Kuanza Kazi

Eine Frau sitzt am Schreibtisch © Goethe-Institut/ Gina Bolle

Umefanikiwa kupata kazi ya kudumu Ujerumani? Basi wewe ni mfanyakazi.

Audio-Player: Artikel anhören

Artikel anhören

Arbeitsaufnahme

Nyaraka Muhimu Unapoanza Kazi

Utahitaji nyaraka fulani kwa ajili ya mwajiri wako. Kwanza, unahitaji uthibitisho kwamba una bima ya afya. Uthibitisho huu unapatikana kwenye shirika lako la bima ya afya. Nchini Ujerumani, kila mja sharti awe na bima ya afya. Pia, unahitaji uthibitisho kuwa unamiliki akaunti ya benki. Mwajiri atakuwekea mshahara wako wa kila mwezi kwenye akaunti hiyo. Mwajiri pia atahitaji nakala ya hati yako ya ukaazi yenye kibali cha kufanya kazi (tazama maandiko kuhusu "Kutafuta Ajira"). Kunao waajiri ambao wanaweza pia kuomba cheti cha hulka njema kutoka kwa polisi. Cheti hiki unapata katika ofisi ya usajili wa wakazi.

Bima, Kodi

Ujerumani, kila mja sharti awe na bima ya afya. Lazima ujiunge nayo mwenyewe kabla ya siku yako ya kwanza kazini. Kama mfanyakazi, kwa kawaida unatakiwa kuchangia kwenye mifuko ya hifadhi ya jamii: Hii ina maana kuwa, pia una bima ya ruzuku ya wastaafu, bima ya ukosefu wa ajira, bima ya uuguzi na bima ya ajali. Mwajiri hulipa sehemu ya ada za bima hizi, na wewe unalipa sehemu nyingine. Ada zako hukatwa moja kwa moja kutoka kwenye mshahara wako. Maelezo zaidi yanapatikana kwenye maandiko ya "Bima".

Unahitaji pia nambari ya kodi na kadi ya kodi ya kielektroniki (ELStAM). Vyote hivi unavipata kutoka kwa Wizara ya Fedha. Kadi ya kodi ya kielektroniki hutumwa moja kwa moja kwa mwajiri na Wizara ya Fedha. Haina haja ya kuhamisha kodi wewe mwenyewe. Mwajiri atahitaji kodi kutoka kwa mshahara wako na kuituma moja kwa moja hadi kwa Wizara ya Fedha. Unaweza (na wakati mwingine ni sharti) kuwasilisha tamko la mapato ya kodi. Hili linafaa, kwani mara nyingi Utapata unarejeshewa kiasi fulani cha ngwenje. Maelezo zaidi yanapatikana kwenye maandiko ya "Fedha na Kodi".

Mkataba wa Ajira

Wafanyakazi hukadhibiwa mkataba wa kazi. Wewe na mwajiri wako,nyote mtatia sahihi kwenye mkataba huo. Soma mkataba wa kazi kwa makini sana bila Kasi yoyote, kabla ya kutia sahihi. Ikiwa huelewi mambo fulani, uliza msaada: Kwa waja wazima, nenda kwenye ushauri wa uhamiaji kwa waja wazima (MBE). Vijana ni waja wachanga kufikia hadi miaka 27, wanapata msaada kwenye huduma za uhamiaji wa vijana (JMD). Pia unaweza kupiga simu kwa huduma ya wananchi ya Wizara ya Kazi na Masuala ya Jamii ya Shirikisho (+49 30 221 911 004). Hapa unaweza kuuliza maswali kuhusu "Haki za Kazi".

Katika mkataba wa kazi kuna sheria zote muhimu. Wewe na mwajiri wako mnapaswa kuzingatia sheria hizo. Mfano, utaona: Unalipwa kiasi gani kwa mwezi? Una siku ngapi za likizo? Unapaswa kufanya nini ukiugua? Kazi mpya mara nyingi huanza na kipindi cha majaribio. kipindi cha majaribio kinaweza kuwa kifupi au kirefu: majuma machache hadi nusu mwaka. Katika kipindi cha majaribio, mwajiri anakufatamia kwa karibu sana ili kufanya maamuzi iwapo utaendelea kufanya kazi baada ya kipindi cha majaribio. Wewe pia utaamua iwapo ungependa kuendelea na kazi hiyo baada ya majaribio. Katika kipindi cha majaribio, muda wa kutoa taarifa ya kuacha kazi ni mfupi (kwa kawaida wiki 2 hadi 3), baada ya hapo kawaida ni miezi 3. Kuna mikataba ya muda maalum na ya kudumu. Mkataba wa muda maalum unakamilika moja kwa moja baada ya muda huo kumalizika bila barua ya kusitisha kazi. Maelezo zaidi kuhusu saa za kazi, likizo, uele na kusitisha kazi yanapatikana kwenye maandiko ya "Mahala pangu ya Kazi".

Kazi Ndogo maalum aina ya Minijobs

Kuna pia kazi ndogo Ujerumani. Kazi ndogo ni kazi ambazo mja hupokea mshahara wa hadi Euro 538 kwa mwezi au mda wa kufanya kazi si zaidi ya siku 70 kwa mwaka wa kalenda. Kuna bima ya ajali. Hata hivyo, kama huna bima ya afya au ya uuguzi moja kwa moja. Lazima ujihudumie kupata bima ya afya wewe binafsi. Unaweza kuchagua kama utachangia kwenye bima ya ruzuku ya wastaafu au kuomba kutoichangia bima hiyo. Kama hauna bima ya ukosefu wa ajira.

Kazi ya Kujitegemea

Unajiajiri mwenyewe, hivyo basi wewe si mfanyakazi? Ukipanga kuanzisha biashara yako mwenyewe, unahitaji cheti cha biashara. Hiki unakipata kutoka kwa Idara ya biashara. Unaweza kuulizia katika halmashauri ya mji wako mahali Idara ya biashara ilipo. Hata ukifungua duka au mkahawa, unahitaji cheti cha biashara.

Unapofanya kazi kama mtaalamu huru, sharti uripoti shughuli yako kwa Wizara ya Fedha. Ni sharti pia upate nambari ya kodi. Wizara ya Fedha inahitaji kufahamu takribani faida yako ya kila mwaka, na itakuelezea utalipa kodi kiasi gani. Kodi hii utahitajika kuilipia mwenyewe.

Pia unahitaji bima ya afya. Ni sharti ulipe gharama ya bima ya afya wewe binafsi. Ni vyema pia kuwa na bima ya ruzuku ya wastaafu. Katika baadhi ya taaluma, kwa mfano katika fani za uashi au ukunga, ni sharti kuwa na bima ya ruzuku ya wastaafu. Bima nyinginezo pia zinaweza kuwa za natija. Ushauri mwingi kuhusu kuanzisha biashara upo kwenye tovuti ya Tunaanzisha Biashara Ujerumani.

Maswali Ya Mara kwa Mara

Tufuatilie