Dansi Tena

Dansi Tena

Said, Asili yetu | © Goethe-Institut Tanzania

Mradi wa kucheza wa Dansi Tena

Ngoma za kisasa! Je hiyo ni nini? Miondoko ya kushangaza? Miondoko ya dhahania (ya kufikirika? Si ya kawaida? Ya ajabu? Uelewi? Usijali utaelewa. Kutana na watunzi wa dansi, katika kipindi kipya ambacho kitakuletea mtiririko wa maonesho ya filamu za dansi kupitia mtandao. Kipindi kinaitwa Dansi tena. Watakufanya upende na kuwa mshabiki mzuri wa dansi za kisasa.
Fuata utaratibu:
  1. Tazama dansi
  2. Msikilize mtunzi
  3. Tazama tena dansi! Furahia, na tupe maoni yako jinsi ulivyohisi baada ya kutazama!

Kuhusu Dansi tena

Muda Africa, kwa kushirikiana na Taasisi ya Goethe-Institut, inakuletea mpango mpya unaoitwa Dansi tena. Huu ni mtiririko wa filamu za dansi za kisasa zilizobuniwa, kuchezwa na kurekodiwa na watunzi, wacheza ngoma na watengeneza video kutoka Tanzania na Afrika ya mashariki. Dansi za kisasa ni aina mpya ya sanaa katika Afrika Mashariki na wakati mwingine huonekana kama ni za ajabu, ni za kushangaza na ni za kufikirika. Filamu za Dansi tena  zitajaribu kutoa mwanga kwa watazamaji kwa kuwa na mazumguzo na watunzi wa dansi ambao wataelezea hadithi, harakati na hisia nyuma ya kila utunzi wao. Mtazamaji anaombwa kutazama filamu ya dansi, kumsikiliza mtunzi, na kisha kuangalia tena filamu ya dansi huku wakiwa na ufahamu mpya ambao utakuwa umetokana na mazumguzo ya mtunzi. Dansi tena itafanyika kuanzia Septemba na itachukua nafasi ya tamasha la Time 2 Dance 2020 la Muda Africa kutokana na janga la COVID-19.

Msimu 01

[Bonyeza kwenye ikoni ya Playlist Icon kutazama orodha ya kucheza]

Msimu 02

Msimu 03

Tufuatilie