijamii. Una mwajiri? Basi unachangia kwenye bima ya kijamii. Soma maelezo zaidi katika maandishi yetu "Kuanza Kazi". Pesa za bima zinakatwa moja kwa moja kutoka kwa mshahara. Hauna haja ya kulipa mwenyewe. Mwajiri wako hukulipia nusu ya gharama. Kiasi cha pesa kinategemea mshahara wako. Anayepata mshahara mkubwa hulipa zaidi. Anayepata kidogo hulipa kidogo. Hivyo basi waja wenye kipato kidogo wanaweza kupata pia wao ulinzi.

Bima ya kijamii inajumlisha bima ya kisheria ya afya, bima ya kisheria ya huduma za uuguzi bima ya ya kisheria ya ajali, bima ya kisheria ya ruzuku ya wastaafu na bima ya kisheria ya ukosefu wa ajira Katika bima hizi, waja wote wanatendewa kwa usawa. Kila mja anapata huduma sawa, hata kama hakuweza kuchangia kiasi kikubwa cha pesa.

Ikiwa wewe ni mjasiriamali, yaani una kampuni yako mwenyewe, hulazimiki kulipa bima ya kijamii. Unapaswa kujipangia bima yako mwenyewe. Waja wasio na ajira au walioko kwenye mpango wa ajira maalum aina ya „Minijob“ hawalipi bima ya kijamii.

Bima ya Afya

Bima ya afya ni ya sharti kwa waja wote nchini Ujerumani. Inalipa gharama unapoenda kwa daktari, unapolazwa hospitalini, au unapohitaji dawa. Kuna bima za afya za serikali na za binafsi. Waja wenye kazi za kudumu mara nyingi wako kwenye bima ya afya ya serikali. Unaweza kuwaingiza watoto wako bila malipo kwenye bima hii. Hii pia inatumika kwa mume au mke wako ikiwa hawafanyi kazi au wanapata kipato kidogo.

Wajasiriamali wanaweza kuchagua kujiunga kwa hiari kwenye bima ya afya ya serikali au kuwa na bima binafsi. Pia baadhi ya makundi ya wafanyakazi wenye ajira ya kudumu wana bima binafsi, kwa mfano wakufunzi. Mara nyingi, bima binafsi inafaa kwa waja wanaopata kipato kikubwa.

Kutoka kwa bima ya afya, utapata kadi ya bima ya afya. Sharti ubebe kadi hii kila mara na uionyeshe unapokwenda kwa daktari.

Bima Nyingine za Sharti

Bima ya ukosefu wa ajira inakulipa pesa unapopoteza kazi na bado hujapata kazi nyingine. Muda na kiasi cha pesa vinategemea mambo mengi: kwa mfano, muda uliokuwa ukifanya kazi na kiasi cha mshahara wako. Hii inatumika tu kama unastahili kupata malipo ya ukosefu wa ajira.

Bima ya ruzuku ya wastaafu pia ni ya lazima kwa wafanyakazi.Unapozeeka, huwezi kufanya kazi tena. Bima ya ruzuku ya wastaafu itakulipa pesa za kutumia kwenye ukongwe.

Wafanyakazi pia wana bima ya ajali. Hii inalipa unapopata ajali ukiwa kazini au kuugua kutokana na kazi.

Bima ya huduma za uuguzi (yaani bima ya uangalizi wa wagonjwa) inalipa pesa unapohitaji huduma za uangalizi wa kudumu. Kwa kawaida ni waja wazee wanaohudumiwa, lakini hata vijana wanaweza kuhitaji huduma hii baada ya ajali mbaya.

Wajasiriamali hawalazimiki kuwa na bima hizi. Lakini wanaweza kujiunga kwa hiari.

Ikiwa una gari au pikipiki unahitaji bima ya motokaa. Ukiigonga gari ya mja mwingine kwenye ajali, bima ya motokaa italipa gharama ya matengenezo au sehemu yake.

Bima za Hiari

Bima zenye natija za hiari ni bima ya dhima na bima ya kutoweza kufanya kazi. Ukiharibu kitu cha mja mwingine, yaweza kukugharimu pesa nyingi. Bima ya dhima hulipa gharama hizi. Haina gharama kubwa.

Unalo jibwa? Basi unapaswa pia kuwa na bima ya dhima kwa ajili ya jibwa lako.

Bima ya kutoweza kufanya kazi inafanya kazi hivi: Ukigundulika na ugonjwa mkubwa na huwezi kufanya kazi, hupokei tena mshahara. Bima hii inakulipa pesa kila mwezi. Bima hii ni ghali. Wanaolipa zaidi hupata malipo zaidi. Wanaolipa kidogo hupata malipo kidogo.

Bima ya mali ya nyumba na bima ya maisha pia zinaweza kuwa na faida. Bima ya mali ya nyumba hulipa ikiwa mali chengoni imeharibika, kwa mfano kutokana na mafuriko.Nayo bima ya maisha hulipa pesa endapo mja atafariki. Pesa hizi zaweza kulipwa kimfano kwa watoto.

Bima ya kisheria ya ruzuku ya wastaafu mara nyingi hulipa kiasi kidogo. . Kuna pia bima binafsi za ruzuku ya wastaafu. Bima ya ziada ya ruzuku ya wastaafu ni ya natija kama unataka kuishi vizuri ukiwa mkongwe. Serikali inasaidia baadhi ya bima hizi.

Kuna bima nyingine nyingi, ambazo zinaweza kufaa kulingana na hali yako ya aushi. Lakini hakikisha kuwa umefanya udadisi kwa makini kuhusu ni bima zipi unazohitaji. Sio nyingi sana zinazohitajika. Kila bima ina gharama. Bima binafsi ya ajali inalipa gharama za ajali zinazotokea wakati wa burudani. Bima ya msaada wa kisheria inalipa gharama za wakili.

Pia kuna bima za safari, meno, miwani, mikopo, au simu. Tafakaria kwa makini kuhusu ukubwa wa hatari. Vitu vingi vinaweza kulipwa na mwenyewe bila kuhitaji bima.

Maswali Ya Mara kwa Mara

Tufuatilie